-->
logo

006 - Al-An'aam

 الأنْعَام

Al-An’aam: 6[1]



Imteremshwa Makkah





بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ





الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١﴾

1. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na nuru; kisha wale ambao wamekufuru wanawasawazisha wengine na Rabb wao.







هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akahukumu muda maalumu, na uko Kwake muda maalumu uliokadiriwa, kisha nyinyi mnatilia shaka.







وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾

3.  Na Yeye ni Allaah mbinguni na ardhini; Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu; na Anajua yale mnayoyachuma.[2]







وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤﴾

4.  Na haiwafikii Aayah yoyote ile katika Aayaat za Rabb wao isipokuwa huwa ni wenye kuipuuza.





فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٥﴾

5. Kwa yakini wameikadhibisha haki ilipowajia; basi zitawafikia khabari muhimu za yale waliyokuwa kwayo wakiyafanyia istihzai.







أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ ﴿٦﴾

6. Je, hawaoni ni karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika ardhi yale ambayo Hatujapata kuwamakinisha nyinyi; na Tukawapelekea mvua tele iendeleayo; na Tukajaalia mito ipitayo chini yao. Tukawaangamiza kwa dhambi zao na Tukaanzisha baada yao karne nyingine.







وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧﴾

7. Na lau Tungelikuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu katika karatasi, kisha wakakigusa kwa mikono yao; bila shaka wale waliokufuru wangelisema: “Hii si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.”







وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِيَ الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ ﴿٨﴾

8. Na wakasema: “Mbona hakuteremshiwa Malaika?” Na lau Tungeliteremsha Malaika; basi ingelihukumiwa amri kisha wasingelipewa muhula.







وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ ﴿٩﴾

9. Na lau Tungelimfanya Malaika, bila shaka Tungelimfanya mtu na Tungeliwatatanishia yale wanayojitatanisha.







وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾

10. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Rusuli kabla yako, lakini wale waliofanya kejeli, yaliwazunguka yale yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.







قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾

11. Sema: “Nendeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.”







قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢﴾

12.  Sema: “Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini?” Sema: “Ni vya Allaah. Ameandika juu ya Nafsi Yake rahmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah; hapana shaka yoyote ndani yake.” Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.







وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣﴾

13. Na ni Vyake vyote vinavyotulia katika usiku na mchana. Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.







قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤﴾

14. Sema: “Je, nimfanye mlinzi asiyekuwa Allaah; Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayelisha na wala halishwi?” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu.” Na wala usijekuwa kabisa miongoni mwa washirikina.







قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥﴾

15. Sema: “Hakika mimi nakhofu, ikiwa nitamuasi Rabb wangu, adhabu ya Siku adhimu.”







مَّن يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ ﴿١٦﴾

16. Atakayeepushwa nayo (adhabu) Siku hiyo; basi kwa yakini (Allaah) Amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu bayana.







وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾

17. Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kukuondolea hiyo isipokuwa Yeye; na Akikugusisha khayr, basi Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.







وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١٨﴾

18. Naye ni Mwenye kudhibiti juu ya waja Wake; Naye ni Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.







قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّـهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿١٩﴾

19. Sema: “Kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi?” Sema: “Allaah; ni Mwenye kushuhudia yote baina yangu na baina yenu. Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia. Je, hivi nyinyi hakika mnashuhudia kwamba wako waabudiwa wengine pamoja na Allaah?” Sema: “Mimi sishuhudii (hayo).” Sema: “Hakika Yeye ni Muabudiwa wa haki Mmoja (Pekee), na kwamba hakika mimi sihusiki na mnavyomfanyia shirki.”







الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾

20. Wale Tuliowapa Kitabu wanaitambua (Tawhiyd au Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyotambua watoto wao. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.







وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٢١﴾

21. Na nani mdhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo au anayekadhibisha Aayaat Zake? Hakika madhalimu hawatofaulu.







وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Na Siku Tutakayowakusanya wote pamoja, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: “Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mnadai (kuwashirikisha na Allaah)?”







ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ ﴿٢٣﴾

23. Kisha haitokuwa fitnah yao isipokuwa kusema: “Wa-Allaahi Rabb wetu, hatukuwa washirikina.”







انظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Tazama vipi wamesema uongo juu ya nafsi zao; na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.







وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا ۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na miongoni mwao, wanaotega sikio kukusikiliza. Na Tumejaalia juu ya nyoyo zao vifuniko wasiyafahamu; na katika masikio yao uziwi. Na wanapoona kila Aayah (ishara, dalili) hawaiamini; hata wanapokujia kukubishia husema wale waliokufuru: “Hizi si chochote ila ni hekaya za watu wa kale.” 







وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٦﴾

26. Nao wanazuia wengine (kufuata haki) naye; nao wenyewe wanajiweka mbali naye. Na (hivyo) hawaangamizi isipokuwa nafsi zao na wala hawahisi. 







وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٧﴾

27. Na lau ungeliona watakaposimamishwa kwenye moto; kisha wakasema: “Laiti tungelirudishwa (duniani) na wala hatutakadhibisha Aayaat za Rabb wetu, na tutakuwa miongoni mwa waumini.”







بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٢٨﴾

28. Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha kabla. Na lau wangelirudishwa; kwa yakini wangeyarudia yale waliyokatazwa; na hakika wao ni waongo.







وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na walisema: “Haya si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia tu; na wala sisi hatutofufuliwa.”







وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na lau ungeliona watakaposimamishwa mbele ya Rabb wao. Atasema:  Je, haya si ya kweli? Watasema: “Ndio, tunaapa kwa Rabb wetu.” Atasema: “Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru.”







قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَا حَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ ﴿٣١﴾

31. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah; hata itakapowajia Saa (mauti) kwa ghafla; watasema: “Ee majuto yetu kwa yale tuliyokusuru humo”, na ilhali wao wanabeba mizigo yao (ya dhambi) migongoni mwao. Tanabahi!  Uovu ulioje wanayobeba!







وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٣٢﴾

32. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao. Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?







قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ ﴿٣٣﴾

33. Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha Aayaat za Allaah.







وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا ۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ وَلَقَدْ جَاءَكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na kwa yakini walikadhibishwa Rusuli kabla yako, wakasubiri juu ya yale waliyokadhibishwa; na wakaudhiwa hata ilipowafikia nusura Yetu. Na hakuna abadilishaye maneno ya Allaah. Zimekwishakujia khabari za Rusuli (waliopita).







وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِيَ نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُم بِآيَةٍ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٣٥﴾

35. Na kama imekuwa kukengeuka kwao ni mashaka mno kwako, basi ukiweza kutafuta upenyo chini kwa chini katika ardhi au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Aayah (basi fanya). Na kama Angetaka Allaah Angeliwakusanya katika uongofu. Basi usiwe miongoni mwa majahili.







إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَالْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٣٦﴾

36. Hakika wanaitikia wale wanaosikia (kwa nyoyo za iymaan). Ama wafu (wa nyoyo) Allaah Atawafufua, kisha Kwake watarejeshwa.





وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يُنَزِّلَ آيَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٧﴾

37.  Na walisema: “Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (muujiza, ishara) kutoka kwa Rabb wake?” Sema: “Hakika Allaah ni Muweza wa kuteremsha Aayah lakini wengi wao hawajui.” 







وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ ﴿٣٨﴾

38. Na hakuna kiumbe chochote kinachotembea katika ardhi na wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umati mfano wenu. Hatukusuru katika Kitabu kitu chochote. Kisha kwa Rabb wao watakusanywa.







وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٣٩﴾

39. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu ni viziwi na mabubu katika viza. Allaah Humpotoa Amtakaye na Humweka Amtakaye juu ya njia iliyonyooka. 







قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٠﴾

40. Sema: “Je, mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Saa, je, mtamwomba ghairi ya Allaah? (Jibuni) mkiwa ni wakweli.”







بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ ﴿٤١﴾

41. Bali Yeye Pekee Ndiye mtayemwomba, kisha Akitaka Ataondoa yale (ya dhiki) mliyomwomba; na mtasahau mnayoyashirikisha (pamoja Naye).







وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na kwa yakini Tulipeleka (Rusuli) kwa ummah nyingi kabla yako; Tukawatia katika dhiki za ufukara na madhara ya magonjwa na misiba ili wapate kunyenyekea.







 فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾

43. Basi kwa nini ilipowafikia adhabu Yetu wasinyenyekee? Lakini nyoyo zao zimekuwa ngumu na shaytwaan akawapambia yale waliyokuwa wakitenda.







فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ ﴿٤٤﴾

44. Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwafungulia milango ya (taanisi za) kila kitu, mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa; Tukawachukua ghafla (kawaadhibu), basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.







فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٥﴾

45. Basi ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu; na AlhamduliLLaah; Rabb wa walimwengu.







قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّـهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ ﴿٤٦﴾

46. Sema: “Mnaonaje ikiwa Allaah Atakuondoleeni kusikia kwenu na kuona kwenu na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu; je, ni muabudiwa wa haki yupi ghairi ya Allaah Atakuleteeni hayo?” Tazama jinsi Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat kisha wao wanakengeuka.







قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٧﴾

47. Sema: “Mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah ghafla au kwa dhahiri; Je, kwani huangamizwa isipokuwa watu madhalimu?”







وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ آمَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na Hatupeleki Rusuli isipokuwa ni wabashiriaji na waonyaji. Basi yeyote atakayeamini na kutengenea; haitokuwa khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.







وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٤٩﴾

49. Na wale waliokadhibisha Aayaat Zetu itawagusa adhabu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki.







قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ ﴿٥٠﴾

50. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah; na wala kwamba najua ya ghayb; na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale nilofunuliwa Wahy.” Sema: “Je, analingana sawasawa kipofu na mwenye kuona?  Basi hamtafakari?”







وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٥١﴾

51. Na waonye kwayo (Qur-aan) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Rabb wao; hawana badala Yake mlinzi wala mwombezi - huenda wapate kuwa na taqwa.







وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢﴾

52. Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata ukawafukuza; utakuja kuwa miongoni mwa madhalimu.[3] 







وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوا أَهَـٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّن بَيْنِنَا ۗ أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ ﴿٥٣﴾

53. Na hivyo ndivyo Tulivyowafanyia mtihani baadhi yao kwa baadhi ili waseme: “Je, hawa ndio wale Aliowafadhilisha Allaah baina yetu?” Je, kwani Allaah Hajui zaidi wanaoshukuru?







وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٤﴾

54. Na wanapokujia wale wanaoamini Aayaat Zetu basi sema: “Salaamun ‘alaykum! Rabb wenu Ameandika juu ya Nafsi Yake rahmah; kwamba yeyote miongoni mwenu atakayetenda ovu kwa ujahili, kisha akatubia baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.”







وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٥٥﴾

55. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat na ili idhihirike njia ya wahalifu.







قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۚ قُل لَّا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ ۙ قَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

56. Sema: “Hakika mimi nimekatazwa kuabudu wale mnaowaomba asiyekuwa Allaah.” Sema: “Sifuati hawaa zenu (kwani nikifuata,) kwa yakini nitakuwa nimepotoka, hapo nami sitokuwa miongoni mwa walioongoka.”







قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧﴾

57. Sema: “Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anasimulia ya haki; Naye ni Mbora wa wenye kuamua hukumu.”







قُل لَّوْ أَنَّ عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ ﴿٥٨﴾

58. Sema: “Lau ningelikuwa ninayo yale mnayoyaharakiza, basi bila shaka lingehukumiwa jambo baina yangu na baina yenu. Na Allaah Anawajua zaidi madhalimu.”







وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾

59. Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, na wala punje katika viza vya ardhi, na wala kilichorutubika na wala kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi.







وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٦٠﴾

60. Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala) na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadiriwa. Kisha Kwake Pekee ni marejeo yenu, kisha Atakujulisheni kuhusu yale mliyokuwa mkiyatenda.







وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ﴿٦١﴾

61. Naye ni Mwenye kudhibiti juu ya waja Wake, na Anakutumieni Malaika wanaohifadhi hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.



    

  

ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ ﴿٦٢﴾

62. Kisha hurudishwa kwa Allaah Rabb wao wa haki. Tanabahi! Hukumu ni Yake Pekee; Naye ni Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu.







قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٦٣﴾

63. Sema: “Nani Anakuokoeni kutoka viza vya bara na bahari mnapomuomba kwa kunyenyekea na kwa siri” (mkisema): “Akituokoa kutokana na (janga) hili; bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru.”







قُلِ اللَّـهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ ﴿٦٤﴾

64. Sema: “Allaah Anakuokoeni katika hayo na katika kila janga; kisha nyinyi mnamshirikisha.”







قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ ﴿٦٥﴾

65. Sema: “Yeye ni Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu, au Akutatanisheni mfarikiane kuwa makundi na Akuonjesheni baadhi yenu (vurugu la) nguvu za wengineo.” Tazama jinsi Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat wapate kufahamu.







وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿٦٦﴾

66. Na wakaikadhibisha (Qur-aan) watu wako na hali ni haki. Sema: “Mimi si mdhamini wenu.”









لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٦٧﴾

67. Kwa kila khabari ina wakati maalumu, na mtakuja kujua.







وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨﴾

68. Na unapowaona wale wanaoshughulika kupiga porojo katika Aayaat Zetu; basi jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.







وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَلَـٰكِن ذِكْرَىٰ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٦٩﴾

69. Wala si juu wale wenye taqwa, kuwa wana jukumu nao (makafiri) kwa lolote, lakini ni ukumbusho ili huenda wapate kuwa na taqwa. 







وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَا ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٧٠﴾

70. Na waachilie mbali wale walioichukua Dini yao mchezo na pumbao, na ukawaghuri uhai wa dunia, basi wakumbushe kwayo (Qur-aan) isije kila nafsi ikaangamizwa kwa yale iliyoyachuma, haina pasi na Allaah mlinzi wala mwombezi. Na hata ikitoa fidia ya kila aina haitopokelewa. Hao ndio wale walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma; watapata kinywaji cha maji ya kutokota na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakiyakufuru.







قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّـهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾

71. Sema: “Je, tumwombe asiyekuwa Allaah ambaye hawezi kutunufaisha wala kutudhuru na tuje kurudishwa nyuma juu ya visigino vyetu baada ya kuwa Ameshatuongoza Allaah? Kama yule ambaye ameshawishiwa na mashaytwaan akikanganyika katika ardhi, anao marafiki wanamwita katika mwongozo:  Njoo kwetu!”  Sema: “Hakika Mwongozo wa Allaah ndio Mwongozo na tumeamrishwa tujisalimishe kwa Rabb wa walimwengu.”







وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na kuwa simamisheni Swalaah na mcheni Yeye, Naye Ndiye Ambaye Kwake mtakusanywa.







وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣﴾

73. Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: “Kun!” basi (jambo) huwa! Kauli Yake ni haki.  Naye Atakuwa na ufalme Siku itakapopulizwa baragumu. Mjuzi wa ghayb na dhahiri. Naye ni Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.







وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً ۖ إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٧٤﴾

74. Na pindi Ibraahiym alipomwambia baba yake Aazar: “Je, unachukua masanamu kuwa ni waabudiwa? Hakika mimi nakuona na watu wako katika upotofu wa bayana.”







وَكَذَٰلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ ﴿٧٥﴾

75. Na hivyo ndivyo Tulivyomwonyesha Ibraahiym ufalme wa mbingu na ardhi na ili awe miongoni mwa wenye yakini.







فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَىٰ كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ ﴿٧٦﴾

76. Na ulipomwingilia usiku akaona sayari ing’aayo. Akasema: “Huyu ni Rabb wangu.” Ilipotoweka akasema: “Hakika mimi sipendi wanaotoweka.” 







فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ ﴿٧٧﴾

77. Kisha alipoona mwezi umechomoza akasema: “Huyu ni Rabb wangu.” Ulipotoweka akasema: “Asiponiongoza Rabb wangu; bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu waliopotea.”







فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَـٰذَا رَبِّي هَـٰذَا أَكْبَرُ ۖ فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿٧٨﴾

78.  Kisha alipoliona jua limechomoza akasema: “Huyu ni Rabb wangu, huyu ni mkubwa zaidi.” Lilipotoweka akasema: “Enyi watu wangu! Hakika mimi simo katika yale mnayoyashirikisha (na Allaah).”







إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٧٩﴾

79. “Hakika mimi nimeelekeza uso wangu kwa Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi nimeelemea haki, nami si katika washirikina.”







وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ ۚ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانِ ۚ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَن يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا ۗ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na watu wake wakamhoji. Akasema: “Je, mnahojiana nami kuhusu Allaah na hali Amenihidi?  Na wala sikhofu mnayomshirikisha Naye (kwani sitodhurika) isipokuwa Rabb wangu Akitaka jambo. Rabb wangu Amezunguka kila kitu (kwa Ujuzi).  Je, basi hamkumbuki?”







وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨١﴾

81. “Na vipi nikhofu yale mnayoyashirikisha, na wala hamkhofu kwamba mnamshirikisha Allaah kwa ambayo Hakuyateremshia kwenu hoja. Je, basi kundi gani kati ya mawili linastahiki zaidi kuwa katika amani kama nyinyi mnajua?”







الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

82. Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika.







وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾

83. Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake.  Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.





وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾

84. Na Tukamtunukia Is-haaq, na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.







وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾

85. Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.







وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luwtw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.





وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾

87. Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.







ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

88. Hiyo ndiyo hidaaya ya Allaah, kwa hiyo, Humwongoza Amtakaye kati ya waja Wake. Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.







أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Hao ndio wale Tuliowapa Kitabu na hikma na Unabiy. Wakiyakanusha hawa (makafiri) basi kwa yakini Tumekwishayawakilisha kwa watu wasioyakanusha.







أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ ﴿٩٠﴾

90. Hao ndio ambao Allaah Amewahidi. Basi fuata kama kigezo mwongozo wao. Sema: “Sikuombeni ujira kwa hayo. Hayakuwa haya ila ni ukumbusho kwa walimwengu.”







وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١﴾

91. Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria, pale waliposema: “Allaah Hakuteremsha chochote kwa mtu.” Sema: “Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu. Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyajui nyinyi na wala baba zenu.” Sema: “Allaah” (Ameiteremsha); kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza.







وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩٢﴾

92. Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale ambayo yaliyokitangulia na ili uonye Mama wa miji, na ambao wameuzunguka. Na wale wanaoamini Aakhirah wanakiamini. Nao wanahifadhi Swalaah zao.







وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣﴾

93. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia uongo Allaah au akasema: “Nimefunuliwa Wahy” na hali hakufunuliwa Wahy wowote.   Na yule asemaye: “Nitateremsha mfano wa yale Aliyoyateremsha Allaah.” Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti, na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): “Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari kuhusu Aayaat Zake.”







وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤﴾

94. Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza; na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao ni washirika wenu. Kwa yakini yamekatika (mahusiano) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.







إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٩٥﴾

95. Hakika Allaah ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Mtoaji kilicho mfu kutokana na kilicho hai. Huyo Ndiye kwenu Allaah. Basi vipi mnaghilibiwa?







فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٩٦﴾

96. Mpasuaji wa mapambazuko ya asubuhi, na Akajaalia usiku kuwa ni    mapumziko; na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hivyo ndio ukadiriaji wa Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote. 







وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧﴾

97. Na Yeye Ndiye Ambaye Aliyekufanyieni nyota ili muongozwe kwazo katika viza vya bara na bahari. Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua.







وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ﴿٩٨﴾

98. Na Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, basi (pako) mahali pa kustakiri na pa kuhifadhiwa. Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaofahamu.[4]







وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji, Tukatoa kwayo mimea ya kila kitu, na Tukatoa kutoka humo mimea ya kijani, Tunatoa kutoka humo punje zinazopandana; na katika mitende, katika makole yake mashada yenye kuning’inia chini kwa chini, na mabustani ya mizabibu na zaytuni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Tazameni matunda yake yanapozaa na na kuiva kwake. Hakika katika hayo mna Aayaat (ishara, zingatio) kwenu kwa watu wanaoamini.







وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Na wakamfanyia Allaah majini kuwa ni washirika Wake; na hali Amewaumba. Na wakampachikia uongo bila ya ujuzi wowote kuwa Ana wana wa kiume na wa kike. Subhaanahu wa Ta’aalaa! (Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Ulwa) kutokana na ambayo wanavumisha.







بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

101. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.







ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾

102. Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.









لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

103. Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.[5]







قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿١٠٤﴾

104. Kwa yakini imekujieni nuru za elimu kutoka kwa Rabb wenu. Basi aliyeona akatambua ni kwa faida ya nafsi yake; na aliyepofuka basi ni dhidi yake, (sema) “nami si mwenye kuwahifadhi.”







وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat na (makafiri) waseme: “Umedurusu” (kutoka Ahlil-Kitaab) na ili Tuibainishe kwa watu wenye kujua.







اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٦﴾

106. Fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy kutokana na Rabb wako: Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye, na jitenge na washirikina.







وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٧﴾

107. Na lau Allaah Angetaka wasingelifanya shirki. Na Hatukukufanya wewe mwenye kuwahifadhi, na wala wewe si mdhamini wao.







وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٠٨﴾

108. Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah; wasije nao kumtukana Allaah kwa uadui bila ya ujuzi. Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah ‘amali zao, kisha kwa Rabb wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakitenda.







وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٩﴾

109. Na waliapa kwa Allaah kwa viapo vya nguvu; kwamba ikiwafikia Aayah (muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: “Hakika Aayaat ziko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba zitakapokuja hawatoamini?”







وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١٠﴾

110. Na Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza. Na Tunawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wanatangatanga kwa upofu.







وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾

111. Na lau kama Sisi Tungeliwateremshia Malaika na wakasemeshwa na wafu na Tukawakusanyia kila kitu mbele yao wasingeliamini ila Allaah Atake, lakini wengi wamo katika ujahili.  







وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾

112. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui - mashaytwaan katika wana Aadam na majini wakidokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya ghururi. Na lau Angetaka Rabb wako wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga.







وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ ﴿١١٣﴾

113. Na ili zielemee katika (udanganyifu) nyoyo za wale wasioamini Aakhirah na ili waridhike nayo na ili wachume (madhambi) wanayoyachumia.







أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١١٤﴾

114. (Sema): “Je, nitafute hakimu ghairi ya Allaah na hali Yeye Ndiye Ambaye Aliyekuteremshieni Kitabu kilichofasiliwa?” Na wale Tuliowapa Kitabu (kabla) wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Rabb wako kwa haki. Basi usijekuwa miongoni mwa wanaotia shaka. 







وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١١٥﴾

115. Na limetimia neno la Rabb wako kwa kweli na uadilifu. Hakuna mwenye kuyabadilisha maneno Yake. Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.







وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza na njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.







إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿١١٧﴾

117. Hakika Rabb wako Anajua zaidi mwenye kupotea na njia Yake. Naye Anajua zaidi wenye kuhidika.







فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾

118. Basi kuleni katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa) mkiwa nyinyi ni wenye kuziamini Aayaat (na hukmu) Zake.







وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ ﴿١١٩﴾

119. Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo. Na hakika wengi wanapotoa (wengine) kwa hawaa zao bila ya elimu. Hakika Rabb wako Yeye Anajua Zaidi wenye kutaadi.







وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ ﴿١٢٠﴾

120. Na acheni dhambi zilizodhihirika na zilizofichika. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.







وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ ﴿١٢١﴾

121. Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ufasiki. Na hakika mashaytwaan wanadokeza marafiki wao wandani wabishane nanyi. Na mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.[6] 







أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٢﴾

122. Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza si mwenye kutoka humo? Hivyo ndivyo walivyopambiwa makafiri yale waliyokuwa wakiyatenda.







وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia katika kila mji wahalifu wao wakuu kabisa ili wafanyie njama humo. Na hawafanyii njama ila nafsi zao, na wala hawahisi.







وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ۘ اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّـهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿١٢٤﴾

124. Na inapowajia Aayah (muujiza, hoja) husema: “Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa yale waliopewa Rusuli wa Allaah.  Allaah Anajua zaidi wapi Aweke risala Yake. Itawasibu wale waliohalifu, udhalilifu mbele ya Allaah na adhabu kali kwa yale waliyokuwa wakifanya makri. 







فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ اللَّـهُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢٥﴾

125. Basi yule ambaye Allaah Anataka kumhidi, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni. Hivyo ndivyo Allaah Anavojaalia unajisi (na adhabu) juu ya wale wasioamini. 







وَهَـٰذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾

126. Na hii ni njia ya Rabb wako iliyonyooka. Kwa yakini Tumefasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaokumbuka.







لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٧﴾

127. Watapata Daarus-Salaam (nyumba ya amani Jannah) kwa Rabb wao.  Naye Ndiye Mlinzi wao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. 







وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُم مِّنَ الْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُم مِّنَ الْإِنسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٢٨﴾

128. Na Siku Atakapowakusanya wote (Allaah Atasema):  Enyi hadhara ya majini! Kwa yakini mmetafuta kwa wingi (kuwapotoa) katika wana Aadam. Na watasema marafiki wao wandani katika wana Aadam: “Rabb wetu! Tulinufaishana baadhi yetu na wengineo, na tumefikia muda wetu ambao Umetupangia.” (Allaah) Atasema: Moto ndio makazi yenu, ni wenye kudumu humo, isipokuwa Atakavyo Allaah. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.





وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٢٩﴾

129. Na hivyo ndivyo Tunavyowafanya baadhi ya madhalimu kuwa marafiki wandani wao kwa wao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.







يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا شَهِدْنَا عَلَىٰ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Enyi hadhara ya majini na wana Aadam! Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na Wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: “Tumeshuhudia dhidi ya nafsi zetu.” Na uliwaghuri uhai wa dunia; na wameshuhudia dhidi ya nafsi zao kwamba hakika wao walikuwa ni makafiri.







ذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَافِلُونَ ﴿١٣١﴾

131. Hivyo ni kwa kuwa Rabb wako Hakuwa Mwenye kuangamiza mji kwa dhulma hali wenyewe wameghafilika.







وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na wote wana daraja mbalimbali kwa yale waliyoyatenda. Na Rabb wako si Mwenye kughafilika na yale waliyoyatenda.







وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِن بَعْدِكُم مَّا يَشَاءُ كَمَا أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ ﴿١٣٣﴾

133. Na Rabb wako ni Mkwasi Mwenye rahmah. Akitaka Atakuondosheni na Aweke wengine watakaofuatia baada yenu kwa Atakao, kama vile Alivyokuzalisheni kutokana na vizazi vya watu wengine.







إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَآتٍ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿١٣٤﴾

134. Hakika mnayoahidiwa bila shaka yatakuja tu! Nanyi si wenye kuweza kukwepa.







قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿١٣٥﴾

135. Sema: “Enyi kaumu yangu! Tendeni kwa tamkini yenu, nami pia natenda yangu. Mtakuja kujua nani atakayekuwa na hatima njema ya makazi Aakhirah. Hakika madhalimu hawatofaulu.”







وَجَعَلُوا لِلَّـهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَـٰذَا لِلَّـهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَائِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّـهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَائِهِمْ ۗ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿١٣٦﴾

136. Na wamemfanyia Allaah fungu katika mimea na wanyama Aliyoumba. Wakasema: “Hili ni la Allaah” kwa madai yao, “na hili ni kwa ajili ya washirika wetu.” Basi yaliyokuwa kwa ajili ya washirika wao havimfikii Allaah. Na yaliyokuwa kwa ajili ya Allaah hufika kwa washirika wao. Uovu ulioje wanayoyahukumu.







وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ ۖ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٧﴾

137. Na hivyo ndivyo washirikina wengi walivyopambiwa na washirika wao (wanaowaabudu) kuua watoto wao ili wawateketeze na wawatatanishe dini yao. Na lau Allaah Angetaka, wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga.







وَقَالُوا هَـٰذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَن نَّشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَّا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٨﴾

138. Na wakasema kwa madai yao: “Hawa wanyama wa mifugo na mazao ni marufuku; hawatowala ila wale tuwatakao, na wanyama imeharamishwa migongo yao (kuwapanda).”  Na wanyama (wengine) hawalitaji Jina la Allaah juu yao (wanapowachinja), wanamtungia uongo (Allaah). Atawalipa kwa yale waliyokuwa wakiyatunga.







وَقَالُوا مَا فِي بُطُونِ هَـٰذِهِ الْأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰ أَزْوَاجِنَا ۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاءُ ۚ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٣٩﴾

139. Na wakasema: “Vilivyokuwemo matumboni mwa wanyama hawa ni makhsusi kwa wanaume wetu na wameharamishiwa kwa wake zetu.” Lakini wanapokuwa ni nyamafu (wanapozaliwa), basi katika hao huwa wanashirikiana (na wanawake kula). Hakika Atawalipa uvumishi wao. Hakika Yeye ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.







قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّـهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٤٠﴾

140. Kwa yakini wamekhasirika wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya ujuzi na wakaharamisha vile Alivyowaruzuku Allaah kwa kumtungia Allaah. Kwa yakini wamepotea wala hawakuwa wenye kuhidika. 







وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٤١﴾

141. Naye (Allaah) Ndiye Ambaye Aliyezalisha mabustani yanayotambaa na yasiyotambaa. Na mitende na mimea yakitofautiana kwa ladha yake, na zaytuni na makomamanga yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Kuleni katika matunda yake yanapotoa mazao na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye Hapendi wafanyao israfu.





وَمِنَ الْأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٤٢﴾

142. Na katika wanyama wa mifugo (Amekuumbieni) wabebao mzigo na wadogodogo. Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah na wala msifuate hatua za shaytwaan, hakika yeye ni adui bayana kwenu.







ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۖ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّئُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٤٣﴾

143. Jozi nane: (za dume na jike) katika kondoo wawili na katika mbuzi wawili. Sema: “Je, Ameharamisha wote madume wawili au majike mawili, au viliomo fukoni la uzazi mwa majike yote mawili? Nijulisheni kwa elimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.”







وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّـهُ بِهَـٰذَا ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٤﴾

144. Na katika ngamia, wawili na katika ng’ombe wawili. Sema: “Je, Ameharamisha madume wawili au majike mawili, au waliomo fukoni la uzazi mwa majike wawili? Au nyinyi mlishuhudia Allaah Alipokuusieni haya?” Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu bila elimu. Hakika Allaah Hawaongozi watu madhalimu.







قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٥﴾

145. Sema: “Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe; kwani hiyo ni najisi au ufasiki; kimetajiwa asiyekuwa Allaah (katika kuchinjwa).” Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Rabb wako ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.





وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ الْبَقَرِ وَالْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَا إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَا أَوِ الْحَوَايَا أَوْ مَا اخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿١٤٦﴾

146. Na kwa wale walio Mayahudi Tuliharamisha kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng’ombe na mbuzi Tuliwaharamishia shahamu zao isipokuwa iliyobeba migongo yao au utumbo wao au iliyochanganyika na mifupa.  Hivyo ndivyo Tulivyowalipa kwa udhalimu wao. Na bila shaka Sisi ni Wakweli.







فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٤٧﴾

147. Wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); basi sema: “Rabb wenu ni Mwenye rahmah iliyoenea. Na wala haizuiliwi adhabu Yake kwa watu wahalifu.”







سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾

148. Watasema wale walioshirikisha: “Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu pia na wala tusingeliharamisha chochote.” Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao mpaka walipoonja adhabu Yetu.  Sema: “Je, mna elimu yoyote mtutolee? Hamfuati isipokuwa dhana tu, nanyi si lolote ila mnabuni uongo.”





قُلْ فَلِلَّـهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ ۖ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٤٩﴾

149. Sema: “Basi ni Allaah Pekee Mwenye hoja timilifu. Na Angelitaka Angelikuhidini nyote.”







قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّـهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Sema: “Leteni mashahidi wenu wanaoshuhudia kwamba Allaah Ameharamisha (wanyama) hawa.” Wakishuhudia; basi usishuhudie pamoja nao. Na wala usifuate hawaa za wale wanaokadhibisha Aayaat Zetu, na wale wasioamini Aakhirah, nao wanawasawazisha wengine na Rabb wao. 







قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾

151. Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya shariy’ah). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni  kwayo mpate kutia akilini.”







وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٢﴾

152. “Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan mpaka afikie umri wa kupevuka. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatukalifishi nafsi isipokuwa kadiri ya uwezo wake. Na mnaposema basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka.”







وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾

153. “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.”[7] 







ثُمَّ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ تَمَامًا عَلَى الَّذِي أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٤﴾

154. Kisha Tukampa Muwsaa Kitabu kutimiza (neema) juu ya yule aliyefanya ihsaan kuwa ni fasili ya kila kitu na ni mwongozo na rahmah wapate kuamini kukutana na Rabb wao.







وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٥٥﴾

155. Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe na taqwa mpate kurehemewa.







أَن تَقُولُوا إِنَّمَا أُنزِلَ الْكِتَابُ عَلَىٰ طَائِفَتَيْنِ مِن قَبْلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمْ لَغَافِلِينَ ﴿١٥٦﴾

156. Msije kusema: “Hakika Kitabu kimeteremshwa juu ya makundi mawili kabla yetu; lakini tulikuwa bila ya shaka tumeghafilika kuhusu waliyokuwa wakiyasoma.”





أَوْ تَقُولُوا لَوْ أَنَّا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْكِتَابُ لَكُنَّا أَهْدَىٰ مِنْهُمْ ۚ فَقَدْ جَاءَكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَصَدَفَ عَنْهَا ۗ سَنَجْزِي الَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ آيَاتِنَا سُوءَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يَصْدِفُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Au mkaseme: “Lau tungeliteremshiwa Kitabu basi, bila shaka tungelikuwa waongofu zaidi kuliko wao.” Kwa yakini imekwishakufikieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu na mwongozo na rahmah. Hivyo basi nani ni dhalimu zaidi kuliko yule aliyekadhibisha Aayaat za Allaah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aayaat Zetu adhabu ovu kwa yale waliyokuwa wakijitenga nayo.





هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ انتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴿١٥٨﴾

158. Je, wanangojea (lolote) isipokuwa wawafikie Malaika (kuwatoa roho) au awafikie Rabb wako (kuwahukumu) au ziwajie baadhi za Aayaat za Rabb wako? Siku zitakapokuja baadhi za Aayaat (alama za Qiyaamah) za Rabb wako haitoifaa nafsi iymaan yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika iymaan yake khayr yoyote. Sema: “Ngojeeni hakika nasi tunangojea.”







إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿١٥٩﴾

159. Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna (uhusiano) wa lolote nao. Hakika amri yao iko kwa Allaah, kisha Atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya.







مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦٠﴾

160. Atakayekuja kwa ‘amali njema basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo. Na Atakayekuja kwa ovu basi hatolipwa ila mfano wake, nao hawatodhulumiwa.





قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٦١﴾

161. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi, Ameniongoza Rabb wangu kuelekea njia iliyonyooka, Dini iliyosimama thabiti, mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.”





قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

162. Sema: “Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.”[8]







لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾

163. “Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.” 







قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾

164. Sema “Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb na hali Yeye ni Rabb wa kila kitu? Na wala nafsi yoyote haitochuma (khayr au shari) ila ni juu yake. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.”







وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾

165. Naye (Allaah) Ndiye Aliyekufanyeni makhalifa wa duniani na Akanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbali mbali ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Hakika Rabb wako ni Mwepesi wa kuakibu, na hakika Yeye bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.








[1]Faida: Atw-Twabaraaniy amenukuu kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kuwa: “Suwrah nzima ya Al-An’aam imeteremshwa Makkah, usiku, ikifuatiliwa na Malaika elfu sabini wakinyanyua sauti zao kumsabbih Allaah.”



[2] Faida:

Wamekhitilafiana Wafasiri katika kauli nne kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ

Na Yeye ni Allaah mbinguni na ardhini.

Kauli ya kwanza:

Maana yake ni: Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Ilaah Anayeabudiwa mbinguni na katika ardhi kwa sababu Yeye Pekee Ndiye Mwabudiwa wa haki katika ardhi na mbingu, kwa ushahidi wa kauli Yake (تعالى):

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ  

Na Yeye Ndiye Mwabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. [Az-Zukhruf 42: 84)]



[Al-Qurtwubiy, Ibn Kathiyr, Ash-Shanqiytwiy, Ibn Al-Anbaariy na wengineo. Taz. Al-Jaami’u li-Ahkaamil-Qur-aan (6/390), Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym (3/240), Adhwaau Al-Bayaan (7/4)]



Kauli Ya Pili: 



Kwamba maana ni: Yeye Allaah Anajua siri zenu mbinguni na katika ardhi na ushahidi ni kauli Yake (تعالى)

قُلْ أَنزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ  

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ameiteremsha Ambaye Anajua siri katika mbingu na ardhi. [Al-Furqaan (25: 6)]



Kwa kuzingatia kwamba kauli Yake: 



“mbinguni na ardhini” [Al-An’aam (6: 3)] inahusiana na: “Anajua siri zenu.”



Na amesema Imaam Ad-Daaniyy: Na imesemwa kuwa maana ni:



Yeye Ndiye Mwabudiwa mbinguni na katika ardhi.



Na kadhaalika, Al-Ashmuwniyy kaunga mkono ufafanuzi huo.



Na amesema An-Nahhaas kuwa kauli hiyo ni bora katika yaliyoelezwa juu ya Aayah hiyo.



[Al-Muktafaa Fiy Al-Waqf Wal-Ibtidaa Fiy KitaabiLLaah ‘Azza Wa Jalla (273), Manaaru Al-Hudaa Fiy Bayaan Al-Waqf Wal-Ibtidaa (265). Adhwaau Al-Bayaan Fiy Iydhwaah Al-Qur-aan bil-Qur-aan (4/7)]



Kauli Ya Tatu:

Kwamba maana yake ni:

Yeye Allaah Ambaye Yeye Yuko mbinguni na katika ardhi Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu katika ardhi.  Naye Yuko juu ya ‘Arsh Yake Akiwa juu ya viumbe Vyake wote, Akiwa Anajua siri za watu wa ardhini na ya dhahiri yao, hakuna kinachofichika Kwake katika hayo. Na ushahidi ni kauli Yake (تعالى):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾

Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?



أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾

Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu. [Al-Mulk (67: 16-17)]



Na kauli Yake (تعالى):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan juu ya ‘Arshi Istawaa. [Twaahaa (20: 5)]





Kauli Ya Nne: 



Ina maana kutangulizwa na kuakhirishwa; yaani: Yeye Allaah Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu mbinguni na ardhini. Na hii kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) .



Kauli iliyo na nguvu kabisa katika kauli hizo nne ni:

Kauli ya kwanza ambayo ni kauli ya wengi katika Mufassariyn, pamoja na kwamba kuna uwezekano wa kauli nyingine katika hizo kwa sababu kila kauli ina ushahidi wake katika Qur-aan.

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله): “Maimaam wakubwa kama Imaam Ahmad na wengineo wameifasiri kwamba: “Kuwa Yeye ni Mwabudiwa mbinguni na ardhini.” [Al-Furqaan Bayna Awliyaair-Rahmaan Wa-Awliyaai Ash-Shaytwaan (244)]

Ibn Kathiyr (رحمه الله) amesema: “Kauli iliyo sahihi kabisa ni kwamba: “Anaombwa Allaah mbinguni na ardhini; yaani Anaabudiwa na Anapwekeshwa na Anakiriwa kwa Uabudiwa Aliyekuwa mbinguni na katika ardhi na Anaitwa Allaah, na Anaombwa kwa utashi na khofu, isipokuwa aliyekanusha katika majini na bin Aadam.”  [Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym, (3/240)]





[3]Sababun-Nuzuwl: Sa’ad (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Tulikuwa watu sita pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na Ibn Mas’uwd alikuwa mmoja wao. Washirikina wakamwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Usiwaweke watu hawa karibu yako.” (Katika riwaayah nyingine ya Muslim): “Wafukuze.” Hapo ikateremka Aayah hii: “Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake…” (6: 52).



[4]Faida: Mahali pa kustakiri ni tumboni mwa mama au duniani. Mahali pa kuhifadhiwa ni ima migongoni mwa baba au kaburini.



[5]Faida: Masruwq (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilimwambia ‘Aaishah (رضي الله عنها) : Ee Mama! Je Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake? Akasema: Hayo uliyoyasema yamefanya nywele zangu zisimame kunisisimka mwili! Tambua kwamba mtu akikutajia mambo matatu yafuatayo basi yeye ni muongo! Atakayesema kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amemuona Rabb wake; Kisha akasoma: “Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana.” (6: 103) “Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa (njia ya) Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi” (42: 51). Kisha akaendelea kusema: Na atakayesema kwamba Nabiy anajua yatakayotokea kesho basi ni muongo. Kisha Akasoma: “Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho” (31: 34). Kisha akasema: Na Atakayesema kuwa Nabiy ameficha aliyofunuliwa Wahyi (na maamrisho) basi ni muongo! Kisha akasoma: “Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake…” (5: 67). Kisha akasema: Lakini Nabiy alimuona Jibriyl katika umbile lake khalisi mara mbili. [Al-Bukhaariy].

Kwa upande mwengine Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Allaah, na akasema kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. [Tafsiyr Ibn Kathiyr].



Al-Haafidhw, Ibn Hajar alisema, “Maelezo ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) yamekuja katika hali ya kutodhibitiwa (hayaelezi kama Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake au vipi) wakati kauli za mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na wenziwe zimedhibitiwa kwa kusema Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah “Kwa macho yake”. Tunaweza kuunganisha kauli hizo mbili kwa kusema mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) alikataa muono “Kwa macho yake” na kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kuwa ni kamuona kiroho.” [Fat-hul-Baariy, 8/608].



Pili, kauli hizo mbili, ya mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), kwa njia nyingine kuwa kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake wakati akiwa katika usingizi, jambo ambalo ni ndoto ya kweli na isiyokuwa alimuona Siku ya Mi’iraaj wakati kauli ya mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) inakataa kuwa Rasuli hakumuona Rabb wake wakati yeye akiwa macho, lakini kauli hiyo haikatazi kuwa  Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake akiwa usingizini. Alichokana hapa ni kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah kwa macho yake meupe, akiwa macho.



Wale ambao wanao msimamo kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake meupe wanaleta Hadiyth dhaifu. Hakuna Hadiyth Sahihi ambayo inaeleza ya kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake akiwa macho. Wenye msimamo huo wanaleta Hadiyth ya At-Tirmidhiy ambayo Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) anasema kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake. Ikrimah alimuuliza: “Vipi Aayah ambayo inasema, “Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho.” Alijibu, kuwa ni wakati tu Allaah amezungukwa na Nuru, lakini Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. “Hadiyth hii ni dhaifu.”



Kwa hali hiyo kwa namna jinsi ilivyo hakuna mgongano wa kauli, na Allaah Anajua zaidi. [Sharh ya Uswuul Al-I’itiqaad cha Al-Laalika’iy, 93/512, As-Sunnah 1/181 na Swifaat Al-Maqdisiy ukurasa 109-111].



Hapa kunathibitishwa kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Rabb wake wakati wa alipopelekwa katika safari ya Mi’raaj, na hii ndio ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jumaa’ah kuwa Allaah Haonekani duniani, kinyume na ‘Aqiydah ya Masufi wanaoamini kuwa Allaah Anaonekana duniani kwa kuegemeza tukio hilo la Mi’raaj. Kadhaalika, Aayah hiyo vilevile haikanushi kuonekana Allaah Qiyaamah, bali Qiyaamah Allaah Ataonekana katika kisimamo cha Qiyaamah na kwenye Pepo kwa dalili nyingi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kinyume na ‘Aqiydah ya makundi potofu yanayoamini kuwa Allaah Hatoonekana Aakhirah.



[6]Sababun-Nuzuwl: Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) Kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na hakika mashaytwaan wanadokeza marafiki wao wandani” Walikuwa washirikina wakisema: Kilichochinjwa kwa ajili ya Allaah msile! Lakini mnachochinja nyinyi basi kuleni! Hapo Allaah Akateremsha: “Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah.” [Ameipokea Abuu Daawuwd].



[7]Faida: Rejea tanbihi: (1: 6)



[8]Faida: Aayah (6: 161- 162) ni mojawapo ya du’aa ya kufungulia Swalaah: Pia Aayah hii ni dalili mojawapo ya haramisho la kuchinja kwa kukusudia asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى).

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.