-->
logo

041 - Fusw-Swilat

 فُصِّلَت
Fusw-Swilat: 41  

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


حم﴿١﴾
1. Haa Miym.


تَنزِيلٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho kutoka kwa Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.


كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿٣﴾
3. Kitabu zimefasiliwa waziwazi Aayaat zake, ni Qur-aan ya Kiarabu kwa watu wanaojua.


بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ﴿٤﴾
4. Kinachobashiria mazuri na kinachoonya; lakini wamekengeuka wengi wao, basi wao hawasikii.


وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِن بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ﴿٥﴾
5. Na wakasema: “Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa yale unayotuitia, na masikioni mwetu mna uziwi na baina yetu na baina yako kuna kizuizi, basi tenda nasi tunatenda.”


قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْمُشْرِكِينَ﴿٦﴾
6. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; hufunuliwa Wahy kwamba: Muabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja, basi thibitikeni imara Kwake, na mwombeni maghfirah. Na ole kwa washirikina.

الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿٧﴾
7. Ambao hawajitakasi kutokana na shirki na wao kwa Aakhirah wenye kuikanusha.


إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ﴿٨﴾
8. Hakika wale walioamini na wakatenda mema watapata ujira usiokatika.


قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٩﴾
9. Sema: “Je, hivi nyinyi mnamkufuru Yule Aliyeumba ardhi kwa siku mbili, na mnamfanyia waliolingana Naye? Huyo Ndiye Rabb wa walimwengu.”


وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ﴿١٠﴾
10. Na Akaweka humo milima juu yake, na Akabariki humo, na Akakadiria humo rizki yake katika siku nne zilizo sawasawa, (ni taarifa) kwa wanaouliza.


ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَاطَائِعِينَ﴿١١﴾
11. Kisha Istawaa[1] kuzielekea mbingu nazo ni moshi; Akaziambia hizo na ardhi: “Njooni kwa khiari au bila kutaka.”  Zikasema: “Tumekuja hali ya kuwa wenye utiifu.”


فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا ۚ وَزَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَحِفْظًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ﴿١٢﴾
12. Akamaliza kuziumba mbingu saba katika siku mbili, na Akatia ilhamu katika kila mbingu jambo lake; na Tukaipamba mbingu ya dunia kwa mataa na hifadhi. Hayo ni takdiri ya Mwenye nguvu zote Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.


فَإِنْ أَعْرَضُوا فَقُلْ أَنذَرْتُكُمْ صَاعِقَةً مِّثْلَ صَاعِقَةِ عَادٍ وَثَمُودَ﴿١٣﴾
13. Wakikengeuka, basi sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nakuhadharisheni radi na umeme angamizi mfano wa radi na umeme angamizi wa kina ‘Aad na Thamuwd.”


إِذْ جَاءَتْهُمُ الرُّسُلُ مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۖ قَالُوا لَوْ شَاءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَائِكَةً فَإِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿١٤﴾
14. Walipowajia Rusuli mbele yao na nyuma yao kwamba: “Msimuabudu isipokuwa Allaah.” Wakasema: “Angelitaka Rabb wetu, bila shaka Angeliteremsha Malaika; na hakika sisi ni wenye kuyakanusha yale mliyotumwa nayo”.


فَأَمَّا عَادٌ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَقَالُوا مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً ۖ أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ﴿١٥﴾
15. Ama kina ‘Aad, walitakabari katika ardhi bila ya haki, na wakasema: “Nani mwenye nguvu kuliko sisi?” Je, hawakuona kwamba Allaah Ambaye Amewaumba Ndiye Mwenye nguvu zaidi kuliko wao? Na walikuwa wanazikanusha Aayaat (ishara) Zetu.


فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖوَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَخْزَىٰ ۖ وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ﴿١٦﴾
16. Basi Tukawapelekea upepo wa dhoruba na mngurumo katika siku za mikosi ili Tuwaonjeshe adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia; na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni ya hizaya zaidi, nao hawatonusuriwa.


وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾
17. Na ama kina Thamuwd, Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko Uongofu basi ikawachukuwa radi na umeme angamizi wa adhabu idhalilishayo kwa yale waliyokuwa wakichuma.


وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿١٨﴾
18. Na Tukawaokoa wale walioamini na walikuwa wenye taqwa.


وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاءُ اللَّـهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ﴿١٩﴾
19. Na Siku watakayokusanywa maadui wa Allaah kwenye moto, nao watakusanywa kupangwa safusafu.


حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٠﴾
20. Mpaka watakapoufikia yatashuhudia dhidi yao, masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.


وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوا أَنطَقَنَا اللَّـهُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٢١﴾
21. Na wataziambia ngozi zao: “Mbona mnashuhudia dhidi yetu?” Zitasema: “Ametutamkisha Allaah Ambaye Ametamkisha kila kitu, Naye Ndiye Aliyekuumbeni mara ya kwanza na Kwake mtarejeshwa.


وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٢٢﴾
22. “Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, na wala macho yenu, na wala ngozi zenu; lakini mlidhania kwamba Allaah Hajui mengi katika yale mnayoyatenda.


وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ﴿٢٣﴾
23. “Na hivyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Rabb wenu, imekuangamizeni, mmekuwa miongoni mwa waliokhasirika.”


فَإِن يَصْبِرُوا فَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ ۖ وَإِن يَسْتَعْتِبُوا فَمَا هُم مِّنَ الْمُعْتَبِينَ﴿٢٤﴾
24. Basi wakivuta subira, lakini moto ndio makazi yao; na wakitafuta kuomba radhi, basi wao hawatokuwa miongoni mwa wenye kuruhusiwa kuridhisha.


وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَاءَ فَزَيَّنُوا لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ﴿٢٥﴾
25. Na Tuliwawekea marafiki wandani wakawapambia yale yaliyo mbele yao na ya nyuma yao na ikahakiki dhidi yao kauli kama iliyohakikii katika umati nyingi zilizokwishapita kabla yao miongoni mwa majini na wanadamu; kwamba wao wamekuwa wenye kukhasirika.


وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَـٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ﴿٢٦﴾
26. Na wale waliokufuru wakasema: “Msiisikilize hii Qur-aan na ifanyieni rabsha huenda mkashinda.”


فَلَنُذِيقَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٧﴾
27. Bila shaka Tutawaonjesha wale waliokufuru adhabu kali, na bila shaka Tutawalipa uovu zaidi wa yale waliokuwa wakiyatenda.


ذَٰلِكَ جَزَاءُ أَعْدَاءِ اللَّـهِ النَّارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا دَارُ الْخُلْدِ ۖ جَزَاءً بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ﴿٢٨﴾
28. Hiyo ndio jazaa ya maadui wa Allaah, moto! Watapata humo makazi yenye kudumu; ndio jazaa kwa sababu walikuwa wakizikanusha Aayaat, (dalili na ishara) Zetu.


وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا رَبَّنَا أَرِنَا اللَّذَيْنِ أَضَلَّانَا مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ نَجْعَلْهُمَا تَحْتَ أَقْدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَالْأَسْفَلِينَ﴿٢٩﴾
29. Na watasema wale waliokufuru: “Rabb wetu! Tuonyeshe wale waliotupotoa miongoni mwa majini na wanadamu tuwaweke chini ya miguu yetu ili wawe miongoni mwa wa chini kabisa.”


إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ﴿٣٠﴾
30. Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia: (kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”


نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ﴿٣١﴾
31. “Sisi ni rafiki zenu walinzi katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba.


نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ﴿٣٢﴾
32. “Ni mapokezi ya takrima kutoka kwa Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.”


وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٣٣﴾
33. Na nani mwenye kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania kwa Allaah na akatenda mema na akasema: “Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu.”


وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّحَمِيمٌ﴿٣٤﴾
34. Na wala haulingani sawa wema na uovu. Lipiza (uovu) kwa ambalo ni zuri zaidi; tahamaki yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui, atakuwa kama ni rafiki mwandani.


وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ﴿٣٥﴾
35. Na hapewi hayo isipokuwa wale waliovuta subira, na hapewi hayo isipokuwa mwenye fungu adhimu.


وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٦﴾
36. Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.


وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِيخَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿٣٧﴾
37. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake, ni usiku na mchana, na jua na mwezi.  Msisujudie jua wala mwezi; bali msujudieni Allaah Ambaye Aliyeviumba ikiwa Yeye Pekee mnawambudu.


فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ ۩﴿٣٨﴾
38. Lakini wakitakabari, basi wale (Malaika) walio kwa Rabb wako wanamsabbih usiku na mchana, nao wala hawachoki.


وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۚ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٩﴾
39. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zakeni kwamba utaona ardhi imetulia kame, kisha Tunapoiteremshia maji inataharaki na huotesha. Hakika Yule Aliyeihuisha, bila shaka ni Mwenye kuhuisha wafu, hakika Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.


إِنَّ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي آيَاتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَا ۗ أَفَمَن يُلْقَىٰ فِي النَّارِ خَيْرٌ أَم مَّن يَأْتِي آمِنًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ ۖ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٤٠﴾
40. Hakika wale wanaozipotosha Aayaat Zetu hawawezi kujificha kwetu. Je, basi yule atakayetupwa katika moto ni bora au yule atakayekuja akiwa katika amani Siku ya Qiyaamah? Tendeni mpendavyo; hakika Yeye ni Mwenye kuona yote myatendayo.


إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ﴿٤١﴾
41. Hakika wale waliokanusha Ukumbusho ulipowajia (wataangamia). Na hakika hicho ni Kitabu chenye utukufu na udhibiti.


لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾
42. Hakitokifikia ubatili mbele yake, na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.


مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ﴿٤٣﴾
43. Huambiwi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa yale yale waliyokwisha ambiwa Rusuli kabla yako. Hakika Rabb wako ni Mwenye maghfirah na Mwenye adhabu iumizayo.


وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ ۖ أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ ۗ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ أُولَـٰئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ﴿٤٤﴾
44. Na lau Tungeliifanya Qur-aan lugha isiyokuwa ya Kiarabu bila shaka wangelisema: “Mbona hazikufasiliwa waziwazi Aayaat zake?  Ah! Ya lugha ya kigeni na hali (Nabiy) ni Mwarabu!?” Sema: “Hiyo ni kwa walioamini ni mwongozo na shifaa. Na wale wasioamini, wana uziwi masikioni mwao nayo ni upofu kwao. Hao wanaitwa kutoka mahali mbali.


وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۗ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ﴿٤٥﴾
45. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu kisha kikahitilafiwa. Na lau si neno lilotangulia kutoka kwa Rabb wako, bila shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao bila shaka wamo katika shaka nayo (Qur-aan) yenye kuwatia wasiwasi.


مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۗ وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ﴿٤٦﴾
46. Yeyote yule atakayetenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na yeyote yule atakayefanya uovu, basi ni dhidi yake; na Rabb wako si Mwenye kudhulumu kamwe waja.  



إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ السَّاعَةِ ۚ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَاتٍ مِّنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ﴿٤٧﴾
47. Kwake Pekee unarudishwa ujuzi wa Saa (Qiyaamah). Na hayatoki matunda yoyote kutoka mafumbani mwake, na wala habebi mimba mwanamke yeyote na wala hazai isipokuwa kwa ujuzi Wake. Na Siku Atakayowaita (Aseme): “Wako wapi (hao mnaodai) washirika Wangu?”  Watasema: “Tunakiri Kwako hapana miongoni mwetu anayeshudia.”


وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَدْعُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَظَنُّوا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ﴿٤٨﴾
48. Na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyaomba kabla na watayakinisha hawana mahali pa kukimbilia.


لَّا يَسْأَمُ الْإِنسَانُ مِن دُعَاءِ الْخَيْرِ وَإِن مَّسَّهُ الشَّرُّ فَيَئُوسٌ قَنُوطٌ﴿٤٩﴾
49. Insani hachoki kuomba du’aa za kheri. Na inapomgusa shari, basi huwa mwenye kukosa tumainio lolote, mwenye kukata tamaa kabisa.


وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِي وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّي إِنَّ لِي عِندَهُ لَلْحُسْنَىٰ ۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِمَا عَمِلُوا وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍغَلِيظٍ﴿٥٠﴾
50. Na Tunapomuonjesha rahmah kutoka Kwetu baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: “Haya nayastahiki mimi na sidhani kama Saa (Qiyaamah) itasimama. Na nitakaporejeshwa kwa Rabb wangu hakika nitapata mazuri Kwake.” Basi bila shaka Tutawabainishia wale waliokufuru yale waliyoyatenda, na bila shaka Tutawaonjesha adhabu nzito.


وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ فَذُو دُعَاءٍ عَرِيضٍ﴿٥١﴾
51. Na Tunapomneemesha insani hukengeuka na kujitenga upande. Na inapomgusa shari, basi mara huwa mwenye du’aa refu refu.



قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ثُمَّ كَفَرْتُم بِهِ مَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ هُوَ فِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ﴿٥٢﴾
52. Sema: “Je, mnaonaje ikiwa (Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, kisha mkaikufuru, ni nani aliyepotoka zaidi kuliko yule aliye katika upinzani wa mbali?”


سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّشَيْءٍ شَهِيدٌ﴿٥٣﴾
53. Tutawaonyesha Aayaat (ishara, dalili) Zetu katika peo za mbali na katika nafsi zao, mpaka iwabainike kwamba hiyo ni haki! Je, haitoshelezi Rabb wako kuwa Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu?


أَلَا إِنَّهُمْ فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَاءِ رَبِّهِمْ ۗ أَلَا إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطٌ﴿٥٤﴾
54. Tanabahi! Hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Rabb wao. Tanabahi! Hakika Yeye kwa kila kitu ni Mwenye kukizunguka kwa ujuzi Wake.



 
[1] Istawaa: Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.