-->
logo

073 - Al-Muzzammil

الْمُزَّمِّل
Al-Muzzammil: 73


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾
1. Ee uliyejifunika.


قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا﴿٢﴾
2. Simama (kuswali) usiku kucha isipokuwa kidogo tu.


نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا﴿٣﴾
3. Nusu yake, au ipunguze kidogo.


أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا﴿٤﴾
4. Au izidishe, na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali.


إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا﴿٥﴾
5. Hakika Sisi Tutakuteremshia juu yako kauli nzito.


إِنَّ نَاشِئَةَ اللَّيْلِ هِيَ أَشَدُّ وَطْئًا وَأَقْوَمُ قِيلًا﴿٦﴾
6. Hakika kuamka usiku (kuswali) ni uthibiti zaidi wa kuathiri moyo na kuifahamu na unyofu zaidi wa maneno kutua.


إِنَّ لَكَ فِي النَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا﴿٧﴾
7. Hakika una mchana mrefu kwa shughuli nyingi.


وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا﴿٨﴾
8. Na dhukuru Jina la Rabb wako, na jitolee Kwake kwa kujitolea kikamilifu.



رَّبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلًا﴿٩﴾
9. Rabb wa Mashariki na Magharibi, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi mfanye kuwa ni Mdhamini wako.


وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا﴿١٠﴾
10. Na subiri juu ya yale wayasemayo, na wahame, mhamo mzuri.


وَذَرْنِي وَالْمُكَذِّبِينَ أُولِي النَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا﴿١١﴾
11. Na Niache Mimi na wanaokadhibisha walioneemeka; na uwape muhula kidogo.


إِنَّ لَدَيْنَا أَنكَالًا وَجَحِيمًا﴿١٢﴾
12. Hakika Sisi Tuna minyororo na moto uwakao vikali mno.


وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا﴿١٣﴾
13. Na chakula cha kusakama kooni, na adhabu iumizayo.


يَوْمَ تَرْجُفُ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ وَكَانَتِ الْجِبَالُ كَثِيبًا مَّهِيلًا﴿١٤﴾
14. Siku itakayotikisika ardhi na majabali, na majabali yatakuwa kama rundo la mchanga tifutifu.


إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا﴿١٥﴾
15. Hakika Sisi Tumekutumieni Rasuli awe shahidi juu yenu, kama Tulivyotuma Rasuli kwa Fir’awn.


فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا﴿١٦﴾
16. Lakini Fir’awn alimuasi huyo Rasuli, Tukamshika kwa maangamizi makali mno.



فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرْتُمْ يَوْمًا يَجْعَلُ الْوِلْدَانَ شِيبًا﴿١٧﴾
17. Basi vipi mtaweza kujikinga, kama mkikufuru Siku itakayowafanya watoto kuwa wenye kutoka mvi?


السَّمَاءُ مُنفَطِرٌ بِهِ ۚ كَانَ وَعْدُهُ مَفْعُولًا﴿١٨﴾
18. Mbingu zitapasuka hapo, ahadi Yake itatimizwa.


إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا﴿١٩﴾
19. Hakika hii ni ukumbusho. Basi atakaye ashike njia ya kuelekea kwa Rabb wake.


إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَاللَّـهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ ۙ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖفَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٢٠﴾
20. Hakika Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Anajua kwamba unasimama (kuswali) karibu na thuluthi mbili za usiku au nusu yake, au thuluthi yake; na kundi miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na Allaah Anakadiria usiku na mchana. Anajua kwamba hamuwezi kuukadiria wakati wake na kusimama kuswali, basi Amepokea tawbah yenu. Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan. (Allaah) Anajua kwamba watakuweko miongoni mwenu wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wanatafuta fadhila za Allaah, na wengineo wanapigana katika njia ya Allaah. Basi someni kile kilicho chepesi humo. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mkopesheni Allaah karadhi nzuri. Na chochote kile cha kheri mnachokadimisha kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Allaah. Ni bora, na ujira mkubwa zaidi. Na muombeni Allaah maghfirah, hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.