-->
logo

088- Al-Ghaashiyah

الْغَاشِيَة
Al-Ghaashiyah: 88


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ ﴿١﴾
1. Je, imekujia hadithi ya kufunikiza?


وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ ﴿٢﴾
2. Nyuso siku hiyo zitadhalilika.


عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ ﴿٣﴾
3. Zenye kufanya kazi ngumu na kuchoka mno.


تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً ﴿٤﴾
4. Zitaingia na kuungua moto uwakao vikali.


تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ ﴿٥﴾
5. Zitanyweshwa katika chemchem yenye kutokota.


لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ ﴿٦﴾
6. Hawatokuwa na chakula isipokuwa kutokana na mti wenye miba, wenye kunuka na mchungu mno.


لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ ﴿٧﴾
7. Hakinenepeshi, na wala hakisaidii kuondoa njaa.


وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ﴿٨﴾
8.  Na nyuso Siku hiyo zitakuwa ziko katika taanisi.


لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ ﴿٩﴾
9. Wakirdhika kwa juhudi zao.


فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ﴿١٠﴾
10. Kwenye Jannah ya juu.


لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً ﴿١١﴾
11. Hazitosikia humo upuuzi na ubatilifu.


فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ ﴿١٢﴾
12.  Humo mna chemchem inayobubujika.


فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ ﴿١٣﴾
13. Humo mna makochi yaliyoinuliwa.


وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ ﴿١٤﴾
14. Na bilauri zilizopangwa tayari.


وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ ﴿١٥﴾
15. Na matakia yaliyopangwa safusafu.


وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ ﴿١٦﴾
16. Na mazulia yaliyopambwa na ya fahari yaliyotandazwa.


أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾
17. Je, hawamtazami ngamia namna walivyoumbwa?


وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾
18. Na mbingu vipi zilivyonyanyuliwa?


وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾
19. Na majabali vipi yamekongomewa imara kabisa.


وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ﴿٢٠﴾
20. Na ardhi vipi ilivyotandazwa?


فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ ﴿٢١﴾
21. Basi kumbusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); hakika wewe ni mkumbushaji tu.


لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ﴿٢٢﴾
22. Wewe si mwenye kuwadhibiti.


إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ ﴿٢٣﴾
23. Isipokuwa yule atayegeuka na akakufuru.


فَيُعَذِّبُهُ اللَّـهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ ﴿٢٤﴾
24. Basi Allaah Atamuadhibu adhabu kubwa kabisa.


إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ ﴿٢٥﴾
25. Hakika ni Kwetu ni marejeo yao.


ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم ﴿٢٦﴾
26. Kisha bila shaka ni juu Yetu hesabu yao.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.