-->
logo

015 - Al-Hijr

الْحِجْر
Al-Hijr: 15

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرّحِيمِ


الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآنٍ مُّبِينٍ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu na Qur-aan iliyo bayana.



رُّبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ كَانُوا مُسْلِمِينَ ﴿٢﴾
2. Huenda wakatamani wale waliokufuru lau wangelikuwa Waislamu.



ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الْأَمَلُ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٣﴾
3. Waache wale na wastarehe na iwashughulishe kupumbazika na matumaini (ya uongo) basi watakuja kujua.



وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤﴾
4. Na Hatukuangamiza mji wowote isipokuwa ulikuwa na majaaliwa yaliyokadiriwa maalumu.



مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ ﴿٥﴾
5. Ummah wowote hauwezi kutanguliza ajali yake na wala hauwezi kuakhirisha.



وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ ﴿٦﴾
6. Na wakasema: “Ee ambaye umeteremshiwa Adh-Dhikru (Qur-aan), hakika wewe bila shaka ni majnuni.”



لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلَائِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٧﴾
7. “Kwa nini usituletee Malaika ukiwa ni miongoni mwa wakweli?”



مَا نُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ إِلَّا بِالْحَقِّ وَمَا كَانُوا إِذًا مُّنظَرِينَ ﴿٨﴾
8. Hatuteremshi Malaika isipokuwa kwa haki na hawatakuwa hapo wenye kupewa muhula.



إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾
9. Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi.



وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الْأَوَّلِينَ ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini Tulipeleka (Rasuli) kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika makundi ya awali.



وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١١﴾
11. Na hakuwafikia Rasuli yeyote ila walikuwa wakiwafanyia istihzai.



كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٢﴾
12. Hivyo ndivyo Tunavyoingiza (kufru) katika nyoyo za wahalifu.



لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾
13. Hawamuamini na hali imekwishapitia ada ya (kuadhibiwa) watu wa awali.  



وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ السَّمَاءِ فَظَلُّوا فِيهِ يَعْرُجُونَ ﴿١٤﴾
14. Na hata kama Tungeliwafungulia mlango wa mbingu wakabakia kupanda huko.


لَقَالُوا إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ ﴿١٥﴾
15. Bila shaka wangelisema: “Hapana ila macho yetu yamelevywa, bali sisi ni watu tuliofanyiwa sihiri.”


وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَزَيَّنَّاهَا لِلنَّاظِرِينَ﴿١٦﴾
16. Na kwa yakini Tumejaalia katika mbingu nyota zilizo kubwa na Tumezipamba kwa wenye kutazama.


وَحَفِظْنَاهَا مِن كُلِّ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ﴿١٧﴾
17. Na Tukazihifadhi na kila shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.



إِلَّا مَنِ اسْتَرَقَ السَّمْعَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ مُّبِينٌ﴿١٨﴾
18. Isipokuwa anayesikiliza kwa wizi, basi humfuatia kimondo bayana.


وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْزُونٍ﴿١٩﴾
19. Na ardhi Tumeitandaza na Tukatupa humo milima iliyosimama thabiti, na Tukaotesha humo kila kitu kwa uwiano. 



وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَن لَّسْتُمْ لَهُ بِرَازِقِينَ﴿٢٠﴾
20. Na Tukakujaalieni humo njia na mbinu za maisha na ya hao ambao nyinyi si wenye kuwaruzuku.



وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ﴿٢١﴾
21. Na hakuna kitu chochote isipokuwa Tuna hazina zake, na Hatukiteremshi isipokuwa kwa kadiri maalumu.



وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ﴿٢٢﴾
22. Na Tukatuma pepo zikibeba umande na Tukateremsha kutoka mbinguni maji kisha Tukakunywesheni kwayo; wala nyinyi si wenye kuyahifadhi.



وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ﴿٢٣﴾
23. Na hakika Sisi Tunahuisha na Tunafisha; na Sisi ndio Warithi.



وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ﴿٢٤﴾
24. Na Tumekwishajua (ummah) waliotangulia miongoni mwenu, na Tumekwishajua wenye kutaakhari.


وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ﴿٢٥﴾
25. Na hakika Rabb wako Ndiye Atakayewakusanya. Na hakika Yeye ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.



وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ﴿٢٦﴾
26. Na kwa yakini Tumemuumba insani kutokana na udongo wa mfinyanzi unaotoa sauti, unaotokana na tope nyeusi iliyotaghayari.



وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ﴿٢٧﴾
27. Na majini Tuliwaumba kabla kutokana na moto ulio mkali mno.



وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ﴿٢٨﴾
28. Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Namuumba mtu kutokana na udongo mkavu unaotoa sauti, unaotokana na tope nyeusi iliyotaghayari.”



فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ﴿٢٩﴾
29. “Basi Nitakapomsawazisha na Nikampuliza Roho Niliyomuumbia; basi muangukieni kumsujudia.”



فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ﴿٣٠﴾
30. Basi wakasujudu Malaika wote pamoja.


إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ أَن يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ﴿٣١﴾
31. Isipokuwa Ibliys alikataa kuwa pamoja na waliosujudu.



قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ﴿٣٢﴾
32. (Allaah) Akasema: “Ee Ibliys! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?”



قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ﴿٣٣﴾
33. (Ibliys) Akasema: “Haiwi mimi nimsujudie mtu Uliyemuumba kutokana na udongo mkavu unaotoa sauti, unaotokana na tope nyeusi iliyotaghayari.”



قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ﴿٣٤﴾
34. (Allaah) Akasema: “Basi toka humo, kwani hakika wewe umetokomezwa mbali na kulaaniwa.”


وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ﴿٣٥﴾
35. “Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.”



قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ﴿٣٦﴾
36.  Akasema: “Rabb wangu! Nipe muhula mpaka Siku watakayofufuliwa.”



قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ﴿٣٧﴾
37. (Allaah) Akasema: “Basi hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula.”


إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ﴿٣٨﴾
38. “Mpaka siku ya wakati maalumu.”



قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٣٩﴾
39. (Ibliys) Akasema: “Rabb wangu! Kwa vile Umenihukumia kupotoka basi bila shaka nitawapambia (maasi) katika ardhi na nitawapotoa wote.”



إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ﴿٤٠﴾
40. “Isipokuwa waja Wako miongoni mwao waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.”


قَالَ هَـٰذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ﴿٤١﴾
41. (Allaah) Akasema: “Hii ni njia ya kufikia Kwangu iliyonyooka.”



إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ﴿٤٢﴾
42. “Hakika waja wangu huna mamlaka nao isipokuwa  ambaye atakayekufuata miongoni mwa waliopotoka.”


وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٤٣﴾
43. “Na hakika Jahannam ni miadi yao wote pamoja.”


لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ﴿٤٤﴾
44“Una milango saba, na kwa kila mlango iko sehemu (makhsusi) iliyogawanywa.”


إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٤٥﴾
45. Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu.



ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ﴿٤٦﴾
46. (Wataambiwa): “Ingieni humo kwa salama mkiwa katika amani.”



وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ﴿٤٧﴾
47. Na Tutaondosha mafundo ya kinyongo yaliyomo vifuani mwao, wakiwa ndugu, juu ya makochi yaliyoinuliwa wakikabiliana.



لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ﴿٤٨﴾
48. Haitowagusa humo machofu nao humo hawatotolewa.


نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٤٩﴾
49. (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Wajulishe waja Wangu, kwamba: Hakika Mimi ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الْأَلِيمُ﴿٥٠﴾
50. Na kwamba Adhabu Yangu, ndiyo adhabu iumizayo.



وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ﴿٥١﴾
51. Na wajulishe kuhusu wageni wa Ibraahiym.



إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ﴿٥٢﴾
52. Pale walipoingia kwake, wakasema: “Salaam!” (Ibraahiym) Akasema: “Hakika sisi tunakuogopeni.”



قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ﴿٥٣﴾
53. (Malaika) Wakasema: “Usiogope! Hakika sisi tunakubashiria ghulamu mjuzi.”



قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَىٰ أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ﴿٥٤﴾
54. (Ibraahiym) Akasema: “Je, mnanibashiria (mwana) na hali uzee umeshanishika, basi kwa njia gani mnanibashiria?”


قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ﴿٥٥﴾
55. Wakasema: “Tunakubashiria kwa haki, basi usiwe miongoni mwa wakatao tamaa.”


قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ﴿٥٦﴾
56. Akasema: “Na nani anayekata tamaa na rahmah ya Rabb wake isipokuwa wapotofu”


قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ﴿٥٧﴾
57.  Akasema: “Basi nini jambo lenu muhimu enyi Wajumbe.”


قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ﴿٥٨﴾
58. Wakasema: “Hakika sisi tumetumwa kwa watu wahalifu.”


إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٥٩﴾
59. “Isipokuwa familia ya Luwtw, hakika Sisi Tutawaokoa wote.”



إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا ۙ إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ﴿٦٠﴾
60. “Isipokuwa mkewe Tumehukumu kwamba yeye bila shaka ni miongoni mwa watakaobakia nyuma (kuangamizwa).”


فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ﴿٦١﴾
61. Basi Wajumbe walipokuja kwa familia ya Luwtw.



قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٦٢﴾
62. (Luwtw) Akasema: “Hakika nyinyi watu msiojulikana.”



قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُونَ﴿٦٣﴾
63. (Malaika) Wakasema: “Bali tumekujia kwa yale waliyokuwa wanatilia shaka.”



وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ﴿٦٤﴾
64. “Na tumekujia kwa haki na hakika sisi ni wakweli.”


فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ﴿٦٥﴾
65. “Basi toka usiku na ahli wako katika nyakati ya usiku na ufuate nyuma yao wala asigeuke nyuma yeyote miongoni mwenu, na endeleeni kwenda mnakoamrishwa.”


وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَٰلِكَ الْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَـٰؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ﴿٦٦﴾
66. Na Tukamjulisha hukumu ya jambo hilo, kwamba: “Mizizi ya hawa (watendaji uliwati) itakatwa asubuhi.”


وَجَاءَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ﴿٦٧﴾
67. Na wakaja watu wa mji ule wakifurahia.



قَالَ إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ ضَيْفِي فَلَا تَفْضَحُونِ﴿٦٨﴾
68. (Luwtw) Akasema: “Hakika hawa ni wageni wangu, basi msinifedheheshe.”



وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ﴿٦٩﴾
69. “Na mcheni Allaah wala msinihizi.”


قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ﴿٧٠﴾
70.  Wakasema: “Je, hatujakukataza kukaribisha (au kuwalinda) watu wowote?”



قَالَ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ﴿٧١﴾
71. Akasema: “Hawa hapa mabinti zangu (kuwaoa kihalali) ikiwa nyinyi ni wafanyaji.”


لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿٧٢﴾
72. Naapa kwa umri wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم!) Hakika wao walikuwa katika ulevi wao wanatangatanga kwa upofu.



فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ﴿٧٣﴾
73. Basi iliwachukuwa ukelele angamizi walipopambaukiwa jua.



فَجَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ﴿٧٤﴾
74. Tuliufanya (mji huo) juu chini, na Tukawenyeshea mvua ya mawe ya udongo uliookwa (motoni).


إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْمُتَوَسِّمِينَ﴿٧٥﴾
75. Hakika katika hayo mna Aayaat (ishara, zingatio, mafunzo) kwa watambuzi.



وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُّقِيمٍ﴿٧٦﴾
76. Na hakika hiyo (miji) iko katika barabara kuu iliyorasimishwa



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٧٧﴾
77. Hakika katika hayo ni Aayah (ishara, zingatio) kwa Waumini.


وَإِن كَانَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ لَظَالِمِينَ﴿٧٨﴾
78. Na hakika watu wa kichakani (wa Nabiy Shu’ayb) bila shaka walikuwa madhalimu.


فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ﴿٧٩﴾
79. Tukawalipiza (kuwaadhibu) na (nchi) zote mbili hizo ziko katika njia kuu bayana.



وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَابُ الْحِجْرِ الْمُرْسَلِينَ﴿٨٠﴾
80. Na kwa yakini watu wa Al-Hijr (kina Thamuwd) waliwakadhibisha Rusuli.



وَآتَيْنَاهُمْ آيَاتِنَا فَكَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ﴿٨١﴾
81. Na Tuliwapa Aayaat (ishara, dalili) Zetu wakawa wenye kuzipuuza.



وَكَانُوا يَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا آمِنِينَ﴿٨٢﴾
82. Na walikuwa wanachonga majumba katika majabali wakiwa katika amani.



فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ﴿٨٣﴾
83. Basi iliwachukua ukelele angamizi walipopambaukiwa asubuhi.



فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٤﴾
84. Basi hayakuwasaidia yale waliyokuwa wakichuma.


وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ ۖ فَاصْفَحِ الصَّفْحَالْجَمِيلَ﴿٨٥﴾
85. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki. Na hakika Saa bila shaka kitafika. Basi samehe msamaha mzuri.



إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ﴿٨٦﴾
86. Hakika Rabb wako Ndiye Mwingi wa kuumba Atakavyo, Mjuzi wa yote.



وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِّنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ﴿٨٧﴾
87. Na kwa yakini Tumekupa (Aayaat) Saba zinazokaririwa (kusomwa) na Qur-aan Adhimu.



لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَلِلْمُؤْمِنِينَ﴿٨٨﴾
88. Usikodoe kabisa macho yako katika Tuliyowasterehesha makundi fulani miongoni mwao, na wala usihuzunike juu yao. Na inamisha bawa lako kwa Waumini (kuwahurumia).


وَقُلْ إِنِّي أَنَا النَّذِيرُ الْمُبِينُ﴿٨٩﴾
89. Na sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha.”


كَمَا أَنزَلْنَا عَلَى الْمُقْتَسِمِينَ﴿٩٠﴾
90. Kama Tulivyowateremshia (adhabu) waliojigawanya.


الَّذِينَ جَعَلُوا الْقُرْآنَ عِضِينَ﴿٩١﴾
91. Ambao wameifanya Qur-aan sehemu mbali mbali (kuisingizia imetungwa, sihiri, n.k)



فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٩٢﴾
92. Basi Naapa kwa Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), bila shaka Tutawauliza wote.


عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٣﴾
93. Kuhusu yale waliyokuwa wakitenda.


فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ﴿٩٤﴾
94. Basi tangaza wazi yale uliyoamrishwa na jitenge na washirikina.



إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ﴿٩٥﴾
95. Hakika sisi Tunakutosheleza dhidi ya wafanyao istihzai.



الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٩٦﴾
96. Ambao wanafanya pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine basi watakuja kujua.



وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ﴿٩٧﴾
97. Na kwa yakini Tunajua kwamba kifua chako kinadhikika kwa yale wanayoyasema.


فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ﴿٩٨﴾
98. Basi Sabbih kwa Himidi za Rabb wako na uwe miongoni mwa wanaosujudu.



وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ﴿٩٩﴾
99. Na mwabudu Rabb wako mpaka ikufikie yakini (mauti).

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.