-->
logo

072 - Al-Jinn

 الْجِنّ
Al-Jinn: 72

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾
1. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza; wakasema: ‘Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu.”


يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾
2. “Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb   wetu na yeyote.”


وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا﴿٣﴾
3. “Na kwamba hakika umetukuka kabisa Ujalali wa Rabb wetu, Hakujifanyia mke wala mwana.”


وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّـهِ شَطَطًا﴿٤﴾
4. “Na kwamba safihi miongoni mwetu alikuwa akisema juu ya Allaah uongo uliopinduka mipaka.”


وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن تَقُولَ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا﴿٥﴾
5. “Na kwamba sisi tulidhania wanadamu na majini hawatosema uongo juu ya Allaah.”


وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾
6. “Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wana Aadam wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.”


وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ اللَّـهُ أَحَدًا﴿٧﴾
7. “Na kwamba wao walidhania kama mlivyodhani kwamba Allaah Hatomfufua yeyote (au Hatomtuma Rasuli).”


وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا﴿٨﴾
8. “Na kwamba sisi tulitafuta kuzifikia mbingu, basi tukazikuta zimejaa walinzi wakali na vimondo.”


وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا﴿٩﴾
9. “Na kwamba sisi tulikuwa tukikaa huko vikao kwa ajili ya kusikiliza, basi atakayetega sikio kusikiliza sasa atakuta kimondo kinamvizia.”


وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا﴿١٠﴾
10. “Na kwamba sisi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa ardhini, au Rabb wao Anawatakia uongofu.”


وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا﴿١١﴾
11. “Na kwamba miongoni mwetu ni wema, na miongoni mwetu kinyume chake; tumekuwa makundi ya njia mbali mbali.”


وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّـهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا﴿١٢﴾
12. “Na kwamba tulikuwa na yakini kwamba hatutoweza kumshinda Allaah ardhini, na wala hatutoweza kumkwepa kutoroka.”


وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَىٰ آمَنَّا بِهِ ۖ فَمَن يُؤْمِن بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا﴿١٣﴾
13. “Na kwamba sisi tuliposikia mwongozo (huu Qur-aan) tukaiamini; basi atakayemuamini Rabb wake hatoogopa kupunjwa mazuri yake na wala kuzidishiwa adhabu ya madhambi.”


وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا﴿١٤﴾
14. “Na kwamba miongoni mwetu ni Waislamu, na miongoni mwetu wakengeukaji haki; hivyo atakayesilimu, hao ndio waliofuata uongofu.”


وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا﴿١٥﴾
15. Ama wakengeukaji haki, watakuwa kuni za Jahannam.


وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقًا﴿١٦﴾
16. (Allaah Anasema):  Na kwamba lau wangelinyooka kwenye njia, bila shaka Tungeliwanywesha maji kwa wingi.


لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا﴿١٧﴾
17. Ili tuwatie katika jaribio kwayo. Na anayepuuza Ukumbusho wa Rabb wake, Atamsukuma kwenye adhabu ngumu ya kumlemea asiiweze.


وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾
18. Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.


وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا﴿١٩﴾
19. Na kwamba mja wa Allaah (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) aliposimama kumwomba (Rabb wake), walikaribia kumzonga.


قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾
20. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.”


قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾
21. Sema: “Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu.”


قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا﴿٢٢﴾
22. Sema: “Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia.


إِلَّا بَلَاغًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِسَالَاتِهِ ۚ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا﴿٢٣﴾
23. “Isipokuwa nibalighishe (haki) kutoka kwa Allaah na risala Zake.” Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Rasuli Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam ni wenye kudumu humo abadi.”


حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا﴿٢٤﴾
24. Mpaka watakapoona yale waliyoahidiwa, basi watajua ni nani msaidizi dhaifu, na mchache zaidi kwa idadi.


قُلْ إِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ مَّا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُ رَبِّي أَمَدًا﴿٢٥﴾
25. Sema: “Mimi sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Rabb wangu Atayaweka muda mrefu.”


عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا﴿٢٦﴾
26.  Mjuzi wa ghayb na wala Hamdhihirishii yeyote ghayb Yake.


إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا﴿٢٧﴾
27Isipokuwa yule Aliyemridhia miongoni mwa Rasuli basi hakika Yeye Anamwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.


لِّيَعْلَمَ أَن قَدْ أَبْلَغُوا رِسَالَاتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَيْءٍ عَدَدًا﴿٢٨﴾
28. Ili Ajue kwamba wamekwishabalighisha risala za Rabb wao; na Ameyazunguka (kwa ujuzi Wake) yale waliyo nayo, na Ametia hesabuni barabara idadi ya kila kitu.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.