-->
logo

030 - Ar-Ruwm

الرُّوم
Ar-Ruwm: 30

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.


غُلِبَتِ الرُّومُ ﴿٢﴾
2. Warumi wameshindwa.


فِي أَدْنَى الْأَرْضِ وَهُم مِّن بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ ﴿٣﴾
3. Katika nchi iliyo karibu, nao baada ya kushindwa kwao, watashinda hivi karibuni.



فِي بِضْعِ سِنِينَ ۗ لِلَّـهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ ۚ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ ﴿٤﴾
4. Katika miaka baina ya mitatu na tisa. Amri ni ya Allaah Pekee kabla na baada. Na Siku hiyo watafurahi Waumini.


بِنَصْرِ اللَّـهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٥﴾
5. Kwa nusura ya Allaah. Anamnusuru Amtakaye, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika,Mwenye kurehemu.


وَعْدَ اللَّـهِ ۖ لَا يُخْلِفُ اللَّـهُ وَعْدَهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦﴾
6.  Ni ahadi ya Allaah. Allaah Hakhalifu ahadi Yake, lakini watu wengi hawajui.


يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ ﴿٧﴾
7. Wanajua yaliyo dhahiri ya uhai wa dunia, lakini wao wameghafilika na Aakhirah.



أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنفُسِهِم ۗ مَّا خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ لَكَافِرُونَ ﴿٨﴾
8. Je, hawatafakari katika nafsi zao? Allaah Hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki na muda maalumu uliokadiriwa. Na hakika wengi miongoni mwa watu bila shaka ni wenye kukanusha kukutana na Rabb wao.



أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا الْأَرْضَ وَعَمَرُوهَا أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
9. Je, hawatembei katika ardhi wakatazama jinsi ilivyokuwa hatima ya wale walio kabla yao? Walikuwa ni wenye nguvu zaidi kuliko wao, na walichimbua ardhi, na wakaistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha (makafiri), na wakawajia Rusuli wao kwa hoja bayana, na Allaah Hakuwa Akiwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.


ثُمَّ كَانَ عَاقِبَةَ الَّذِينَ أَسَاءُوا السُّوأَىٰ أَن كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَكَانُوا بِهَا يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾
10. Kisha uovu ukawa hatima ya wale waliofanya uovu kwa vile walikadhibisha Aayaat za Allaah na walikuwa ni wenye kuzifanyia istihzai.


اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾
11. Allaah Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurudisha, kisha Kwake mtarejeshwa.


وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُبْلِسُ الْمُجْرِمُونَ ﴿١٢﴾
12. Na Siku itakaposimama Saa, wahalifu watakata tamaa.


وَلَمْ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَائِهِمْ شُفَعَاءُ وَكَانُوا بِشُرَكَائِهِمْ كَافِرِينَ ﴿١٣﴾
13. Na wala hawatokuwa na waombezi miongoni mwa waliokuwa wakiwashirikisha (na Allaah) na wao wenyewe watakuwa ni wenye kuwakanusha washirikishwa wao.


وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَتَفَرَّقُونَ ﴿١٤﴾
14. Na siku itakaposimama Saa, Siku hiyo watafarikiana.


فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَهُمْ فِي رَوْضَةٍ يُحْبَرُونَ ﴿١٥﴾
15. Ama wale walioamini na wakatenda mema, basi wao watakuwa katika mabustani mazuri wakifurahishwa.


وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ فَأُولَـٰئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ ﴿١٦﴾
16. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat Zetu na makutano ya Aakhirah, basi hao katika adhabu watahudhurishwa.


فَسُبْحَانَ اللَّـهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ ﴿١٧﴾
17. Basi Subhaana Allaah! Msabbihini Allaah mnapoingia jioni na mnapoingia asubuhi.


وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Na Ana Himidi katika mbingu na ardhi, na jioni na wakati wa Adhuhuri.


يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ ﴿١٩﴾
19. Anatoa kilichohai kutokana na kilichokufa, na Anatoa kilichokufa kutokana na kilicho hai, na Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa (kufufuliwa).


وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ ﴿٢٠﴾
20. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni kwamba Amekuumbeni kutokana na mchanga; tahamaki mmekuwa watu mnaotawanyika.



وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾
21. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni kwamba Amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na rahmah. Hakika pana katika hayo, bila shaka Aayah (ishara, zingatio nk) kwa watu wanaotafakari.



وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ﴿٢٢﴾
22. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni uumbaji wa mbingu na ardhi, na kukhitilafiana lugha zenu na rangi zenu. Hakika pana katika hayo, bila shaka Aayah (ishara, zingatio nk) kwa wenye ujuzi.


وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٢٣﴾
23. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni kulala kwenu usiku na mchana na kutafuta kwenu fadhila Zake. Hakika pana katika hayo, bila shaka Aayah (ishara, zingatio nk) kwa watu wanaosikia.


وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٤﴾
24. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake Anakuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na matumaini; na Anateremsha kutoka mbinguni maji, Anahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hakika pana katika hayo, bila shaka Aayah (ishara, zingatio nk) kwa watu wenye akili.


وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ۚ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ﴿٢٥﴾
25. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake, ni kwamba mbingu na ardhi zimesimama kwa amri Yake, kisha Atakapokuiteni wito mmoja mara mtatoka ardhini.


وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿٢٦﴾
26. Na ni Wake Pekee wote waliomo katika mbingu na ardhi, na wote Kwake wanatii.


وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ۚ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚوَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٧﴾
27. Naye Ndiye Aliyeanzisha uumbaji, kisha Anaurudisha, nayo ni sahali mno Kwake. Naye Ana Sifa za juu kabisa katika mbingu na ardhi. Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.



ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ ۖ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن شُرَكَاءَ فِي مَا رَزَقْنَاكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَاءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾
28. (Allaah) Amekupigieni mfano kwa hali ya nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kuume mnao washirika wowote katika vile Tulivyokuruzukuni; kisha mkawa nyinyi katika hivyo sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopeana wenyewe kwa wenyewe. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat kwa watu wenye akili.


بَلِ اتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَهْوَاءَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ فَمَن يَهْدِي مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٢٩﴾
29. Bali wale waliodhulumu wamefuata hawaa zao bila ya elimu. Basi nani atamwongoa ambaye Allaah Amempotowa? Na hawatokuwa na wowote wa kuwanusuru.


فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾
30. Basi elekeza uso wako kwenye Dini yenye kujiengua na upotofu inayoelemea haki. Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah. Hivyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui.


مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٣١﴾
31. Ilhali wenye kurudia kutubu kwa ikhlasi Kwake (Allaah) na mcheni, na simamisheni Swalaah; na wala msiwe miongoni mwa washirikina.


مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ ﴿٣٢﴾
32. (Wala msiwe) Miongoni mwa wale walioitenganisha dini yaowakawa makundi makundi. Kila kundi wananafurahia waliyonayo.


وَإِذَا مَسَّ النَّاسَ ضُرٌّ دَعَوْا رَبَّهُم مُّنِيبِينَ إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا أَذَاقَهُم مِّنْهُ رَحْمَةً إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na inapowagusa watu dhara, humwomba Rabb wao ilhali wenye kurudia kutubu kwa ikhlasi Kwake, kisha Anapowaonjesha rahmah kutoka Kwake, tahamaki kundi miongoni mwao humshirikisha Rabb wao.


لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣٤﴾
34. Ili wayakanushe Tuliyowapa; basi stareheni, karibuni mtakuja kujua.



أَمْ أَنزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا بِهِ يُشْرِكُونَ ﴿٣٥﴾
35. Au Tumewateremshia hoja ya wazi ambayo inazungumzia ambayo walikuwa wakimshirikisha Naye?


وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً فَرِحُوا بِهَا ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ إِذَا هُمْ يَقْنَطُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na Tunapowaonjesha watu rahmah huzifurahia, na inapowasibu uovu kutokana na iliyotanguliza mikono yao, mara wao wanakata tamaa. 


أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣٧﴾
37. Je, hawaoni kwamba Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye, na Adhikisha (kwa Amtakaye). Hakika katika hayo bila shaka mna Aayaat (ishara, zingatio) kwa watu wanaoamini.


فَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٣٨﴾
38. Basi wape jamaa wenye uhusiano wa karibu haki zao, na masikini na msafiri (aliyeharibikiwa). Hivyo ndivyo bora kwa wale wanaotaka Wajihi wa Allaah, na hao ndio wenye kufaulu.


وَمَا آتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَ فِي أَمْوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرْبُو عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا آتَيْتُم مِّن زَكَاةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُضْعِفُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na mlichotoa katika ribaa ili kizidi katika mali za watu, basi hakizidi kwa Allaah. Na mlichotoa katika Zakaah mnataka Wajihi wa Allaah, basi hao ndio wenye kuzidishiwa.


اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۖ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَفْعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَيْءٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٠﴾
40. Allaah, Ambaye Amekuumbeni, kisha Akakuruzukuni, kisha Anakufisheni, kisha Atakuhuisheni; je, kati ya washirika wenu yuko yeyote yule awezaye kufanya lolote katika hayo? Subhaanahu wa Ta’aalaa! Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale anayomshirikisha.


ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٤١﴾
41. Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu ili (Allaah) Awaonjeshe baadhi ya ambayo wameyatenda ili wapate kurejea.


قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلُ ۚ كَانَ أَكْثَرُهُم مُّشْرِكِينَ ﴿٤٢﴾
42. Sema: “Nendeni katika ardhi, mkatazame vipi iikuwa hatima ya wale waliotangulia; wengi wao walikuwa ni washirikina.


فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ الْقَيِّمِ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّـهِ ۖ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ ﴿٤٣﴾
43. Basi elekeza uso wako kwenye Dini iliyonyooka kabla haijafika Siku haina marudio hiyo inayotoka kwa Allaah. Siku hiyo watatengana.


مَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِأَنفُسِهِمْ يَمْهَدُونَ ﴿٤٤﴾
44. Anayekufuru, basi kufuru yake ni dhidi yake, na anayetenda mema, basi wanajiandalia mahali pa kupumzika kwa ajili ya nafsi zao. 


لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٤٥﴾
45. Ili (Allaah) Awalipe wale walioamini na wakatenda mema katika fadhila Zake. Hakika Yeye Hapendi makafiri.


وَمِنْ آيَاتِهِ أَن يُرْسِلَ الرِّيَاحَ مُبَشِّرَاتٍ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَلِتَجْرِيَ الْفُلْكُ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni kwamba Anapeleka pepo zenye bishara nzuri na ili Akuonjesheni katika rahmah Zake, na ili merikebu ziende kwa amri Yake, na ili watafute katika fadhila Zake na ili mpate kushukuru.


وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا ۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na kwa yakini Tuliwatuma kabla yako, Rusuli kwa watu wao, wakawajia kwa hoja bayana; basi Tukawalipiza wale ambao wamefanya uhalifu. Na ni haki daima Kwetu kuwanusuru Waumini.



اللَّـهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَيَبْسُطُهُ فِي السَّمَاءِ كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ ۖ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Allaah Ambaye Anatuma pepo kisha zikatimua mawingu, kisha Akayatawanya mbinguni Atakavyo, na Akajaalia mapande mapande, basi utaona matone ya mvua yanatoka baina yake. Anapowafikishia Awatakao kati ya waja Wake, mara hao wanafurahia.


وَإِن كَانُوا مِن قَبْلِ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْهِم مِّن قَبْلِهِ لَمُبْلِسِينَ ﴿٤٩﴾
49. Na ingawa kabla ya kuteremshiwa (mvua), walikuwa wenye kukata tamaa.



فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللَّـهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٥٠﴾
50. Basi tazama athari za rahmah ya Allaah vipi Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika (Afanyayo) hayo, Ndiye bila shaka Mwenye Kuhuisha wafu, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.



وَلَئِنْ أَرْسَلْنَا رِيحًا فَرَأَوْهُ مُصْفَرًّا لَّظَلُّوا مِن بَعْدِهِ يَكْفُرُونَ ﴿٥١﴾
51. Na Tungelituma upepo (mbaya) na wakauona umekuwa manjano; wangeendelea baada yake kukufuru.


فَإِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٥٢﴾
52. Basi hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu, na wala huwezi kusikilizisha viziwi wito wanapokengeua wakigeuza migongo yao.


وَمَا أَنتَ بِهَادِ الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na wala wewe huwezi kuwaongoa vipofu kutoka upotofu wao; humsikilizishi isipokuwa yule anayeamini Aayaat Zetu nao ndio Wenye kusilimu (kwa Allaah).


اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً ۚيَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ ﴿٥٤﴾
54. Allaah Ambaye Amekuumbeni kutokana na udhaifu, kisha Akajaalia baada ya udhaifu, nguvu, kisha Akajaalia baada ya nguvu udhaifu na ukongwe. Anaumba Atakacho. Naye Ndiye Mjuzi wa yote, Mweza wa yote.


وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُقْسِمُ الْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا غَيْرَ سَاعَةٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَانُوا يُؤْفَكُونَ ﴿٥٥﴾
55. Na Siku itakayosimama Saa, wataapa wahalifu kwamba hawakubakia (duniani) ila saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakighilibiwa.



وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَالْإِيمَانَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِي كِتَابِ اللَّـهِ إِلَىٰ يَوْمِ الْبَعْثِ ۖ فَهَـٰذَا يَوْمُ الْبَعْثِ وَلَـٰكِنَّكُمْ كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na wale waliopewa elimu na iymaan watasema: “Kwa yakini mmekaa kwa majaaliwa na hukmu ya Allaah mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ni Siku ya kufufuliwa, lakini nyinyi mlikuwa hamjui.”


فَيَوْمَئِذٍ لَّا يَنفَعُ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَعْذِرَتُهُمْ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ ﴿٥٧﴾
57. Siku hiyo haitowafaa wale waliodhulumu udhuru wao, na wala hawataachiliwa kuomba kuridhisha (kwa Allaah). 



وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَلَئِن جِئْتَهُم بِآيَةٍ لَّيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُبْطِلُونَ ﴿٥٨﴾
58. Kwa yakini Tumewapigia watu mifano ya kila namna katika hii Qur-aan. Na kama ungewajia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Aayah (ishara, hoja, dalili) bila shaka wale waliokufuru watasema: “Nyinyi (Waumini) si chochote ila wabatilifu.”


كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya nyoyo za wale wasiojua.



فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ الَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ ﴿٦٠﴾
60. Basi subiri, hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Na wala wasikuvunje moyo wale ambao hawana yakini ukataradadi (kubalighisha ujumbe).


Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.