-->
logo

005 - Al-Maaidah

الْمَائِدَة

Al-Maaidah: 5

Imeteremka Madiynah



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ





 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ الْأَنْعَامِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّي الصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ ﴿١﴾

1. Enyi walioamini! Timizeni mikataba. Imehalalishwa kwenu wanyama wa mifugo wanaopelekwa malishoni, isipokuwa mnaosomewa (humu) - kuwinda imeharamishwa (pia) mkiwa katika ihraam. Hakika Allaah Anahukumu Atakayo.





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحِلُّوا شَعَائِرَ اللَّـهِ وَلَا الشَّهْرَ الْحَرَامَ وَلَا الْهَدْيَ وَلَا الْقَلَائِدَ وَلَا آمِّينَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَانًا ۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَن تَعْتَدُوا ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢﴾

2. Enyi walioamini! Msihalifu utukufu wa ishara za Allaah, wala miezi mitukufu wala wanyama wanaopelekwa kuchinjwa, wala vigwe (vyao), wala (kuhalifu amani kwa) wanaoiendea Nyumba Tukufu (Makkah) wanatafuta fadhila kutoka kwa Rabb wao na radhi. Na mkishatoka kwenye ihraam windeni (mkitaka). Na wala isikuchocheeni chuki ya watu kwa vile walikuzuieni na Masjid-Al-Haraam ikakupelekeni kufanya uonevu. Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.





حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣﴾

3. Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake, na aliyenyongwa au aliyepigwa akafa, au aliyeporomoka, au aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama mwitu, isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa); na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa, na kupiga ramli kwa mishale. Hayo kwenu ni ufasiki. Leo wamekata tamaa wale waliokufuru katika Dini yenu; basi msiwaogope, na Niogopeni Mimi. Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. Basi atakayelazimika katika njaa kali bila kuinamia kwenye dhambi basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.[1]





يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٤﴾

4. Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: “Mmehalalishiwa vizuri na mlichowafunza wanyama au ndege wa kuwinda; mkiwafuga kuwafunza uwindaji, mnawafunza katika ambayo Amekufunzeni Allaah. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie Jina la Allaah. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.”





الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٥﴾

5. Leo mmehalalishiwa vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na wanawake walioimarisha sitara (wasiozini) miongoni mwa Waumini wanawake na wanawake walioimarisha sitara miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu; mtakapowapa mahari yao mkijistahi bila ya kuwa maasherati wala kuchukua hawara. Na yeyote atakayekanusha iymaan; basi kwa yakini imeporomoka ‘amali yake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٦﴾

6. Enyi walioamini!  Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah; osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni (kwa kupaka maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu hadi vifundoni. Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni. Na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akitoka msalani, au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji; basi tayammamuni (ikusudieni) ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki kukufanyieni magumu, lakini Anataka kukutwaharisheni na Akutimizieni neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.[2]





وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَاقَهُ الَّذِي وَاثَقَكُم بِهِ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٧﴾

7. Na kumbukeni neema ya Allaah juu yenu na fungamano Lake ambalo Amekufungamanisheni nalo mliposema: “Tumesikia na Tumetii.” Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani.







يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

8. Enyi walioamini!  Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah mkitoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki ya watu isikuchocheeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo. 





وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۙ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿٩﴾

9. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema; watapata maghfirah na ujira adhimu.





وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٠﴾

10. Na waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat Zetu, hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَن يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾

11. Enyi walioamini! Kumbukeni neema ya Allaah juu yenu, pale walipopania watu kukunyosheeni mikono yao (kukushambulieni), kisha Allaah Akazuia mikono yao isikufikieni. Na mcheni Allaah; na kwa Allaah pekee watawakali Waumini.





وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ۖ وَقَالَ اللَّـهُ إِنِّي مَعَكُمْ ۖ لَئِنْ أَقَمْتُمُ الصَّلَاةَ وَآتَيْتُمُ الزَّكَاةَ وَآمَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَلَأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ فَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ﴿١٢﴾

12. Na kwa yakini Allaah Alichukua fungamano la wana wa Israaiyl na Tukawapelekea miongoni mwao wakuu kumi na mbili. Na Allaah Akasema: Hakika Mimi Niko pamoja nanyi; mtakaposimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kuamini Rusuli Wangu, na kuwaunga mkono, na kumkopesha Allaah mkopo mzuri; bila shaka Nitakufutieni maovu yenu, na Nitakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Na yeyote atakayekufuru baada ya hapo miongoni mwenu; basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.





فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣﴾

13. Kwa sababu ya kuvunja kwao fungamano lao, Tuliwalaani na Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanageuza maneno (ya Allaah) kutoka mahali pake, na wakasahu sehemu ya yale waliyokumbushwa. Na utaendelea kupata khabari za khiyana kutoka kwao isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na achilia mbali. Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.[3]





وَمِنَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ اللَّـهُ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿١٤﴾

14. Na kwa wale waliosema: “Hakika sisi ni Naswara” Tulichukua fungamano lao, wakasahau sehemu ya yale waliyokumbushwa. Basi Tukapandikiza baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Atawajulisha waliyokuwa wakiyatenda.





يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

15. Enyi Ahlal-Kitaab! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anasamehe mengi. Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainisha.







يَهْدِي بِهِ اللَّـهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٦﴾

16. Allaah Anamwongoza kwa hicho (Kitabu) yeyote atayefuata radhi Zake katika njia za salama; na Anawatoa katika viza kuingia katika nuru kwa idhini Yake, na Anawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.





لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ أَن يُهْلِكَ الْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾

17. Kwa yakini, wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah Ndiye Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Sema: “Nani anayemiliki chochote mbele ya Allaah, Akitaka kumhilikisha Al-Masiyh mwana wa Maryam na mama yake na walioko ardhini wote? Na ufalme ni wa Allaah wa mbingu na ardhi na vyote vilivyo baina yake, Anaumba Atakacho. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.”





وَقَالَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَىٰ نَحْنُ أَبْنَاءُ اللَّـهِ وَأَحِبَّاؤُهُ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُم ۖ بَلْ أَنتُم بَشَرٌ مِّمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿١٨﴾

18. Na Mayahudi na Manaswara wamesema: “Sisi ni wana wa Allaah na vipenzi Vyake.” Sema: “Kwa nini basi Anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu miongoni mwa Alioumba. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na ufalme ni wa Allaah wa mbingu na ardhi na vyote vilivyo baina yake na Kwake Pekee ndio mahali pa kuishia.” 





يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ فَتْرَةٍ مِّنَ الرُّسُلِ أَن تَقُولُوا مَا جَاءَنَا مِن بَشِيرٍ وَلَا نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَاءَكُم بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٩﴾

19. Enyi Ahlal-Kitaab! Kwa yakini amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni (mambo) katika mkatizo wa Rusuli. Msije kusema: “Hakutujia mbashiriaji yeyote wala mwonyaji.” Kwa yakini amekujieni mbashiriaji na mwonyaji. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. 





وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنبِيَاءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكًا وَآتَاكُم مَّا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٠﴾

20. Na pindi Muwsaa alipoambia kaumu yake:  “Enyi kaumu yangu!  Kumbukeni neema ya Allaah juu yenu Alipojaalia miongoni mwenu Nabiy, na Akakufanyeni wenye kumiliki (na ufalme) na Akakupeni yale Asiyowahi kumpa yeyote miongoni mwa walimwengu.” ‏





يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿٢١﴾

21. “Enyi kaumu yangu! Ingieni ardhi iliyotakaswa ambayo Amekuandikieni Allaah kwenu, na wala msirudi kugeuka nyuma kukimbia (kupigana) hapo mtageuka kuwa wenye kukhasirika.” 





قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىٰ يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ ﴿٢٢﴾

22. Wakasema: “Ee Muwsaa! Hakika humo kuna watu majabari; nasi hatutoingia humo mpaka watoke humo; watakapotoka humo; basi hakika sisi tutaingia.”





قَالَ رَجُلَانِ مِنَ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِمَا ادْخُلُوا عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَالِبُونَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٣﴾

23. Wakasema watu wawili miongoni mwa wale waliokhofu (Allaah) ambao Allaah Aliowaneemesha: “Waingilieni katika mlango; mkiwaingilia, basi hakika nyinyi mtashinda. Na kwa Allaah tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini.”





قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا أَبَدًا مَّا دَامُوا فِيهَا ۖ فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ﴿٢٤﴾

24. Wakasema: “Ee Muwsaa!  Hakika sisi hatutoingia humo abadani madamu watabakia humo; basi nenda wewe na Rabb wako mkapigane, hakika sisi tunakaa hapa hapa.”





قَالَ رَبِّ إِنِّي لَا أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِي وَأَخِي ۖ فَافْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٥﴾

25. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu; basi Tutenganishe baina yetu na watu mafasiki.”





قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ ۛ أَرْبَعِينَ سَنَةً ۛ يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. (Allaah) Akasema: “Basi hakika ardhi hiyo imeharamishwa kwao miaka arubaini; watatangatanga ardhini. Basi usisikitike juu ya watu mafasiki.”





وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾

27. Na wasomee khabari za wana wawili wa Aadam; kwa haki walipotoa dhabihu ya kafara ikakubaliwa ya mmoja wao, na haikukubaliwa ya mwengine; (asiyekubaliwa) akasema: “Bila shaka nitakuua.” (Aliyekubaliwa) Akasema: “Hakika Allaah Anatakabalia wenye taqwa.”





لَئِن بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِي مَا أَنَا بِبَاسِطٍ يَدِيَ إِلَيْكَ لِأَقْتُلَكَ ۖ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾

28. “Ukininyoshea mkono wako ili uniue, mimi sitokunyoshea mkono wangu kukuua; hakika mimi namkhofu Allaah Rabb wa walimwengu.”





إِنِّي أُرِيدُ أَن تَبُوءَ بِإِثْمِي وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾

29. “Hakika mimi nataka urudi na ubebe dhambi zangu na dhambi zako hapo utakuwa miongoni mwa watu wa motoni; na hiyo ndiyo jazaa ya madhalimu.”





فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٣٠﴾

 30. Basi nafsi yake ikamwezesha kwa wepesi kumuua ndugu yake; akamuua na akawa miongoni mwa waliokhasirika.





فَبَعَثَ اللَّـهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الْأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَا وَيْلَتَىٰ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءَةَ أَخِي ۖ فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ ﴿٣١﴾

31. Kisha Allaah Akamleta kunguru akifukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi asitiri maiti ya ndugu yake. (Muuaji) Akasema: “Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa mimi kama huyu kunguru nikamsitiri ndugu yangu?” Akawa miongoni mwa wajutao.





مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ ﴿٣٢﴾

32. Kwa ajili ya hivyo, Tukawaandikia shariy’ah wana wa Israaiyl kwamba; atakayeiua nafsi bila ya nafsi (kuua), au kufanya ufisadi katika ardhi; basi ni kama ameua watu wote. Na atakayeiokoa kuihuisha, basi ni kama amewaokoa watu wote. Na bila shaka walifikiwa na Rusuli Wetu kwa hoja bayana; kisha wengi miongoni mwao baada ya hayo wamekuwa wapindukao mipaka ya kuasi.





إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٣٣﴾

33. Hakika jazaa ya wale wanaompiga vita Allaah na Rasuli Wake na wanafanya bidii kufanya ufisadi katika ardhi; ni kwamba wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha au watolewe katika nchi. Hiyo ndiyo hizaya yao duniani. Na Aakhirah watapata adhabu kuu.[4]





إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Isipokuwa wale waliotubia kabla ya kuwashinda nguvu basi jueni kwamba hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾

35. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni njia za kumkurubia; na fanyeni jihaad katika njia Yake ili mpate kufaulu.





إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لِيَفْتَدُوا بِهِ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنْهُمْ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٣٦﴾

36. Hakika wale waliokufuru, kama watakuwa na yale yote yaliyomo ardhini na mengineyo mfano kama hayo, ili watoe fidia kwayo kuepukana na adhabu ya Siku ya Qiyaamah, hayatokubaliwa kutoka kwao, na watapata adhabu iumizayo.





يُرِيدُونَ أَن يَخْرُجُوا مِنَ النَّارِ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنْهَا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ ﴿٣٧﴾

37. Watataka kutoka katika moto, lakini wao hawatatoka kamwe humo, na watapata adhabu ya kudumu.





وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٣٨﴾

38. Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke ikateni (kitanga cha) mikono yao; ni malipo kwa yale waliyoyachuma, ndio adhabu ya kupigiwa mfano kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.





فَمَن تَابَ مِن بَعْدِ ظُلْمِهِ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ اللَّـهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٩﴾

 39. Lakini atakayetubia baada ya dhulma yake na akatengenea basi hakika Allaah Atapokea tawbah yake. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.





أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٤٠﴾

40. Je, hujui ya kwamba Allaah Anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humwadhibu Amtakae na Humghufiria Amtakae. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.





يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ مِنَ الَّذِينَ قَالُوا آمَنَّا بِأَفْوَاهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ الَّذِينَ هَادُوا ۛ سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّاعُونَ لِقَوْمٍ آخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ مِن بَعْدِ مَوَاضِعِهِ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَاحْذَرُوا ۚ وَمَن يُرِدِ اللَّـهُ فِتْنَتَهُ فَلَن تَمْلِكَ لَهُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَمْ يُرِدِ اللَّـهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٤١﴾

41. Ee Rasuli, wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru miongoni mwa wasemao kwa midomo yao: “Tumeamini” na hali nyoyo zao hazikuamini. Na miongoni mwa Mayahudi wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya uongo, wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia. Wanageuza maneno kutoka mahali pake; wanasema: “Mkipewa haya basi yachukueni, na msipopewa hayo basi jihadharini!” Na yule ambaye Allaah Anataka kumtia mtihanini, hutokuwa na uwezo wowote (kusaidia) kwa ajili yake mbele ya Allaah. Hao ndio ambao Allaah Hakutaka kuzitakasa nyoyo zao. Watapata hizaya duniani na Aakhirah watapata adhabu kuu.[5]





سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْئًا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٤٢﴾

42. (Hao) Wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji kwa pupa ya haramu. Basi wakikujia wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, hawatoweza kukudhuru chochote. Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu.[6]





وَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ التَّوْرَاةُ فِيهَا حُكْمُ اللَّـهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٣﴾

43. Na vipi watakufanya wewe kuwa hakimu wao na hali wana Tawraat iliyomo ndani yake hukumu ya Allaah; kisha baada ya hayo wanakengeuka. Na hao si wenye kuamini.





إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾

44. Hakika Tumeteremsha Tawraat humo mna mwongozo na nuru; ambayo kwayo, Nabiy waliojisalimisha (kwa Allaah), waliwahukumu Mayahudi. Na (kadhalika) wanachuoni waswalihina na wanachuoni mafuqahaa wa dini kwa sababu waliyokabidhiwa kuhifadhi Kitabu cha Allaah; na wakawa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali Niogopeni Mimi, na wala msibadilishe Aayaat Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.





وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾

45. Na Tumewaandikia shariy’ah humo kwamba uhai kwa uhai, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino; na majaraha ni kisasi. Lakini atakayesamehe kwa kutolea swadaqah basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.





وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na Tukatuma kufuatisha nyao zao (Manabii hao), ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl iliyomo ndani yake mwongozo na nuru; na isadikishayo yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.





وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na watu wa Injiyl wahukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah ndani yake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.





وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ ۚ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha Vitabu vilivyokuwa kabla yake na chenye kudhibiti, kushuhudia na kuhukumu juu yake (hivyo Vitabu). Basi hukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah; na wala usifuate hawaa zao kwa kuacha haki iliyokujia. Kwa kila (ummah) katika nyinyi Tumeujaalia shariy’ah na manhaj. Na kama Angetaka Allaah Angelikufanyeni ummah mmoja; lakini ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Basi shindaneni katika khayraat. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote; kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkikhitilafiana.





وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ ﴿٤٩﴾

49. Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, na wala usifuate hawaa zao, na tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya yale Aliyokuteremshia Allaah. Na wakikengeuka, basi jua kuwa hakika Allaah Anataka kuwasibu kwa baadhi ya madhambi yao. Na hakika wengi katika watu ni mafasiki.





أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾

50. Je, wanataka hukumu za kijahiliya? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥١﴾

51. Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.





فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ ۚ فَعَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ ﴿٥٢﴾

52. Basi utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi (ya unafiki) wanakimbilia kwao wakisema: “Tunakhofu usitusibu mgeuko. Basi asaa Allaah Akaleta ushindi au jambo (jengine) litokalo Kwake; wakawa wenye kujuta kwa waliyoyaficha katika nafsi zao.





وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ ﴿٥٣﴾

 53. Na wale walioamini wanasema: “Je, hawa ndio wale ambao waliapa kwa Allaah kwa viapo vyao vya nguvu, kwamba hakika wao wapo pamoja nanyi?” Zimeporomoka ‘amali zao, na wamekuwa wenye kukhasirika.





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

54. Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.





إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾

55. Hakika Mlinzi wenu ni Allaah na Rasuli Wake na wale walioamini, ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah na hali ya kuwa wananyenyekea.





وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٥٦﴾

56. Na atakayemfanya Allaah kuwa ni Mlinzi na Rasuli Wake na wale walioamini, basi hakika kundi la Allaah ndio washindi.





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٥٧﴾

57. Enyi walioamini!  Msiwafanye wale walioifanya Dini yenu mzaha na mchezo - miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu, na makafiri kuwa marafiki wandani. Na mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini.





وَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ اتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ﴿٥٨﴾

58. Na mnapoita kuadhini Swalaah; huifanyia mzaha na mchezo. Hivyo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotia akilini.





قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ أَكْثَرَكُمْ فَاسِقُونَ ﴿٥٩﴾

59. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab Je, mnatuchukia tu kwa vile tumemwamini Allaah na yale yaliyoteremshwa kwetu na yale yaliyoteremshwa kabla; na kwamba wengi wenu ni mafasiki?”





قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ ۚ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٦٠﴾

60. Sema: “Je, nikujulisheni la shari zaidi kuliko hayo kwa malipo (mabaya) mbele ya Allaah? Yule ambaye Allaah Amemlaani na Akamghadhibikia na Akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na wakaabudu twaghuti hao wana mahali pabaya mno (Aakhirah) na wapotofu zaidi na njia iliyo sawa (duniani).”





وَإِذَا جَاءُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَقَد دَّخَلُوا بِالْكُفْرِ وَهُمْ قَدْ خَرَجُوا بِهِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا كَانُوا يَكْتُمُونَ ﴿٦١﴾

61. Na wanapokujieni husema: “Tumeamini.” Na hali wameingia na ukafiri na wakatoka nao. Na Allaah Anajua zaidi yale waliyokuwa wakiyaficha.





وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٢﴾

62. Na utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia katika dhambi na uadui na kula kwao haramu. Bila shaka mabaya mno waliyokuwa wanatenda.





لَوْلَا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿٦٣﴾

63. Mbona hawawakatazi wanachuoni waswalihina na wanachuoni mafuqahaa wa dini kuhusu kauli zao za dhambi na ulaji wao wa haramu. Bila shaka mabaya mno waliyokuwa wanatimiliza.





وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۚ وَأَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ كُلَّمَا أَوْقَدُوا نَارًا لِّلْحَرْبِ أَطْفَأَهَا اللَّـهُ ۚ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا ۚ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٦٤﴾

64. Na Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” Mikono yao ndio iliyofumbwa; na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali Mikono Yake (Allaah) imefumbuliwa Hutoa Atakavyo. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Na Tumewatilia baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Kila wanapouwasha moto wa vita (dhidi yako), Allaah Huuzima. Na wanafanya bidii kufanya ufisadi katika ardhi. Na Allaah Hapendi mafisadi.





وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَكَفَّرْنَا عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأَدْخَلْنَاهُمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٦٥﴾

65. Na lau kama Ahlal-Kitaab wangeamini na wakawa na taqwa, bila shaka Tungeliwafutia maovu yao, na bila shaka Tungeliwaingiza katika Jannaat za neema.





وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ ﴿٦٦﴾

66. Na lau kama wangeliisimamisha Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Rabb wao; bila shaka wangelikula (rizki) kutoka juu yao na chini ya miguu yao. Miongoni mwao ni watu walioko katika njia ya sawa na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno.





يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

67. Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri.[7]





قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾

68. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab! Hamko juu ya chochote mpaka muisimamishe kutekeleza Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Rabb wenu.” Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Basi usisikitike juu ya watu makafiri.





إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٩﴾

69. Hakika wale walioamini na wale (kabla ya Uislamu;) Mayahudi na Masabii na Manaswara, atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho na akatenda mema, basi hawatokuwa na khofu na wala hawatohuzunika





لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَأَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ رُسُلًا ۖ كُلَّمَا جَاءَهُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ ﴿٧٠﴾

70. Kwa yakini Tulichukua fungamano la wana wa Israaiyl na Tukawapelekea Rusuli. Basi kila alipowajia Rasuli kwa yale yasiyopenda nafsi zao; kundi waliwakadhibisha na kundi wakawaua.





وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٧١﴾

71. Na walidhani kwamba haitokuwa fitnah (mitihani au adhabu), basi wakawa vipofu na wakawa viziwi; kisha Allaah Akapokea tawbah yao; kisha tena wengi wao wakawa vipofu na wakawa viziwi. Na Allaah ni Mwenye kuona yale wayatendayo.





لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

72. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.”





لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

73. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Na hali hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.





أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧٤﴾

74. Je, hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfirah? Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.





مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٧٥﴾

75. Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Rasuli (tu); bila shaka wamekwishapita kabla yake Rusuli (wengine). Na mama yake ni aliyeamini na mkweli khasa. Wote wawili walikuwa wanakula chakula. Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayaat kisha tazama vipi wanavyoghilibiwa.





قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٧٦﴾

76. Sema: “Vipi mnaabudu asiyekuwa Allaah asiyekuwa na uwezo wa kukudhuruni wala kukunufaisheni! Na Allaah Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.”





قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ غَيْرَ الْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوا أَهْوَاءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا كَثِيرًا وَضَلُّوا عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٧٧﴾

77. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab! Msipindukie mipaka katika dini yenu bila ya haki; na wala msifuate hawaa za watu waliokwishapotea kabla na wakapotosha wengi na wakapotea njia iliyo sawa.”





لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾

78. Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.





كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾

79. Walikuwa hawakatazani munkari waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya.





تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ ﴿٨٠﴾

80. Utawaona wengi miongoni mwao wanawafanya marafiki wandani wale waliokufuru. Ubaya ulioje yale yaliyowatangulizia nafsi zao, ndipo Allaah Amewaghadhibikia na katika adhabu wao watadumu.





وَلَوْ كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٨١﴾

81. Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wandani, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.





لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٨٢﴾

82. Bila shaka utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa wale walioamini, ni Mayahudi na wale washirikina. Na bila shaka utawakuta walio karibu zaidi kimapenzi kwa Waumini ni wale wanaosema: “Sisi ni Manaswara.” Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Makasisi na Wamonaki wenye uchaji na kwamba wao hawatakabari.[8]





وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾

83. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema: “Rabb wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.”





وَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾

84. “Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Rabb wetu Atuingize (Jannah) pamoja na Swalihina?”





فَأَثَابَهُمُ اللَّـهُ بِمَا قَالُوا جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٥﴾

85. Basi Allaah Akawalipa thawabu kwa yale waliyoyasema, Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya wafanyao ihsaan.





وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٨٦﴾

86. Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha Aayaat Zetu hao ni watu wa moto uwakao vikali mno. 





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٨٧﴾

87. Enyi walioamini! Msiharamishe vizuri Aliyokuhalalishieni Allaah, na wala msipindukie mipaka. Hakika Allaah Hapendi wapindukao mipaka. 







وَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na kuleni katika vile Alivyowaruzuku Allaah vya halali na vizuri. Na mcheni Allaah Ambaye nyinyi mnamwamini. 





لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾

89. Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu (msiape kila mara). Hivyo ndivyo Allaah Anavokubainishieni Aayaat (na hukmu) Zake ili mpate kushukuru.[9]







يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

90. Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; ni najisi na chukizo kutokana na kitendo cha shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.[10]





إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

91. Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah; basi je mtakoma?





وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٩٢﴾

92. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli na tahadharini! Mkikengeuka, basi jueni kwamba juu ya Rasuli Wetu ni kubalighisha ujumbe tu ulio bayana.







لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا وَّآمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ثُمَّ اتَّقَوا وَّآمَنُوا ثُمَّ اتَّقَوا وَّأَحْسَنُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٣﴾

93. Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharimishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini na wakatenda mema; kisha wakawa na taqwa na wakaamini, kisha wakawa na taqwa na wakafanya ihsaan. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.[11]





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَيَبْلُوَنَّكُمُ اللَّـهُ بِشَيْءٍ مِّنَ الصَّيْدِ تَنَالُهُ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَخَافُهُ بِالْغَيْبِ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٩٤﴾

94. Enyi walioamini! Bila shaka Allaah Atakujaribuni kwa baadhi ya wanyama wa kuwinda inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Allaah Ajue mwenye kumkhofu kwa ghayb. Na atakayetaadi baada ya hayo, basi atapata adhabu iumizayo. 





يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّـهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّـهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾

95. Enyi walioamini! Msiue mawindo na hali mko katika ihraam. Na atakayemuua (mnyama) miongoni mwenu kwa kusudi, basi malipo yake itakuwa ni kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wa mifugo. Kama wanavyohukumu wawili wenye uadilifu miongoni mwenu. Mnyama huyo afikishwe Ka’bah, au kafara ya kulisha maskini, au badala ya hayo, kufunga swiyaam ili aonje matokeo maovu ya jambo lake. Allaah Ameshasamehe yaliyopita; na yeyote atakayerudia tena, basi Allaah Atamlipiza (kumuadhibu). Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kulipiza.







أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩٦﴾

96. Mmehalalishiwa mawindo ya bahari na chakula chake ni manufaa kwenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu mtakuwa katika ihraam. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mtakusanywa.





جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ وَالشَّهْرَ الْحَرَامَ وَالْهَدْيَ وَالْقَلَائِدَ ۚ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٩٧﴾

97. Allaah Amejaalia Ka’bah Nyumba Tukufu kuwa tegemeo la watu, na miezi mitukufu na wanyama wa kafara na vigwe. Hivyo ili mpate kujua kuwa Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini na kwamba Allaah ni kwa kila kitu Mjuzi. 







اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٨﴾

98. Jueni kuwa Allaah ni Mkali wa kuakibu na kwamba Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.





مَّا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ﴿٩٩﴾

99. Hapana (jukumu) juu ya Rasuli ila ubalighisho (wa risala). Na Allaah Anayajua yale mnayoyadhihirisha na yale mnayoyaficha.







قُل لَّا يَسْتَوِي الْخَبِيثُ وَالطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ الْخَبِيثِ ۚ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Sema: “Haviwi sawasawa viovu na vizuri japokuwa utakupendezea wingi wa viovu.” Basi mcheni Allaah, enyi wenye akili ili mpate kufaulu.







يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

101. Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mvumilivu.[12]





قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ ﴿١٠٢﴾

102. Walikwishayauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha kutokana nayo, wakawa makafiri.







مَا جَعَلَ اللَّـهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَـٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٠٣﴾

103. Allaah Hakufanya (uharamu wa) bahiyrah (ngamia aliyezaa matumbo matano), wala saaibah (ngamia aliyeachiliwa kwa nadhiri), wala waswiylah (kondoo aliyezaa matumbo saba), wala haam (fahali lililozalisha matumbo kumi), lakini wale waliokufuru wanamtungia Allaah uongo, na wengi wao hawatumii akili.







وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٠٤﴾

104. Na wanapoambiwa: “Njooni katika yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli” Husema: “Yanatutosheleza yale tuliyowakuta nayo baba zetu.” Je, japokuwa walikuwa baba zao hawajui chochote na wala hawakuongoka?







يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka. Kwa Allaah Pekee ni marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.







يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ ﴿١٠٦﴾

106. Enyi walioamini! Mauti yanapomfikia mmoja wenu wakati anapousia, basi chukueni ushahidi wa wawili wenye uadilifu miongoni mwenu; au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi pale mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa mauti. Muwazuie baada ya Swalaah, na waape kwa Allaah mkitilia shaka, (waseme): “Hatutovibadilisha (viapo vyetu) kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa karibu. Na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah, kwani hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi.”[13]





فَإِنْ عُثِرَ عَلَىٰ أَنَّهُمَا اسْتَحَقَّا إِثْمًا فَآخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ الَّذِينَ اسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْأَوْلَيَانِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ لَشَهَادَتُنَا أَحَقُّ مِن شَهَادَتِهِمَا وَمَا اعْتَدَيْنَا إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٧﴾

107. Ikigundilikana kwamba hao wawili wana hatia ya dhambi, basi wawili wengine wasimame mahali pao, wanaostahiki kudai haki ki-shariy’ah, walio karibu zaidi (na mrithiwa); kisha waape kwa Allaah: “Bila shaka ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wawili wao; nasi hatukufanya taksiri; kwani bila shaka hapo sisi tutakuwa miongoni mwa madhalimu.”





ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo au watakhofu visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na mcheni Allaah na sikizeni!  Na Allaah Haongoi watu mafasiki.[14]





يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١٠٩﴾

109. Siku Allaah Atakayowakusanya Rusuli na Kuwaambia: “Mlijibiwa nini?” Watasema: “Hatuna ujuzi nalo; hakika Wewe Ndiye Mjuzi wa ghayb.”







إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٠﴾

110. (Siku) Allaah Ataposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kumbuka neema Yangu juu yako na juu ya mama yako; Nilipokusaidia kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام; unasemesha watu katika utoto na utu uzimani; na Nilipokufunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl; na ulipounda kutokana na udongo kama umbo la ndege kwa idhini Yangu; ukapulizia likawa ndege kwa idhini Yangu; na ulipowaponyesha vipofu na ubarasi kwa idhini Yangu; na ulipowafufua wafu kwa idhini Yangu; na Nilipowazuia wana wa Israaiyl dhidi yako, ulipowajia kwa hoja bayana; wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: ‘Haya si chochote ila ni sihiri bayana.’’





وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾

111. Na Nilipowatia ilhamu wafuasi watiifu kwamba: Niaminini Mimi na Rasuli Wangu. Wakasema: “Tumeamini na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu.”







إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾

112. Pindi waliposema wafuasi watiifu: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, Anaweza Rabb wako Kututeremshia meza iliyotandazwa chakula kutoka mbinguni?” Akasema: “Mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini.”







قَالُوا نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿١١٣﴾

113. Wakasema: “Tunataka kula katika hicho; na ili nyoyo zetu zitulie; na tujue kwamba kwa yakini umetuambia kweli; na tuwe juu yake miongoni mwa wanaoshuhudia.”





قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾

114. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: “Ee Allaah, Rabb wetu, Tuteremshie meza iliyotandazwa chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu; na iwe Aayah (ishara, hoja) itokayo Kwako; basi Turuzuku; kwani Wewe ni Mbora wa wenye kuruzuku.”





قَالَ اللَّـهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿١١٥﴾

115. Akasema Allaah: “Hakika Mimi Nitaiteremsha kwenu; Lakini atakayekufuru miongoni mwenu baada ya hapo; basi hakika Nitamuadhibu adhabu ambayo Sitomuadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.”







وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾

116. Na pindi Allaah Atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!  Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah?” (‘Iysaa) Atasema: “Subhaanak! (Utakasifu ni Wako) hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua; Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu; na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako; hakika Wewe ni Mjuzi wa ghayb.”





مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾

117. “Sijawaambia (lolote) ila yale Uliyoniamrisha kwayo kwamba: Mwabuduni Allaah Rabb wangu na Rabb wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponichukua kikamilifu juu Ulikuwa Wewe Mwangalizi juu yao. Na Wewe juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia.”





إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

118. “Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.”





قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾

119. Allaah Atasema: “Hii ndiyo Siku itakayowafaa Asw-Swaadiqiyna ukweli wao; watapata Jannaat zipitazo chini yake mito; ni wenye kudumu humo abadi.  Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Huko ni kufuzu adhimu.”





لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٢٠﴾

120. Ni wa Allaah ufalme wa mbingu na ardhi na yale yote yaliyomo humo.  Naye juu ya kila kitu ni Muweza.








[1]Faida: ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Myahudi mmoja alimwambia: Ewe Amiri wa Waumini, lau ingeliteremka kwetu sisi Aayah hii “Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu.” (5: 3) tungeliifanya ‘Iyd siku hiyo. ‘Umar akasema: Wa-Allaahi, naijua siku gani imeteremka Aayah hii. Imeteremka Siku ya ‘Arafah siku ya Ijumaa. [Al-Bukhaariy].

[2]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa kama ilivyoelezewa katika tanbihi ya Aayah (4: 43) kuhusiana na hukmu ya tayammum.

[3]An-Naasikh Wal-Mansuwkh:  Kufutwa hukmu ya kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi wasamehe na achilia mbali. Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.” Amri ya kuwasamehe baada ya kuvunja kwao ahadi na fungamano na kufanya khiyana, imefutwa na Aayaat za As-Sayf (upanga); “Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki…” (9: 29) kwa kuwa baada ya hapo waliamrishwa kupigana jihaad na Makafiri.



[4]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa baada ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotuma watu waliokuwa mahodari wa kufuatilia na kukamata wakaletwa kwake. Hapo Allaah (تبارك وتعالى) Akateremsha: “Hakika jazaa ya wale wanaompiga vita Allaah na Rasuli Wake na wanafanya bidii kufanya ufisadi katika ardhi…” (5: 33) [Amehadithia Anas bin Maalik (رضي الله عنه) ameipokea Abuu Daawuwd katika Kitaab Al-Huduwd].



Faida: Maana ya kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha”; ni kukatwa mikono ya kulia kwa miguu ya kushoto au miguu ya kushoto kwa mikono ya kulia.

[5]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba: Myahudi mmoja aliyejaa weusi usoni na aliyepigwa mijeledi alipita kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita akaumuuliza: “Je, hivyo ndivyo mlivyokuta (shari’yah) katika Kitabu chenu kuhusu hadd ya mzinifu?” Wakasema: Ndio. Akamwita mtu mmoja miongoni mwa wanachuoni wao akasema: “Nakuuliza kwa kuapia Jina la Allaah Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa; je, hivyo ndivyo mnavyokuta hadd ya mzinifu katika Kitabu chenu?” Akasema: Hapana! Usingeniuliza hilo kwa kuapia Jina la Allaah, nisingelikuelezea. (Ni kweli) Tunaikuta Ar-Rajm (adhabu ya kupigwa mawe mpaka kufa) kama ilivyo shari’yah katika Tawraat lakini jarima imezoeleka kwa watu wetu wenye hadhi tu. Hivyo, tunapomkamata tajiri (aliyezini) tunamuachia (huru), lakini tukimkamata aliye duni tunamsimamishia adhabu ya hadd. Kisha tukasema: Njooni tukubaliane (adhabu) tutakayoisimamisha kwa wote; matajiri na walio duni. Hivyo tukaamua kumpaka (mzinifu) masinzi usoni na kumpiga mijeledi badala ya rajm. Hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Allaah, hakika mimi wa kwanza kuihuisha amri Yako wakati wao (Mayahudi) wameifisha. Basi akaamrisha, na (mhalifu huyo) akasimamishiwa rajm. Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: “Ee Rasuli, wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru… (mpaka kauli ya): “Mkipewa haya basi yachukueni.” (5: 41) Ikasemwa na Mayahudi: Nendeni kwa Muhammad, akikuamrisheni kukupakeni masinzi na kupigwa mijeledi basi pokeeni, lakini akikupeni hukumu ya rajm, basi tahadharini (jiepusheni). Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: “Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri” (5: 44). “Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (5: 45). “Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (5: 47) Aayah zote hizo (5: 41 – 47) zimeteremshwa kuwahusu makafiri.



[6]Sababun-Nuzuwl: Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba: Walikuweko Quraydhwah na An-Nadhwiyr (makabila ya Mayahudi Madiynah). An-Nadhwiyr walikuwa wenye hadhi zaidi kuliko Quraydhwah. Ikawa pale mtu wa Quraydhwah anapoua mtu wa An-Nadhwiyr, huuliwa, lakini inapokuwa mtu wa An-Nadhwiyr ameua mtu wa Quraydhwah huitwa akapigwa mikaanga mia ya mitende kama diya. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotumwa kuwa ni Rasuli, mtu mmoja wa An-Nadhwiyr alimuua mtu wa Quraydhwah wakasema: Mleteni kwetu tumuue! Wakajibu: Sasa baina yetu na yenu yupo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) basi mleteni (atuhukumu)! Hapo ikateremka: “Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu” (5: 42) Na uadilifu ni (kisasi cha) nafsi kwa nafsi. Kisha ikateremka: “Je, wanataka hukumu ya kijaahiliyyah?” (5: 50) [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan na wengineo] Ibn Kathiyr amesema: Inaweza kuwa zimejumuika sababu mbili hizi (5: 41-42) kwa wakati mmoja zikateremka Aayaat hizo kuhusu hayo na Allaah Mjuzi zaidi.





[7]Sababun-Nuzuwl: Kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu.” Imeteremka pale Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliposhuka chini ya kivuli cha mti na akalitundika panga lake juu ya huo mti kisha akasinzia. Bedui mmoja akamjia akiwa katika hali ya usingizi, akalikamata panga la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha akamuamsha, akamwambia huku amelishika panga lake juu: Nani ana uwezo wa kunizuia nisikuue? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu yule bedui: “Allaah Ndiye mwenye uwezo wa kukuzuia.” Hapo ikateremka kauli hii ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu.” (5: 67)  [Amehadithia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) - Ameipokea Ibn Hibbaan].

Faida: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametimiza Risala: Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliifikisha na kuitangaza Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى) na akaieneza da’wah yake mpaka ikawafikia majini na watu.  Na akawafundisha yote aliyoyaweka Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni shariy’ah. Akausimamia uwajibu huu kwa nguvu zote, na Allaah (سبحانه وتعالى) Hakumfisha mpaka Alipoinyoosha kupitia yeye dini iliyopindishwa na Akayafungua kupitia yeye macho yenye upofu na kuzifungua nyoyo zilizokuwa zimefunikwa na ujinga.



[8]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii na zinazofuatia (5: 82-85) zimeteremshwa kuhusu An-Najaashiy ambaye alikuwa mfalme wa Habash pamoja na watu wake. Aliwakilisha wajumbe wamwendee Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili wamsikilize maneno yake na watambue sifa zake. Walipokutana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na akawasomea Qur-aan, waliingia Uislamu wakalia na kunyenyekea. Kisha wakarudi kwa An-Najaashiy kumjulisha yaliyojiri. [Athaar kutoka kwa Saiy’d bin Jubayr, As-Suddi na wengineo – Tafsiyr Ibn Kathiyr].



Sababun-Nuzuwl: Pia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Waislamu walipohajiri kutoka Makkah kwenda Habash wakiwa katika uongozi wa Ja’far bin Abiy Twaalib na Ibn Mas’uwd (رضي الله عنهم), walimkuta mfalme wao An-Najaashiy akiwa mkarimu na mwenye huruma kwao. Akawauliza kama wana chochote cha Wahyi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Walipomsomea Aayaat za Qur-aan wakati alikuwa pamoja na makasisi na wamonaki wake, wakamiminikwa na machozi kutokana na kutambua haki. Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: “Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Makasisi na Wamonaki na kwamba wao hawatakabari. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki…” (5: 82-84). Na katika riwaayah nyengine: “Ja’far (رضي الله عنه) aliwasomea Suwrat Maryam wakamiminkwa machozi…”

[9]Sababun-Nuzuwl: Kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu.” (5: 89) Imeteremka kutokana na mtu alikuwa akilisha familia yake chakula kingi cha kutosheleza, lakini akilisha wengine chakula hafifu kisichotoleza. Hapo ikateremshwa: “cha wastani mnachowalisha ahli zenu.” [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Ibn Maajah].



[10]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa kuwa ni haramisho la mwisho kunywa pombe. Rejea tanbihiaat za (2: 219), (4: 43) ambako kuna maelezo bayana ya Sababun-Nuzuwl ya Aayah hii. Baada ya kuteremshwa Aayah hii, hapo hapo Swahaba wakaacha moja kwa moja kulewa ikawa ndio kikomo cha kunywa pombe.



Sababun-Nuzuwl: Pia, Imeteremshwa kuhusu makabila mawili katika Answaar walipokunywa pombe mpaka wakalewa mno kisha wakagombana na kuchafuana baadhi yao kwa baadhi mpaka athari zikawa zinaonekana katika nyuso zao. Kisha pale ulevi ulipowaondokea na akili zao zikawarejea, viliingia vinyongo katika nyoyo zao, hapo ikateremka Aayah hii inayoharamisha pombe moja kwa moja: “Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; ni najisi na chukizo kutokana na kitendo cha shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.” (5: 90). [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) – amepokea Ibn Jariyr].



[11]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa baada ya kuteremshwa Aayah ya uharamisho wa pombe moja kwa moja (5: 90). Kisha baadhi ya Swahaba wakasema kuwa watu wengi wamefariki wakiwa wana pombe matumboni mwao, wakataka hukmu yake, hapo ikateremka Aayah hii: “Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharimishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini na wakatenda mema;…” (5: 93). [Amehadithia Anas (رضي الله عنه), wameipokea; Al-Bukhaariy na Muslim]





[12]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa kwa sababu ya wingi wa maswali waliyokuwa wakiuliza watu katika hali na wakati mbali mbali; ima kwa istihzaa au mitihani iliyowasibu au kwa talbiys (kufunika haki na kuipotosha). Mfano pale ilipoteremka Aayah ya kuwajibika Hajj: “Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba…” (3: 97) akashikilia mtu kuuliza kuhusu kuwajibika Hajj kama inawajibikia kila mwaka, jambo ambalo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) angejibu kuwa “Naam”, basi ingewajibikia kisha hapo ingekuwa ni amri na jambo gumu mno kulitekeleza. [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo].



Sababun-Nuzuwl: Pia, kama alivyohadithia Anas bin Maalik (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoa khutbah ambayo sijapatapo kuisikia kama hiyo kisha akasema: “Mngelikuwa mnayajua yale ninayoyajua, basi mngelicheka kidogo na mngelilia sana.” Waliposikia hivyo Swahaba wa Rasuli wa Allaah walijifunika nyuso zao wakalia mpaka sauti za vilio vyao vikasikika. Kisha mtu mmoja hapo akamuuliza: Nani baba yangu? Akamjibu: “Fulani.” Hapo ikateremka Aayah hii: “Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni…” (5:  101) [Al-Bukhaariy].  



Sababun-Nuzuwl: Pia Anas (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku moja walianza kumuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maswali mengi mpaka akaghadhibika akapanda minbar akasema: “Hamtaniuliza lolote leo ila nitawajibu tu.” Nikatazama kuliani na kushotoni nikaona kila mtu amejifunika uso wake kwa nguo akilia. Hapo alikuweko mtu mmoja ambaye kila alipogombana na wenziwe aliitwa ‘mwana wa fulani asiyekuwa ni baba yake’. Akamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah, nani baba yangu? Akasema: “Hudhaafah.” Hapo ‘Umar akainuka akasema: Tumeridhika na Allaah kuwa ni Rabb, na Uislamu kuwa Dini, na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni Rasuli. Tunajikinga kwa Allaah na fitnah! Hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Sijapatapo kuona khayr au shari kama siku ya leo, kwani imedhihirishwa mbele yangu Jannah na moto hadi kwamba nimeviona viwili hivi nyuma ya ukuta.”  Qataadah alipokuwa akihadithia Hadiyth hii alikuwa akitaja Aayah hii: “Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni…” (5: 101) [Al-Bukhaariy].







[13]An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Kufutwa hukmu kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi.” Imefutwa baada ya kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allaah.” [Atw-Twalaaq (65: 2)].

[14]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa pamoja na Aayah mbili kabla yake (5: 106-107) pale bwana mmoja katika Baniy Sahm alitoka pamoja na Tamiym  Ad-Daariy na ‘Adiyy kisha katika msafara wao akafariki huyu mtu ambaye ni katika Baniy Sahm, na walikuwa katika kijiji ambacho hakuna Muislamu. Pale waliporejea akina Tamiym na vitu vyake alivyoviacha baada ya kufariki, walikikosa chombo kimoja cha fedha ambacho kimezibiwa kwa dhahabu. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaapisha. Kisha baada ya hapo walikuja kukipata kile chombo Makkah. Wakasema wale waliokipata huko Makkah kwamba: Tulikinunua kwa ‘Adiy na Tamiym. Wakasimama watu wawili katika ndugu wa yule As-Sahm wakaapa na wakasema kumuambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ushahidi wetu ni bora kuliko ushahidi wao, na kwamba hao ni waongo wanamsingizia Tamiym na ‘Adiy na kuwa hicho chombo si cha huyo ndugu yao bali ni cha jamaa yao wenyewe, hapo zikateremka Aayaat hizi: “Enyi walioamini! Mauti yanapomfikia mmoja wenu wakati anapousia, basi chukueni ushahidi wa wawili wenye uadilifu miongoni mwenu… (5 : 106) mpaka mwisho wa Aayah (5 : 108). [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), ameipokea Al-Bukhaariy].

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.