-->
logo

043 - Az-Zukhruf

 الزُّخْرُف
Az-Zukhruf: 43


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


حم﴿١﴾
1. Haa Miym. 


وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ﴿٢﴾
2. Naapa kwa Kitabu kinachobainisha.


إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumefanya Qur-aan ya Kiarabu ili mpate kutia akilini.


وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٤﴾
4. Na hakika hii (Qur-aan) iko katika Mama wa Kitabu yaliyoko Kwetu, bila shaka imetukuka, yenye hikmah.


أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ﴿٥﴾
5. Je, Tuwaondoshelee mbali Ukumbusho huu kwa vile nyinyi mmekuwa wapindukao mipaka?


وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِن نَّبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ﴿٦﴾
6. Na Manabii wangapi Tumewatuma kwa watu wa awali?


وَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٧﴾
7. Na hawakuwafikia Nabiy yeyote isipokuwa walikuwa wakimfanyia istihzai.


فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾
8. Basi Tukawaangamiza walio na nguvu zaidi kuliko wao na imeshapita mfano wa watu wa awali.


وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ﴿٩﴾
9. Na ukiwauliza:  “Ni nani yule aliyeumba mbingu na ardhi?” Bila shaka watasema: “Ameziumba Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.


الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٠﴾
10. Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na Akakufanyieni humo njia ili mpate muongoze.


وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ﴿١١﴾
11. Na Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji kwa kipimo, Tukafufua kwayo nchi iliyokufa, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa.


وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ﴿١٢﴾
12. Na Ambaye Ameumba kila kitu jozi; dume na jike, na Akakufanyieni katika merikebu na wanyama mnaowapanda.


لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ﴿١٣﴾
13. Ili mlingamane sawasawa juu ya mgongo wake, kisha mkumbuke neema ya Rabb wenu mtakapolingamana sawasawa juu yao, na mseme: “Subhaana, Utakasifu ni wa Ambaye Ametutiishia haya, na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti.


وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ﴿١٤﴾
14. “Na hakika kwa Rabb wetu, bila shaka tutarejea.”


وَجَعَلُوا لَهُ مِنْ عِبَادِهِ جُزْءًا ۚ إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ مُّبِينٌ﴿١٥﴾
15. Na wakamfanyia kati ya waja Wake sehemu (kuwa Allaah Ana watoto), hakika insani bila shaka ni mwingi wa kukufuru, aliye bayana.


أَمِ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَاكُم بِالْبَنِينَ﴿١٦﴾
16. Je, Amejichukulia katika Aliowaumba mabanati, na Akakukhitarieni nyinyi watoto wa kiume?


وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَـٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿١٧﴾
17. Na anapobashiriwa mmoja wao kwa (binti) aliyepigiwa mfano Ar-Rahmaan husawijika uso wake naye ni mwenye kuzuia ghadhabu na huzuni.


أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ﴿١٨﴾
18. Ah! Yule aliyelelewa katika mapambo naye katika mabishano si mbainifu?


وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ إِنَاثًا ۚ أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ ۚ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ﴿١٩﴾
19. Na wakawafanya Malaika ambao ni waja wa Ar-Rahmaan kuwa ni wa kike. Je, kwani wameshuhudia uumbaji wao?  Utaandikwa ushahidi wao, na wataulizwa.


وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَـٰنُ مَا عَبَدْنَاهُم ۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿٢٠﴾
20. Na wakasema: “Angelitaka Ar-Rahmaan tusingeliyaabudu (miungu ya uongo). Hawana elimu yoyote wa hayo, hawana isipokuwa wanabuni uongo.


أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا مِّن قَبْلِهِ فَهُم بِهِ مُسْتَمْسِكُونَ﴿٢١﴾
21. Au Tumewapa Kitabu kabla yake (hii Qur-aan), basi wao kwacho wanakishikilia?


بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ﴿٢٢﴾
22. Bali wamesema: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini na hakika sisi tunajiongoza kwa kufuata nyayo zao.”


وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ﴿٢٣﴾
23. Na hivyo ndivyo Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa wamesema matajiri wake wenye starehe na taanusi: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi ni wenye kufuata nyao zao.”


قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿٢٤﴾
24. (Kila Rasuli) Alisema: “Japo kama nimekujieni na uongofu zaidi kuliko ambao mliyowakuta nao baba zenu?” Wakasema: “Hakika sisi tunayakanusha yale mliyotumwa nayo.”


فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٢٥﴾
25. Basi Tukawalipizia, kisha tazama vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.


وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ﴿٢٦﴾
26. Na Ibraahiym alipomwambia baba yake na kaumu yake: “Hakika mimi nimejitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu.


إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ﴿٢٧﴾
27. “Isipokuwa Ambaye Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoza.”


وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٢٨﴾
28. Na akalifanya neno (la ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.


بَلْ مَتَّعْتُ هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ﴿٢٩﴾
29. Bali Niliwastarehesha hawa (makafiri wa Makkah) na baba zao mpaka ikawajia haki na Rasuli anayebainisha.


وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ﴿٣٠﴾
30. Na ilipowajia haki, walisema: “Hii ni sihiri na hakika sisi ni wenye kuikanusha.”


وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ﴿٣١﴾
31. Na wakasema: “Kwa nini isiteremshwe hii Qur-aan juu ya mtu adhimu kutoka miji miwili?”


أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٣٢﴾
32. Je, wao wanaigawanya rahmah za Rabb wako? Sisi Tumegawanya baina yao maisha yao katika uhai wa dunia, na Tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengineo daraja za vyeo ili wawafanye baadhi yao kuwa watumishi wa wengineo. Na rahmah ya Rabb wako ni bora kuliko wanayoyajumuisha.


وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِالرَّحْمَـٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ﴿٣٣﴾
33. Na lau isingelikuwa watu kuwa jamii mmoja Tungejaalia wanaomkufuru Ar-Rahmaan wana nyumba zao zina dari za fedha na ngazi pia wanazozipandia. 


وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ﴿٣٤﴾
34. Na kwenye nyumba zao milango na makochi wanayoyaegemea.


وَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٣٥﴾
35. Na mapambo ya dhahabu. Lakini hayo yote si chochote isipokuwa ni starehe ya uhai wa dunia. Na Aakhirah iliyo kwa Rabb wako ni kwa wenye taqwa.


وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ﴿٣٦﴾
36. Na anayejifanya kipofu na ukumbusho wa Ar-Rahmaan Tunamwekea shaytwaan awe ndiye rafiki yake mwandani.


وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ﴿٣٧﴾
37. Na hakika wao wanawazuia njia na wanadhania kwamba wao wameongoka.


حَتَّىٰ إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَا لَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ﴿٣٨﴾
38. Mpaka atakapotujia (Siku ya Qiyaamah), atasema: “Laiti ingelikuwa baina yangu na baina yako umbali wa Mashariki na Magharibi, basi muovu mno rafiki mwandani wewe!.”


وَلَن يَنفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ﴿٣٩﴾
39. Haikufaeni chochote leo kwani mmedhulumu, na kwamba nyinyi mtashirikiana kwenye adhabu


أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَن كَانَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٤٠﴾
40. Je, kwani wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unaweza kusikilizisha viziwi au kumuongoa kipofu na yule aliyekuwa katika upotofu bayana?


فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ﴿٤١﴾
41. Na hata kama Tukikuondoa (kukufisha ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Sisi ni Wenye kuwalipizia.


أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ﴿٤٢﴾
42. Au Tukuonyesha yale Tuliyowatishia basi hakika Sisi ni Wenye uwezo juu yao.


فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٤٣﴾
43. Basi shikilia yale uliyofunuliwa Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wewe uko juu ya njia iliyonyooka.


وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ ۖ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ﴿٤٤﴾
44. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni ukumbusho kwako na kwa watu wako na mtakuja ulizwa.


وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ﴿٤٥﴾
45. Na waulize wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rusuli Wetu; je, Tulifanya badala ya Ar-Rahmaan  waabudiwa wengine ili waabudiwe?”


وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَقَالَ إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٤٦﴾
46. Na kwa yakini Tulimtuma Muwsaa kwa Aayaat (ishara, dalili) Zetu kwa Fir’awn na wakuu wake; akasema: “Hakika mimi ni Rasuli wa Rabb wa walimwengu.”


فَلَمَّا جَاءَهُم بِآيَاتِنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ﴿٤٧﴾
47. Basi alipowajia kwa Aayaat (ishara, hoja, dalili) Zetu tahamaki wao wanazicheka.


وَمَا نُرِيهِم مِّنْ آيَةٍ إِلَّا هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا ۖ وَأَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٤٨﴾
48. Na Hatukuwaonyesha Aayah (ishara) yoyote isipokuwa ni kubwa zaidi kuliko ya mwenziwe na Tukawachukua kwa adhabu ili wapate kurejea.


وَقَالُوا يَا أَيُّهَ السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ﴿٤٩﴾
49. Na wakasema: “Ee mchawi! Tuombee kwa Rabb wako kwa yale Aliyokuahidi kwako. Hakika sisi bila shaka tutaongoka.”


فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ﴿٥٠﴾
50. Lakini Tulipowaondoshea adhabu tahamaki wao wanavunja ahadi.


وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِهِ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَـٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِن تَحْتِي ۖأَفَلَا تُبْصِرُونَ﴿٥١﴾
51. Na Fir’awn akanadi kwa kaumu yake, akasema: “Enyi kaumu yangu! Je, kwani ufalme wa Misri si wangu! Na hii mito inapita chini yangu? Je, hamuoni?


أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ﴿٥٢﴾
52. “Au mimi si bora kuliko huyu ambaye yeye ni dhalili na wala hawezi kukaribia kujieleza wazi?


فَلَوْلَا أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ الْمَلَائِكَةُ مُقْتَرِنِينَ﴿٥٣﴾
53. “Basi kwanini asitupiwe vikuku vya dhahabu au wakaja pamoja naye Malaika wenye kuandamana naye?”


فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٤﴾
54. Basi aliwachezea akili watu wake nao wakamtii. Hakika wao walikuwa watu mafasiki.


فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٥٥﴾
55. Basi walipotukasirisha; Tuliwalipizia, Tukawagharikisha wote.


فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِّلْآخِرِينَ﴿٥٦﴾
56. Tukawafanya wenye kutangulia na mfano (wa funzo, zingatio) kwa wengineo.


وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ﴿٥٧﴾
57. Na mwana wa Maryam aliponukuliwa kama mfano, tahamaki watu wako wanaupigia kelele na kushangilia.


وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ ۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ﴿٥٨﴾
58. Na wakasema: “Je, waabudiwa wetu ni bora au yeye?” Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka kubisha. Bali wao ni watu makhasimu.


إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ﴿٥٩﴾
59. Yeye (Nabiy ‘Iysaa) si chochote isipokuwa ni mja Tuliyemneemesha, na Tukamfanya ni mfano kwa wana wa Israaiyl.


وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَائِكَةً فِي الْأَرْضِ يَخْلُفُونَ﴿٦٠﴾
60. Na lau Tungelitaka basi Tungewajaalia Malaika badala yenu wanarithishana katika ardhi.


وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦١﴾
61. Na hakika yeye (Nabiy ‘Iysaa) ni alama ya Saa basi usiitilie shaka na nifuateni. Hii ndio njia liyonyooka.


وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴿٦٢﴾
62. Na wala asikuzuieni shaytwaan, hakika yeye kwenu ni adui bayana.


وَلَمَّا جَاءَ عِيسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِالْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيهِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ﴿٦٣﴾
63. Na alipokuja ‘Iysaa kwa hoja bayana, akasema: “Nimekujieni kwa hikmah, na ili nikubainishieni baadhi ya yale mnayokhitilafiana nayo, basi mcheni Allaah na nitiini.


إِنَّ اللَّـهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦٤﴾
64. “Hakika Allaah Ndiye Rabb wangu na Rabb wenu, basi mwabuduni Yeye Pekee, hii ndio njia liyonyooka.”


فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ﴿٦٥﴾
65. Basi wakakhitilafiana makundi kwa makundi baina yao. Basi ole kwa wale waliodhulumu kutokana na adhabu ya Siku iumizayo.


هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿٦٦﴾
66. Je, wanangojea isipokuwa Saa tu iwafikie ghafla nao hawatambui.


الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ﴿٦٧﴾
67. Rafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye taqwa.


يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ﴿٦٨﴾
68. “Enyi waja Wangu! Hakuna khofu juu yenu leo, na wala nyinyi hamtohuzunika.”


الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ﴿٦٩﴾
69. “Ambao wameamini Aayaat Zetu na wakawa Waislamu.”


ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ﴿٧٠﴾
70. Ingieni Jannah nyinyi na wake zenu mfurahishwe.


يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٧١﴾
71. Watapitishiwa sahani za dhahabu na bilauri, na humo mna yale yanayotamani nafsi na ya kuburidisha macho, nanyi humo ni wenye kudumu.


وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٧٢﴾
72. Na hiyo ni Jannah ambayo mmerithishwa kwa yale mliyokuwa mkitenda.


لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٧٣﴾
73. Mtapata humo matunda mengi mtakayokuwa mnakula.


إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ﴿٧٤﴾
74. Hakika wahalifu wamo kwenye adhabu ya Jahannam ni wenye kudumu.


لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ﴿٧٥﴾
75. Hawatopumzishwa nayo nao humo watakata tamaa.


وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ﴿٧٦﴾
76. Na wala Hatukuwadhulumu lakini walikuwa wao wenyewe ndio madhalimu.


وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ﴿٧٧﴾
77. Na wataita: “Ee Maalik! (Mlinzi wa moto) Na Atumalize tufe Rabb wako.” Atasema: “Hakika nyinyi ni wenye kubakia kuishi humo.”


لَقَدْ جِئْنَاكُم بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ﴿٧٨﴾
78. “Kwa yakini Tulikujieni kwa haki, lakini wengi wenu ni mlikuwa wenye kuichukia haki.”


أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ﴿٧٩﴾
79. Au walipanga njama?  Basi hakika Sisi ni Wenye kulipiza njama.


أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ﴿٨٠﴾
80. Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! (Tunasikia!) Na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika.


قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾
81. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Kama ingelikuwa Ar-Rahmaan Ana mwana (kama mnavyodai), basi mimi ningekuwa wa mwanzo kumwabudu.”


سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ﴿٨٢﴾
82. Subhaana, Utakasifu ni wa Rabb wa mbingu na ardhi, Rabb wa ‘Arsh kutokana na yale wanayoyavumisha. 


فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ﴿٨٣﴾
83. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na wacheze mpaka wakutane na Siku yao waliyoahidiwa.


وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٨٤﴾
84. Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. Naye Ndiye Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.


وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٨٥﴾
85. Na Amebarikika Ambaye ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake na vilivyo baina yake, na Kwake Pekee upo ujuzi wa Saa na Kwake mtarejeshwa.


وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٨٦﴾
86. Na wala wale wanaowaomba badala Yake hawana uwezo wa kumiliki uombezi isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki nao wanajua.


وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٨٧﴾
87. Na ukiwauliza: Ni nani kawaumba? Bila shaka watasema: “Allaah.”  Basi vipi wanaghilibiwa?


وَقِيلِهِ يَا رَبِّ إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿٨٨﴾
88. Na (Allaah Anajua) kauli yake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ee Rabb
wangu!  Hakika hawa watu hawaamini.”


فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾
89. Basi wapuuzilie mbali (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na sema: “Salaamun!” Na karibuni hivi watakuja jua.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.