-->
logo

016 - An-Nahl

 النَّحْل
An-Nahl: 16


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


أَتَىٰ أَمْرُ اللَّـهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١﴾
1. Amri ya Allaah (ya Qiyaamah) itafika tu basi msiihimize. Subhaanahu wa Ta’aalaa (Utakasifu ni Wake na Ametukuka) kutokana na yale wanayomshirikisha nayo.



يُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ بِالرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ أَنْ أَنذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ﴿٢﴾
2. Anateremsha Malaika na Ar-Ruwh (Wahy) kwa amri Yake juu ya Amtakaye miongoni mwa waja Wake, kwamba: “Onyeni: Hakika hapana muabudiwa wa haki ila Mimi basi Nicheni.”



خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ تَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣﴾
3.  Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Ametukuka kwa Uluwa kutokana na yale wanayoshirikisha.



خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ﴿٤﴾
4. Amemuumba insani kutokana na tone la manii tahamaki yeye ni mbishani bayana.


وَالْأَنْعَامَ خَلَقَهَا ۗ لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَافِعُ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٥﴾
5. Na wanyama wa mifugo Amewaumba. Mnapata humo (sufi, ngozi za kutia) ujotojoto na manufaa (mengineyo) na miongoni mwao mnawala.



وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ﴿٦﴾
6. Na mnapata humo jamala wakati wa mnaporudisha jioni na mnapopeleka machungani asubuhi.



وَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ إِلَىٰ بَلَدٍ لَّمْ تَكُونُوا بَالِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ الْأَنفُسِ ۚ إِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٧﴾
7. Na wanabeba mizigo yenu kupeleka nchi msizoweza kuzifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi. Hakika Rabb wenu bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.



وَالْخَيْلَ وَالْبِغَالَ وَالْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴿٨﴾
8. Na farasi na baghala na punda ili muwapande na wawe mapambo. Na Anaumba msivyovijua.



وَعَلَى اللَّـهِ قَصْدُ السَّبِيلِ وَمِنْهَا جَائِرٌ ۚ وَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ﴿٩﴾
9. Na juu ya Allaah kubainisha njia (ya haki), na humo ziko miongoni mwazo za kupotoka. Na kama Angetaka Angekuhidini nyote.



هُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً ۖ لَّكُم مِّنْهُ شَرَابٌ وَمِنْهُ شَجَرٌ فِيهِ تُسِيمُونَ﴿١٠﴾
10. Yeye Ndiye Yule Aliyeteremesha kutoka mbinguni maji, kutokana hayo, mnapata kinywaji na (mnaotesha) miti ambayo mnalishia.



يُنبِتُ لَكُم بِهِ الزَّرْعَ وَالزَّيْتُونَ وَالنَّخِيلَ وَالْأَعْنَابَ وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١١﴾
11. Anakuotesheeni mimea kwa hayo (maji) na mizaytuni na mitende na mizabibu na kila (aina ya) mazao. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayah (ishara, dalili) kwa watu wanaotafakari.



وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ وَالنُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍيَعْقِلُونَ﴿١٢﴾
12. Na Amekutiishieni usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zinazotiishwa kwa amri Yake. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayaat (ishara, dalili) kwa watu wanaotia akilini.


وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ﴿١٣﴾
13. Na (Ametiisha pia) Alivyoviumba katika ardhi vya rangi tofauti. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayah (ishara, dalili, zingatio) kwa watu wanaokumbuka.


وَهُوَ الَّذِي سَخَّرَ الْبَحْرَ لِتَأْكُلُوا مِنْهُ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُوا مِنْهُ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى الْفُلْكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٤﴾
14. Naye Ndiye Ambaye Ametiisha bahari ili mle humo nyama laini safi na mtoe humo mapambo mnayoyavaa na utaona merikebu zikipasua maji humo; (Amezitiisha) ili mtafute katika fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.


وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَارًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٥﴾
15. Na Ameweka katika ardhi milima iliyosimama imara ili isiyumbeyumbe kwenu, na (Akaweka) mito na njia ili mpate kujiongoza.


وَعَلَامَاتٍ ۚ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ﴿١٦﴾
16. Na alama za kutambulisha na kwa nyota wanaojiongoza (njia).



أَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ ۗ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿١٧﴾
17. Je, (Allaah) Anayeumba ni sawa kama asiyeumba? Je, basi hamkumbuki?



وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٨﴾
18. Na mkihesabu neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni. Hakika Allaah bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ﴿١٩﴾
19. Na Allaah Anajua mnayoyafanya siri na mnayoyadhihirisha.


وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ﴿٢٠﴾
20. Na wale wanaowaomba badala ya Allaah hawaumbi kitu chochote, bali wao wanaumbwa.


أَمْوَاتٌ غَيْرُ أَحْيَاءٍ ۖ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ﴿٢١﴾
21. Ni wafu si wahai; na hawatambui lini watafufuliwa.



إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ فَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ﴿٢٢﴾
22. Muabudiwa wa haki wenu ni Ilaah (Allaah) Mmoja. Basi wale wasioamini Aakhirah nyoyo zao zinakanusha nao wanatakabari.



لَا جَرَمَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْتَكْبِرِينَ﴿٢٣﴾
23. Hapana shaka kwamba Allaah Anajua wanayoyafanya siri na wanayayoyadhihirisha. Hakika Yeye Hapendi wanaotakabari.



وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿٢٤﴾
24. Na pale wanapoambiwa: “Nini Ameteremsha Rabb wenu (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?” Husema: “Hekaya za watu wa kale.”



لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ﴿٢٥﴾
25. Ili wabebe mizigo (ya madhambi) yao kwa ukamilifu Siku ya Qiyaamah, na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya kujua. Tanabahi!  Uovu ulioje wanayoyabeba.



قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللَّـهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٢٦﴾
26. Walikwishafanya makri wale wa kabla yao, basi Allaah Aliyasukua majengo yao kwenye misingi, sakafu zikawaporomokea juu yoa, na ikawajia adhabu kutoka pande wasizozitambua.   



ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تُشَاقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ﴿٢٧﴾
27. Kisha Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atawahizi na Atasema: “Wako wapi washirika Wangu ambao mlikuwa kwa ajili yao mnapingana kuwahasimu (Rusuli na Waumini)?” Watasema waliopewa elimu: “Hakika hizaya leo na uovu ni juu ya makafiri.”



الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾
28. Ambao Malaika huwafisha wakiwa wamejidhulumu nafsi zao, watasalimu amri (watasema): “Hatukuwa tukitenda uovu wowote.” (Wataambiwa): “Hapana! Hakika Allaah ni Mjuzi kwa yale mliyokuwa mkitenda.”



فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٢٩﴾
29. “Basi ingieni milango ya Jahannam ni wenye kudumu humo.” Ni uovu ulioje makazi ya wanaotakabari.



وَقِيلَ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا مَاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ ۚوَلَنِعْمَ دَارُ الْمُتَّقِينَ﴿٣٠﴾
30. Na wanapoambiwa wale waliokuwa na taqwa: “Nini Ameteremsha Rabb wenu?” Husema: “Kheri.” Kwa wale waliofanya ihsaan katika dunia hii watapata hasanah (mazuri). Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi. Na uzuri ulioje nyumba ya wenye taqwa.



جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِي اللَّـهُ الْمُتَّقِينَ﴿٣١﴾
31. Jannaat za kudumu milele wataziingia humo, zipitazo chini yake mito. Watapata humo wayatakayo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowalipa wenye taqwa.



الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾
32. Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema watasema: “Salaamun ‘Alaykum, (amani iwe juu yenu) ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.”



هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ أَمْرُ رَبِّكَ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٣٣﴾
33. Je, wanangojea lolote isipokuwa wawafikie Malaika (kuwatoa roho) au iwafikie amri ya Rabb wako (ya adhabu). Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Na Allaah Hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.



فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٣٤﴾
34. Basi ikawasibu maovu ya waliyoyatenda, na ikawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.



وَقَالَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ نَّحْنُ وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ فَهَلْ عَلَى الرُّسُلِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٣٥﴾
35. Na wale washirikina wakasema: “Kama Angelitaka Allaah tusingeliabudu chochote pasi Naye, sisi wala baba zetu; wala tusingeliharamisha chochote bila (ya amri) Yake.” Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Basi je, kuna lolote juu ya Rusuli isipokuwa ubalighisho bayana?



وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّـهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٣٦﴾
36. Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti.” Basi miongoni mwao ambao Allaah Amewahidi, na miongoni mwao ambao umethibiti kwake upotofu. Basi nendeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.


إِن تَحْرِصْ عَلَىٰ هُدَاهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَن يُضِلُّ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٣٧﴾
37. Ukiwa na hima ya kutaka kuwaongoza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Allaah Hamhidi aliyepotea. Na hawatopata yeyote mwenye kunusuru.



وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ لَا يَبْعَثُ اللَّـهُ مَن يَمُوتُ ۚ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٨﴾
38. Na wakaapa kwa Jina la Allaah nguvu ya viapo vyao kwamba: “Allaah Hatomfufua aliyekufa.” Ndio!  Ahadi Yake ni haki (Atafufua wote); lakini watu wengi hawajui.




لِيُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ كَانُوا كَاذِبِينَ﴿٣٩﴾
39. Ili Awabainishie yale waliyokhitilafiana, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.



إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَيْءٍ إِذَا أَرَدْنَاهُ أَن نَّقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴿٤٠﴾
40. Hakika Kauli Yetu juu ya kitu Tunapokikusudia; Tunakiambia: “Kun!” Basi kinakuwa!



وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٤١﴾
41. Na wale waliohajiri kwa ajili ya Allaah baada ya kudhulumiwa, Tutawapa makazi mazuri duniani. Na bila shaka ujira wa Aakhirah ni mkubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.



الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٤٢﴾
42. (Hao ndio) Wale waliosubiri na wakatawakali kwa Rabb wao.



وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۚ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٤٣﴾
43. Na Hatukutuma (Rasuli) kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni wanaume Tunawafunulia Wahy. Basi ulizeni watu wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.



بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾
44. (Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari.




أَفَأَمِنَ الَّذِينَ مَكَرُوا السَّيِّئَاتِ أَن يَخْسِفَ اللَّـهُ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٤٥﴾
45. Je, wameaminisha wale waliopanga makri za uovu kwamba Allaah Hatowadidimiza katika ardhi au haitowafikia adhabu kutoka wasipotambua?



أَوْ يَأْخُذَهُمْ فِي تَقَلُّبِهِمْ فَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ﴿٤٦﴾
46. Au (Allaah) Hatowateka katika harakati zao? Basi wao si wenye kuweza kukwepa.



أَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٤٧﴾
47. Au (Allaah) Hatowateka katika hali ya khofu kuwapunguza kidogo kidogo, basi hakika Rabb wako bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.



أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ﴿٤٨﴾
48. Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinasogea huku na kule, kuliani na kushotoni vikimsujudia Allaah na huku vinanyenyekea?  



وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٩﴾
49. Na ni kwa Allaah pekee vinasujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.



يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩﴿٥٠﴾
50. Wanamkhofu Rabb wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa.


وَقَالَ اللَّـهُ لَا تَتَّخِذُوا إِلَـٰهَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ﴿٥١﴾
51. Na Allaah Anasema: “Msijichukulie waungu wawili; hakika Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki Mmoja Pekee basi niogopeni Mimi tu.”



وَلَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَهُ الدِّينُ وَاصِبًا ۚ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ تَتَّقُونَ﴿٥٢﴾
52. Na ni Vyake vyote viliomo katika mbingu na ardhi, na Kwake Pekee inastahiki ‘ibaadah ya kudumu ya ikhlaasw na utiifu. Je, basi mtamcha asiyekuwa Allaah?



وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْأَرُونَ﴿٥٣﴾
53. Na neema yoyote mliyo nayo, basi ni kutoka kwa Allaah. Kisha inapokuguseni dhara Kwake mnamlilia msaada.



ثُمَّ إِذَا كَشَفَ الضُّرَّ عَنكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنكُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ﴿٥٤﴾
54. Kisha Anapokuondosheeni dhara tahamaki kundi miongoni mwenu wanamshirikisha Rabb wao.



لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ﴿٥٥﴾
55. Ili wakanushe (neema) Tulizowapa. Basi stareheni kidogo, mtakuja kujua.



وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًا مِّمَّا رَزَقْنَاهُمْ ۗ تَاللَّـهِ لَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ﴿٥٦﴾
56. Na wanawawekea (waabudiwa wao) wasiojua (wanayofanyiwa), fungu katika ambavyo Tumewaruzuku. Wa-Allaahi! Bila shaka mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatunga.




وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ الْبَنَاتِ سُبْحَانَهُ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ﴿٥٧﴾
57. Na wanamfanyia Allaah mabinti Subhaanah! (Utakasifu ni Wake) na hali wao wanao (wana wa kiume) wanaowatamani.




وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿٥٨﴾
58. Na anapobashiriwa mmoja wao (mtoto) wa kike, husawijika uso wake naye huku amezuia ghaidhi na majonzi.



يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِن سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿٥٩﴾
59. Anajificha kwa watu kwa ubaya aliobashiriwa. Je, amzuie kwa fedheha au amfukie ardhini (mzimamzima). Tanabahi! Uovu ulioje wanayohukumu.



لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ مَثَلُ السَّوْءِ ۖ وَلِلَّـهِ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٦٠﴾
60. Kwa wale wasioamini Aakhirah wana mfano mbaya (ya upungufu); na Allaah Ana Sifa kamilifu tukufu kabisa. Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.



وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٦١﴾
61. Na kama Allaah Angeliwachukulia watu kwa dhulma zao, Asingeliacha juu ya ardhi kiumbe chochote; lakini Anawaakhirisha mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao hawataakhirisha saa na wala hawatatanguliza.



وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ مَا يَكْرَهُونَ وَتَصِفُ أَلْسِنَتُهُمُ الْكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ الْحُسْنَىٰ ۖ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ النَّارَ وَأَنَّهُم مُّفْرَطُونَ﴿٦٢﴾
62. Na wanamfanyia Allaah yale wanayoyachukia (wao wenyewe) na ndimi zao zinaeleza uongo kwamba watapata mazuri kabisa. Hapana shaka kwamba watapata moto na kwamba wao watapelekwa haraka humo na kutelekezwa.




تَاللَّـهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ الْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦٣﴾
63. Wa-Allaahi kwa yakini Tumepeleka (Rusuli) kwa umati kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi shaytwaan akawapambia ‘amali zao, basi yeye leo ni rafiki mwandani wao, na watapata adhabu iumizayo.


وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٦٤﴾
64. Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana, na ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini.




وَاللَّـهُ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٦٥﴾
65. Na Allaah Ameteremsha kutoka mbinguni maji Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayah (ishara, dalili, zingatio) kwa watu wanaosikia.



وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِ مِن بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَائِغًا لِّلشَّارِبِينَ﴿٦٦﴾
66. Na hakika katika wanyama wamifugo mna funzo kwenu. Tunakunywisheni katika yale yaliyomo matumboni mwao yaliyo baina ya kinyesi na damu; (nayo ni) maziwa safi ya ladha anisi kwa wanywaji.



وَمِن ثَمَرَاتِ النَّخِيلِ وَالْأَعْنَابِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿٦٧﴾
67. Na katika matunda ya mitende na mizabibu mnafanya humo vinywaji vikali vya ulevi (vinavyokatazwa) na riziki nzuri. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayah (ishara, dalili) kwa wanaotia akilini.



وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ﴿٦٨﴾
68. Na Rabb wako Akamtia ilhamu nyuki kwamba: “Jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika wanavyojenga.”



ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٦٩﴾
69. “Kisha kula katika kila matunda, na fuata njia za Rabb wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita). Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayah (ishara, dalili) kwa watu wanaotafakari.


وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّاكُمْ ۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ﴿٧٠﴾
70. Na Allaah Amekuumbeni, kisha Anakufisheni. Na miongoni mwenu wanaorudishwa katika umri mbaya na dhaifu zaidi awe hajui kitu chochote baada ya (kuwa na) elimu. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Muweza wa yote.



وَاللَّـهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الرِّزْقِ ۚ فَمَا الَّذِينَ فُضِّلُوا بِرَادِّي رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَاءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ﴿٧١﴾
71. Na Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengineo katika riziki. Basi wale waliofadhilishwa hawagawi riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika hiyo (riziki). Je, basi wanakanusha neema za Allaah?



وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ اللَّـهِ هُمْ يَكْفُرُونَ﴿٧٢﴾
72.  Na Allaah Amekufanyieni wake katika jinsi yenu; na Amekufanyieni katika wake zenu wana na wajukuu; na Amekuruzukuni vizuri. Je, basi wanaamini ya batili na wanakufuru neema za Allaah?



وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ شَيْئًا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ﴿٧٣﴾
73. Na wanaabudu pasi na Allaah wasiowamilikia riziki ya kitu chochote kutoka mbinguni na ardhini na wala hawawezi. 



فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٧٤﴾
74. Basi msimpigie mifano Allaah. Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.



ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَمَن رَّزَقْنَاهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُونَ ۚ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٧٥﴾
75. Allaah Amepiga mfano wa mja anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote na (mwingine) ambaye Tumemruzuku kutoka Kwetu riziki nzuri; naye anatoa katika humo kwa siri na dhahiri. Je, wanalingana sawa? AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah!). Bali wengi wao hawajui.



وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾
76. Na Allaah amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote naye ni mzigo kwa bwana wake, popote unapomuelekeza haleti kheri. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka.?



وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٧٧﴾
77. Na ni ya Allaah ghayb ya mbingu na ardhi. Na wala haikuwa amri ya Saa isipokuwa kama upepeso wa jicho au karibu zaidi. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.



وَاللَّـهُ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۙ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿٧٨﴾
78. Na Allaah Amekutoeni kutoka matumboni mwa mama zenu mkiwa hamjui lolote, na Amekujaalieni kusikia na kuona na nyoyo ili mpate kushukuru.



أَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ مُسَخَّرَاتٍ فِي جَوِّ السَّمَاءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا اللَّـهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٧٩﴾
79. Je, hawaoni ndege wanavyotiishwa katika anga la mbingu, hakuna anayewashika isipokuwa Allaah. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayaat (ishara, dalili, zingatio) kwa watu wanaoamini.



وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّن بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ﴿٨٠﴾
80. Na Allaah Amekufanyieni majumba yenu yawe maskani, na Amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama wa mifugo nyumba mnazihisi nyepesi (mahema) siku ya kusafiri kwenu na siku ya kupiga kwenu kambi na kutokana na sufi zao na manyoya yao, na nywele zao (mnatengeneza) fanicha ni manufaa mpaka muda fulani.


وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَالًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْجِبَالِ أَكْنَانًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَابِيلَ تَقِيكُمُ الْحَرَّ وَسَرَابِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ﴿٨١﴾
81. Na Allaah Amekufanyieni vivuli katika Alivyoumba na Akakujaalieni katika majabali mahali pa kukimbilia na Amekujaalieni mavazi yanakukingeni na joto na mavazi (ya chuma) yanakukingeni katika vita vyenu. Hivyo ndivyo Anavyotimiza neema Yake juu yenu huenda mkapata kujisalimisha.



فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٨٢﴾
82. Wakikengeuka, basi hakika ni juu yako ubalighisho wa bayana.


يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللَّـهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ﴿٨٣﴾
83. Wanazijua neema za Allaah, kisha wanazikanusha; na wengi wao ni makafiri.


وَيَوْمَ نَبْعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا ثُمَّ لَا يُؤْذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ﴿٨٤﴾
84. Na Siku Tutakapowafufua katika kila ummah shahidi kisha haitoruhusiwa kwa wale waliokufuru (kutoa nyudhuru) na wala hawataachiliwa kuomba kuridhisha (kwa Allaah).



وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ ظَلَمُوا الْعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ﴿٨٥﴾
85. Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, basi hawatopunguziwa   na wala hawatopewa muhula.


وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ أَشْرَكُوا شُرَكَاءَهُمْ قَالُوا رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ شُرَكَاؤُنَا الَّذِينَ كُنَّا نَدْعُو مِن دُونِكَ ۖ فَأَلْقَوْا إِلَيْهِمُ الْقَوْلَ إِنَّكُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٨٦﴾
86. Na wale waliomshirikisha (Allaah) watakapowaona washirika wao watasema: “Rabb wetu! Hawa ni washirikishwa wetu ambao tulikuwa tunawaomba badala Yako.” Lakini watawatupia kauli: “Hakika nyinyi ni waongo.”


وَأَلْقَوْا إِلَى اللَّـهِ يَوْمَئِذٍ السَّلَمَ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٨٧﴾
87. Na watajisalimisha kwa Allaah Siku hiyo. Na yatawapotea waliyokuwa wakiyatunga.



الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ﴿٨٨﴾
88. Wale waliokufuru na wakazuia njia ya Allaah, Tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufisadi.



وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿٨٩﴾
89. Na Siku Tutakayofufua katika kila ummah shahidi dhidi yao kutokana na jinsi zao. Na Tutakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uwe shahidi juu ya hawa (ummah wako). Na Tumekuteremshia Kitabu kikiwa ni kielezo bayana cha kila kitu na ni mwongozo na rahmah na bishara kwa Waislamu.


إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴿٩٠﴾
90. Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini ili huenda mkapata kukumbuka.



وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللَّـهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ﴿٩١﴾
91. Na timizeni ahadi ya Allaah mnapoahidi, na wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha; na mmekwishamfanya Allaah kuwa ni Mdhamini wenu.  Hakika Allaah Anajua yale mnayoyafanya.


وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ اللَّـهُ بِهِ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wala msiwe kama yule mwanamke aliyezongoa uzi wake vipande vipande baada ya (kuusokota na) kuwa mgumu, mnafanya viapo vyenu kuwa njia ya kudaganyana baina yenu, kwa kuwa ummah mmoja uko juu kwa wingi na nguvu kuliko ummah mwengine. Hakika hapana ila Allaah Anakujaribuni kwavyo.  Na bila shaka Atakubainishieni Siku ya Qiyaamah yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.



وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَلَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٣﴾
93. Na kama Allaah Angelitaka Angelikufanyeni ummah mmoja, lakini Humpotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye. Na bila shaka mtaulizwa kuhusu yale mliyokuwa mkiyatenda.



وَلَا تَتَّخِذُوا أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ فَتَزِلَّ قَدَمٌ بَعْدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُوا السُّوءَ بِمَا صَدَدتُّمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَلَكُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٩٤﴾
94. Na wala msifanye viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu ukateleza mguu baada ya kuthibitika kwake, na mkaonja uovu wenu (duniani) kwa sababu ya kuzuia kwenu njia ya Allaah. Na mtapata (Aakhirah) adhabu kuu.



وَلَا تَشْتَرُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ إِنَّمَا عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩٥﴾
95. Na wala msibadilishe ahadi ya Allaah kwa thamani ndogo. Hakika yaliyoko kwa Allaah ni bora kwenu, mgelikuwa mnajua.



مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٦﴾
96. Mlivyo navyo nyinyi vinatoweka, na vilioko kwa Allaah ni vya kubakia. Na kwa yakini Tutawalipa wale waliosubiri ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.



مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾
97. Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.



فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾
98. Unaposoma kusoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.


إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٩٩﴾
99. Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na kwa Rabb   wao wanatawakali.



إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ مُشْرِكُونَ﴿١٠٠﴾
100. Hakika mamlaka yake ni juu ya wale wanaomfanya rafiki mwandani na ambao wao wanamshirikisha (Allaah) naye.



وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٠١﴾
101. Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine, na Allaah Anajua zaidi Anayoyateremsha, husema: “Hakika wewe ni mtungaji.” Bali wengi wao hawajui.



قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿١٠٢﴾
102. Sema: Ameiteremsha Ruwhul-Qudus (Jibriyl) kutoka kwa Rabb wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini na ni mwongozo na bishara kwa Waislamu.



وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ﴿١٠٣﴾
103. Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: “Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan).” Lisani wanayomnasibishia nao ni ya kigeni, na hii ni lisani ya Kiarabu bayana.



إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ لَا يَهْدِيهِمُ اللَّـهُ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٠٤﴾
104. Hakika wale wasioamini Aayaat za Allaah, Allaah Hatowahidi, na watapata adhabu iumizayo.



إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ﴿١٠٥﴾
105. Hakika wanaotunga uongo ni wale ambao hawaamini Aayaat za Allaah. Na hao ndio waongo.



مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Atakayemkufuru Allaah baada ya iymaan yake - isipokuwa yule aliyekirihishwa (kukanusha) na huku moyo wake umetua juu ya iymaan - lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu.



ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿١٠٧﴾
107. Hivyo kwa sababu wao wamestahabu uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah; na kwamba Allaah Haongoi watu makafiri.


أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٠٨﴾
108. Hao ni wale ambao Allaah Amepiga chapa juu ya nyoyo zao, na masikio yao, na macho yao. Na hao ndio walioghafilika.


لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿١٠٩﴾
109. Hakuna shaka kwamba wao Aakhirah niwenye kukhasirika.


ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِن بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٠﴾
110. Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliohajiri baada ya kutiwa katika mtihani kisha wakafanya jihaad na wakasubiri; hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


يَوْمَ تَأْتِي كُلُّ نَفْسٍ تُجَادِلُ عَن نَّفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿١١١﴾
111. Siku itakapokuja kila nafsi kutetea nafsi yake na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyofanya; nao hawatodhulumiwa.



وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ آمِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ اللَّـهِ فَأَذَاقَهَا اللَّـهُ لِبَاسَ الْجُوعِ وَالْخَوْفِ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴿١١٢﴾
112. Na Allaah Amepiga mfano wa mji uliokuwa katika amani na utulivu, inaifikia riziki yake maridhawa kutoka kila mahali; kisha ukakufuru neema za Allaah basi Allaah Akauonjesha funiko la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakitenda.



وَلَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ وَهُمْ ظَالِمُونَ﴿١١٣﴾
113. Na kwa yakini aliwajia Rasuli miongoni mwao wakamkadhibisha, basi ikawachukuwa dhabu hali ya kuwa ni madhalimu.



فَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا وَاشْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿١١٤﴾
114. Basi kuleni katika vile Alivyokuruzukuni Allaah vya halaal vizuri na shukuruni neema za Allaah ikiwa mnamwabudu Yeye Pekee.


إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٥﴾
115. Hakika (Allaah) Amekuharamishieni nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake ghairi ya Allaah. Basi atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka; basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.



وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿١١٦﴾
116. Na wala msiseme zinayotetea ndimi zenu uongo; hii halaal na hii haraam ili mumtungie Allaah uongo. Hakika wale wanaomtungia Allaah uongo hawafaulu.


مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١٧﴾
117. Ni starehe ndogo (tu duniani), na watapata adhabu iumizayo.


وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا مَا قَصَصْنَا عَلَيْكَ مِن قَبْلُ ۖ وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿١١٨﴾
118. Na wale Mayahudi Tuliwaharamishia yale Tuliyokusimulia kabla (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Hatukuwadhulumu, lakini walikuwa wanajidhulumu nafsi zao wenyewe.


ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٩﴾
119. Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliotenda uovu kwa ujahili, kisha wakatubu baada yake, na wakatengenea; hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٠﴾
120. Hakika Ibraahiym alikuwa Imaam mtiifu kwa Allaah, aliyeelemea haki na wala hakuwa miongoni mwa washirikina.


شَاكِرًا لِّأَنْعُمِهِ ۚ اجْتَبَاهُ وَهَدَاهُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿١٢١﴾
121. Mwenye kushukuru neema Zake, (Naye Allaah) Akamteua na Akamuongoza kuelekea njia iliyonyooka.


وَآتَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ﴿١٢٢﴾
122. Na Tukampa duniani mazuri. Na hakika yeye Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa Swalihina.


ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٣﴾
123. Kisha Tukakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba fuata mila ya Ibraahim aliyeelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.


إِنَّمَا جُعِلَ السَّبْتُ عَلَى الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٢٤﴾
124. Hakika As-Sabt imefanywa kwa wale waliokhitilafiana kwayo. Na hakika Rabb wako Atawahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wanakhitilafiana kwayo.


ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ﴿١٢٥﴾
125. Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. Na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi. Hakika Rabb wako Yeye Anamjua zaidi aliyepotea njia Yake, Naye Anawajua zaidi waliohidika.


وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ﴿١٢٦﴾
126. Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkisubiri, basi bila shaka hivyo ni bora kwa wenye kusubiri.


وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na haiwi subira yako isipokuwa kupitia kwa Allaah. Na wala usiwahuzunukie, na wala usiwe katika dhiki kutokana na njama wanazozifanya. 


إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ﴿١٢٨﴾
128. Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni wenye kufanya ihsaan.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.