-->
logo

004 - An-Nisaa


 النِّسَاء

An-Nisaa: 4

Suwrah hii yote imeteremka Madiynah isipokuwa kauli ya Allaah: “Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe” (58)

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾ 

1. Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwachunga daima.

 

 

وَآتُوا الْيَتَامَىٰ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَتَبَدَّلُوا الْخَبِيثَ بِالطَّيِّبِ ۖ وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَهُمْ إِلَىٰ أَمْوَالِكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ حُوبًا كَبِيرًا ﴿٢﴾ 

2. Na wapeni mayatima mali zao, na wala msibadilishe kibaya (chenu) kwa kizuri (chao). Na wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika hilo limekuwa ni dhambi kubwa.

 

 

وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾

3. Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima; basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu.[1]

 

 

وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً ۚ فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَّرِيئًا ﴿٤﴾ 

4. Na wapeni wanawake mahari zao kwa maridhawa. Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa khiari zao, basi kuleni kwa kufurahia na kunufaika.

 

 

وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ قِيَامًا وَارْزُقُوهُمْ فِيهَا وَاكْسُوهُمْ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٥﴾ 

5. Wala msiwape wasiokomaa kiakili mali yenu ambayo Allaah Ameijaalia kuwa ni kisaidizi chenu cha maisha, na walisheni humo na wavisheni na waambieni maneno ya haki na kwa huruma.

 

 

وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا ۚ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُوا عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٦﴾

6. Na wajaribuni mayatima (akili zao) mpaka wakifikia umri wa kuoa. Na mkihisi kupevuka kwao, basi wapeni mali zao. Wala msiile kwa israfu na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliyekuwa tajiri basi ajizuilie (kuchukua ujira); na aliyekuwa fakiri basi ale kwa kadiri ya kukubalika ki-shariy’ah. Mtapowapa mali zao washuhudizeni. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye kuhisabu.[2]

 

 

لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿٧﴾

7. Wanaume wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu. Na wanawake wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu, ikiwa ni kidogo au kingi; ni mgao uliofaridhishwa.

 

 

 وَإِذَا حَضَرَ الْقِسْمَةَ أُولُو الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينُ فَارْزُقُوهُم مِّنْهُ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٨﴾

8. Na wakati wa kugawa, wakihudhuria jamaa wa karibu na mayatima na masikini, basi wapeni kitu katika hayo na wasemezeni kauli ifaayo ya haki na kwa huruma.

 

 

وَلْيَخْشَ الَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَافًا خَافُوا عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا اللَّـهَ وَلْيَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٩﴾ 

9. Na waogope (wasimamizi kukhini) wale ambao lau nao wangeliacha nyuma yao dhuriya dhaifu wangeliwakhofia; basi wamche Allaah na waseme kauli iliyo sawa ya haki.

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾

10. Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto, na watauingia moto uliowashwa vikali mno.

 

 

يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۚ فَإِن كُنَّ نِسَاءً فَوْقَ اثْنَتَيْنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ ۖ وَإِن كَانَتْ وَاحِدَةً فَلَهَا النِّصْفُ ۚ وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ وَلَدٌ ۚ فَإِن لَّمْ يَكُن لَّهُ وَلَدٌ وَوَرِثَهُ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ الثُّلُثُ ۚ فَإِن كَانَ لَهُ إِخْوَةٌ فَلِأُمِّهِ السُّدُسُ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ لَا تَدْرُونَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ لَكُمْ نَفْعًا ۚ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١﴾ 

11. Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni zaidi ya wawili basi watastahiki theluthi mbili za alichoacha (maiti). Lakini akiwa mtoto wa kike ni mmoja pekee basi atastahiki nusu, na wazazi wake wawili kila mmoja wao atastahiki sudusi katika alichoacha ikiwa anaye mtoto. Na ikiwa hakuwa na mtoto na wazazi wake wawili ndio warithi wake, basi mama yake atastahiki theluthi moja. Na ikiwa anao ndugu basi mama yake atastahiki sudusi, baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu hamjui ni yupi miongoni mwao aliye karibu zaidi kwenu kwa manufaa. Ni shariy’ah kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.[3]

 

 

وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۚ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم ۚ مِّن بَعْدِ وَصِيَّةٍ تُوصُونَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلَالَةً أَوِ امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ ۚ فَإِن كَانُوا أَكْثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمْ شُرَكَاءُ فِي الثُّلُثِ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصَىٰ بِهَا أَوْ دَيْنٍ غَيْرَ مُضَارٍّ ۚ وَصِيَّةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Nanyi mtastahiki nusu katika walichoacha wake zenu ikiwa hawakuwa na mtoto. Na ikiwa wana mtoto, basi mtastahiki robo katika walichoacha, baada ya kutoa wasia waliyousia au kulipa deni. Nao wake zenu watastahiki robo katika mlichoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto basi watastahiki thumni katika mlichoacha, baada ya kutoa wasia mliousia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao atastahiki sudusi. Na wakiwa ni wengi ya hivyo basi watashirikiana katika theluthi, baada ya kutoa wasia uliousiwa na kulipwa deni pasipo kuleta dhara.  Huu ni wasia kutoka kwa Allaah, na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu.

 

 

تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٣﴾

13. Hiyo ni mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayemtii Allaah na Rasuli Wake Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, watadumu humo, na huko ndiko kufuzu kukubwa.

 

 

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٤﴾

14. Na yeyote atakayemuasi Allaah na Rasuli Wake na akataadi mipaka Yake Atamuingiza motoni, ni mwenye kudumu humo na atapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

وَاللَّاتِي يَأْتِينَ الْفَاحِشَةَ مِن نِّسَائِكُمْ فَاسْتَشْهِدُوا عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖ فَإِن شَهِدُوا فَأَمْسِكُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّاهُنَّ الْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ اللَّـهُ لَهُنَّ سَبِيلًا ﴿١٥﴾

15. Na wale wanaofanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, basi washuhudisheni mashahidi wanne kati yenu. Na wakishuhudia basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafishe au Allaah Awajaalie njia (nyingine).[4]

 

 

وَاللَّذَانِ يَأْتِيَانِهَا مِنكُمْ فَآذُوهُمَا ۖ فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا عَنْهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿١٦﴾ 

16. Na wale wawili wanaofanya huo (uchafu) waadhibuni. Wakitubu na kutengenea basi waacheni. Hakika Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.

 

 

 إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُولَـٰئِكَ يَتُوبُ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧﴾

17. Hakika tawbah inayokubaliwa na Allaah ni ya wale wanaofanya uovu kwa ujahili kisha wakatubia haraka, basi hao Allaah Anapokea tawbah yao. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّىٰ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الْآنَ وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٨﴾ 

18. Lakini tawbah si kwa wale wanaofanya maovu mpaka mauti yanapohudhuria kwa mmoja wao husema: “Hakika mimi sasa nimetubu.” Na wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri. Hao Tumewaandalia adhabu iumizayo.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩﴾

19. Enyi walioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwakirihisha. Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya uchafu bayana. Na kaeni nao kwa wema. Na mkiwachukia, basi asaa ikiwa mnachukia jambo na Allaah Akalijaalia kuwa lenye khayr nyingi.[5]

 

 

وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا مِنْهُ شَيْئًا ۚ أَتَأْخُذُونَهُ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٢٠﴾

20. Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na mmempa mmoja wao mirundi ya mali, basi msichukue humo chochote. Je, mnakichukua kwa dhulma na dhambi iliyo bayana?

 

 

وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أَفْضَىٰ بَعْضُكُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٢١﴾

21. Na mtachukuaje na hali nyinyi kwa nyinyi mmeingiliana, na wao wanawake wakapokea kwenu fungamano thabiti?

 

 

وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٢٢﴾

22. Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika hayo yalikuwa ni uchafu na chukizo na njia ovu.[6]

 

 

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٣﴾

23. Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na mabinti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na makhalati zenu (mama wakubwa na wadogo), na mabinti wa kaka, na mabinti wa dada, na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na ndugu zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia. Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa). Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni shariy’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya yaliyowajibika. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.[7]

 

 

 

وَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ مِنكُمْ طَوْلًا أَن يَنكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُم ۚ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۚ فَانكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ فَإِذَا أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَاحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى الْمُحْصَنَاتِ مِنَ الْعَذَابِ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ الْعَنَتَ مِنكُمْ ۚ وَأَن تَصْبِرُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٥﴾

25. Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake Waumini walio huru, basi (aoe) katika wale iliyomiliki mikono yenu ya kulia miongoni mwa wajakazi wenu Waumini. Na Allaah Anajua zaidi iymaan yenu. Nyinyi kwa nyinyi. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao na wapeni mahari yao kwa ada inayokubalika, wawe wanawake wanaojistiri na machafu si makahaba na wala si wenye kuchukua hawara. Na watakapohifadhiwa katika ndoa, kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu ya waliyowekewa wanawake walio huru (wasioolewa). Hayo ni kwa yule anayeogopa dhambi ya zinaa miongoni mwenu. Na mkisubiri ni khayr kwenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمْ وَيَهْدِيَكُمْ سُنَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ وَيَتُوبَ عَلَيْكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦﴾

26. Allaah Anataka kukubainishieni na kukuongozeni nyendo za wale walio kabla yenu, na Apokee tawbah kwenu. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

وَاللَّـهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُوا مَيْلًا عَظِيمًا ﴿٢٧﴾

27. Na Allaah Anataka kupokea tawbah kwenu; na wale wanaofuata matamanio wanataka mkengeuke, mkengeuko mkubwa mno.

 

 

يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا ﴿٢٨﴾

28. Allaah Anataka kukukhafifishieni (tabu zenu); kwani insani ameumbwa dhaifu. 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾

29. Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatilifu, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Allaah ni Mwenye kuwarehemuni.

 

 

وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾

30. Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza motoni. Na hilo kwa Allaah ni mepesi. 

 

 

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾

31. Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.[8]

 

 

وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّـهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُوا ۖ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ ۚ وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٣٢﴾

32. Wala msitamani ambayo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu katika waliyoyachuma, na wanawake wana sehemu katika waliyoyachuma. Na muombeni Allaah fadhila Zake. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

وَلِكُلٍّ جَعَلْنَا مَوَالِيَ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ ۚ وَالَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَانُكُمْ فَآتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٣٣﴾

33. Na kila mmoja Tumemuwekea warithi katika yale waliyoyaacha wazazi wawili na jamaa wa karibu. Na wale mliofungamana nao viapo (vya undugu) basi wapeni fungu lao. Hakika Allaah daima ni Shahidi juu ya kila kitu.[9]

 

 

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا ﴿٣٤﴾

34. Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. Na wale ambao mnakhofu uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni (kipigo kisichodhuru). Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao (ya kuwaudhi). Hakika Allaah daima ni Mwenye Uluwa, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa.[10]

 

وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ﴿٣٥﴾

35. Na mkikhofu mafarikiano baina yao wawili, basi pelekeni mwamuzi kutoka watu wa mume na mwamuzi kutoka watu mke. Wakitaka sulhu Allaah Atawawafikisha baina yao.  Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

 

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾

36. Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye majivuno mwenye kujifakharisha.

 

 

الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٣٧﴾

37. Wale wanaofanya ubakhili na wanawaamrisha watu ubakhili na wanaficha Aliyowapa Allaah katika fadhila Zake. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha. 

 

 

وَالَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ وَمَن يَكُنِ الشَّيْطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا ﴿٣٨﴾

38. Na wale wanaotoa mali zao kwa kujionyesha kwa watu na wala hawamwamini Allaah wala Siku ya Mwisho. Na yule ambaye shaytwaan amekuwa ni rafiki yake mwandani, basi mbaya alioje rafiki mwandani (huyo).

 

 

وَمَاذَا عَلَيْهِمْ لَوْ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِهِمْ عَلِيمًا ﴿٣٩﴾

39. Na ingekuwa nini juu yao lau wangelimwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wakatoa katika yale Aliyowaruzuku Allaah. Na Allaah ni Mwenye kuwajua vyema. 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾

40. Hakika Allaah Hadhulumu hata uzito au chembe (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira adhimu. 

 

 

فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾

41. Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?

 

 

 

يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَعَصَوُا الرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ الْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ اللَّـهَ حَدِيثًا ﴿٤٢﴾

42. Siku hiyo wale waliokufuru na wakamuasi Rasuli watatamani lau ardhi isawazishwe juu yao.  Na wala hawatoweza kumficha Allaah kauli hata moja. 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٤٣﴾

43. Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema, na wala mkiwa  mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammam (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga, pakeni nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria.[11]

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يَشْتَرُونَ الضَّلَالَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا السَّبِيلَ ﴿٤٤﴾

44. Je, huoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanakhiari upotofu na wanataka mpotee njia?

 

 

وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِأَعْدَائِكُمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَلِيًّا وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ نَصِيرًا ﴿٤٥﴾

45. Na Allaah Anawajua zaidi maadui zenu, na Allaah Anatosha kuwa Mlinzi Msimamizi na Allaah Anatosha kuwa Mwenye kunusuru. 

 

 

مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَـٰكِن لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٤٦﴾

46. Katika Mayahudi wako wanaobadilisha maneno kuyatoa mahali pake, na husema: “Tumesikia” na “Tumeasi”; na (wanamwambia Rasuli): “Sikia bila ya kusikilizwa.” Na (husema): “Raa’inaa” kwa kuzipotoa ndimi zao na kutukana Dini. Na lau wangesema: “Tumesikia na tumetii na sikia na “undhwurnaa” ingelikuwa khayr kwao na yenye kufaa zaidi. Lakini Allaah Amewalaani kwa kufru yao; basi hawaamini isipokuwa wachache tu.[12]

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ آمِنُوا بِمَا نَزَّلْنَا مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبْلِ أَن نَّطْمِسَ وُجُوهًا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰ أَدْبَارِهَا أَوْ نَلْعَنَهُمْ كَمَا لَعَنَّا أَصْحَابَ السَّبْتِ ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٤٧﴾

47. Enyi mliopewa Kitabu! Aminini yale Tuliyoyateremsha (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) yanayosadikisha yale mliyonayo, kabla hatujabadilisha nyuso Tukazirudisha kisogoni, au Tukawalaani kama Tulivyowalaani watu wa As-Sabt. Na amri ya Allaah ni ya kufanyika tu.[13]

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

48. Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم ۚ بَلِ اللَّـهُ يُزَكِّي مَن يَشَاءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٤٩﴾

49. Je, hukuwaona wale wanaojitakasa nafsi zao? Bali Allaah Humtakasa Amtakaye; na wala hawatodhulumiwa hata kadiri ya uzi katika kokwa ya tende. 

 

 

انظُرْ كَيْفَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَكَفَىٰ بِهِ إِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٠﴾

50. Tazama vipi wanavyomtungia  uongo Allaah; na yatosha haya kuwa dhambi za dhahiri.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾

51. Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: “Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.”[14]

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾

52. Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hatopata wa kumnusuru.

 

 

أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّنَ الْمُلْكِ فَإِذًا لَّا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيرًا ﴿٥٣﴾

53. Au wanayo sehemu ya ufalme (wa Allaah?) basi hapo wasingeliwapa watu kadiri ya kitone cha kokwa ya tende.

 

 

أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۖ فَقَدْ آتَيْنَا آلَ إِبْرَاهِيمَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَآتَيْنَاهُم مُّلْكًا عَظِيمًا ﴿٥٤﴾

54. Au wanawahusudu watu (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na Waumini) kwa yale Aliyowapa Allaah katika fadhila Zake? Basi kwa yakini Tuliwapa kizazi cha Ibraahiym; Kitabu na Hikmah na Tukawapa ufalme adhimu.

 

 

فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ بِهِ وَمِنْهُم مَّن صَدَّ عَنْهُ ۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا ﴿٥٥﴾

55. Basi miongoni mwao wako waliomuamini (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na miongoni mwao wako waliomkengeuka. Na Jahannam inatosheleza kuwa ni moto uliowashwa vikali mno.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿٥٦﴾

56. Hakika wale waliokanusha Aayaat (ishara) Zetu Tutawaingiza motoni. Kila ngozi zao zitakapobanikika zikaungua Tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje adhabu. Hakika Allaah daima ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّا ظَلِيلًا ﴿٥٧﴾

57. Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo abadi. Watapata humo wake waliotakasika na Tutawaingiza katika vivuli vya kina.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٥٨﴾

58. Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika uzuri ulioje Anayokuwaidhini nayo Allaah; hakika Allaah daima ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.[15]

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

59. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi.[16]

 

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾

60. Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hiyo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.[17]

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ﴿٦١﴾

61. Na wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli; utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.

 

 

فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَاءُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا ﴿٦٢﴾

62. Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Kisha wakakujia wakiapa “Wa-Allaahi hatukutaka ila mazuri na mapatano.” 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَعْلَمُ اللَّـهُ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِي أَنفُسِهِمْ قَوْلًا بَلِيغًا ﴿٦٣﴾ 

63. Hao ndio ambao Allaah Anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali na wape mawaidha na uwaambie maneno yatakayofikia kuathiri (nafsi zao). 

 

 

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا﴿٦٤﴾

64. Na Hatukutuma Rasuli yeyote ila atiiwe kwa idhini ya Allaah. Na lau wao pale walipojidhulumu nafsi zao wangelikujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwomba Allaah maghfirah na Rasuli akawaombea maghfirah, basi wangelimkuta Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. 

 

 

 

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

65. Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu.[18]

 

 

وَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ اقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ أَوِ اخْرُجُوا مِن دِيَارِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ ۖ وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا مَا يُوعَظُونَ بِهِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا ﴿٦٦﴾

66. Na lau Tungeliwaandikia amri: “Jiueni nafsi zenu na tokeni katika majumba yenu”; wasingelifanya hayo ila wachache miongoni mwao. Na lau wangelifanya yale waliyowaidhiwa nayo ingelikuwa khayr kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi (wa iymaan zao).

 

 

وَإِذًا لَّآتَيْنَاهُم مِّن لَّدُنَّا أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٦٧﴾

67. Na hapo Tungeliwapa kutoka Kwetu ujira adhimu.

 

 

وَلَهَدَيْنَاهُمْ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿٦٨﴾

68. Na Tungewaongoza njia iliyonyooka. 

 

 

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

69. Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao.[19]

 

 

ذَٰلِكَ الْفَضْلُ مِنَ اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ عَلِيمًا ﴿٧٠﴾

70. Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa ni Mjuzi wa yote. 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ فَانفِرُوا ثُبَاتٍ أَوِ انفِرُوا جَمِيعًا ﴿٧١﴾

71. Enyi walioamini! Shikeni hadhari yenu; tokeni kwa vikosi vikosi au tokeni kwa pamoja. 

 

 

وَإِنَّ مِنكُمْ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنْ أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَالَ قَدْ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيَّ إِذْ لَمْ أَكُن مَّعَهُمْ شَهِيدًا ﴿٧٢﴾

72. Na hakika miongoni mwenu wako wanaobakia nyuma (wasiende vitani); inapokusibuni msiba husema: “Kwa yakini Allaah Amenineemesha nilivyokuwa sikuhudhuria pamoja nao.” 

 

 

وَلَئِنْ أَصَابَكُمْ فَضْلٌ مِّنَ اللَّـهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمْ تَكُن بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُ مَوَدَّةٌ يَا لَيْتَنِي كُنتُ مَعَهُمْ فَأَفُوزَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧٣﴾

73. Na ikikufikieni fadhila kutoka kwa Allaah husema; kama kwamba hakukuwa baina yenu na yake pendo (husema): “Laiti ningelikuwa pamoja nao nikapata kufuzu mafanikio adhimu.” 

 

 

فَلْيُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يَشْرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۚ وَمَن يُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيُقْتَلْ أَوْ يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٧٤﴾

74. Basi wapigane katika njia ya Allaah wale wanaouza uhai (wao) wa dunia kwa Aakhirah. Na atakayepigana katika njia ya Allaah akauliwa au akashinda basi Tutampa ujira adhimu.

 

 

وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا ﴿٧٥﴾

75. Na mna nini hampigani katika njia ya Allaah, na walio wanyonge kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao husema: “Rabb wetu Tutoe kutoka katika mji huu ambao watu wake ni dhalimu, na Tujaalie kutoka Kwako mlinzi na Tujaalie kutoka Kwako mwenye kunusuru. 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا ﴿٧٦﴾

76. Wale walioamini hupigana katika njia ya Allaah. Na wale waliokufuru hupigana katika njia ya twaghuti (kumtii shaytwaan) Basi wapigeni marafiki wandani wa shaytwaan. Hakika hila za shaytwaan daima ni dhaifu.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّـهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ وَقَالُوا رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا الْقِتَالَ لَوْلَا أَخَّرْتَنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ ۗ قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ اتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧٧﴾

77. Je, huoni wale walioambiwa: “Zuieni mikono yenu (msipigane) na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah.” Basi walipoandikiwa amri kupigana, mara kundi miongoni mwao linakhofu watu kama kumkhofu Allaah au khofu zaidi. Na husema: “Rabb wetu!  Kwa nini Umetuamrisha kupigana? Lau Ungelituakhirishia hadi muda kidogo hivi!” Sema: “Starehe za dunia ni chache; na Aakhirah ni bora zaidi kwa mwenye kuwa na taqwa; wala hamtodhulumiwa kadiri ya uzi katika kokwa ya tende.”[20]

 

 

أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ ۗ وَإِن تُصِبْهُمْ حَسَنَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِكَ ۚ قُلْ كُلٌّ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ فَمَالِ هَـٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا ﴿٧٨﴾

78. Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika minara iliyojengwa kifakhari na madhubuti. Na likiwafikia jambo zuri husema: “Hili ni kutoka kwa Allaah.” Na likiwasibu ovu husema: “Hili kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).” Sema: “Yote ni kutoka kwa Allaah.” Basi wana nini hawa watu hawakaribii kufahamu kauli?

 

 

مَّا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ ۚ وَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٧٩﴾

79. Zuri lilokufikia ni kutoka kwa Allaah. Na ubaya uliokusibu (ee bin-Aadam) ni kutokana na nafsi yako. Na Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watu uwe Rasuli na inatosheleza Allaah kuwa ni Mwenye kushuhudia yote. 

 

 

 

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾

80. Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao.

 

 

وَيَقُولُونَ طَاعَةٌ فَإِذَا بَرَزُوا مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَائِفَةٌ مِّنْهُمْ غَيْرَ الَّذِي تَقُولُ ۖ وَاللَّـهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ ۖ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٨١﴾

81. Na husema: “Tunatii.” Lakini wanapotoka kutoka kwako, kundi miongoni mwao hukesha kushauriana kinyume na unayoyasema. Na Allaah Anayaandika yale wanayokeshea. Basi waachilie mbali na tawakali kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.

 

 

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا ﴿٨٢﴾

82. Je, hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.[21]

 

 

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٣﴾

83. Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, wangelijua wale wanaotafiti wakabainisha ya sahihi miongoni mwao. Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan ila wachache tu.[22] 

 

 

فَقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفْسَكَ ۚ وَحَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ عَسَى اللَّـهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَاللَّـهُ أَشَدُّ بَأْسًا وَأَشَدُّ تَنكِيلًا ﴿٨٤﴾

84. Basi pigana (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika njia ya Allaah, hukalifishwi ila nafsi yako. Na wahimize Waumini (wakuunge). Asaa Allaah Akazuia mashambulizi ya nguvu ya waliokufuru. Na Allaah ni Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu adhabu ya uzindusho. 

 

 

مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا ﴿٨٥﴾

85. Atakayeombea uombezi mzuri atapata fungu lake katika hayo. Na atakayeombea uombezi mbaya atapata sehemu yake katika hayo. Na Allaah daima ni Mwenye kudhibiti na Mwangalizi wa kila kitu. 

 

 

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا ﴿٨٦﴾

86. Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo. Hakika Allaah daima ni Mwenye kuhesabu kila kitu.

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا ﴿٨٧﴾

87. Allaah; hapana muabudiwa wa haki ila Yeye. Bila ya shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?

 

 

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

88. Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu waliyoyachuma. Je, mnataka kumwongoa ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoa).[23]

 

 

وَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُوا فَتَكُونُونَ سَوَاءً ۖ فَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ أَوْلِيَاءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ ۖ وَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٨٩﴾

89. Wanatamani kama mtakufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msifanye miongoni mwao marafiki wandani mpaka wahajiri katika njia ya Allaah. Wakikengeuka basi wakamateni na waueni popote muwapatapo. Wala msifanye marafiki wandani miongoni mwao wala mwenye kunusuru. 

 

 

إِلَّا الَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ أَوْ جَاءُوكُمْ حَصِرَتْ صُدُورُهُمْ أَن يُقَاتِلُوكُمْ أَوْ يُقَاتِلُوا قَوْمَهُمْ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَسَلَّطَهُمْ عَلَيْكُمْ فَلَقَاتَلُوكُمْ ۚ فَإِنِ اعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَاتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ فَمَا جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلًا ﴿٩٠﴾

90. Isipokuwa wale waliochukua kimbilio kwa watu ambao baina yenu na baina yao mna mkataba au wamekujieni vifua vyao vimedhikika kupigana nanyi au kupigana na watu wao, (hao msiwapige). Na lau Allaah Angelitaka, Angeliwasaliti juu yenu, wakapigana nanyi. Watakapojitenga nanyi na wasipigane nanyi, na wakakuwekeeni amani, basi Allaah Hakukufanyieni njia dhidi yao.

 

 

سَتَجِدُونَ آخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوا إِلَى الْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا فِيهَا ۚ فَإِن لَّمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ وَيَكُفُّوا أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُولَـٰئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿٩١﴾

91. Mtawakuta wengine wanaotaka kupata amani kwenu na kupata amani kwa watu wao; kila wanaporudishwa katika fitnah huangushwa humo. Wasipojitenga nanyi na wakakuleteeni amani na wakazuia mikono yao (kukupigeni), basi wachukueni na waueni popote muwapatapo. Na hao Tumekufanyieni hoja zilizo bayana dhidi yao.

 

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً ۚ وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَن يَصَّدَّقُوا ۚ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٩٢﴾

92. Na haiwi kwa Muumin amuue Muumin ila kwa kukosea tu. Na atakayemuua Muumin kwa kukosea basi aachilie huru mtumwa Muumin na atoe diya kwa kuifikisha kwa ahli zake, isipokuwa watolee wenyewe swadaqah. Na ikiwa ni miongoni mwa watu wa maadui zenu naye ni Muumin, basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumin. Na ikiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao; basi wapewe diya kuifikisha kwa ahli wake na aachiliwe huru mtumwa Muumin. Asiyepata, afunge Swiyaam miezi miwili mfululizo; kuwa ni tawbah kwa Allaah. Na Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote. 

 

 

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿٩٣﴾

93.  Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo na Allaah Atamghadhibikia na Atamlaani na Atamuandalia adhabu kuu.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

94. Enyi walioamini! Mnapotembea katika njia ya Allaah thibitisheni, wala msimwambie anayekuamkieni kwa “As-salaam”: “Wewe si Muumin” kwa kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan basi hakikisheni. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.[24]

 

 

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ فَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى الْقَاعِدِينَ دَرَجَةً ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَفَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ عَلَى الْقَاعِدِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٩٥﴾

95. Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani) wasiokuwa na dharura na kati ya Mujaahiduwna katika njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao. Allaah Amewafadhilisha kwa cheo Mujaahidiyna kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaaa nyuma. Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (Jannah). Na Allaah Amewafadhilisha Mujaahidiyna kwa ujira mkubwa mno kuliko wanaokaa (nyuma).[25]

 

 

دَرَجَاتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٩٦﴾

96. Ni daraja za vyeo (vya juu) kutoka Kwake na maghfirah na rahmah. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

97. Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao; (Malaika) watawaambia: “Mlikuwa katika hali gani?”  Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.”  (Malaika) Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia.[26]

 

 

إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا ﴿٩٨﴾

98. Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia.  

 

 

فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٩٩﴾

99. Basi hao asaa Allaah Akawasamehe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria. 

 

     

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

100. Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na rizki. Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.[27]

 

 

وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا مِنَ الصَّلَاةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا ﴿١٠١﴾

101. Na mtakaposafiri katika ardhi basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah mkikhofu kwamba waliokufuru watakushambulieni. Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui dhahiri. 

 

 

وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٠٢﴾

102. Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu basi wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.[28]

 

 

فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾

103. Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu.[29]

 

 

وَلَا تَهِنُوا فِي ابْتِغَاءِ الْقَوْمِ ۖ إِن تَكُونُوا تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ ۖ وَتَرْجُونَ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا يَرْجُونَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٠٤﴾

104. Wala msilegee kuwaandama watu (maadui). Mkiwa mnaumia basi nao pia wanaumia kama mnavyoumia. Na mnataraji kutoka kwa Allaah wasiyoyataraji wao. Na Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ﴿١٠٥﴾

105. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa Aliyokuonyesha Allaah. Wala usiwe mtetezi kwa makhaini. 

 

 

وَاسْتَغْفِرِ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٦﴾

106. Na muombe Allaah maghfirah. Hakika Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

وَلَا تُجَادِلْ عَنِ الَّذِينَ يَخْتَانُونَ أَنفُسَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا ﴿١٠٧﴾

107. Wala usiwatetee wale wanaokhini nafsi zao. Hakika Allaah Hampendi aliye mwingi wa kukhini na kutenda dhambi. 

 

 

يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّـهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا ﴿١٠٨﴾

108. Wanaficha kwa watu (uhalifu wao) na wala hawawezi kuficha kwa Allaah, Naye Yu pamoja nao (kwa ujuzi Wake) pale wanapokesha kupanga makri kwa zile kauli Asizozikubali. Na Allaah daima kwa yale wayatendayo, ni Mwenye kuyazunguka (kwa ujuzi Wake). 

 

 

هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ جَادَلْتُمْ عَنْهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَمَن يُجَادِلُ اللَّـهَ عَنْهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا ﴿١٠٩﴾

109. Ha! Nyinyi ndio hawa mliowatetea katika uhai wa dunia. Basi nani atakayemjadili Allaah kwa ajili yao Siku ya Qiyaamah au nani atakayekuwa mwakilishi wao? 

 

 

وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾

110. Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake; kisha akamwomba Allaah maghfirah; atamkuta Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

وَمَن يَكْسِبْ إِثْمًا فَإِنَّمَا يَكْسِبُهُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١١﴾

111. Na atakayechuma dhambi, basi hakika anaichumia nafsi yake. Na Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote. 

 

 

وَمَن يَكْسِبْ خَطِيئَةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِ بَرِيئًا فَقَدِ احْتَمَلَ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿١١٢﴾

112. Na atakayechuma kosa au dhambi kisha akamtupia asiye na hatia; basi kwa yakini atajitweka usingiziaji na dhambi zilizo bayana.

 

 

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ وَرَحْمَتُهُ لَهَمَّت طَّائِفَةٌ مِّنْهُمْ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ ۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيْءٍ ۚ وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚ وَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا ﴿١١٣﴾

113. Na lau kuwa si fadhila ya Allaah na rahmah Yake juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); bila shaka kundi miongoni mwao lingefanya hima kudhamiria kukupoteza. Na hawazipotezi ila nafsi zao, na hawakudhuru kwa chochote. Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah na Akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua. Na fadhila za Allaah juu yako ni adhimu.

 

 

لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾

114. Hakuna khayr katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha swadaqah, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka radhi za Allaah, basi Tutampa ujira adhimu.

 

 

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿١١٥﴾

115. Na atakayempinga Rasuli baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya Waumini; Tutamgeuza alikogeukia na Tutamuingiza Jahannam. Na uovu ulioje mahali pa kuishia. 

 

 

 إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١١٦﴾

116. Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.

 

 

إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾

117. Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi.

 

 

لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾

118. Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: “Kwa hakika nitashika katika waja Wako sehemu maalumu.”

 

 

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾

119. “Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah.” Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana.[30]

 

 

يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ ۖ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢٠﴾

120. Anawaahidi na anawashawishi matamanio ya uongo. Na shaytwaan hawaahidi isipokuwa ulaghai.

 

 

أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا ﴿١٢١﴾

121. Hao makaazi yao ni Jahannam, na wala hawatopata makimbilio ya kutoka humo. 

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا ﴿١٢٢﴾

122. Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo abadi. Ahadi ya Allaah ni haki. Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah? 

 

 

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

123. “Si kwa matamanio yenu wala si matamanio ya Ahlil-Kitaab. Atakayefanya uovu atalipwa kwayo, na wala hatopata pasi na Allaah mlinzi wala mwenye kunusuru.[31]

 

 

وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ مِن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ نَقِيرًا ﴿١٢٤﴾

124. Na atakayefanya mema akiwa mwanamume au mwanamke hali yeye ni Muumini; basi hao wataingia Jannah na wala hawatodhulumiwa watu kadiri ya kitone cha kokwa ya tende. 

 

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

125. Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye ni mtendaji mazuri na akafuata millah ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki. Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni kipenzi.

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطًا ﴿١٢٦﴾

126. Na ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na Allaah daima ni Mwenye kuzunguka kila kitu (kwa ujuzi Wake).

 

 

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا ﴿١٢٧﴾

127. Na wanatafuta fatwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: “Allaah Atakupeni hukmu kuhusu wao na yale mnayosomewa kwenu katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa; na mna raghba ya kuwaoa. Na juu ya wanaokandamizwa miongoni mwa watoto. Na kwamba muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na lolote mlifanyalo katika la khayr basi hakika Allaah daima kwa hilo ni Mjuzi.[32]

 

 

 

 

 

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

128. Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya juu yake wakisikilizana baina yao kwa suluhu Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa uchoyo. Na mkifanya ihsaan na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah daima kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.[33]

 

 

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٢٩﴾

129. Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msimili muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mwengine) kama kining’inio. Na mkisuluhisha na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ اللَّـهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ وَاسِعًا حَكِيمًا ﴿١٣٠﴾

130. Na wakifarikiana basi Allaah Atampa utajiri kila mmoja katika wasaa Wake. Na Allaah daima ni Mwenye wasaa, Mwenye hikmah wa yote. 

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَنِيًّا حَمِيدًا ﴿١٣١﴾

131. Na ni vya Allaah vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na kwa yakini Tumewausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu na nanyi kwamba: “Mcheni Allaah.” Na mkikufuru basi hakika ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na Allaah daima ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa. 

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٣٢﴾

132. Na ni vya Allaah vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na inatosheleza Allaah kuwa ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.

 

 

إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ أَيُّهَا النَّاسُ وَيَأْتِ بِآخَرِينَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرًا ﴿١٣٣﴾

133. Akitaka, Atakuondoeni mbali enyi watu, na Ataleta wengine. Na Allaah daima kwa hayo ni Muweza wa yote.

 

 

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿١٣٤﴾

134. Anayetaka thawabu za dunia basi kwa Allaah kuna thawabu za dunia na Aakhirah. Na Allaah daima ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّـهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا ۚ وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٣٥﴾

135. Enyi walioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu mtoapo ushahidi kwa ajili ya Allaah japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili, au jamaa wa karibu. Akiwa tajiri au maskini Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate hawaa mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkikanusha basi hakika Allaah daima kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي أَنزَلَ مِن قَبْلُ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٣٦﴾

136. Enyi walioamini! Mwaminini Allaah na Rasuli Wake na Kitabu Alichokiteremsha kwa Rasuli Wake na Kitabu Alichokiteremsha kabla. Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Rusuli Wake na Siku ya Mwisho, basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ سَبِيلًا ﴿١٣٧﴾

137. Hakika wale walioamini kisha wakakufuru kisha wakaamini kisha wakakufuru, kisha wakazidi kufru, Allaah Hatowaghufiria na wala Hatowaongoa njia.

 

 

بَشِّرِ الْمُنَافِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٣٨﴾

138. Wabashirie wanafiki kwamba watapata adhabu iumizayo. 

 

 

الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ﴿١٣٩﴾

139. Wale wanaofanya makafiri kuwa ni marafiki wandani badala ya Waumini. Je, wanatafuta utukufu kutoka kwao? Basi hakika utukufu wote ni wa Allaah Pekee. 

 

 

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا ﴿١٤٠﴾

140. Na kwa yakini Amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayaat za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Au sivyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah Atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.[34] 

 

 

الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللَّـهِ قَالُوا أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوا أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا ﴿١٤١﴾

141.  Wale wanaokungojeeni kwa uangalifu, inapokuwa ni ushindi kwenu kutoka kwa Allaah; husema: “Je, hatukuwa pamoja nanyi?” Na inapokuwa kwa makafiri sehemu ya ushindi; husema: “hatukuwa wenye kukudhibitini na tukakuzuilieni kukukingeni na Waumini?” Basi Allaah Atawahukumu baina yenu Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Hatojaalia kwa makafiri njia dhidi ya Waumini (ya kuwashinda).  

 

 

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٤٢﴾

142. Hakika wanafiki (wanadhani) wanamhadaa Allaah, na hali Yeye (Allaah) Ndiye Mwenye kuwahadaa. Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, wakijionyesha kwa watu na wala hawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu.

 

 

مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَلَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿١٤٣﴾

143. Madhabidhabina baina ya hayo (iymaan na kufru), huku hawako wala huko hawako. Na ambaye Allaah Amempotoa huwezi kumpatia njia (ya kumwongoa).

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا لِلَّـهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٤٤﴾

144. Enyi walioamini! Msiwafanye makafiri kuwa marafiki wandani badala ya Waumini. Je, mnataka Allaah Awe na hoja bayana dhidi yenu?

 

 

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ﴿١٤٥﴾

145. Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto; na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٤٦﴾

146. Isipokuwa wale waliotubu na wakatengenea na wakashikamana na Allaah na wakakhalisisha Dini yao kwa ajili ya Allaah; basi hao watakuwa pamoja na Waumini. Na Allaah Atawapa Waumini ujira adhimu. 

 

 

مَّا يَفْعَلُ اللَّـهُ بِعَذَابِكُمْ إِن شَكَرْتُمْ وَآمَنتُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ شَاكِرًا عَلِيمًا ﴿١٤٧﴾

147. Allaah Hatokuadhibuni ikiwa mtashukuru na mtaamini. Na Allaah daima ni Mwenye kupokea shukurani, Mjuzi wa yote.

 

 

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا عَلِيمًا ﴿١٤٨﴾

148. Allaah Hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa. Na Allaah daima ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا ﴿١٤٩﴾

149. Mkidhihirisha khayr au mkiificha au mkisamehe uovu; basi hakika Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Muweza wa yote.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١٥٠﴾

150. Hakika wale waliomkufuru Allaah na Rusuli Wake; na wanataka kufarikisha baina ya Allaah na Rusuli Wake; na wanasema: “Tunaamini baadhi na tunawakanusha baadhi”; na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٥١﴾

151. Hao ndio makafiri wa kweli. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَلَمْ يُفَرِّقُوا بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُولَـٰئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٥٢﴾

152. Na wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake na hawakumfarikisha yeyote baina yao; hao Atawapa ujira wao. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

يَسْأَلُكَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَابًا مِّنَ السَّمَاءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا مُوسَىٰ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوا أَرِنَا اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ ۚ وَآتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٥٣﴾

153. Wanakuuliza Ahlul-Kitaabi uwateremshie kitabu juu yao kutoka mbinguni. Kwa yakini walimuuliza Muwsaa makubwa kuliko hayo. Walisema: “Tuonyeshe Allaah waziwazi”. Basi iliwachukua radi na umeme angamizi kwa dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumwabudu baada ya kwisha kuwajia hoja bayana. Tukawasamehe hayo; na Tukampa Muwsaa mamlaka bayana.

 

 

وَرَفَعْنَا فَوْقَهُمُ الطُّورَ بِمِيثَاقِهِمْ وَقُلْنَا لَهُمُ ادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُلْنَا لَهُمْ لَا تَعْدُوا فِي السَّبْتِ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا﴿١٥٤﴾

154. Na kwa fungamano lao Tukaunyanyua juu yao mlima; na Tukawaambia: “Ingieni mlangoni hali mkiwa mmeinama kwa kunyenyekea”; na Tukawaambia: “Msitaadi mipaka ya As-Sabt”. Na Tukachukua kutoka kwao fungamano madhubuti.[35]

 

 

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِآيَاتِ اللَّـهِ وَقَتْلِهِمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَلْ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٥٥﴾

155. Na kwa kuvunja kwao fungamano lao, na kufru zao kwa Aayaat (ishara, dalili) za Allaah, na kuua kwao Nabiy bila ya haki, na kauli yao: “Nyoyo zetu zimefumbwa”; bali Allaah Amezipiga chapa juu yake kwa sababu ya kufuru zao; basi hawatoamini ila kidogo. 

 

 

وَبِكُفْرِهِمْ وَقَوْلِهِمْ عَلَىٰ مَرْيَمَ بُهْتَانًا عَظِيمًا ﴿١٥٦﴾

156. Na kwa kufuru zao na kauli yao juu ya Maryam ni usingiziaji mkuu wa kashfa.

 

 

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾

157. Na kauli yao: “Hakika sisi tumemuua Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam, Rasuli wa Allaah.” Na wala hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Na hakika wale waliokhitilafiana katika hayo, kwa hakika wamo katika shaka nalo. Hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua. 

 

 

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٥٨﴾

158. Bali Allaah Alimnyanyua Kwake. Na Allaah daima ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.[36] 

 

 

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾

159. Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.[37]  

 

فَبِظُلْمٍ مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ طَيِّبَاتٍ أُحِلَّتْ لَهُمْ وَبِصَدِّهِمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ كَثِيرًا ﴿١٦٠﴾

160. Basi kwa dhulma ya Mayahudi; Tuliwaharamishia vizuri yaliyohalalishwa kwao; na kwa sababu ya kuwazuilia wengi njia ya Allaah.  

 

 

وَأَخْذِهِمُ الرِّبَا وَقَدْ نُهُوا عَنْهُ وَأَكْلِهِمْ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٦١﴾

161. Na kuchukua kwao ribaa na hali walikatazwa kuichukua; na kula kwao mali za watu kwa ubatilifu. Na Tumeandalia kwa makafiri miongoni mwao adhabu iumizayo. 

 

 

لَّـٰكِنِ الرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ مِنْهُمْ وَالْمُؤْمِنُونَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ ۚ وَالْمُقِيمِينَ الصَّلَاةَ ۚ وَالْمُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالْمُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أُولَـٰئِكَ سَنُؤْتِيهِمْ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٦٢﴾

162. Lakini wenye msingi madhubuti katika elimu miongoni mwao, na Waumini wanaoamini yale aliyoteremshwa kwako (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; na wasimamishao Swalaah, na watoao Zakaah na wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hao Tutawapa ujira adhimu.

 

 

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾

163. Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Nabiy baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na dhuriya, na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr.[38]

 

 

وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾

164. Na Rusuli Tuliokwishakusimulia kabla; na Rusuli (wengine) Hatukukusimulia. Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja.[39]

 

 

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾

165. Rusuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rusuli. Na Allaah daima ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. 

 

 

لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَشْهَدُونَ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿١٦٦﴾

166. Lakini Allaah Anayashuhudia Aliyoyateremsha kwako; Ameyateremsha kwa elimu Yake; na Malaika pia wanashuhudia. Na Anatosheleza Allaah kuwa Mwenye kushuhudia yote.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ قَدْ ضَلُّوا ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٦٧﴾

167. Hakika wale waliokufuru na wakazuia njia ya Allaah, kwa yakini wamekwishapotea upotofu wa mbali. 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَظَلَمُوا لَمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا ﴿١٦٨﴾

168. Hakika wale waliokufuru na wakadhulumu; haitokuwa kwa Allaah kuwaghufuria wala kuwaongoza njia. 

 

 

إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿١٦٩﴾

169. Isipokuwa njia ya Jahannam ni wenye kudumu humo abadi. Na hayo kwa Allaah ni mepesi.

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الرَّسُولُ بِالْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَآمِنُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧٠﴾

170. Enyi watu! Kwa yakini amekujieni Rasuli kwa haki kutoka kwa Rabb wenu; basi aminini; ni bora kwenu. Na mkikufuru; basi hakika ni vya Allaah Pekee vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّـهُ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖسُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٧١﴾

171. Enyi Ahlal-Kitaabi! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Allaah isipokuwa ukweli. Hakika Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam ni Rasuli wa Allaah na ni neno Lake (la Kun!) Alompelekea Maryam na Ruwh (roho Aliyoumba kwa amrisho) kutoka Kwake. Basi mwaminini Allaah na Rusuli Wake; wala msiseme: ‘watatu’. Komeni, ni khayr kwenu. Hakika Allaah ni Muabudiwa wa haki Mmoja Pekee, Subhaanah! (Utakasifu ni Wake) kuwa ana mwana! Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Na Anatosheleza Allaah kuwa ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.[40]

 

 

لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّـهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا ﴿١٧٢﴾

172. Al-Masiyh hatoona bezo kamwe kukataa kuwa ni mja kwa Allaah, wala Malaika waliokurubishwa. Na atakayebeua Kumwabudu Kwake (Allaah) na akatakabari, basi Atawakusanya wote Kwake.

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ اسْتَنكَفُوا وَاسْتَكْبَرُوا فَيُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٧٣﴾

173. Ama wale walioamini na wakatenda mema; (Allaah) Atawalipa kwa ukamilifu ujira wao; na Atawazidishia kwa fadhila Zake. Ama waliobeua na wakatakabari; Atawaadhibu adhabu iumizayo; na wala hawatopata pasi na Allaah mlinzi wala mwenye kunusuru.

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾

174. Enyi watu!  Kwa yakini imekujieni burhani kutoka kwa Rabb wenu na Tumekuteremshieni Nuru bayana. 

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿١٧٥﴾

175. Ama wale waliomwamini Allaah, na wakashikamana Naye; Atawaingiza katika rahmah kutoka Kwake na fadhila, na Atawaongoza Kwake njia iliyonyooka. 

 

 

يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾

176. Wanatafuta kwako fatwa. Sema: Allaah Atakufutuni kuhusu Al-Kalaalah (asiye na wazazi wala watoto) Ikiwa mtu amefariki hana mtoto lakini ana dada; basi atastahiki nusu ya yale aliyoyaacha. Na yeye (huyo mtu) atamrithi huyo dada kama hana mtoto. Na ikiwa wao madada ni wawili; basi watastahiki thuluthi mbili ya yale aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake; basi mwanamme atastahiki sehemu iliyo sawa na sehemu ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni  ili msipotee; na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.[41]

 

 

 

 

 

 

 
[1]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها): “Kuna bwana mmoja alimuoa binti ambaye ni yatima aliyekuwa akimlea na msimamizi wake kwa sababu hakuwa na mtu wa kumsimamia. Huyo bwana hakumuoa kwa sababu ya kumpenda kwani alikuwa haamiliani naye vizuri. Akamuoa kwa ajili yatima huyo alikuwa ana (mali) shamba la mitende. Hapo ikateremka Aayah hii.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

[2]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka ikiwa inabainisha hukmu kuhusu mali ya yatima. Mlezi wa yatima huyo anapokuwa ni fakiri, basi anaweza kula katika mali hiyo kwa wema bila ya israaf. [Amehadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

[3] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii pamoja na Aayah ya mwisho katika Suwrah hii (3: 176) imeteremka kuhusu Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) pale alipotembelewa na Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) wakamkuta  amezimia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatawadha na akamrashia maji kutokana na wudhuu wake.  Kisha Jaabir (رضي الله عنه) akamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Niifanye vipi mali yangu?“ Hapo ikateremka hii Aayah. [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) aimeipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

[4] An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Aayah hii  imefutwa hukmu yake kwa Aayah ya kupigwa mijeledi mia moja kwa bikra waliozini, na Hadiyth za rajmi (kuwapiga mawe) waliozini baada ya ndoa, imehadithiwa kutoka kwa  ‘Ubaadah  bin Asw-Swaamit  (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Chukueni kutoka kwangu, chukueni kutoka kwangu, Allaah  Amekwishawajalia  wanawake njia;  bikra kwa bikra, wakizini hukmu yao ni kuchapwa mijeledi mia moja, na kutolewa maeneo hayo mwaka mzima,  na Ath-Thayyib (aliyekwishaoa au kuolewa) kwa Ath-Thayyib, wakizini hukmu yao  ni mijeledi mia moja, na rajmu (kupigwa mawe) [Muslim].

 

 

[5]Sababun-Nuzuwl: Walikuwa Waarabu zama za Jaahiliyyah pindi anapokufa mwanaume na akaacha mke, basi wale ndugu wa mume wake wanakuwa na haki zaidi kwa mwanamke, na   baadhi yao wakitaka wanamuoa, na wakitaka wanamuozesha, na wakitaka hawamuozeshi, na wao wanakuwa wana haki naye zaidi kuliko hata ndugu zake mwanamke na wazazi wake. Ndipo Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha Aayah hii. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Al-Bukhaary]. 

 

 

[6] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kwa kuwa watu wa zama za Jaahiliyyah walikuwa wanaharamisha yaliyo ya haramu isipokuwa mke wa baba. Na walikuwa wanakusanya mabinti wawili ambao ni ndugu katika ndoa moja na wakati mmoja, kisha ikateremka Aayah hii pamoja na kauli ya Allaah Aliposema: “Na (mmeharamishwa) kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita.”  [An-Nisaa 4: 23] Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameitaja Ibn Jariyr Atw-Twabariy katika Tafsiyr yake].

 

[7] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu Maswahaba (رضي الله عنهم) kwani wao siku ya Awtwaas (eneo lilipo baina ya Makkah na Twaaif ambapo walipatikana mateka baada ya vita vya Hunayn mwaka wa 8 Hijriyyah) walipata wanawake ambao ni mateka, basi wakaona uzito kuwaingilia kwa sababu waume zao ni washirikina. Allaah  (عزّ وجلّ) Akateremsha hii Aayah: “Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.” [Amehadithia Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه) ameipokea Muslim].

 

Uharamisho wa ndoa ya mut’ah: Sabrah bin Ma’bad Al-Juhniy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba baba yake aliandamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Fat-hi Makkah akasema: “Enyi watu! Nilikuruhusuni ndoa ya mut’ah hapo mwanzo. Leo Allaah Ameiharamisha mpaka Siku ya Qiyaamah! Basi ikiwa kuna yeyote ambaye ana mke wa ndoa ya mut’ah amwache na wala asichukue chochote katika alichompa.” [Muslim na wengineo].

 

[8]Al-Kabaair (dhambi kubwa): ni lile lililotajiwa ndani yake laana, au haddi (adhabu) hapa duniani, au limeahidiwa juu yake ghadhabu za Allaah au moto. Na pia kuhusu madhambi saba yanayoangamiza [Al-Bukhaariy, Muslim]

[9]An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Hapo mwanzo Muhaajiriyn walipofika Madiynah, Answaar walichukua viapo vya kuungana nao kiundugu na kurithiana. Kisha hukmu ya Aayah hii  ikafutwa baada ya  hukmu ya Aayah (8: 75) katika Suwrat Al-Anfaal nayo ni kauli ya Allaah: “Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika shariy’ah (na hukmu) ya Allaah. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila.”

 

[10]Faida: Kuhusu: “na wahameni katika malazi.” Imekusudiwa kutokulala nao na kutokujimai nao, kwa ujumla ni kuwagomea. Ama kuhusu: “na wapigeni.”  Imekusudiwa kipigo kidogo kisichokuwa cha kumdhuru, wala haipasi kupigwa usoni.  

[11]Sababun-Nuzuwl: Sababu ya kuteremshwa hukmu ya tayammum: Mama wa ‘Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)  amehadithia: “Tulikwenda katika moja ya safari tukafika Al-Baydaa au Dhaatul-Jaysh ambako kidani changu kilivunjika (na kikapotea). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anakitafuta, kisha pia watu wengineo wakainuka kukitafuta. Hapakuweko na maji sehemu hiyo, basi watu wakamwendea Abuu Bakr Asw-Swiddiyq na kusema: Huoni alivyofanya ‘Aaishah? Kamfanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na watu wakae sehemu ambayo hakuna maji! Abuu Bakr akaja wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelaa akiwa amelaza kichwa chake mapajani mwangu. Akaniambia: Umemzuia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu sehemu ambako hakuna maji na wala hawana (akiba ya) maji. Basi akanigombesha na akasema Aliyomjaalia (Allaah) kusema kuhusu mimi na akanipiga ubavuni kwa mkono wake. Hakuna kilichonizuia kusogea (kutokana na maumivu) isipokuwa kwa vile Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilala mapajani mwangu. Hapo Allaah Akateremsha Aayah ya tayammum, basi wakatayammam. ‘Usayd bin Al-Hudhwayr akasema: Ee ahli ya Abuu Bakr! Hii si baraka ya kwanza kwenu. Kisha akaendeshwa ngamia ambaye nilikuwa nimempanda na tukakipata kidani chini yake.” [Al-Bukhaariy].

Sababun-Nuzuwl: Kuhusu kuteremshwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala): “Enyi waloamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa.” Ni kwamba, hatua ya kwanza kuhusu pombe imetahadharishwa katika Suwratul-Baqarah (2: 219): “Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema…” Hii ni hatua ya pili ya kukatazwa pombe katika nyakati za Swalaah kwa sababu Maswahaba walikosea kusoma Qur-aan katika Swalaah kutokana na kulewa. Baada ya hapo ikafutwa hukmu hii na ikabakia pombe kuwa ni haramu nyakati zote kwa kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrat Al-Maaidah (5: 90): “Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na (kuabudu) masanamu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; ni rijsun (uchafu na uovu) katika kitendo cha shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.” 

 

[12] Miongoni mwa ada za Mayahudi ni kuyapotosha maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) kuyatoa kwenye makusudio yake na pia wanayatafsiri kwa isiyokuwa tafsiri yake. Na watu wa bid’ah wamejifananisha nao katika kupindisha na kupotosha maana ya Majina ya Allaah na Sifa Zake.

 

[13] Ifahamu historia ya Mayahudi kwa mukhtasari namna walivyokuwa jeuri kwa Manabii wao: Mayahudi walikatazwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kuvua samaki siku ya As-Sabt (Jumamosi) lakini wao kwa ujeuri wao wakavua samaki siku hiyo na kwa kutumia hila. Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Akawakumbusha wajukuu zao kuhusu siku hiyo ya As-Sabt (Jumamosi) ambayo babu zao Mayahudi waliasi ndani yake kiasi kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwageuza kuwa nyani na nguruwe. Na mwenye kusoma visa vya Mayahudi dhidi ya Manabii wao na miongoni mwa swaalihiyna katika wao, atakuta kuwa waliwaudhi mno Manabii wao na wakawapinga na kwenda kinyume nao. Na pia wakafanyia inadi na ujeuri maamrisho ya Allaah (سبحانه وتعالى) na wakawa na ujeuri uliopindukia. Miongoni mwa mifano ya hayo ni; kisa cha ng’ombe na ndama. Pia kutaka kwao kumuona Allaah (سبحانه وتعالى) wazi wazi. Tena hayo wameyafanya baada tu ya kuvukishwa bahari kwa salama na kuokolewa kutona na adui wao Fir-‘awn aliyezamishwa baharini. Pia uasi wao kuwaua baadhi ya Manabii bila ya haki. Na mifano mingine mingi kuhusu uasi na ujeuri wa Mayahudi.

 

[14]Sababun-Nuzwul: Aayah hii imeteremshwa kama alivyohadithia ‘Ikrimah kwamba: Huyay bin Akhtab na Ka’b Al-Ashraf (Wakuu wa ki-Yahudi) walikuja kwa watu wa Makkah (washirikina) wakawaambia: Nyinyi (Mayahudi) ni Ahlul-Kitaab na wenye ‘ilmu, hivyo basi tujulisheni (tofauti zetu) kuhusu sisi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Jielezeni kuhusu nyinyi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Sisi tunaunga ujamaa wa uhusiano wa damu, tunachinja ngamia (kwa ajili ya mafukara), tunasamehe madeni, tunawapa maji Mahujaji. Ama Muhammad, yeye hana watoto wa kiume, amekata ujamaa wa uhusiano wa damu, na wevi wa Mahujaji (kabila la) Ghifar wanamfuata. Basi je, sisi bora au yeye? Wakasema: Nyinyi bora zaidi na mlioongoka zaidi katika njia. Hapo Allaah Akateremsha: “Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: “Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini... mpaka kauli Yake: “basi hatopata wa kumnusuru.” (4: 52).

[15]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii ni ya pekee katika Suwrah hii ya An-Nisaa (4: 58) ambayo imeteremka Makkah. Imeteremshwa Siku ya Fat-hu Makkah (Ushindi). Ibn Jurayj amehadithia kwamba imeteremshwa kuhusu ‘Uthmaan bin Twalhah ambaye pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alichukua ufunguo wa Ka’bah kutoka kwake akaingia Ka’bah. Alipotoka nje ya Ka’bah, alitoka huku akiwa anasoma: “Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe.” Hapo akamwita ‘Uthmaan bin Twalhah na akampa funguo [Tafsiyr Ibn Kathiyr]. Funguo hizo zimeendelea kubakia katika ukoo huo, kizazi baada ya kizazi mpaka sasa, na mpaka Siku ya Qiyaamah ukoo huo umefadhilishwa kuwa ndio wenye amana ya kukamata funguo za Al-Ka’bah.

 

 

 

[16]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu ‘Abdullaah Ibn Hudhaafah (رضي الله عنه) pale alipotumwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenye msafara wa Jihaad. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Pia Imeteremshwa pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotuma jeshi chini ya uongozi wa mtu mmoja wa Answaar. Walipoondoka, aliwaghadhibikia kwa sababu fulani akawaambia: Kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukuamrisheni mnitii? Wakasema: Ndio! Akasema: Okoteni kuni. Kisha akawasha moto akasema: Nakuamrisheni muingie motoni humu. Wakakaribia watu kuuingia lakini kijana mmoja miongoni mwao akasema: Nyinyi mmekimbia moto kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hivyo msikimbilie mpaka mrudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha akikuamrisheni kuingia hapo muuingie. Waliporudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwelezea yaliyojiri, kisha yeye akasema: “Mngeliuingia, msingetoka kamwe humo. Hakika utiifu ni katika mema.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Amri ya kuwatii kwa wema watawala na viongozi wa mambo ya Waislamu, ni jambo ambalo limenukuliwa na Ijmaa’ juu yake, bali ndiyo ‘Aqiydah iliyokuwa sahihi ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah. Lakini kwa masikitiko makubwa jambo hili wamelipuuza wengi katika Waislamu na wale wasiofahamu mafunzo ya Dini yao. Na matokeo ya kwenda kinyume na jambo hilo na ‘Aqiydah hiyo ni kuleta munkari mkubwa katika Ummah na ufisadi mpana; kuna wanaofanya maandamano kupinga viongozi kuna wanaojilipua kwa mabomu na kuua watu, kuna wanaoua watu kwa njia mbali mbali na kadhalika kumwaga damu za bin Aadam bure! Na wametumia  njia hiyo maadui wa Uislamu  ili kuuchafua Uislamu na kuudidimiza.

 

[17] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii pamoja na mbili zinazofuatia (4: 60-62) zimeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kuwa alikuwa Abuu Barzat Al-Aslamiyy ni Kuhani akitoa hukumu kuhusu magomvi yanayotokea baina ya Mayahudi. Siku moja baadhi ya watu katika washirikina walileta magomvi kwake, kisha Allaah Akateremsha Aayah hii: “Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako…”  [Abuu Haatim Atw-Twabaraaniy, Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy (4/19) amesema isnaad yake ni nzuri].

Sababun-Nuzuwl nyingine pia ya Aayah hii ni kwamba waligombana mtu kutoka Answaar na Myahudi kisha Myahudi akasema: “Twende kwa Muhammad akatuhukumu.” Na yule Answaar akasema: “Twende kwa Ka’ab Al-Ashraf.” Imesemwa pia kuwa miongoni mwa wanafiki walliokuwa wakijidai kuwa ni Waislamu, lakini huku wakitafuta hukmu za kijaahiliyyah. [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

Pia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Abuu Barzah Al-Aslamiy alikuwa mtabiri na akihukumu magomvi ya Mayahudi. Baadhi ya Waislamu walipomwendea kutaka awahukumu, Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: “Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako… mpaka: “Wa-Allaahi hatukutaka ila mazuri na mapatano.” (4: 60-62) [Atw-Twabaraaniy].

 

 

 

[18] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam (رضي الله عنه)  na bwana mmoja katika Answaar, pale walipokhitilafiana kuhusu mfereji wa kupitisha maji ya mvua waliokuwa wakitumia maji yake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa hukmu baina yao kwamba Az-Zubayr amwagilie maji ardhini mwake kisha ayaache yatiririke kwa Answaar. Akakasirika Answaar huyo na kumwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Umempendelea yeye kwa kuwa ni mtoto wa ‘ammat yako! Hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akabadilika uso rangi kwa hasira akamwambia tena Az-Zubayr amwagie maji kwanza kisha yatiririke kwa jirani yake huyo kwa kuwa hukumu hiyo ilikuwa kwa manufaa ya wote wawili. Hivyo akampatia Az-Zubayr haki yake. Ikateremka Aayah hii: “Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao… (4: 67). [Amehadithia Az-Zubayr (رضي الله عنه) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

[19] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu Answaar mmoja ambaye alikuwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na huzuni. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Mbona nakuona umehuzunika?” Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nilikuwa natafakari jambo. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Jambo gani?” Akajibu: Kila siku tunakuja kwako asubuhi na usiku tukitazama uso wako na kukaa kitako nawe. Kesho (Aakhirah), utakuja kufufuliwa pamoja na Manabii na hivyo sisi hatutoweza kukuona tena.  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakusema kitu, kisha Jibriyl (عليه السلام) akamjia kumteremshia Aayah hii: “Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii... (4: 69)” [Ibn Jariyr, Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

Sababun-Nuzuwl  nyingine pia ya Aayah hii, ni kama alivyohadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe ni kipenzi kwangu kuliko nafsi yangu na kipenzi kwangu kuliko ahli yangu, na kipenzi kwangu kuliko wanangu, na hakika ninapokuwa nyumbani kwangu nakukumbuka basi huwa siwezi kusubiri mpaka nije kukutazama. Na napokumbuka mauti yangu na mauti yako, hutambua kwamba wewe utakapoingia Jannah utapanda pamoja na Manabii, lakini nitakapoingia mimi Jannah nakhofu kuwa sitokuona! Basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumjibu mpaka hapo ikateremshwa: “Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii...(4: 69)” [At-Twabaraaniy katika Al-Mu’jamu Asw-Swaghiyr].

 

 

 

 

[20]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba: ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf na Maswahaba wenzake  (رضي الله عنهم) walipokuwa Makkaah walimwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Tulipokuwa washirikina tulikuwa kwenye ‘izzah (hadhi na utukufu) lakini sasa tumeingia Uislamu tumekuwa madhalili. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika mimi nimeamrishwa kusamehe basi msifanye qitaal (vita).” Kisha Allaah Alipomuamrisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhajiri Madiynah, Alimuamrisha jihaad na qitaal (kwa washirikina), basi (wao Waislamu) wakasita. Hapo ikateremshwa Aayah hii. [An-Nasaaiy na Al-Haakim].

 

 

[21]Faida: Aayah hii ni miongoni mwa dalili na radd juu ya madh-hab ya Al-Mufawwidhwah (wanaokubali sifa ya Allaah lakini wakidai maana yake haijulikani; kwa hivyo, wanamzulia Allaah kuwa kawaletea mafundisho waja Wake ambayo hayajulikani maana yake!) ambao wanasema kuwa Majina ya Allaah na Swifaat Zake hazifahamiki maana yake, na hiyo ni itikadi batili mno, bali Shaykhul-Islaam (رحمه الله)  amesema alipolizungumzia hili pote la Mufawwidhwah kuwa ni katika mapote ya bid’ah yaliyokuwa ya shari. Kisha wakainasibisha kauli hii kuwa ndiyo kauli ya Salaf! Huko ni kuwazulia wema waliotangulia (رحمهم الله). Imaam Ahmad anawaona Mufawwidhwah kuwa ni wabaya zaidi kuliko Jahmiyyah.

 

[22]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipojitenga mbali na wake zake, niliingia Masjid nikakuta watu wakipiga ardhi kwa changarawe wakisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki wake zake! Na hivyo ni kabla ya kuamrishwa hijaab. ‘Umar akasema: Nitatambua hilo leo. Basi nikamwendea ‘Aaishah  (رضي الله عنها) nikamwambia: Yaa bint Abiy Bakr! Je, hivi imekufikia kumuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Haijakuhusu jambo kwangu, nami hainihusu jambo kwako yaa bin Al-Khattwaab, juu yako kumuwaidhi (bint yako)! Nikamwendea Hafswah bint ‘Umar nikamwambia: Yaa Hafswah! Imenifikia (khabari) kwamba umemuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na nimetambua kuwa hakupendi! Na lau ningekuwa (si baba yako) angekutaliki! Hafswah akalia sana. Nikamwambia: Yuko wapi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Yuko chumba cha darini. Nikaenda nikamkuta Rabaah, mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekaa kitako kingoni mwa dirisha akinin’giniza miguu yake juu katika ufumbi wa shina la mtende ambalo likimsaidia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kupanda (chumba cha darini) na kuteremkia. Nikamwambia: Yaa Rabaah! Niombee idhini kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rabaah akatazama chumbani kisha akanitazama mimi wala hakusema kitu. Kisha nikasema: Yaa Rabaah! Niombee idhini kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rabaah akatazama chumbani kisha akanitazama mimi wala hakusema kitu. Kisha nikapandisha sauti yangu nikasema: Yaa Rabaah! Niombee idhini kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), mimi nadhani kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anadhania kuwa nimekuja kwa ajili ya Hafswah! Wa-Allaahi kama Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ataniamrisha nimpige (nimkate) shingo yake nitampiga! Nikapandisha sauti yangu akaniashiria nipande (kuingia chumba cha darini). Nikaingia kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikamkuta amelalia jamvi.

Nikakaa kitako akaivuta shuka yake na hakuwa na nyingine (isipokuwa hiyo tu) na jamvi hilo lilimfanyia alama ubavuni mwake. Nikatazama kwa macho yangu hicho kijichumba cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikakuta shayiri kiasi kiasi cha kibaba kimoja na kiasi cha matawi ya mimosa yamewekwa pembeni mwa chumba na mkoba wa ngozi uliobadilishwa rangi. Nikatokwa na machozi (kuona maisha duni anayoishi).

Akasema: “Nini kinachokuliza yaa Ibn Al-Khattwaab?” Nikasema: Ee Nabiyy wa Allaah! Na kwanini nisilie na hali jamvi limekufanyia alama ubavuni mwako na sioni kitu chumbani mwako humu (isipokuwa vitu vichache mno); (Mfalme) Qayswar na Kisraa wanaishi maisha ya kifakhari lakini wewe Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye Amekuteua (Allaah) hichii ndio kijichumba chako? Akasema: “Ee Ibn Al-Khattwaab! Hivi huridhiki kuwa sisi tuna Aakhirah nao wana dunia?” Nikasema: Ndio. Kisha nilipoingia kwanza niliona usoni mwake alama za ghadhabu, basi nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Unatatizwa nini na wanawake? Ungeliwataliki basi hakika Allaah Yuko pamoja nawe, na Malaika Wake na Jibriyl, na Mikaaiyl na mimi, na Abuu Bakr, na Waumini (wote) tuko nawe. Na kichache nilichosema (siku ile) na namhimidi Allaah, nilitaraji kwamba Allaah Atasadikisha kauli yangu. Basi ikateremka Aayah hii ya At-Takhyiyr (chaguo): “Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (ni khayr kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kumchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi (na Msaidizi) wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu…” (66: 4- 5) Na walikuwa ni ‘Aaishah bint wa Abuu Bakr na Hafswah ambao walishikilia na kusaidiana (kudai mali) kuliko wake wote wengine wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, umewataliki? Akasema: “Hapana.” Nikasema:  Ee Rasuli wa Allaah! Hakika niliingia Masjid nikakuta Waislamu wanacheza kwa vichangarawe (huku dhana zimewashughulisha) wakisema kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki wake zake. Je, niende kuwajulisha kuwa hukuwataliki? Akasema: “Naam ukipenda.” Nikaendelea kuongea naye mpaka (nikatanabahi) alama za ghadhabu zimepotea usoni mwake na mpaka (huzuni yake ikageuka kuwa ni furaha na hivyo) uso wake ukarudi kuwa na bashasha kama kawaida yake, akacheka na meno yake yalikuwa ya kupendeza mno kuliko watu wote! Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremka, nami nikateremka huku nikikamata shina la mtende, naye Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremka (kwa wepesi kabisa) bila ya kukamata chochote mkononi mwake (kujizuilia). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ulikuwa chumbani mwako siku ishirini na tisa. Akasema: (Mara nyingine) “Mwezi huwa ni siku ishirini na tisa.” Nikasimama mlangoni mwa Masjid nikaita kwa sauti yangu ya juu kabisa: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwataliki wake zake! Hapo ikataremka Aayah hii: “Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, wale wanaotafiti miongoni mwao wangelielewa… (4: 83). Ikawa ni mimi niliyetafiti jambo hilo. Na Allaah Akateremsha Aayah ya At-Takhyiyr (At-Tahriym 66: 4 – 5) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

[23] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu baadhi ya watu ambao walikuwa wametoka pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Maswahaba zake kwenda katika vita vya Uhud. Wakarejea nyuma na hawakuungana na wenzao. Pakawa katika Maswahaba, kuna makundi mawili; kundi moja likawa linasema tuwapige vita! Na kundi jingine likawa linasema hapana! Hapo ikateremka Aayah hii: “Basi mna nini (hata) mkawa makundi mawili kuhusu wanafiki… (4: 88) [Amehadithia Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

Sababun-Nuzuwl: Pia Al-‘Awf (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba Aayah hii imeteremshwa kuhusu baadhi ya watu Makkah ambao walisema wameingia Uislamu lakini huku wakiwaunga mkono washirikina. Walipokwenda Makkah kutimiza mahitaji yao wakaambizana: “Tutakapokutana na Maswahaba wa Muhammad hakutakuwa na madhara yoyote upande wetu.” Waumini walipopata khabari kwamba watu hao wameenda Makkah, wakasema baadhi yao: “Twendeni kwa waoga hao tuwaue kwa sababu wanawaunga mkono maadui zenu dhidi yenu!” Lakini kundi jingine la Waumini wakasema: “Subhaana Allaah! Mnataka kuua watu wanaosema kama mlivyosema kwa sababu tu hawakuhajiri au kuacha ardhi yao. Kwani inaruhusiwa kumwaga damu na kutaifisha mali yao katika hali hii?” Basi wakagawanyika makundi mawili, na wakati huo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa nao na hakukataza kundi lolote kuhusu mabishano yao. Hapo Allaah Akateremsha: “Basi mna nini (hata) mkawa makundi mawili kuhusu wanafiki…” (4: 88) [Ibn Abiy Haatim Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

[24] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu bwana mmoja ambaye alionekana kwenye vita akiwa ana msururu wa ghanima (ngawira) kisha Waislamu wakamfuata mbio. Yule bwana alipoona Waislamu wamemfikia akawasalimia lakini Waislamu wakamuua na wakachukua ghanima zake, hapo ikateremka hii Aayah: “Enyi walioamini! Mnaposafiri (kupigana jihaad) katika njia ya Allaah thibitisheni, wala msimwambie anayekutoleeni (maamkizi ya) salamu (kwamba): “Wewe si Muumini” kwa kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia…” (3: 94). [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

Na At-Tirmidhiy na Imaam Ahmad wamerekodi kwamba: Wakanong’onezana kwamba: “Anasema salaam apate kujihami tu!” Wakamuua kisha wakaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na kondoo hao, ndipo ikateremshwa Aayah hii (3: 94)

 

Na Imaam Ahmad amerekodi kwamba Al-Qa’qaa’ bin ‘Abdillaah bin Abiy Hadrad amehadithia kwamba baba yake ‘Abdullaah bin Abiy Hadrad alisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutuma (maeneo ya) ‘Adhwam. Nikatoka pamoja na kundi la Waislamu ambamo alikuweko Abuu Qataadah, Al-Haarith bin Rab’iy na Muhallam bin Juthmaamah bin Qays. Tukaendelea mpaka tukafika eneo la ‘Adhwam ambako ‘Aamir Al-Ashja’iy alitupitia akiwa amepanda ngamia wake. Alipotupitia akatusalimia na hatukumhujumu. Lakini Muhallam bin Juthmaamah alimuua na kuchukua ngamia wake kwa sababu ya matatizo baina yao. Tuliporudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tukamuhadithia yaliyotokea, hapo ikatuteremkia Qur-aan: “Enyi walioamini! Mnapotembea katika njia ya Allaah thibitisheni, wala msimwambie anayekuamkieni kwa “As-salaam…” mpaka “kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.” (4: 94)

 

[25] Sababun-Nuzuwl: Ilipoteremka kauli ya Allaah  (سبحانه وتعالى): “Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani).” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuamrisha Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) kuiandika, mara hapo akaja ‘Abdullaah bin Ummi Maktuwm(رضي الله عنه)  akilalamika kuhusu upofu wa macho yake, hapo ikateremka kauli ya Allaah kwa kuongezeka: “Wasiokuwa na dharura…” “Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani) wasiokuwa na dharura…” (4: 95) [Amehadithia Baraa bin ‘Aazib na Zayd bin Thaabit (رضي الله عنهما) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

Na katika riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy, Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy amehadithia kwamba: Nilimuona Marwaan bin Al-Hakam amekaa kitako Masjid. Nikamkabili na nikaketi karibu naye. Akatujulisha kwamba Zayd bin Thaabit amemwambia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesomea imla Aayah hii: “Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani) wasiokuwa na dharura na kati ya Mujaahiduwn katika njia ya Allaah… (4: 95). Kisha Ibn Ummi Maktuwm akaja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati akanisomea Aayah ili niiandike. Ibn Ummi Maktuwm akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ningekuwa na uwezo bila shaka ningeshiriki katika jihaad. Alikuwa ni kipofu basi hapo Allaah Akamteremshia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati mapaja yake yalikuwa juu yangu na yakawa mazito mno kwangu (kutokana na Wahyi kuteremka) mpaka nikakhofia kuwa mapaja yangu yatavunjika. Kisha Allaah Akateremsha: “wasiokuwa na dharura…”

Pia At-Tirmidhiy amerekodi kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: “Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani) wasiokuwa na dharura (4: 95) inahusiana na wale wasiotoka kwenda kupigana vita vya Badr na ambao waliokwenda Badr. Wakati vita vya Badr vilipokaribia kuanza, Abuu Ahmad bin Jahsh na Ibn Maktuwm walisema: Ee Rasuli wa Allaah! Sisi ni vipofu, je, tuna udhuru? Hapo ikateremshwa: “Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani) wasiokuwa na dharura…”

 

[26] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Muhammad bin ‘Abdir-Rahmaan bin Al-Aswad (رضي الله عنه) kwamba: Watu wa Madiynah walilazimishwa kuandaa jeshi (kupigana na watu wa Ash-Shaam katika khilaafah ya Ibn Az-Zubayr Makkah) na nikawa nimeandikwa humo. Kisha nikakutana na ‘Ikrimah, mtumwa wa Ibn ‘Abbaas aliyekuwa huru, nikamjulisha (hayo), akanikataza mno (kuingia katika orodha ya jeshi), akasema: Ibn ‘Abbaas amenijulisha kwamba baadhi wa Waislamu walikuwa na washirikina hivyo wakikithiri idadi ya washirikina dhidi ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Mshale ulikuwa unarushwa ambao ulimpiga mmoja wao (Waislamu wakiwa pamoja na washirikina) na kumuua, au hupigwa na kuuliwa (kwa upanga).” Hapo Allaah Akateremsha: “Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao…” (4: 97) Abuu Aswad akaongezea: “Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya  wanaume na wanawake na watoto… (4: 98) [Al-Bukhaariy].

Pia Adhw-Dhwahaak amesema kwamba Aayah hii imeteremshwa kuhusu baadhi ya wanafiki ambao hawakuungana na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), bali walibakia Makkah kisha wakatoka na washirikina katika vita vya Badr. Wakauawa pamoja na waliouawa. Hapo Aayah hii (4: 97) ikateremshwa kuhusu hao waliobakia pamoja na washirikina hali ya kuwa waliweza kufanya hijrah lakini hawakufanya na wakashindwa kuthibitisha Uislamu wao. Watu kama hao wamejidhulumu nafsi zao na wakaingia katika uharamisho kama ilivyokubalika na ijmaa’ na kutokana na kauli ya Allaah: “Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao” (4: 97).

 

 

[27]Sababun-Nuzuwl: Ilipoteremka kauli ya Allaah: “Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao” (4: 97).  Palikuweko mtu mmoja Makkah akiitwa Dhwamrah, yeye alikuwa ni mgonjwa akaiambia familia yake: “Nitoeni Makkah kwani nahisi joto kali la maradhi.” Familia yake wakamuuliza: “Tukupeleke wapi?” Akaashiria kwa mkono wake kuwa wampeleke Madiynah. Hapo ikateremka Aayah hii: “Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia na wasaa. Na atakayetoka nyumbani kwake…” (4; 100). [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Ibn Jariyr].

 

 

[28] Sababun-Nuzuwl: ‘Abuu ‘Ayyaash Az-Zuraqiy amesema: “Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) eneo la ‘Usfaan (sehemu maarufu karibu na Makkah) wakati washirikina walikutana na sisi wakiwa chini ya uongozi wa Khaalid bin Waliyd, nao walikuwa baina yetu na Qiblah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatuswalisha Swalaah ya Adhuhuri, basi washirikina wakasema: “Wameshughulishwa na jambo ambalo tulikuwa na fursa ya kuwahujumu.”  Kisha wakasema: “Inayofuatia ni Swalaah (ya ‘Alasiri) ambayo ni kipenzi zaidi kwao kuliko watoto wao na nafsi zao.” Hapo Jibriyl (عليه السلام) aliteremka kuleta Aayah hizi wakati wa baina ya Adhuhuri na Alasiri: “Na utakapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha…” (4: 102)  [Imaam Ahmad, Tafsiyr Ibn Kathiyr].

Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba kuhusu kauli ya Allaah: “Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu… (4: 102) inahusiana na ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf ambaye alijeruhiwa [Al-Bukhaariy].

 

[29] Maamrisho ya kutimiza Swalaah kwa wakati wake, na makemeo ya kuipuuza yamesisitizwa katika Qur-aan ana Sunnah na miongoni mwa Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni: “Kitu cha kwanza atakachohesabiwa nacho mja Siku ya Qiyaamah katika ‘amali zake ni Swalaah, ikitengenea atakuwa amefuzu na amefanikiwa, na ikiharibika atakuwa ameshapita patupu na amekhasirika…” [At-Tirmidhy na amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh].

Imaam ibn Baaz (رحمه الله)  amesema: “Yeyote atakayeweka kengele ya saa makusudi imuamshe baada ya kutoka jua akakosa Swalaah ya Alfajiri, basi mtu huyo amepuuza kuswali kwa wakati wake na hivyo ni kufru kubwa kama walivyokubaliana ‘Ulamaa wengi kwa sababu amekusudia kuswali baada ya jua kutoka. Ni sawa na mtu ambaye anachelewesha kuswali Alfajiri akaiswali karibu na Adhuhuri. [Fataawa Ibn Baaz, Kitaab As-Swalaah 10/374].

 

[30]Sababun-Nuzuwl: Sababu ya kuteremka kauli ya Allaah: “na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah. Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana.” (4: 119). Imeteremka katika jambo la kuwahasi beberu kuwa ni katika njia ya kumtii shaytwaan. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) Athaar hii ameipokea Ibn Jariyr].

 

 

 

[31]Sababun-Nuzuwl: Al-‘Awfiy amehadithia kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuhusu Aayah hii (4: 123): Watu wa Dini mbali mbali walibishana; Watu wa Tawraat walisema: “Kitabu chetu ni Kitabu bora kabisa na Nabiy wetu (Muwsaa  عليه السلام) ni Nabiy bora kabisa.” Watu wa Injiyl wakasema kama hivyo. Waislamu wakasema: “Hakuna Dini isipokuwa ya Kiislamu, Kitabu chetu kimefuta vitabu vyote vingine na Nabiy wetu ni Nabiy wa mwisho na nyinyi mmeamrishwa katika vitabu vyenu kuamini na kufuata Kitabu chetu.” Hapo Allaah Akateremsha Aayah hii: “Si kwa matamanio yenu wala si (kwa) matamanio ya Ahlil-Kitaab Atakayefanya uovu atalipwa kwayo. (4: 127) [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

[32]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadihtia Mama wa waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba: Kuhusu kauli ya Allaah: “Na wanatafuta fatwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: “Allaah Atakupeni hukmu kuhusu wao na yale mnayosomewa kwenu katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa; na mna raghba ya kuwaoa.” (4: 127) imeteremshwa kuhusu kesi ya bwana aliyekuwa anamlea bint yatima na ni msimamzi wake na mrithi wake. yatima huyo alishirikiana naye katika mali ya huyo bwana mpaka katika (shamba la) mtende. Mlezi huyo akawa na raghba ya kumuoa yatima (juu ya kuwa hakumpenda) na hakupenda kumuozesha mtu mwengine asije kushirikiana naye mali yake (ya yatima) ambayo anashirikiana naye (huyo bwana mlezi) kwa hiyo kwa sababu hii mlezi huyo alimzuia yatima huyo kuolewa, hapo ikateremshwa Aayah hii (4: 127) na inayofuatia (4: 128) [Al-Bukhaariy].

 

Katika riwaayah nyengine, ‘Urwah alimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها) kuhusu Aayah: “Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima; basi oeni waliokupendezeni katika wanawake;…” (4: 3).  Aaishah (رضي الله عنها) akahadithia kisa kama hicho cha bint yatima kwa nyongeza kuwa huyo bwana mlezi alitaka kumuoa kwa mahari kidogo kabisa kuliko walivyokuwa wakipewa wanawake wengine walio kama hali yake. Kisha watu wakaenda kutafuta fatwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ndipo Allaah Akateremsha Aayah: “Na wanatafuta fatwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake” (4: 127). [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Dhulma waliyokuwa wakifanyiwa mayatima zama za jaahiliyyah: ‘Aliy bin Abiy Twalhah amesema: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Ilikuwa wakati wa jahaaliyya, Mlezi wa yatima mwanamke humfunga kamba binti yatima, hapo huwa hakuna ruhusa mtu kumuoa. Akiwa mzuri na akipenda kumuoa anamuoa na kudhibiti mali yake. Akiwa si mzuri, hamruhusu aolewe mpaka afariki, na hapo akifariki yeye hurithi mali yake. Allaah Akaharamisha hii Akasema: “Na juu ya wanaokandamizwa miongoni mwa watoto…” (4: 127).

 

[33]Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa kuhusu bwana mmoja aliyekuwa na mke lakini hakuwa akimuonyesha mahaba wala hamkithirishii katika mahaba na wala hamuonyeshi mwenendo uliokuwa mzuri. Huyo bwana hakutaka kuendelea (kuwa katika ndoa naye), na alishazaa naye mtoto, lakini huyo mke hakupenda apewe talaka. Basi akamwambia mumewe: “Nakuruhusu uishi na mke mwengine” [Al-Bukhaariy na Muslim]. Katika riwaaya nyengine mwanamke huyo alisema: “Naachilia mbali haki zangu, lakini usinitaliki.” Hapo ikateremka Aayah hii: “Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe nushuwzaa (uonevu wa ndoa) au kutengwa…” (4: 120).

 

[34]Faida: Miongoni mwa yanayomtoa mtu nje ya Uislamu ni kufanyia istihzai Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kama ilivyotajwa katika Nawaaqidhw Al-Islaam: “Mwenye kufanyia istihzai (shere) kwa chochote katika Dini ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) au akafanya utani katika thawabu au katika adhabu za Allaah, basi amekufuru.” [Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab, Nawaaqidhw Al-Islaam].

 

[35]As-Sabt: Rejea tanbihi (2: 65) (4: 47).

[36]Faida: Hii Aayah pia ni dalili nyengineyo inayothibitisha kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) hakufishwa bali amenyanyuliwa na Allaah mbinguni. Maelezo zaidi rejea tanbihi (3: 55).

[37]Faida: Rejea tanbihi (3: 55) ni hoja na dalili bayana kwa wanaokanusha kuteremka kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) zama za mwisho kukaribia Qiyaamah kama ni dalili mojawapo kubwa ya kutokea Qiyaamah. Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) atateremka kutoka mbinguni kuja duniani kama ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah.

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾

Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao. [An-Nisaa: 159].

((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا)) 

((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu)). [Al-Bukhaariy, Muslim].

Na pia kuna Ahaadiyth nyingi nyingine za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zimethibiti kama ifuatayo:

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu na atavunja misalaba, na kuua nguruwe, na ataondosha jizyah (ushuru kutoka kwa wasio Waislamu ambao wamo katika himaya ya serikali ya Waislamu). Kisha kutakuwa na mali nyingi hadi itafikia kuwa hakuna mtu wa kupokea sadaka. Wakati huu sijda moja itakuwa ni bora kwao kuliko maisha haya na yote yaliyomo (katika dunia).” Kisha Abuu Huraryah akasema: Someni mkipenda: “Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.” (4: 159)[Al-Bukhaariy]

 

 

 

[38]Al-Asbaatw: Ni makabila yaliyotokana na wana kumi na mbili wa Nabiy Ya’quwb (عليه السلام)   waliotoka Manabii.

 

[39]Faida: Allaah (سبحانه وتعالى) Alimsemesha Muwsaa (عليه السلام) Maneno kwa uhakika wake na si majazi kama wanavyosema watu wa bid’ah  bali ni maneno yaliyojengeka kwa herufi na sauti na Swiffah ya Al-Kalaam (Maneno) ni Swiffah iliyothibiti kwa Allaah kwa uhakika wake bila kuifanyia Swiffah hii tamthiyl wala takyiyf na bila kuifanyia ta’twiyl wala tahriyf na hii ndiyo kauli ya sawa ambayo wamepita kwayo Salaf na Maimaamu wa haki katika Uislamu katika Swifaat zote zilizokuja ndani ya Qur-aan na Sunnah zilizokuwa Swahiyh.

 

[40]Allaah (سبحانه وتعالى) Amewakataza Ahlul-Kitaab wasimfanye ‘Iysaa na Mama yake kuwa ni washirika wa Allaah bali hao ni waja wawili katika waja wema wa Allaah na si washirika Wake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) Akimzungumzia ‘Iysaa (عليه السلام) katika Suwrat Maryam (19: 30-36) Na pia katika Suwratul-Maaidah (5: 17, 72-76). 

 

 

 

[41]Sababun-Nuzuwl: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtembelea Jaabir (رضي الله عنه) alipokuwa mgonjwa, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta Jaabir akiwa amezimia kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatawadha na akamrashia maji ya wudhuu, Jaabir akazindukana, kisha Jaabir akamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) namna gani ataigawa mali yake kwa sababu hali yake ni hali ya Al-Kalaalah (asiye watoto, wala wazazi. Au asiye na mrithi wa kwenda juu wala kwenda chini.), hapo ikateremka hii Aayah. [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim]. Na katika riwaayah ya At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd: “Alikuwa na dada tisa.”

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.