-->
logo

014 - Ibraahiym

إِبْرَاهِيم

Ibraahiym: 14


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الر ۚ كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwatoe watu kutoka kwenye viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Rabb wao, waelekee katika njia ya Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.



اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ ﴿٢﴾
2. Allaah Ambaye ni Vyake viliyomo katika mbingu na katika ardhi. Na ole kwa makafiri kutokana na adhabu kali. 


الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ ﴿٣﴾
3. Ambao wanaositahabu uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah, na wanazuia njia ya Allaah, na wanaitafutia ionekane kombo. Hao wamo katika upotofu wa mbali.



وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚوَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٤﴾
4. Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie (risala). Basi Allaah Humpotoa Amtakaye na Humhidi Amtakaye. Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.



وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا أَنْ أَخْرِجْ قَوْمَكَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَذَكِّرْهُم بِأَيَّامِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ﴿٥﴾
5. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa kwa Aayaat (miujiza, dalili) Zetu nyingi (Tukimwambia): “Itoe kaumu yako kutoka kwenye viza kwenda katika nuru, na wakumbushe Siku za Allaah. Hakika katika hayo kuna Aayaat (ishara, zingatio, mafunzo) kwa kila mwingi wa kusuburi na kushukuru.



وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ أَنجَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٦﴾
6.  Na pindi Muwsaa alipoiambia kaumu  yake: “Kumbukeni neema ya Allaah juu yenu, Alipokuokoeni kutokana na watu wa Fir’awn, walipokusibuni adhabu mbaya na wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb wenu. 



وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ﴿٧﴾
7.  Na pindi Alipotangaza Rabb wenu: “Ikiwa mtashukuru, bila shaka Nitakuzidishieni (neema Zangu); na mkikufuru, basi hakika adhabu Yangu ni kali.



وَقَالَ مُوسَىٰ إِن تَكْفُرُوا أَنتُمْ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا فَإِنَّ اللَّـهَ لَغَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٨﴾
8. Na Muwsaa alisema: “Mkikufuru nyinyi na wote walioko ardhini, basi hakika Allaah ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.



أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ ۛ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ ۛ لَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا اللَّـهُ ۚجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرَدُّوا أَيْدِيَهُمْ فِي أَفْوَاهِهِمْ وَقَالُوا إِنَّا كَفَرْنَا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ وَإِنَّا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَنَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ ﴿٩﴾
9. Je, haijakufikieni habari ya wale wa kabla yenu; watu wa Nuwh, na ‘Aad na Thamuwd, na wale wa baada yao. Hakuna Awajuao isipokuwa Allaah. Waliwajia Rusuli wao kwa hoja bayana. Wakarudisha mikono yao katika midomo yao na wakasema: “Hakika sisi tumeyakanusha yale mliyotumwa nayo, na hakika sisi tumo katika shaka kutokana na mnayotuitia kwayo na tunayashuku.”



قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِي اللَّـهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ قَالُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا تُرِيدُونَ أَن تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿١٠﴾
10. Wakasema Rusuli wao: “Je, kuna shaka kuhusiana na Allaah, Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Anakuiteni ili Akughufurieni madhambi yenu na Akuakhirisheni mpaka muda maalumu uliokadiriwa?” Wakasema: “Nyinyi si chochote isipokuwa ni watu kama sisi, mnataka kutuzuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni hoja bayana.”



قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِن نَّحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَمَا كَانَ لَنَا أَن نَّأْتِيَكُم بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾
11. Wakasema Rusuli wao: “Sisi si chochote isipokuwa ni watu kama nyinyi, lakini Allaah Anamfadhilisha Amtakaye miongoni mwa waja Wake. Na haikutupasa sisi kukujieni kwa mamlaka (na buruhani) isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na kwa Allaah watawakali Waumini.



وَمَا لَنَا أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانَا سُبُلَنَا ۚ وَلَنَصْبِرَنَّ عَلَىٰ مَا آذَيْتُمُونَا ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُتَوَكِّلُونَ ﴿١٢﴾
12. Na tuna nini (sisi) hata tusitawakali kwa Allaah na hali Amekwishatuongoza njia yetu? Na kwa yakini tutasubiri juu ya maudhi yenu kwetu. Na kwa Allaah watawakali wanaotawakali.”



وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّكُم مِّنْ أَرْضِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۖ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ لَنُهْلِكَنَّ الظَّالِمِينَ ﴿١٣﴾
13. Wakasema wale waliokufuru kuwaambia Rusuli wao: “Bila shaka tutakutoeni katika ardhi yetu, au mtarudi kwa hakika katika mila zetu.”  Basi Rabb wao Akawafunulia Wahy kwamba: “Bila shaka Tutawahiliki madhalimu.”



وَلَنُسْكِنَنَّكُمُ الْأَرْضَ مِن بَعْدِهِمْ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَافَ مَقَامِي وَخَافَ وَعِيدِ ﴿١٤﴾
14. “Na bila shaka Tutakuwekeni maskani katika ardhi baada yao. Haya ni kwa yule anayekhofu kusimamishwa mbele Yangu na akakhofu maonyo Yangu.”



وَاسْتَفْتَحُوا وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ﴿١٥﴾
15. Na wakaomba ushindi (kwa Allaah), na akapita patupu kila (aliyejifanya) jabari, mkaidi.


مِّن وَرَائِهِ جَهَنَّمُ وَيُسْقَىٰ مِن مَّاءٍ صَدِيدٍ ﴿١٦﴾
16. Nyuma yake kuna Jahannam, na atanyweshwa maji ya usaha.



يَتَجَرَّعُهُ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُ وَيَأْتِيهِ الْمَوْتُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَمَا هُوَ بِمَيِّتٍ ۖ وَمِن وَرَائِهِ عَذَابٌ غَلِيظٌ﴿١٧﴾
17. Atayagugumia kwa tabu na wala hatakaribia kuyameza kiulaini, na yatamjia mauti kutoka kila upande, naye hatokufa hata kidogo. Na nyuma yake kuna adhabu nzito.



مَّثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ۖ أَعْمَالُهُمْ كَرَمَادٍ اشْتَدَّتْ بِهِ الرِّيحُ فِي يَوْمٍ عَاصِفٍ ۖ لَّا يَقْدِرُونَ مِمَّا كَسَبُوا عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٨﴾
18. Mfano wa wale waliomkufuru Rabb wao, ‘amali zao ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo siku ya dhoruba. Hawatoweza kupata chochote katika yale waliyoyachuma. Huo ndio upotofu wa mbali. 



أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿١٩﴾
19. Je, huoni kwamba Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Akitaka Atakuondosheleeni mbali na Alete viumbe vipya.



وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ بِعَزِيزٍ ﴿٢٠﴾
20. Na hivyo kwa Allaah si la kushindwa.



وَبَرَزُوا لِلَّـهِ جَمِيعًا فَقَالَ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا مِنْ عَذَابِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ قَالُوا لَوْ هَدَانَا اللَّـهُ لَهَدَيْنَاكُمْ ۖ سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَجَزِعْنَا أَمْ صَبَرْنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٍ ﴿٢١﴾
21. Na watahudhuria wote mbele ya Allaah, wanyonge watawaambia wale waliotakabari: “Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu (tukikutiini). Basi je, nyinyi mtaweza kutuondolea chochote katika adhabu ya Allaah?” Watasema: “Kama Allaah Angetuhidi, bila shaka tungelikuongozeni. Ni sawasawa kwetu; tukipapatika au tukisubiri, hatuna mahali pa kukimbilia.”



وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّـهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم ۖ مَّا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنتُم بِمُصْرِخِيَّ ۖ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ ۗ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٢﴾
22. Na shaytwaan atasema itakapokidhiwa jambo: “Hakika Allaah Alikuahidini ahadi ya haki (na Ameitimiza); nami nilikuahidini kisha nikakukhalifuni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu isipokuwa nilikuiteni mkaniitikia. Basi msinilaumu, bali laumuni nafsi zenu. Mimi siwezi kukusaidieni kukuokeeni wala nyinyi hamuwezi kunisaidia kuniokoa. Hakika mimi nilikanusha yale mliyonishirikisha zamani. Hakika madhalimu watapa adhabu iumizayo.”



وَأُدْخِلَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ ۖ تَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ﴿٢٣﴾
23. Na wataingizwa wale walioamini na wakatenda mema, Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo kwa idhini ya Rabb wao. Maamkizi yao humo yatakuwa ni “Salaam”.



أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ﴿٢٤﴾
24. Je, huoni vipi Allaah Amepiga mfano wa neno zuri kama mti mzuri mizizi yake imethibitika imara na matawi yake yanafika mbinguni? (marefu mno).



تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Unatoa mazao yake kila wakati kwa idhini ya Rabb wake. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu ili wapate kukumbuka.



وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ ﴿٢٦﴾
26. Na mfano wa neno baya ni kama mti mbaya uliong’olewa juu ya ardhi hauna imara.



يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚوَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾
27. Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo.



أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ﴿٢٨﴾
28. Je, huoni wale waliobadilisha neema ya Allaah kwa kufru, na wakawafikisha watu wao nyumba ya mateketezi?



جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا ۖ وَبِئْسَ الْقَرَارُ ﴿٢٩﴾
29. Jahannam watauingia na kuungua, na ubaya ulioje mahala pa kutulia.



وَجَعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلُّوا عَن سَبِيلِهِ ۗ قُلْ تَمَتَّعُوا فَإِنَّ مَصِيرَكُمْ إِلَى النَّارِ ﴿٣٠﴾
30. Na wakamfanyia Allaah walinganishi ili wapoteze (watu) na njia Yake. Sema: “Stareheni! (Na uhai mfupi); kwani hakika mahali penu pa kurudia hatimaye ni motoni.”



قُل لِّعِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا يُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خِلَالٌ ﴿٣١﴾
31. Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) waja Wangu ambao wameamini: Wasimamishe Swalaah na watoe katika yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri kabla haijafika Siku ambayo hakutakuweko biashara na wala rafiki wa kweli.



اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖوَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ﴿٣٢﴾
32. Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi, na Akateremsha maji kutoka mbinguni, Akataoa kwayo mazao kuwa ni riziki kwenu. Na Akakutiishieni majahazi ili zipitie baharini kwa amri Yake. Na Akakutiishieni mito.



وَسَخَّرَ لَكُمُ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ دَائِبَيْنِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ﴿٣٣﴾
33. Na Akakutiishieni jua na mwezi katika mwendo wa daima dawamu na Akakuitishieni usiku na mchana.



وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ﴿٣٤﴾
34. Na Akakupeni kila mnachomuomba. Na mkihesabu neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni.  Hakika insani ni mwingi wa dhulma, mwingi wa kukufuru akosaye shukurani.



وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا الْبَلَدَ آمِنًا وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ ﴿٣٥﴾
35. Na pindi Ibraahiym aliposema: “Ee Rabb wangu! Ujaalie mji huu (Makkah) uwe wa amani; na Uniepushe na wanangu kuabudu masanamu.”



رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ وَمَنْ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٣٦﴾
36. “Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza wengi kati ya watu.  Basi atakayenifuata, huyo ni katika mimi, na atakayeniasi, basi hakika Wewe ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.



رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾
37. “Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu. Rabb wetu, ili wasimamishe Swalaah na Ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru.”



رَبَّنَا إِنَّكَ تَعْلَمُ مَا نُخْفِي وَمَا نُعْلِنُ ۗ وَمَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِن شَيْءٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ﴿٣٨﴾
38. “Rabb wetu! Hakika Wewe Unajua tunayoyaficha na tunayoyadhihirisha. Na hakifichiki kitu chochote kwa Allaah katika ardhi wala katika mbingu.”



الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٩﴾
39. “AlhamduliLLaah, Ambaye Amenitunukia juu ya umri mkubwa wangu Ismaa’iyl na Is-haaq. Hakika Rabb wangu bila shaka ni Mwenye kusikia du’aa yangu.”



رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ﴿٤٠﴾
40. “Rabb wangu! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swalaah na dhuria wangu. Rabb wetu! Nitakabalie du’aa yangu.”



رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾
41. “Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu.”



وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّـهَ غَافِلًا عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ ۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ ﴿٤٢﴾
42. Na wala usidhanie kabisa kwamba Allaah Ameghafilika na yale wanayoyatenda madhalimu. Hakika Anawaakhirisha kwa ajili ya Siku ambayo macho yatakodoka (kwa kiwewe).


مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لَا يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ ۖ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ ﴿٤٣﴾
43. (Watakuwa) Wenye kukimbia huku shingo zao zimenyooka juu, macho yao hayapepesi; na nyoyo zao ni tupu (kwa kiwewe).



وَأَنذِرِ النَّاسَ يَوْمَ يَأْتِيهِمُ الْعَذَابُ فَيَقُولُ الَّذِينَ ظَلَمُوا رَبَّنَا أَخِّرْنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ نُّجِبْ دَعْوَتَكَ وَنَتَّبِعِ الرُّسُلَ ۗ أَوَلَمْ تَكُونُوا أَقْسَمْتُم مِّن قَبْلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٍ﴿٤٤﴾
44. Na waonye watu Siku itakayowafikia adhabu; wale waliodhulumu watasema: “Rabb wetu! Tuakhirishe mpaka muda mdogo ili tuitikie wito Wako na tuwafuate Rusuli.” (Wataambiwa): “Je, kwani hamkuwa mmeapa kabla kwamba hamtokuwa wenye kuondoshwa (duniani?).”



وَسَكَنتُمْ فِي مَسَاكِنِ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ وَتَبَيَّنَ لَكُمْ كَيْفَ فَعَلْنَا بِهِمْ وَضَرَبْنَا لَكُمُ الْأَمْثَالَ ﴿٤٥﴾
45. “Na mkakaa katika maskani ya wale waliodhulumu nafsi zao na ikakubainikieni vipi Tulivyowafanya, na Tukakupigieni mifano mingi?”



وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِندَ اللَّـهِ مَكْرُهُمْ وَإِن كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ﴿٤٦﴾
46. Na kwa yakini wakafanya mipango ya makri zao, na kwa Allaah kuna (rekodi ya) makri zao, na japokuwa makri  zao haziwezi kuondosha majabali.



فَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّـهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِ رُسُلَهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤٧﴾
47. Basi usidhanie kwamba Allaah ni Mwenye kukhalifu ahadi Yake kwa Rusuli Wake. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kulipiza.



يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ ۖ وَبَرَزُوا لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿٤٨﴾
48. Siku ardhi itakapobadilishwa kuwa ardhi nyingine na mbingu pia na (viumbe wote) watahudhuria kwa Allaah Mmoja Pekee, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Asiyepingika.



وَتَرَى الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ مُّقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ ﴿٤٩﴾
49. Na utawaona wahalifu Siku hiyo wamezongoreshwa katika minyororo.



سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٍ وَتَغْشَىٰ وُجُوهَهُمُ النَّارُ﴿٥٠﴾
50.  Mavazi yao ya chuma ni ya utomvu mweuzi wa lami, na moto utafunika nyuso zao.


لِيَجْزِيَ اللَّـهُ كُلَّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٥١﴾
51. Ili Allaah Alipe kila nafsi yale iliyoyachuma. Hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.



هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ﴿٥٢﴾
52. Hii (Qur-aan) ni ubalighisho wa risala kwa watu, na ili wawaonye kwayo, na ili wapate kujua kwamba hakika Yeye ni Muabudiwa wa haki Mmoja Pekee na ili wakumbuke (na wawaidhike) wenye akili.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.