-->
logo

035 - Faatwir

 فَاطِر
Faatwir: 35

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَۚ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾
1. AlhamduliLLahi, Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mwenye kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, na tatu-tatu na nne-nne. Huzidisha katika uumbaji Atakavyo. Hakika Allaah ni Muweza juu ya kila kitu.


مَّا يَفْتَحِ اللَّـهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا ۖ وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢﴾
2. Rahmah yoyote Anayoifungua Allaah kwa watu, basi hakuna wa kuizuia, na Anayoizuia, basi hakuna wa kuipeleka baada Yake, Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


يَا أَيُّهَا النَّاسُ اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣﴾
3. Enyi watu! Kumbukeni neema za Allaah kwenu. Je, kuna muumbaji yeyote badala ya Allaah Anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhi? Hakuna  Muabudiwa wa haki ila Yeye, basi wapi mnapogeuzwa?


وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٤﴾
4. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi   wamekwisha kadhibishwa Rusuli kabla yako. Na kwa Allaah yanarejeshwa mambo yote.


يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۖ وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٥﴾
5. Enyi watu!  Hakika ahadi ya Allaah ni haki; basi usikughururini uhai wa dunia, na wala (shaytwaanmwenye kughuri asikughururini kuhusu Allaah.


إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا ۚ إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿٦﴾
6. Hakika shaytwaan kwenu ni adui, basi mfanyeni kuwa ni adui. Hakika anaitia kikosi chake ili wawe miongoni mwa watu wa moto uliowashwa vikali mno. 


الَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿٧﴾
7. Wale waliokufuru watapata adhabu kali, na wale walioamini na wakatenda mema watapata maghfirah na ujira mkubwa.


أَفَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا ۖ فَإِنَّ اللَّـهَ يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۖ فَلَا تَذْهَبْ نَفْسُكَ عَلَيْهِمْ حَسَرَاتٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَصْنَعُونَ ﴿٨﴾
8. Je, yule aliyepambiwa uovu wa ‘amali yake akaiona ni nzuri (je, ni sawa na aliyeongoka?) Basi hakika Allaah Anampotoa Amtakaye na Anamhidi  Amtakaye, basi isihiliki nafsi yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili ya majuto. Hakika Allaah ni Mjuzi kwa yale wayatendayo.


وَاللَّـهُ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَسُقْنَاهُ إِلَىٰ بَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَحْيَيْنَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚكَذَٰلِكَ النُّشُورُ ﴿٩﴾
9. Na Allaah Ambaye Ametuma pepo kisha zitimue mawingu, Tukayaendesha katika nchi iliyokufa, Tukahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Kadhalika ndivyo kufufuliwa.


مَن كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا ۚ إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ ۚوَالَّذِينَ يَمْكُرُونَ السَّيِّئَاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۖ وَمَكْرُ أُولَـٰئِكَ هُوَ يَبُورُ ﴿١٠﴾
10. Yeyote Anayetaka utukufu, basi utukufu wote uko kwa Allaah. Kwake Pekee linapanda neno zuri na amali njema Huitukuza. Na wale wanaopanga njama za maovu watapata adhabu shadidi. Na njama za hao ni zenye kuangamia.


وَاللَّـهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ جَعَلَكُمْ أَزْوَاجًا ۚ وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴿١١﴾
11. Na Allaah Amekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na tone na manii, kisha Akakufanyeni jozi; mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote habebi mimba na wala hazai isipokuwa kwa ujuzi Wake. Na hapewi umri mrefu yeyote yule mwenye umri mrefu na wala hapunguziwi katika umri wake isipokuwa imo Kitabuni. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.


وَمَا يَسْتَوِي الْبَحْرَانِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ سَائِغٌ شَرَابُهُ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ ۖ وَمِن كُلٍّ تَأْكُلُونَ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُونَ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا ۖ وَتَرَى الْفُلْكَ فِيهِ مَوَاخِرَ لِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢﴾
12. Na bahari mbili hazilingani sawa; haya ni (maji) matamu ladha yake, yenye kukata kiu, anisi kinywaji chake, na haya ni ya chumvi kali. Na katika kila moja mnakula nyama laini safi na mnatoa mapambo mnayoyavaa, na utaona merikebu humo zikipasua maji ili mtafute fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.


يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾
13. Anauingiza usiku katika mchana, na Anauingiza mchana katika usiku, na Anaitisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, ufalme ni Wake Pekee.  Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende.


إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚوَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾
14.  Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni.  Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kama Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.


يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿١٥﴾
15. Enyi watu!  Nyinyi ni mafakiri kwa Allaah! Na Allaah Ndiye Mkwasi,  Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.


إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿١٦﴾
16. Akitaka Atakuondosheni mbali na Alete viumbe vipya.


وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ بِعَزِيزٍ ﴿١٧﴾
17. Na hayo si ya kushindwa kwa Allaah.



وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَىٰ حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰۗ إِنَّمَا تُنذِرُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ ۚ وَمَن تَزَكَّىٰ فَإِنَّمَا يَتَزَكَّىٰ لِنَفْسِهِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿١٨﴾
18. Na wala mbebaji yeyote hatobeba mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Na aliyeelemeshwa mzigo akiita ili kusaidiwa kubebewa mzigo wake, hatobebewa chochote, japokuwa ni jamaa wa karibu. Hakika wewe unaonya wale wanaomkhofu Rabb wao kwa ghayb, na wakasimamisha Swalaah. Na yeyote anayejitakasa, basi hakika anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake; na kwa Allaah ndio mahali pa kuishia.


وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ﴿١٩﴾
19. Na halingani sawa kipofu na mwenye kuona.


وَلَا الظُّلُمَاتُ وَلَا النُّورُ ﴿٢٠﴾
20. Na wala viza na nuru.


وَلَا الظِّلُّ وَلَا الْحَرُورُ ﴿٢١﴾
21. Na wala kivuli na joto.


وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ﴿٢٢﴾
22. Na wala hawalingani sawa walio hai na wafu. Hakika Allaah Anamsikilizisha Amtakaye; nawe huwezi kuwasikilizisha walioko kaburini.


إِنْ أَنتَ إِلَّا نَذِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) si chochote isipokuwa mwonyaji.



إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۚ وَإِن مِّنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ ﴿٢٤﴾
24. Hakika Sisi Tumekupeleka kwa haki ili ubashiri na uonye. Na hakuna ummah wowote isipokuwa amepita humo mwonyaji.


وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالزُّبُرِ وَبِالْكِتَابِ الْمُنِيرِ﴿٢٥﴾
25. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi wamekwishakadhibisha wale wa nyuma yao; waliwajia Rusuli wao kwa hoja bayana na Maandiko Matakatifu na Kitabu chenye Nuru.


ثُمَّ أَخَذْتُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۖ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿٢٦﴾
26. Kisha Nikawashika kuwaadhibu wale waliokufuru, basi ilikuwa vipi kukana Kwangu.



أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا ۚ وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ ﴿٢٧﴾
27. Je, huoni kwamba Allaah Ameteremsha maji kutoka mbinguni, Tukatoa kwayo matunda ya rangi mbalimbali. Na miongoni mwa majabali iko michirizi meupe, na mekundu yenye kutofautiana rangi zake na meusi yaliyokoza sana.



وَمِنَ النَّاسِ وَالدَّوَابِّ وَالْأَنْعَامِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ كَذَٰلِكَ ۗ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ ﴿٢٨﴾
28. Na miongoni mwa watu na viumbe wanaotembea na wanyama wa mifugo, wenye kutofautiana rangi zake kadhalika. Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni ‘Ulamaa. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa kughufuria.


إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾
29. Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea.


لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾
30. Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani.


وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ هُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِعِبَادِهِ لَخَبِيرٌ بَصِيرٌ﴿٣١﴾
31. Na yale ambayo Tumefunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ya Kitabu ndio haki yenye kusadikisha yale yaliyoko kabla yake. Hakika Allaah kwa waja Wake bila shaka ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichikaMwenye kuona yote.


ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ ﴿٣٢﴾
32. Kisha Tukawarithisha Kitabu wale Tuliowakhitari miongoni mwa waja Wetu. Basi miongoni mwao ni mwenye kudhulumu nafsi yake na miongoni mwao aliyekuwa wastani na miongoni mwao aliyesabiki kwa mambo mengi ya kheri kwa idhini ya Allaah. Hiyo ndio fadhila kubwa.


جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا ۖ وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ ﴿٣٣﴾
33. Jannaat za kudumu milele wataziingia, watapambwa humo kwa vikuku vya dhahabu na lulu, na mavazi yao humo ni hariri.


وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَذْهَبَ عَنَّا الْحَزَنَ ۖ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٤﴾
34. Na watasema: “AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Ambaye Ametuondoshea huzuni. Hakika Rabb wetu bila shaka ni Mwingi wa kughufuria,  Mwingi wa kupokea shukurani.



الَّذِي أَحَلَّنَا دَارَ الْمُقَامَةِ مِن فَضْلِهِ لَا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٌ وَلَا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٌ ﴿٣٥﴾
35. Ambaye Ametuweka nyumba yenye kudumu kwa fadhila Zake, hayatugusi humo taabu na mashaka na wala haitugusi humo machovu.


وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُم مِّنْ عَذَابِهَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي كُلَّ كَفُورٍ ﴿٣٦﴾
36. Na wale waliokufuru watapata moto wa Jahannam.  Hautahukumiwa uwafishe kikamilifu wafe na wala hawatakhafifishiwa adhabu yake. Hivyo ndivyo Tunavyomlipa kila mwenye kukufuru mno.


وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ ۖ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٣٧﴾
37.  Nao watapiga mayowe humo: “Rabb wetu! Tutoe tutende mema ghairi ya yale tulokuwa tukitenda.” (Wataambiwa): “Je, kwani Hatukukupeni umri wa kukumbuka mwenye kukumbuka humo? Na alikujieni mwonyaji. Basi onjeni! Kwani madhalimu hawana yeyote yule wa kuwanusuru.”


إِنَّ اللَّـهَ عَالِمُ غَيْبِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٣٨﴾
38. Hakika Allaah ni Mjuzi wa ghayb za mbingu na ardhini. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.


هُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَمَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ ۖ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ إِلَّا مَقْتًا ۖ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ إِلَّا خَسَارًا ﴿٣٩﴾
39. Yeye Ndiye Ambaye Amekufanyeni makhalifa kwenye ardhi. Basi yeyote aliyekufuru, kufuru yake ni juu yake, na kufuru za makafiri wala haziwazidishii mbele ya Rabb wao isipokuwa kuchukiwa; na kufuru za makafiri wala haziwazidishii isipokuwa khasara.


قُلْ أَرَأَيْتُمْ شُرَكَاءَكُمُ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا فَهُمْ عَلَىٰ بَيِّنَتٍ مِّنْهُ ۚ بَلْ إِن يَعِدُ الظَّالِمُونَ بَعْضُهُم بَعْضًا إِلَّا غُرُورًا ﴿٤٠﴾
40. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, mnawaona washirika wenu ambao mnawaomba badala ya Allaah? Nionyesheni ni nini walichoumba katika ardhi au wana ushirika wowote ule mbinguni? Au Tumewapa kitabu chochote kile, kisha wao kwa hicho wakawa na hoja bayana?” Hapana! Bali madhalimu hawaahidiani wao kwa wao isipokuwa ghururi.


إِنَّ اللَّـهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَن تَزُولَا ۚ وَلَئِن زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّن بَعْدِهِ ۚ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤١﴾
41. Hakika Allaah Anazuia mbingu na ardhi zisitoweke. Na zikitoweka, hakuna yeyote wa kuzishikilia baada Yake, hakika Yeye daima Mvumilivu,  Mwingi wa kughufuria.


وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَهُمْ نَذِيرٌ لَّيَكُونُنَّ أَهْدَىٰ مِنْ إِحْدَى الْأُمَمِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُمْ نَذِيرٌ مَّا زَادَهُمْ إِلَّا نُفُورًا ﴿٤٢﴾
42. Na wakaapa kwa Jina la Allaah nguvu ya viapo vyao kwamba akiwajia mwonyaji, bila shaka watakuwa walioongoka zaidi kuliko umati zozote zile.  Lakini alipowajia mwonyaji haikuwazidishia isipokuwa kukimbia kwa chuki.


اسْتِكْبَارًا فِي الْأَرْضِ وَمَكْرَ السَّيِّئِ ۚ وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ ۚ فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ الْأَوَّلِينَ ۚ فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَحْوِيلًا ﴿٤٣﴾
43. Kwa kutakabari katika ardhi na kupanga njama ovu. Lakini njama ovu hazimzunguki isipokuwa mwenyewe. Je, basi wanangojea nini isipokuwa desturi ya watu wa awali. Basi hutapata katika desturi ya Allaah mabadiliko, na wala hutapata katika desturi ya Allaah mageuko.


أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَكَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا ﴿٤٤﴾
44. Je, hawakutembea katika ardhi, wakatazama vipi ilikuwa hatima ya wale walio kabla yao, na walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao? Na hakuna lolote limshindalo Allaah mbinguni na wala ardhini; hakika Yeye daima ni Mjuzi wa yote, Mweza wa yote.


وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِعِبَادِهِ بَصِيرًا ﴿٤٥﴾
45. Na lau Allaah Angeliwaadhibu watu kwa sababu ya waliyoyachuma, Asingeliacha juu ya ardhi kiumbe chochote kitembeacho, lakini Anawaakhirisha mpaka muda maalumu uliokadiriwa; utakapofika muda wao, basi hakika Allaah daima ni Mwenye kuona waja Wake.


Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.