-->
logo

068 - Al-Qalam

 الْقَلَم
Al-Qalam: 68

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



ن ۚ وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ﴿١﴾
1. Nuwn. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo.


مَا أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ﴿٢﴾
2. Kwa neema ya Rabb wako, wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) si majnuni.


وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ﴿٣﴾
3. Na hakika wewe bila shaka una ujira usiokatika.


وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ﴿٤﴾
4. Na hakika wewe bila shaka una tabia adhimu.


فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ﴿٥﴾
5. Basi hivi karibuni utaona, na wao wataona.


بِأَييِّكُمُ الْمَفْتُونُ﴿٦﴾
6. Ni nani kati yenu aliyesibiwa na uwendawazimu.


إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ﴿٧﴾
7. Hakika Rabb wako Yeye Anamjua zaidi aliyepotea njia Yake, Naye Anawajua zaidi walioongoka.


فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ﴿٨﴾
8. Basi usiwatii wanaokadhibisha.


وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ﴿٩﴾
9. Wanatamani lau kama ungelilegeza nao pia walegeze.


وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ﴿١٠﴾
10. Na wala usimtii kila mwingi wa kuapa, dhalili.


هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ﴿١١﴾
11. Mwingi wa kukashifu, mpitaji huku na kule kwa kufitinisha.


مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ﴿١٢﴾
12. Mwingi wa kuzuia ya kheri, mwenye kutaadi, mwingi wa kutenda dhambi.


عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ﴿١٣﴾
13. Katili, na baada ya hivyo ni mwenye kujipachika tu kabila.


أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ﴿١٤﴾
14. Kwa kuwa mwenye kumiliki mali na watoto?


إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٥﴾
15. Anaposomewa Aayaat Zetu, anasema: “Hekaya za watu wa kale.”


سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ﴿١٦﴾
16. Tutamtia chapa juu pua yake.


إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ﴿١٧﴾
17. Hakika sisi Tumewajaribu (Maquraysh) kama Tulivyowajaribu watu wa bustani, pale walipoapa kuwa bila shaka watayavuna (mazao yake) watakapopambaukiwa asubuhi.


وَلَا يَسْتَثْنُونَ﴿١٨﴾
18. Na wala hawakusema In-Shaa Allaah.  


فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ﴿١٩﴾
19. Basi (shamba lao) likazungukwa na chenye kuzunga (moto) kutoka kwa Rabb wako na hali wao wamelala.


فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ﴿٢٠﴾
20. Likawa kama lilovunwa ikabakishwa majivu meusi.


فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ﴿٢١﴾
21. Wakaitana, walipopambaukiwa asubuhi.


أَنِ اغْدُوا عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ﴿٢٢﴾
22. Kwamba nendeni asubuhi mapema shambani mwenu, mkiwa mnataka kuvuna.


فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ﴿٢٣﴾
23. Wakatoka na huku wanakwenda kimya kimya wakinong’onezana.


أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ﴿٢٤﴾
24. Kwamba: “Asikuingilieni humo kwa hali yoyote leo masikini.”


وَغَدَوْا عَلَىٰ حَرْدٍ قَادِرِينَ﴿٢٥﴾
25. Wakatoka asubuhi mapema kwa kusudio la nguvu, wakidhani wana uwezo (wa kuwazuia maskini).


فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ﴿٢٦﴾
26. Basi walipoliona wakasema: “Hakika sisi bila shaka Tumepotea.”


بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ﴿٢٧﴾
27. (Walivyotanabahi!): “Bali sisi tumenyimwa!”


قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ﴿٢٨﴾
28. Mbora wao akasema: “Je, sikukuambieni kwanini hamumsabbih (Allaah?)”


قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ﴿٢٩﴾
29. Wakasema: “Subhaana Rabbinnaa! Ametakasika Mola wetu! Hakika Sisi tulikuwa madhalimu.”


فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ﴿٣٠﴾
30. Wakakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakilaumiana.


قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ﴿٣١﴾
31. Wakasema: “Ole wetu! Hakika sisi tumekuwa warukao mipaka.”


عَسَىٰ رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا رَاغِبُونَ﴿٣٢﴾
32. “Asaa Rabb wetu Akatubadilishia lililo bora kuliko hilo hakika sisi kwa Rabb wetu ni wenye raghba.”


كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٣٣﴾
33. Hivyo ndivyo adhabu, na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.


إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٣٤﴾
34. Hakika wenye taqwa watapata kwa Rabb wao Jannaat za neema.


أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ﴿٣٥﴾
35. Je, Tuwafanye Waislamu (watiifu) sawa kama wahalifu?


مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ﴿٣٦﴾
36. Mna nini! Vipi mnahukumu?


أَمْ لَكُمْ كِتَابٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ﴿٣٧﴾
37.  Au mna Kitabu mnachodurusu humo?


إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ﴿٣٨﴾
38.  Kwamba hakika mtapata humo mnachopendelea?


أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۙ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ﴿٣٩﴾
39. Au mnazo ahadi za viapo juu Yetu zinazofikia mpaka Siku ya Qiyaamah, kwamba mtapata mnayojihukumia?


سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ﴿٤٠﴾
40. Waulize (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ni nani kati yao mdhamini wa hayo?”


أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِن كَانُوا صَادِقِينَ﴿٤١﴾
41. Au wana washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wakweli.


يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ﴿٤٢﴾
42. Siku utakapofunuliwa Muundi na wataitwa kusujudu lakini hawatoweza.



خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ﴿٤٣﴾
43. Macho yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika. Na hali walikuwa wakiitwa wasujudu (kuswali duniani) walipokuwa wazima wa afya.


فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ ۖ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٤﴾
44. Basi Niache (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na anayekadhibisha Qur-aan hii Tutawavuta pole pole adhabuni kwa namna wasiyoijua.


وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ﴿٤٥﴾
45. Na Ninawapa muhula, hakika mpango Wangu ni thabiti.


أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ﴿٤٦﴾
46. Au unawaomba ujira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi wao wamekuwa wazito kwa gharama zake?


أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ﴿٤٧﴾
47. Au wanayo (elimu) ya ghayb, basi wao wanaandika?


فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ﴿٤٨﴾
48. Basi subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hukumu ya Rabb wako, na wala usiwe kama swahibu wa samaki (Nabiy Yuwnus) pale aliponadi (kutuomba) naye akiwa amebanwa na dhiki.


لَّوْلَا أَن تَدَارَكَهُ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ﴿٤٩﴾
49. Lau isingelimfikia neema kutoka Rabb wake, bila shaka angelitupwa ufukoni mtupu hali akiwa mwenye kulaumiwa.


فَاجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَجَعَلَهُ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿٥٠﴾
50.  Lakini Rabb wake Akamteua na akamjaalia miongoni mwa Swalihina.


وَإِن يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ﴿٥١﴾
51. Na wale waliokufuru hukaribia bila shaka kukutelezesha kwa macho yao wanaposikia Ukumbusho na wanasema: “Hakika yeye bila shaka ni majnuni.”


وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ﴿٥٢﴾
52. Na haikuwa (hii Qur-aan) isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.


Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.