-->
logo

042 - Ash-Shuwraa

الشُّورى
Ash-Shuwraa: 42


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم


حم﴿١﴾
1. Haa Miym.


عسق﴿٢﴾
2. ‘Ayn Siyn Qaaaf.


كَذَٰلِكَ يُوحِي إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣﴾
3. Hivyo ndivyo Anavyokufunulia Wahy na kwa wale walio kabla yako, Allaah Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴿٤﴾
4. Ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, Naye ni (Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka,  Mwenye Taadhima, Mkuu kabisa.


تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِن فَوْقِهِنَّ ۚ وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥﴾
5. Zinakaribia mbingu kuraruka kutoka juu yake, na Malaika wanasabbih kwa Himidi za Rabb wao, na wanawaombea maghfirah walioko ardhini. Tanabahi! Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ اللَّـهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ﴿٦﴾
6. Na wale waliojichukulia badala Yake walinzi; Allaah ni Mhifadhi wao, nawe si mdhamini wao.


وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنذِرَ يَوْمَ الْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚفَرِيقٌ فِي الْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِي السَّعِيرِ﴿٧﴾
7. Na hivyo ndivyo Tulivyokufunulia Wahy wa Qur-aan ya Kiarabu ili uonye mama wa miji (Makkah), na wale waliozunguka pembezoni mwake, na uonye Siku ya kujumuika isiyokuwa na shaka ndani yake. Kundi litakuwa katika Jannah, na kundi katika moto uliowashwa vikali mno.


وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَهُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٨﴾
8. Na lau Angelitaka Allaah Angeliwafanya ummah mmoja, lakini Anamuingiza Amtakaye katika rahmah Yake. Na madhalimu hawana mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.


أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۖ فَاللَّـهُ هُوَ الْوَلِيُّ وَهُوَ يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٩﴾
9. Je, wamejichukulia badala Yake walinzi? Basi Allaah Yeye Ndiye Mlinzi, Msaidizi Naye Ndiye Anayehuisha wafu, Naye Ndiye juu ya kila kitu ni Muweza.


وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ﴿١٠﴾
10. Na katika lolote lile mlilokhitilafiana, basi hukumu yake ni kwa Allaah. Huyo Ndiye Allaah Rabb wangu, Kwake nimetawakali na Kwake narudi kutubia.


فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَمِنَ الْأَنْعَامِ أَزْوَاجًا ۖ يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ ۚلَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾
11. Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Amekujaalieni kutokana na nafsi zenu mume na mke na katika wanyama wa mifugo dume na jike. Anakusambazeni humo. Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.


لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٢﴾
12. Ni Zake funguo za mbingu na ardhi, Anamkunjulia riziki Amtakaye na Anadhikisha. Hakika Yeye ni Mjuzi kwa kila kitu. 


شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ ۚ اللَّـهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ ﴿١٣﴾
13. “Amekuamuruni katika Dini yale Aliyomuusia kwayo Nuwh, na ambayo Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na Tuliyomuusia kwayo Ibraahiym, na Muwsaa na ‘Iysaa kwamba: “Simamisheni Dini na wala msifarikiane humo. Yamekuwa magumu kwa washirikina yale unayowalingania. Allaah Anamteua Kwake Amtakaye, na Anamuongoza Kwake anayerudia rudia kutubia.


وَمَا تَفَرَّقُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى لَّقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ أُورِثُوا الْكِتَابَ مِن بَعْدِهِمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ ﴿١٤﴾
14. Na hawakufarikiana isipokuwa baada ya kuwajia elimu kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Na kama si neno lilotangulia (kuakhirisha adhabu) kutoka kwa Rabb wako mpaka muda maalumu uliokadiriwa, bila shaka ingelikidhiwa baina yao. Na hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao bila shaka wamo katika shaka na wasiwasi nayo.


فَلِذَٰلِكَ فَادْعُ ۖ وَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ ۖ وَقُلْ آمَنتُ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِن كِتَابٍ ۖوَأُمِرْتُ لِأَعْدِلَ بَيْنَكُمُ ۖ اللَّـهُ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ ۖ لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ ۖ لَا حُجَّةَ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ ۖ اللَّـهُ يَجْمَعُ بَيْنَنَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿١٥﴾
15. Basi kwa hayo walinganie (ee Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم, na thibitika imara kama ulivyoamrishwa, na wala usifuate hawaa zao. Na sema: “Nimeamini yale Aliyoyateremsha Allaah katika Vitabu, na nimeamrishwa niadilishe baina yenu. Allaah ni Rabb wetu na Rabb wenu; sisi tuna ‘amali zetu, nanyi mna ‘amali zenu. Hakuna kubishana baina yetu na baina yenu; Allaah Atatujumuisha baina yetu, na Kwake ndio mahali pa kuishia.


وَالَّذِينَ يُحَاجُّونَ فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا اسْتُجِيبَ لَهُ حُجَّتُهُمْ دَاحِضَةٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ﴿١٦﴾
16. Na wale wanaobishana kuhusu Allaah baada ya kuitikiwa, hoja yao ni batilifu mbele ya Rabb wao na juu yao iko ghadhabu na watapata adhabu shadidi.


اللَّـهُ الَّذِي أَنزَلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَالْمِيزَانَ ۗ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ قَرِيبٌ﴿١٧﴾
17. Allaah Ambaye Ameteremsha Kitabu hiki kwa haki na mizani. Na nini kitakachokujulisha pengine Saa (Qiyaamah) iko karibu?


يَسْتَعْجِلُ بِهَا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِهَا ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا مُشْفِقُونَ مِنْهَا وَيَعْلَمُونَ أَنَّهَا الْحَقُّ ۗ أَلَا إِنَّ الَّذِينَ يُمَارُونَ فِي السَّاعَةِ لَفِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ﴿١٨﴾
18. Wanaihimiza wale wasioiamini; na wale walioamini wanaiogopa na wanaitambua kwamba hiyo ni haki. Tanabahi!  Hakika wale wanaotilia shaka kuhusu Saa; bila shaka wamo katika upotofu wa mbali.


اللَّـهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿١٩﴾
19. Allaah ni Latifu kwa waja Wake, Anamruzuku Amtakaye, Naye Ndiye Al- Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.


مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾
20. Yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya Aakhirah Tunamzidishia katika mavuno yake; na yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote.


أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۗوَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢١﴾
21. Je, wanao washirika waliowaamuru Dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea idhini? Na lau si neno la uamuzi, bila shaka ingelikidhiwa baina yao; na hakika madhalimu watapata adhabu iumizayo.


تَرَى الظَّالِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا كَسَبُوا وَهُوَ وَاقِعٌ بِهِمْ ۗ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِي رَوْضَاتِ الْجَنَّاتِ ۖ لَهُم مَّا يَشَاءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ﴿٢٢﴾
22. Utawaona madhalimu ni wenye kuogopa kwa yale waliyoyachuma, nayo yatawafikia tu. Na wale walioamini na wakatenda mema watakuwa katika mabustani yaliyositawi ya Jannaat, watapata wayatakayo kwa Rabb wao, hiyo ndio fadhila kubwa.


ذَٰلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّـهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ ۗ وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ شَكُورٌ﴿٢٣﴾
23. Hayo ndiyo Aliyowabashiria Allaah waja Wake wale walioamini na wakatenda mema. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Sikuombeni ujira wowote juu yake isipokuwa mapenzi kwa ajili ya ujamaa wa karibu.” Na yeyote yule anayechuma mazuri, Tutamzidishia humo zuri. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani.


أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ۖ فَإِن يَشَإِ اللَّـهُ يَخْتِمْ عَلَىٰ قَلْبِكَ ۗ وَيَمْحُ اللَّـهُ الْبَاطِلَ وَيُحِقُّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٢٤﴾
24. Je, wanasema: “Amemtungia Allaah uongo?” Basi Allaah Akitaka Atapiga mhuri juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Anaufuta ubatilifu, na Ataihakiki haki kwa maneno Yake. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.


وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ﴿٢٥﴾
25. Naye Ndiye Ambaye Anapokea tawbah kutoka kwa waja Wake, na Anasamehe maovu, na Anayajua mnayoyafanya.


وَيَسْتَجِيبُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ وَالْكَافِرُونَ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ﴿٢٦﴾
26. Na Anawaitika wale walioamini na wakatenda mema, na Anawazidishia kutoka fadhila Zake. Na makafiri watapata adhabu kali.


وَلَوْ بَسَطَ اللَّـهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ وَلَـٰكِن يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَّا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ بِعِبَادِهِ خَبِيرٌ بَصِيرٌ﴿٢٧﴾
27. Na lau kama Allaah Angelikunjua riziki kwa waja Wake, bila shaka wangefanya ufidhuli katika ardhi; lakini Anateremsha kwa kiasi Akitakacho. Hakika Yeye kwa waje Wake ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika, Mwenye kuona yote.


وَهُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ الْغَيْثَ مِن بَعْدِ مَا قَنَطُوا وَيَنشُرُ رَحْمَتَهُ ۚ وَهُوَ الْوَلِيُّ الْحَمِيدُ﴿٢٨﴾
28. Naye Ndiye Anayeteremsha mvua baada ya kuwa wamekata tamaa, na Anaeneza rahmah Yake. Naye Ndiye Mlinzi Msaidizi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.


وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَابَّةٍ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ﴿٢٩﴾
29. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake; ni uumbaji wa mbingu na ardhi, na Aliowatawanya humo kati ya viumbe vinavyotembea, Naye kwa kuwakusanya Atakapo ni Muweza.


وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ﴿٣٠﴾
30. Na haukusibuni katika msiba wowote basi ni kwa sababu ya yale yaliyochuma mikono yenu, na Anasamehe mengi.


وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ ۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٣١﴾
31. Nanyi si wenye kushinda kukwepa ardhini, na wala hamna badala Yake mlinzi yeyote na wala mwenye kunusuru.


وَمِنْ آيَاتِهِ الْجَوَارِ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ﴿٣٢﴾
32. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni merikebu zinazotembea baharini kama milima.


إِن يَشَأْ يُسْكِنِ الرِّيحَ فَيَظْلَلْنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهْرِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ﴿٣٣﴾
33. Akitaka Anautuliza upepo wa dhoruba basi zikatuama juu ya bahari. Hakika katika hayo mna Aayaat (zingatio, ishara) kwa kila mwingi wa kuvuta subira na mwingi wa kushukuru.


أَوْ يُوبِقْهُنَّ بِمَا كَسَبُوا وَيَعْفُ عَن كَثِيرٍ﴿٣٤﴾
34. Au Aziangamize kwa sababu ya waliyoyachuma, na Anasamehe mengi.


وَيَعْلَمَ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِنَا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ﴿٣٥﴾
35. Na watajua wale wanaojadiliana kuhusu Aayaat, (ishara, dalili) Zetu; kwamba hawana mahali popote pa kukimbilia.


فَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ لِلَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٣٦﴾
36. Basi chochote mlichopewa katika kitu ni starehe ndogo za uhai wa dunia.  Na yale yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na ni ya kudumu kwa wale walioamini na kwa Rabb wao wanatawakali.


وَالَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُوا هُمْ يَغْفِرُونَ﴿٣٧﴾
37. Na wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu na wanapoghadhibika wao wanasamehe.


وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ﴿٣٨﴾
38. Na wale waliomuitikia Rabb wao, wakasimamisha Swalaah, na jambo lao hushauriana baina yao, na kutokana na vile Tulivyowaruzuku wanatoa.


وَالَّذِينَ إِذَا أَصَابَهُمُ الْبَغْيُ هُمْ يَنتَصِرُونَ﴿٣٩﴾
39. Na wale inapowasibu baghi; ukandamizaji na dhulma, wao wanajitetea.


وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا ۖ فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ﴿٤٠﴾
40. Na jazaa ya uovu ni uovu mfano wake. Lakini atakayesamehe na akasuluhisha, basi ujira wake uko kwa Allaah, hakika Yeye Hapendi madhalimu.


وَلَمَنِ انتَصَرَ بَعْدَ ظُلْمِهِ فَأُولَـٰئِكَ مَا عَلَيْهِم مِّن سَبِيلٍ﴿٤١﴾
41. Na bila shaka anayelipiza kisasi baada ya kudhulumiwa, basi hao hawana sababu ya kulaumiwa.



إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤٢﴾
42. Hakika sababu ya kulaumiwa ni juu ya wale wanaodhulumu watu na wanakandamiza katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iumizayo.


وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ﴿٤٣﴾
43. Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa.


وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن وَلِيٍّ مِّن بَعْدِهِ ۗ وَتَرَى الظَّالِمِينَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ يَقُولُونَ هَلْ إِلَىٰ مَرَدٍّ مِّن سَبِيلٍ﴿٤٤﴾
44. Na aliyepotolewa na Allaah basi hatopata mlinzi baada Yake. Na utawaona madhalimu watakapoiona adhabu, wakisema: “Je, ipo njia yoyote ya kurudi (duniani)?”


وَتَرَاهُمْ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا خَاشِعِينَ مِنَ الذُّلِّ يَنظُرُونَ مِن طَرْفٍ خَفِيٍّ ۗ وَقَالَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ الظَّالِمِينَ فِي عَذَابٍ مُّقِيمٍ﴿٤٥﴾
45. Na utawaona wanahudhurishwa (kwenye moto) wakiwa wanyenyekevu kutokana na udhalilifu, wanatazama kwa mtazamo wa kificho. Na watasema wale walioamini: “Hakika wenye kukhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na ahli zao Siku ya Qiyaamah. Tanabahi!  Hakika madhalimu wamo katika adhabu ya kudumu.


وَمَا كَانَ لَهُم مِّنْ أَوْلِيَاءَ يَنصُرُونَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن سَبِيلٍ﴿٤٦﴾
46. Na wala hawatokuwa na walinzi wowote wa kuwanusuru badala ya Allaah. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hatopata njia (ya kuongoka).



اسْتَجِيبُوا لِرَبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّـهِ ۚ مَا لَكُم مِّن مَّلْجَإٍ يَوْمَئِذٍ وَمَا لَكُم مِّن نَّكِيرٍ﴿٤٧﴾
47. Muitikieni Rabb wenu kabla haijafika Siku isiyo rudishwa nyuma kutoka kwa Allaah. Hamtokuwa na mahali popote pa kukimbilia Siku hiyo na wala hamtopata cha kupinza.


فَإِنْ أَعْرَضُوا فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ إِنْ عَلَيْكَ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَإِنَّا إِذَا أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً فَرِحَ بِهَا ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَإِنَّ الْإِنسَانَ كَفُورٌ﴿٤٨﴾
48. Wakikengeuka, basi Hatukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uwe mwenye kuwahifadhi. Si juu yako isipokuwa ubalighisho (wa ujumbe). Na hakika Sisi Tunapomwonjesha insani rahmah kutoka Kwetu, huifurahia. Na linapowasibu ovu kwa sababu ya yaliyotanguliza mikono yao, basi hakika insani ni mwingi wa kukufuru.


لِّلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ يَهَبُ لِمَن يَشَاءُ إِنَاثًا وَيَهَبُ لِمَن يَشَاءُ الذُّكُورَ﴿٤٩﴾
49. Ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anaumba Atakavyo. Humtunukia Amtakaye wana wa kike, na Humtunukia Amtakaye wana wa kiume.


أَوْ يُزَوِّجُهُمْ ذُكْرَانًا وَإِنَاثًا ۖ وَيَجْعَلُ مَن يَشَاءُ عَقِيمًا ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ قَدِيرٌ﴿٥٠﴾
50. Au Huwachanganya wa  kiume na wa kike, na Humjaalia Amtakaye kuwa ni tasa, hakika Yeye ni Mjuzi wa yote, Muweza wa yote.


وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾
51. Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa idhini Yake; hakika Yeye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka,  Mwenye hikmah wa yote.


وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾
52. Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutoka amri Yetu. Hukuwa unajua nini Kitabu wala iymaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.


صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ﴿٥٣﴾
53. Njia ya Allaah Ambaye ni Vyake Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! Kwa Allaah Pekee yanaishia mambo yote.


Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.