-->
logo

089 - Al-Fajr

الْفَجْر
Al-Fajr: 89

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


وَالْفَجْرِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa Alfajiri.


وَلَيَالٍ عَشْرٍ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa masiku kumi.


وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa shufwa na witri.


وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ ﴿٤﴾
4. Na Naapa kwa usiku unapopita.


هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ ﴿٥﴾
5. Je, hakuna katika hayo kiapo kwa watu wenye uelekevu?


أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ﴿٦﴾
6. Je, hukuona vipi Rabb wako Alivyowafanya kina ‘Aad?


إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ ﴿٧﴾
7. Wa Iram, wenye urefu na nguvu kama nguzo ndefu?


الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ ﴿٨﴾
8. Ambao hawakuumbwa mfano wao katika nchi.


وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ ﴿٩﴾
9. Na kina Thamuwd ambao wamechonga miamba mabondeni.


وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ ﴿١٠﴾
10. Na Fir’awn wenye vigingi.


الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ ﴿١١﴾
11. Ambao wamevuka mipaka kuasi katika nchi.


فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ ﴿١٢﴾
12. Wakakithirisha humo ufisadi.


فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ ﴿١٣﴾
13. Rabb wako Akawamiminia mjeledi wa adhabu.


إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾
14. Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Awavizia. 


فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ ﴿١٥﴾
15. Basi mwana Aadam pale Rabb wake Anapomtia mtihanini, Akamtakaramu na Akamneemesha, husema: “Rabb wangu Amenitakarimu.”


وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ ﴿١٦﴾
16. Ama Anapomtia mtihanini, Akamdhikishia riziki yake, husema: “Rabb wangu Amenidunisha.”


كَلَّاۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ ﴿١٧﴾
17.  Laa hasha! Bali hamuwatakaramu mayatima.


وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿١٨﴾
18. Na wala hamhamasishani katika kulisha maskini.


وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا ﴿١٩﴾
19. Na mnakula urithi ulaji kamilifu na kwa uroho.


وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا ﴿٢٠﴾
20. Na mnapenda mali upendo mkubwa wa kupita kiasi.



كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا ﴿٢١﴾
21. Laa hasha! Pale ardhi pale itakapo vunjwavunjwa na kupondwapondwa.  


وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ﴿٢٢﴾
22. Na Atakapokuja Rabb wako, na Malaika safusafu.


وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾
23. Na italetwa siku hiyo Jahannam; siku hiyo mwana Aadam atakumbuka, lakini wapi atapata ukumbusho?


يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾
24. Atasema: “Ee, laiti ningelikadimisha (mazuri) kwa ajili ya uhai wangu (wa Aakhirah)”.


فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾
25. Basi siku hiyo hakuna yeyote atakayeadhibu kama adhabu Yake. 


وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ ﴿٢٦﴾
26. Na wala hakuna yeyote atakayefungisha (madhubuti) kama kufungisha Kwake (waovu).


يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾
27. (Mwema ataambiwa) “Ee nafsi iliyotua.”


ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾
28. “Rejea kwa Rabb wako ukiwa umeridhika na mwenye kuridhiwa (na Allaah).


فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾
29. “Basi ingia miongoni mwa waja Wangu.


وَادْخُلِي جَنَّتِي ﴿٣٠﴾
30. “Na ingia Jannah Yangu.”

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.