-->
logo

067 - Al-Mulk

 الْمُلْكُ
Al-Mulk: 67


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾
1. Amebarikika Ambaye Mkononi Mwake umo ufalme Naye juu ya kila kitu ni Muweza.


الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ﴿٢﴾
2. Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa kughufuria.


الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ ۖ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ﴿٣﴾
3. Ambaye Ameumba mbingu saba matabaka, hutaona katika uumbaji wa Ar-Rahmaan tofauti yoyote. Basi rejesha jicho je, unaona mpasuko wowote ule?


ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِئًا وَهُوَ حَسِيرٌ﴿٤﴾
4. Kisha rejesha jicho tena na tena litakupindukia jicho likiwa limehizika na lenye kunyong’onyezwa.


وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا لِّلشَّيَاطِينِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ السَّعِيرِ﴿٥﴾
5. Na kwa yakini Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mataa, na Tukazifanya kuwa ni makombora ya kuvurumisha kwa mashaytwaan, na Tumewaandalia adhabu ya moto uliowashwa vikali mno. 


وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٦﴾
6. Na kwa wale waliomkufuru Rabb wao kuna adhabu ya Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kuishia. 


إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ﴿٧﴾
7. Watakapotupwa humo, watausikia mkoromo wa pumzi wa kuchukiza nao unafoka.


تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ ۖ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ﴿٨﴾
8. Unakaribia kupasuka kwa ghadhabu. Kila wanapotupwa humo kundi, walinzi wake watawauliza: “Je, hajakufikieni mwonyaji yeyote?” 


قَالُوا بَلَىٰ قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ﴿٩﴾
9. Watasema: Ndio! Kwa yakini alitujia mwonyaji, lakini tulikadhibisha, na tukasema: “Allaah Hakuteremsha kitu chochote; nyinyi si chochote isipokuwa mumo katika upotofu mkubwa.”


وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ﴿١٠﴾
10. Na watasema: “Lau tungelikuwa tunasikiliza au tunatia akilini, tusingelikuwa katika watu wa motoni.” 


فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ﴿١١﴾
11. Basi watakiri madhambi yao, na (wataambiwa): “Tokomeeni mbali watu wa motoni.” 


إِنَّ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ﴿١٢﴾
12. Hakika wale wanaomkhofu Rabb wao kwa ghayb watapata maghfirah na ujira mkubwa.


وَأَسِرُّوا قَوْلَكُمْ أَوِ اجْهَرُوا بِهِ ۖ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿١٣﴾
13. Na fanyeni siri kauli zenu, au zidhihirisheni, hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.


أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ﴿١٤﴾
14. Kwani Hajui Yule Aliyeumba! Na hali Yeye ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.


هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ ۖ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ﴿١٥﴾
15. Yeye Ndiye Aliyeidhalilisha ardhi kwa ajili yenu basi nendeni katika pande zake na kuleni katika riziki Yake, na Kwake kufufuliwa.


أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾
16. Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?


أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾
17. Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu.


وَلَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ﴿١٨﴾
18. Na kwa yakini walikadhibisha wale walio kabla yao, basi ilikuwaje adhabu Yangu.


أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ ۚ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَـٰنُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ﴿١٩﴾
19. Je, hawawaoni ndege juu yao, wakiwa wakikunjua na kukunja (mbawa) hakuna anayewashikilia isipokuwa Ar-Rahmaan hakika Yeye ni Mwenye kuona kila kitu.


أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ جُندٌ لَّكُمْ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ ۚ إِنِ الْكَافِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ﴿٢٠﴾
20. Au ni lipi hilo jeshi lenu linaloweza kukunusuruni badala ya Ar-Rahmaan? Makafiri hawamo isipokuwa katika ghururi.


أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي يَرْزُقُكُمْ إِنْ أَمْسَكَ رِزْقَهُ ۚ بَل لَّجُّوا فِي عُتُوٍّ وَنُفُورٍ﴿٢١﴾
21. Au ni nani huyu ambaye atakuruzukuni ikiwa (Allaah) Atazuia riziki Yake? Bali wanang’ang’ania kwenye ufidhuli na kukimbilia mbali kwa chuki.


أَفَمَن يَمْشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِ أَهْدَىٰ أَمَّن يَمْشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٢٢﴾
22. Je, yule anayekwenda akiwa gubigubi juu ya uso wake ameongoka zaidi, au yule anayekwenda sawasawa kuelekea njia iliyonyooka? 


قُلْ هُوَ الَّذِي أَنشَأَكُمْ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۖ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ﴿٢٣﴾
23. Sema: “Yeye Ndiye Yule Aliyekuanzisheni na Akakujaalieni kusikia na kuona na nyoyo za kutafakari.” Ni kidogo sana mnayoshukuru.


قُلْ هُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿٢٤﴾
24. Sema: “Yeye Ndiye Yule Aliyekutawanyeni kwenye ardhi, na Kwake mtakusanywa.”


وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٢٥﴾
25. Na wanasema: “Ni lini hiyo ahadi (ya kufufuliwa), mkiwa ni wasemao kweli?”


قُلْ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّـهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢٦﴾
26. Sema: “Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah; na hakika mimi ni mwonyaji tu bayana.”


فَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيئَتْ وُجُوهُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَقِيلَ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَدَّعُونَ﴿٢٧﴾
27. Basi watakapoiona (adhabu ya Qiyaamah) inakaribia, zitadhikika nyuso za wale waliokufuru, na itasemwa: “Hii ndio ambayo mlikuwa mkiomba.”


قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِيَ اللَّـهُ وَمَن مَّعِيَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَن يُجِيرُ الْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٢٨﴾
28. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, mnaonaje ikiwa Allaah Ataniangamiza na walio pamoja nami, au Akiturehemu; basi ni nani atakayewakinga makafiri na adhabu iumizayo?”


قُلْ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢٩﴾
29. Sema: “Yeye Ndiye Ar-Rahmaan tumemwamini, na Kwake tunatawakali, basi karibuni hivi mtakuja kujua ni nani ambaye yumo katika upotofu wa bayana.”


قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَصْبَحَ مَاؤُكُمْ غَوْرًا فَمَن يَأْتِيكُم بِمَاءٍ مَّعِينٍ﴿٣٠﴾
30. Sema: “Mnaonaje yakijakuwa maji yenu yamedidimia; basi ni nani atakayeweza kukuleteeni maji (ya chemchemu) yatiririkayo?”

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.