-->
logo

040 - Ghaafir

غَافِر
Ghaafir: 40

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم


حم﴿١﴾
1. Haa Miym.


تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu Kutoka kwa Allaah Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.


غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾
3. Mwenye kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa kuakibu, Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia.


مَا يُجَادِلُ فِي آيَاتِ اللَّـهِ إِلَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَا يَغْرُرْكَ تَقَلُّبُهُمْ فِي الْبِلَادِ﴿٤﴾
4. Habishani katika Aayaat za Allaah isipokuwa wale waliokufuru, basi isikughururi kutamba kwao huku na kule katika nchi.


كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَالْأَحْزَابُ مِن بَعْدِهِمْ ۖ وَهَمَّتْ كُلُّ أُمَّةٍ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ ۖ وَجَادَلُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ﴿٥﴾
5. Walikadhibisha kabla yao watu wa Nuwh, na makundi baada yao, na kila ummah ulitilia hima kufanya njama juu ya Rasuli wake ili wamkamate, na wakabishana kwa ubatilifu ili waitengue haki, Nikawakamata, basi vipi ilikuwa ikabu Yangu!


وَكَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ أَصْحَابُ النَّارِ﴿٦﴾
6. Na hivyo ndivyo limehakiki neno la Rabb wako juu ya wale waliokufuru kwamba wao ni watu wa motoni.


الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٧﴾
7.  (Malaika) Ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih kwa Himidi za Rabb wao, na wanamwamini; na wanawaombea maghfirah wale walioamini:  “Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa rahmah na ujuzi, basi waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno.”


رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٨﴾
8. “Rabb wetu! Waingize Jannaat za kudumu milele ambazo Umewaahidi, pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na dhuria wao.  Hakika Wewe Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ ۚ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٩﴾
9. “Na wakinge maovu, kwani Unayemkinga na maovu Siku hiyo, basi kwa yakini Umemrehemu. Na huko ndiko kufuzu adhimu.


إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنَادَوْنَ لَمَقْتُ اللَّـهِ أَكْبَرُ مِن مَّقْتِكُمْ أَنفُسَكُمْ إِذْ تُدْعَوْنَ إِلَى الْإِيمَانِ فَتَكْفُرُونَ﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliokufuru watanadiwa: “Bila shaka kuchukia kwa Allaah ni kukubwa zaidi kuliko kujichukia nafsi zenu (leo motoni) pale mlipokuwa mnaitwa kwenye iymaan mkakufuru.”


قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ فَاعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ﴿١١﴾
11. Watasema: “Rabb wetu! Umetufisha mara mbili na Umetuhuisha mara mbili basi tumekiri madhambi yetu; basi je, kuna njia ya kutoka?”


ذَٰلِكُم بِأَنَّهُ إِذَا دُعِيَ اللَّـهُ وَحْدَهُ كَفَرْتُمْ ۖ وَإِن يُشْرَكْ بِهِ تُؤْمِنُوا ۚ فَالْحُكْمُ لِلَّـهِ الْعَلِيِّ الْكَبِيرِ﴿١٢﴾
12. (Wataambiwa:) “Hivyo kwenu ni kwa sababu Alipoombwa Allaah Pekee, mlikufuru, na aliposhirikishwa, mliamini. Basi hukumu ni ya Allaah Pekee Mwenye ‘Ulwa, Ametukuka, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa.”


هُوَ الَّذِي يُرِيكُمْ آيَاتِهِ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ رِزْقًا ۚ وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ﴿١٣﴾
13. Yeye Ambaye Anakuonyesheni Aayaat (ishara, dalili) Zake na Anakuteremshieni kutoka mbinguni riziki, na hakumbuki (na kuwaidhika) isipokuwa mwenye kurudia rudia kutubu.


فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿١٤﴾
14. Basi mwombeni Allaah wenye kumtakasia Dini japokuwa wanachukia makafiri.


رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Mwenye uluwa juu ya vyeo na daraja. Mwenye ‘Arsh, Anapelekea Ar-Ruwh (Wahy) kwa amri Yake kwa Amtakaye miongoni mwa waja Wake, ili aonye Siku ya kukutana.


يَوْمَ هُم بَارِزُونَ ۖ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ ۚ لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ۖ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿١٦﴾
16. Siku watakayotokeza wao, hakitofichika kitu chochote chao kwa Allaah. “Ufalme ni wa nani leo?” (Allaah Mwenyewe Atajijibu): “Ni wa Allaah Pekee Mmoja, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Asiyepingika.”


الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۚ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴿١٧﴾
17. Leo kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyachuma, hakuna dhulma leo!  Hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.


وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْآزِفَةِ إِذِ الْقُلُوبُ لَدَى الْحَنَاجِرِ كَاظِمِينَ ۚ مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ﴿١٨﴾
18. Na waonye Siku inayokurubia sana pale nyoyo zitakapofikia kooni wamejaa huzuni na majuto. Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, na wala mwombezi anayetiiwa.


يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ﴿١٩﴾
19. (Allaah) Anajua khiyana za macho na yale yanayoficha vifua.


وَاللَّـهُ يَقْضِي بِالْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَقْضُونَ بِشَيْءٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿٢٠﴾
20. Na Allaah Anahukumu kwa haki. Na wale wanaowaomba badala Yake hawawezi kuhukumu kwa chochote. Hakika Allaah Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.


أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ كَانُوا مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِن وَاقٍ﴿٢١﴾
21. Je, hawakutembea katika ardhi, wakatazama vipi ilikuwa hatima ya wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao, na athari katika ardhi lakini Allaah Aliwakamata kwa sababu ya madhambi zao; na wala hawakuwa na wa kuwalinda dhidi ya Allaah.


ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَكَفَرُوا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّهُ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٢٢﴾
22. Hivyo ni kwa sababu wao ilikuwa wakiwafikia Rusuli wao kwa hoja bayana, wakakufuru, basi Allaah Aliwakamata, hakika Yeye ni Mwenye nguvu zote, Mkali wa kuakibu.


وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿٢٣﴾
23. Na kwa yakini Tulimtuma Muwsaa kwa Aayaat (ishara, dalili) Zetu na mamlaka bayana.


إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَقَارُونَ فَقَالُوا سَاحِرٌ كَذَّابٌ﴿٢٤﴾
24. Kwa Fir’awn na Haamaan na Qaaruwn, wakasema: “Mchawi muongo.”


فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْحَقِّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا اقْتُلُوا أَبْنَاءَ الَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ وَاسْتَحْيُوا نِسَاءَهُمْ ۚ وَمَا كَيْدُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ﴿٢٥﴾
25. Na alipowajia kwa haki kutoka Kwetu; walisema: “Wauweni watoto wa kiume wa wale walioamini pamoja naye, na waacheni hai wanawake wao. Na njama za makafiri haziwi isipokuwa katika upotofu.


وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِي أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُ ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِي الْأَرْضِ الْفَسَادَ﴿٢٦﴾
26. Na Fir’awn akasema: “Niacheni nimuue Muwsaa, naye amwite Rabb wake! Hakika mimi nakhofu asije kukubadilishieni dini yenu, au adhihirishe ufisadi katika ardhi.”


وَقَالَ مُوسَىٰ إِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لَّا يُؤْمِنُ بِيَوْمِ الْحِسَابِ﴿٢٧﴾
27. Na Muwsaa akasema: “Hakika mimi najikinga kwa Rabb wangu na Rabb wenu, kutokana na kila mwenye kutakabari asiyeamini Siku ya Hesabu.”


وَقَالَ رَجُلٌ مُّؤْمِنٌ مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَانَهُ أَتَقْتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ اللَّـهُ وَقَدْ جَاءَكُم بِالْبَيِّنَاتِ مِن رَّبِّكُمْ ۖ وَإِن يَكُ كَاذِبًا فَعَلَيْهِ كَذِبُهُ ۖ وَإِن يَكُ صَادِقًا يُصِبْكُم بَعْضُ الَّذِي يَعِدُكُمْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ كَذَّابٌ﴿٢٨﴾
28. Na akasema mtu mmoja Muumini miongoni mwa familia ya Fir’awn, aliyeficha iymaan yake: “Je, mnamuua mtu kwa kuwa tu anasema: Rabb wangu ni Allaah? Na hali amekujieni na hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu? Na akiwa ni muongo, basi uongo wake ni dhidi yake mwenyewe, na akiwa ni mkweli yatakusibuni baadhi ya yale anayokuahidini, hakika Allaah Hamwongoi yule anayepindukia mipaka, muongo mkubwa.


يَا قَوْمِ لَكُمُ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ظَاهِرِينَ فِي الْأَرْضِ فَمَن يَنصُرُنَا مِن بَأْسِ اللَّـهِ إِن جَاءَنَا ۚ قَالَ فِرْعَوْنُ مَا أُرِيكُمْ إِلَّا مَا أَرَىٰ وَمَا أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ الرَّشَادِ﴿٢٩﴾
29. “Enyi watu wangu!  Leo mna ufalme, mmeshinda katika ardhi. Basi ni nani atakayetunusuru kutokana na adhabu ya Allaah ikitujia?” Fir’wan akasema: “Sikuonyesheni isipokuwa yale ninayoyaona (ni sahihi), na sikuongozeni isipokuwa njia ya uongofu.”


وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُم مِّثْلَ يَوْمِ الْأَحْزَابِ﴿٣٠﴾
30. Na yule aliyeamini akasema: “Enyi watu wangu! Hakika mimi nakukhofieni mfano wa siku za makundi.


مِثْلَ دَأْبِ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ ۚ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعِبَادِ﴿٣١﴾
31. “Mfano wa ada za kaumu ya Nuwh, na ‘Aad, na Thamuwd na wale wa baada yao, na Allaah Hakusudii dhulma kwa waja.


وَيَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ يَوْمَ التَّنَادِ﴿٣٢﴾
32. “Enyi kaumu yangu! Hakika mimi nakukhofieni Siku ya kuitana.


يَوْمَ تُوَلُّونَ مُدْبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ ۗ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ﴿٣٣﴾
33. “Siku mtakayogeuka nyuma mkimbie wala hamtokuwa na wa kukulindeni dhidi ya Allaah. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana yeyote wa kumwongoa.”


وَلَقَدْ جَاءَكُمْ يُوسُفُ مِن قَبْلُ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا زِلْتُمْ فِي شَكٍّ مِّمَّا جَاءَكُم بِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَن يَبْعَثَ اللَّـهُ مِن بَعْدِهِ رَسُولًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُّرْتَابٌ﴿٣٤﴾
34. Na kwa yakini alikujieni Yuwsuf kabla kwa hoja bayana, lakini mliendelea katika shaka kwa yale aliyokuleteeni, mpaka alipokufa mkasema: “Allaah Hatotuma Rasuli baada yake.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa yule apindukiaye mipaka mwenye kutia shaka.


الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ ۖ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ وَعِندَ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَيَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ﴿٣٥﴾
35. Wale wanaobishana kuhusu Aayaat za Allaah bila ya hoja yoyote kuwafikia, ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah na mbele ya wale walioamini. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya kila moyo wa mwenye kutakabari, jabari.


وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ﴿٣٦﴾
36. Na Fir’awn akasema: “Ee Haamaan nijengee mnara ili nifikie njia.


أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا ۚ وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرْعَوْنَ سُوءُ عَمَلِهِوَصُدَّ عَنِ السَّبِيلِ ۚ وَمَا كَيْدُ فِرْعَوْنَ إِلَّا فِي تَبَابٍ﴿٣٧﴾
37. “Njia za mbinguni ili nimchungulie Ilaah wa Muwsaa, kwani hakika mimi namdhania ni muongo.” Na hivyo ndivyo alivyopambiwa Fir’awn uovu wa amali yake, na akazuiliwa njia (ya haki). Na njama za Fir’awn hazikuwa isipokuwa katika kuteketea.


وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُونِ أَهْدِكُمْ سَبِيلَ الرَّشَادِ﴿٣٨﴾
38. Na yule aliyeamini akasema: “Enyi kaumu yangu! Nifuateni nikuongozeni njia ya uongofu.


يَا قَوْمِ إِنَّمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا مَتَاعٌ وَإِنَّ الْآخِرَةَ هِيَ دَارُ الْقَرَارِ﴿٣٩﴾
39. “Enyi kaumu yangu! Hakika huu uhai wa dunia ni starehe ya kupita tu, na hakika Aakhirah ndiyo nyumba ya kustakiri milele.


مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ﴿٤٠﴾
40. “Yeyote atakayetenda uovu, basi hatolipwa isipokuwa mfano wake; na yeyote atakayetenda mema kati ya mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Jannah wataruzukiwa humo bila ya hesabu.


وَيَا قَوْمِ مَا لِي أَدْعُوكُمْ إِلَى النَّجَاةِ وَتَدْعُونَنِي إِلَى النَّارِ﴿٤١﴾
41. “Enyi kaumu yangu! Iweje mimi nakuiteni kwenye uokovu, nanyi mnaniita kwenye moto?


تَدْعُونَنِي لِأَكْفُرَ بِاللَّـهِ وَأُشْرِكَ بِهِ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ وَأَنَا أَدْعُوكُمْ إِلَى الْعَزِيزِ الْغَفَّارِ﴿٤٢﴾
42. “Mnaniita ili nimkufuru Allaah na nimshirikishe na yale nisiyokuwa nayo kwayo elimu, na hali mimi nakuiteni kwa Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa kughufuria?


لَا جَرَمَ أَنَّمَا تَدْعُونَنِي إِلَيْهِ لَيْسَ لَهُ دَعْوَةٌ فِي الدُّنْيَا وَلَا فِي الْآخِرَةِ وَأَنَّ مَرَدَّنَا إِلَى اللَّـهِ وَأَنَّ الْمُسْرِفِينَ هُمْ أَصْحَابُ النَّارِ﴿٤٣﴾
43. “Hapana shaka kwamba ambaye mnayeniitia kwake hastahiki wito duniani na wala Aakhirah, na kwamba marudio yetu ni kwa Allaah, na kwamba wapindukao mipaka wao ndio watu wa motoni.


فَسَتَذْكُرُونَ مَا أَقُولُ لَكُمْ ۚ وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ﴿٤٤﴾
44. “Basi mtakumbuka karibuni yale ninayokuambieni; na naaminisha mambo yangu kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye kuona waja Wake.”


فَوَقَاهُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا ۖ وَحَاقَ بِآلِ فِرْعَوْنَ سُوءُ الْعَذَابِ﴿٤٥﴾
45. Basi Allaah Akamlinda na maovu ya yale waliyoyapangia njama, na watu wa Fir’awn ikawazunguka adhabu mbaya kabisa.


النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ﴿٤٦﴾
46. Wanadhihirishiwa moto asubuhi na jioni, na Siku itakayosimama Saa (itasemwa): “Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali kabisa.”


وَإِذْ يَتَحَاجُّونَ فِي النَّارِ فَيَقُولُ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا نَصِيبًا مِّنَ النَّارِ﴿٤٧﴾
47. Na watakapobishana motoni, watasema walio wanyonge kuwaambia wale waliotakabari: “Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi je, nyinyi mnaweza kutuondelea sehemu yoyote ya moto?”


قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُلٌّ فِيهَا إِنَّ اللَّـهَ قَدْ حَكَمَ بَيْنَ الْعِبَادِ﴿٤٨﴾
48. Watasema wale waliotakabari: “Hakika sisi sote tumo humo, hakika Allaah Amekwishahukumu baina ya waja.”


وَقَالَ الَّذِينَ فِي النَّارِ لِخَزَنَةِ جَهَنَّمَ ادْعُوا رَبَّكُمْ يُخَفِّفْ عَنَّا يَوْمًا مِّنَ الْعَذَابِ﴿٤٩﴾
49. Na watasema wale waliokuweko motoni kuwaambia Walinzi wa Jahannam: “Mwombeni Rabb wenu Atukhafifishie siku moja ya adhabu.”


قَالُوا أَوَلَمْ تَكُ تَأْتِيكُمْ رُسُلُكُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۚ قَالُوا فَادْعُوا ۗ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِيضَلَالٍ﴿٥٠﴾
50. Watasema: “Je, kwani hawakuwa wakikufikieni Rusuli wenu kwa hoja bayana?” Waseme: “Naam!” Watasema: “Basi ombeni. Na hazikuwa du’aa za makafiri isipokuwa katika upotofu.”


إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ﴿٥١﴾
51. Hakika Sisi Tutawanusuru Rusuli Wetu, na wale walioamini katika uhai wa dunia na Siku watakayosimama mashahidi.


يَوْمَ لَا يَنفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ ۖ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ﴿٥٢﴾
52. Siku hazitowafaa madhalimu udhuru wao; na watapata laana na watapata makazi mabaya.


وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْهُدَىٰ وَأَوْرَثْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ﴿٥٣﴾
53. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa mwongozo na Tukawarithisha wana wa Israaiyl Kitabu.


هُدًى وَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ﴿٥٤﴾
54. Ni mwongozo na ukumbusho kwa wenye akili.


فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ﴿٥٥﴾
55. Basi vuta subira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika ahadi ya Allaah ni haki, na omba maghfirah kwa dhambi zako, na sabbih kwa Himidi za Rabb wako jioni na asubuhi.


إِنَّ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ ۙ إِن فِي صُدُورِهِمْ إِلَّا كِبْرٌ مَّا هُم بِبَالِغِيهِ ۚفَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿٥٦﴾
56. Hakika wale wanaobishana kuhusu Aayaat za Allaah bila ya dalili yoyote kuwafikia, hamna vifuani mwao isipokuwa kiburi, lakini hawatoufikia (Utume). Basi jikinge kwa Allaah, hakika Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.


لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٥٧﴾
57.  Bila shaka uumbaji wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kuliko uumbaji wa watu, lakini watu wengi hawajui.


وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَلَا الْمُسِيءُ ۚ قَلِيلًا مَّا تَتَذَكَّرُونَ﴿٥٨﴾
58. Na halingani sawa kipofu na mwenye kuona, na (wala) wale walioamini na wakatenda mema na muovu. Kidogo sana mnayoyakumbuka.


إِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٥٩﴾
59. Hakika Saa bila shaka itafika tu, haina shaka ndani yake, lakini watu wengi hawaamini.


وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَدَاخِرِينَ﴿٦٠﴾
60. Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na kuniabuduwataingika Jahanam wadhalilike. 


اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ﴿٦١﴾
61. Allaah Ambaye Amekufanyieni usiku ili mpate utulivu humo, na mchana wenye kuangaza. Hakika Allaah ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini watu wengi hawashukuru.


ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾
62. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, Muumba wa kila kitu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi vipi mnaghilibiwa?


كَذَٰلِكَ يُؤْفَكُ الَّذِينَ كَانُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ﴿٦٣﴾
63. Hivyo ndivyo wanalivyoghilibiwa wale waliokuwa wakizikanusha Aayaat (na ishara) za Allaah.


اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٦٤﴾
64. Allaah Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa mahali pa makazi, na mbingu kama ni paa na Akakutieni sura, Akazifanya nzuri zaidi sura zenu, na Akakuruzukuni katika vizuri. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu. Basi Tabaaraka-Allaah, Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.


هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٥﴾
65. Yeye Ndiye Aliye hai daima hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi muombeni Yeye wenye kumtakasia Dini. AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu.


قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَمَّا جَاءَنِيَ الْبَيِّنَاتُ مِن رَّبِّي وَأُمِرْتُ أَنْ أُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٦﴾
66. Sema: “Hakika mimi nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaomba badala ya Allaah ziliponijia hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, na nimeamrishwa nijisalimishe kwa Rabb wa walimwengu.”


هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا شُيُوخًا ۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبْلُ ۖ وَلِتَبْلُغُوا أَجَلًا مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٦٧﴾
67. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na tone la manii, kisha kutokana na pande la damu linaloning’inia, kisha Anakutoeni hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie umri wenu wa kupevuka, kisha ili muwe wazee. Na miongoni mwenu ambaye hufishwa kabla, na ili mfikie muda maalumu uliokadiriwa na ili mpate kutia akilini.


هُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴿٦٨﴾
68. Yeye ni Yule Anayehuisha na Anayefisha. Basi Anapolikidhia jambo lolote basi huliambia: “Kun” (Kuwa) nalo linakuwa. 


أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ أَنَّىٰ يُصْرَفُونَ﴿٦٩﴾
69. Je, hukuona wale wanaobishana kuhusu Aayaat (na ishara) za Allaah wanageuziwa wapi?


الَّذِينَ كَذَّبُوا بِالْكِتَابِ وَبِمَا أَرْسَلْنَا بِهِ رُسُلَنَا ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٧٠﴾
70. Wale waliokadhibisha Kitabu na yale Tuliyowatuma nayo Rusuli Wetu, basi karibuni hivi watakuja kujua. 


إِذِ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ وَالسَّلَاسِلُ يُسْحَبُونَ﴿٧١﴾
71. Zitakapokuwa pingu shingoni mwao, na minyororo wanaburutwa.


فِي الْحَمِيمِ ثُمَّ فِي النَّارِ يُسْجَرُونَ﴿٧٢﴾
72. Kwenye maji yachemkayo, kisha kwenye moto wataunguzwa.


ثُمَّ قِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تُشْرِكُونَ﴿٧٣﴾
73. Kisha wataambiwa: “Wako wapi wale mliokuwa mkiwashirikisha?


مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا بَل لَّمْ نَكُن نَّدْعُو مِن قَبْلُ شَيْئًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ الْكَافِرِينَ﴿٧٤﴾
74. “Badala ya Allaah?”  Watasema: “Wametupotea!  Bali hatukuwa tokea mwanzo tukiomba kitu chochote!” Hivyo ndivyo Allaah Anavyopotoa makafiri.


ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمْ تَفْرَحُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَمْرَحُونَ﴿٧٥﴾
75. (Wataambiwa): “Hivyo ni kwa kuwa mlikuwa mkifurahi kwa kutakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa yale mliyokuwa mnashangilia kwa majivuno.”


ادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٧٦﴾
76. “Ingieni milango ya Jahannam ni wenye kudumu humo. Basi uovu ulioje makazi ya wenye kutakabari.”


فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۚ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ﴿٧٧﴾
77. Basi vuta subira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)! Hakika ahadi ya Allaah ni haki. Na ikiwa Tutakuonyesha baadhi ya yale Tunayowaahidi au Tukikufisha, basi Kwetu Pekee watarejeshwa.



وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ ۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ فَإِذَا جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ قُضِيَ بِالْحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْمُبْطِلُونَ﴿٧٨﴾
78. Na kwa yakini Tumewapeleka Rusuli kabla yako; miongoni mwao wako Tuliokusimulia na miongoni mwao wako ambao Hatukukusimulia. Na haiwi kwa Rasuli yeyote kuleta Aayah (au ishara) yoyote ile isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Basi itakapokuja amri ya Allaah kutahukumiwa kwa haki, na hapo watakhasirika wabatilifu.


اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَنْعَامَ لِتَرْكَبُوا مِنْهَا وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٧٩﴾
79. Allaah Ambaye Amekufanyieni wanyama wa mifugo ili muwapande baadhi yao na baadhi yao muwale.


وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَلِتَبْلُغُوا عَلَيْهَا حَاجَةً فِي صُدُورِكُمْ وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ﴿٨٠﴾
80. Na mnapata humo manufaa na ili mpate kufikia kupitia wao, haja zilizomo vifuani mwenu, na juu yao na juu ya merikebu mnabebwa.


وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَأَيَّ آيَاتِ اللَّـهِ تُنكِرُونَ﴿٨١﴾
81. Na Anakuonyesheni Aayaat (ishara, dalili) Zake basi zipi Aayaat za Allaah mnazikanusha?



أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا أَكْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٢﴾
82. Je, hawajatembea katika ardhi wakatazame vipi ilikuwa hatima ya wale wa kabla yao? Walikuwa wengi kuliko wao na wenye nguvu zaidi na athari katika ardhi. Hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma.


فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرِحُوا بِمَا عِندَهُم مِّنَ الْعِلْمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٨٣﴾
83. Basi walipowajia Rusuli wao kwa hoja bayana, walifurahia kwa kujivunia kwa yale waliyokuwa nayo katika elimu, na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.


فَلَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا قَالُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ وَكَفَرْنَا بِمَا كُنَّا بِهِ مُشْرِكِينَ﴿٨٤﴾
84. Basi walipoina adhabu Yetu; walisema: “Tumemwamini Allaah Pekee, na tunakanusha (vyote) ambavyo tulikuwa tunamshirikisha Naye.”


فَلَمْ يَكُ يَنفَعُهُمْ إِيمَانُهُمْ لَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا ۖ سُنَّتَ اللَّـهِ الَّتِي قَدْ خَلَتْ فِي عِبَادِهِ ۖ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْكَافِرُونَ﴿٨٥﴾
85. Basi haikuwa iymaan yao yenye kuwafaa walipoiona adhabu Yetu. (Hii) Ni desturi ya Allaah ambayo imekwishapita katika waja Wake, na hapo wamekhasirika makafiri.


Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.