-->
logo

029 - Al-'Ankabuwt

الْعَنْكَبُوت
Al-‘Ankabuwt: 29

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.


أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾
2. Je, wanadhani watu kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao ndio wasijaribiwe? 


وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾
3. Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao, ili Allaah Awatambulishe wale walio wakweli na ili Awatambulishe walio waongo.


أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ أَن يَسْبِقُونَا ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿٤﴾
4. Je, wanadhania wale wanaotenda maovu kwamba watatushinda? Uovu ulioje yale wanayohukumu.


مَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ اللَّـهِ فَإِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ لَآتٍ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٥﴾
5. Anayetaraji kukutana na Allaah basi hakika muda uliopangwa na Allaah utafika tu. Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.


وَمَن جَاهَدَ فَإِنَّمَا يُجَاهِدُ لِنَفْسِهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَغَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾
6. Na anayefanya juhudi basi hakika hapana isipokuwa anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Allaah bila shaka ni si Mhitaji wa walimwengu.


وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَحْسَنَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٧﴾
7. Na wale walioamini na wakatenda mema bila shaka Tutawafutia maovu yao, na bila shaka Tutawalipa mazuri zaidi kuliko yale waliyokuwa wakitenda.



وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ وَإِن جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۚ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾
8. Na Tumemuusia insani kuwafanyia wema wazazi wake wawili. Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii; Kwangu ni marejeo yenu, Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.


وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُدْخِلَنَّهُمْ فِي الصَّالِحِينَ ﴿٩﴾
9. Na wale walioamini na wakatenda mazuri bila shaka Tutawaingiza pamoja na  Swalihina.



وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ وَلَئِن جَاءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ ۚ أَوَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾
10. Na miongoni mwa watu wako wasemao: “Tumemwamini Allaah;” lakini wanapoudhiwa kwa ajili ya Allaah, hufanya fitnah za watu kama kwamba ni adhabu ya Allaah. Na inapowajia nusura kutoka kwa Rabb wako husema: “Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi.” Je, kwani Allaah Hayajui yale yaliyomo katika vifua vya walimwengu?


وَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْمُنَافِقِينَ ﴿١١﴾
11. Na bila shaka Allaah Atatambulisha wale walioamini, na bila shaka Atawatambulisha wanafiki.



وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا اتَّبِعُوا سَبِيلَنَا وَلْنَحْمِلْ خَطَايَاكُمْ وَمَا هُم بِحَامِلِينَ مِنْ خَطَايَاهُم مِّن شَيْءٍ ۖ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٢﴾
12. Na wale waliokufuru wakasema kuwaambia walo walioamini: “Fuateni njia yetu, nasi tutabeba madhambi yenu.” Na wala wao hawatokuwa wenye kubeba katika madhambi yao chochote kile. Hakika wao ni waongo.


وَلَيَحْمِلُنَّ أَثْقَالَهُمْ وَأَثْقَالًا مَّعَ أَثْقَالِهِمْ ۖ وَلَيُسْأَلُنَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَمَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣﴾
13. Na bila shaka watabeba mizigo yao (ya dhambi) na mizigo mingine pamoja na mizigo yao; na bila shaka wataulizwa Siku ya Qiyaamah kuhusu yale waliyokuwa wakiyatunga.



وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٤﴾
14. Na kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa watu wake akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini, basi ikawachukua tufani nao ni madhalimu.


فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٥﴾
15. Basi Tukamuokoa na watu wa jahazi, na Tukaifanya kuwa ni Aayah (ishara, zingatio) kwa walimwengu.


وَإِبْرَاهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ ۖ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٦﴾
16. Na Ibraahiym pale alipowaambia kaumu yake: “Mwabuduni Allaah na mcheni. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.


إِنَّمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ وَاشْكُرُوا لَهُ ۖ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١٧﴾
17. “Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnaunda uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye na mshukuruni, Kwake mtarejeshwa.


وَإِن تُكَذِّبُوا فَقَدْ كَذَّبَ أُمَمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ۖ وَمَا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٨﴾
18. Na mkikadhibisha, basi kwa yakini zilikwishakadhibisha ummah nyingi kabla yenu. Na si juu ya Rasuli isipokuwa kubalighisha ujumbe bayana.”


أَوَلَمْ يَرَوْا كَيْفَ يُبْدِئُ اللَّـهُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿١٩﴾
19. Je, hawaoni jinsi Allaah Anavyoanzisha uumbaji kisha Anaurudisha? Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.


قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ بَدَأَ الْخَلْقَ ۚ ثُمَّ اللَّـهُ يُنشِئُ النَّشْأَةَ الْآخِرَةَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾
20. Sema: “Nendeni katika ardhi, na mtazame jinsi (Allaah) Alivyoanzisha uumbaji; kisha Allaah Ataanzisha umbo la Aakhirah (mtakapofufuliwa). Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.


يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَرْحَمُ مَن يَشَاءُ ۖ وَإِلَيْهِ تُقْلَبُونَ ﴿٢١﴾
21. “Anamuadhibu Amtakaye, na Anamrehemu Amtakaye; na Kwake mtarudishwa.


وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٢٢﴾
22. “Nanyi si wenye kushinda kukwepa ardhini na wala mbinguni. Na hamna mlinzi wala mwenye kunusuru yeyote badala ya Allaah”.


وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَلِقَائِهِ أُولَـٰئِكَ يَئِسُوا مِن رَّحْمَتِي وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Na wale waliozikanusha Aayaat za Allaah pamoja na kukutana Naye, hao wamekata tamaa na rahmah Yangu, na hao watapata adhabu iumizayo.



فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا اقْتُلُوهُ أَوْ حَرِّقُوهُ فَأَنجَاهُ اللَّـهُ مِنَ النَّارِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٢٤﴾
24. Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: “Muuweni, au muunguzeni.” Basi Allaah Akamuokoa na moto. Hakika katika hayo mna Aayaat (ishara, zingatio n.k) kwa watu wanaoamini.


وَقَالَ إِنَّمَا اتَّخَذْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا مَّوَدَّةَ بَيْنِكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُ بَعْضُكُم بِبَعْضٍ وَيَلْعَنُ بَعْضُكُم بَعْضًا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٥﴾
25. Na (Ibraahiym) akasema: “Hakika mmefanya badala ya Allaah masanamu kuwa ni mapenzi makubwa baina yenu katika uhai wa dunia, kisha Siku ya Qiyaamah mtakanushana nyinyi wenyewe kwa wenyewe, na mtalaaniana wenyewe kwa wenyewe; na makazi yenu ni moto, na hamtokuwa na mwenye kunusuru.”


فَآمَنَ لَهُ لُوطٌ ۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٦﴾
26. Basi Luwtw akamwamini; na (Ibraahiym) akasema: “Hakika mimi nahajiri kwa Rabb wangu; hakika Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika,  Mwenye hikmah wa yote.



وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِ النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ وَآتَيْنَاهُ أَجْرَهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾
27. Tukamtunukia Is-haaq na (mjukuu) Ya’quwb, na Tukajaalia katika dhuria wake Unabii na Kitabu; na Tukampa ujira wake duniani, na hakika yeye katika Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa Swalihina.


وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾
28. Na Luwtw alipowaambia watu wake: “Hakika nyinyi mnaendea uchafu ambao hakuna yeyote aliyekutangulieni hayo katika walimwengu.



أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ وَتَقْطَعُونَ السَّبِيلَ وَتَأْتُونَ فِي نَادِيكُمُ الْمُنكَرَ ۖ فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتِنَا بِعَذَابِ اللَّـهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٢٩﴾
29. Je, nyinyi mnawaendea wanaume na mnawaibia (na kuwaua) wasafiri, na mnafanya katika mikutano yenu munkari? Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: “Tuletee adhabu ya Allaah ukiwa ni miongoni mwa wakweli.”


قَالَ رَبِّ انصُرْنِي عَلَى الْقَوْمِ الْمُفْسِدِينَ ﴿٣٠﴾
30. (Luwtw) Akasema: “Rabb wangu! Ninusuru dhidi ya watu mafisadi.”


وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا إِنَّا مُهْلِكُو أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ ۖ إِنَّ أَهْلَهَا كَانُوا ظَالِمِينَ﴿٣١﴾
31. Na Wajumbe Wetu walipomjia Ibraahiym kwa bishara walisema: “Hakika sisi tutawahiliki watu wa mji huu. Hakika watu wake wamekuwa madhalimu.”


قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطًا ۚ قَالُوا نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَن فِيهَا ۖ لَنُنَجِّيَنَّهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ﴿٣٢﴾
32. (Ibraahiym) Akasema: “Hakika humo yumo Luwtw.” (Malaika) Wakasema: “Sisi tunajua zaidi waliokuwemo humo; tutamuokoa na ahli zake isipokuwa mke wake amekuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma.”



وَلَمَّا أَن جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالُوا لَا تَخَفْ وَلَا تَحْزَنْ ۖ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهْلَكَ إِلَّا امْرَأَتَكَ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٣﴾
33. Na Wajumbe Wetu walipomjia Luwtw aliwasikitikia, na akadhikika na kukosa raha kwa ajili yao; (Malaika) wakasema: “Usikhofu na wala usihuzunike; hakika sisi tutakuokoa na ahli zako isipokuwa mke wako amekuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma.”


إِنَّا مُنزِلُونَ عَلَىٰ أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٣٤﴾
34. Hakika Sisi Tutawateremshia juu ya watu wa mji huu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa sababu ya ule ufasiki waliokuwa wanafanya.


وَلَقَد تَّرَكْنَا مِنْهَا آيَةً بَيِّنَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٣٥﴾
35. Na kwa yakini Tuliacha humo Aayah (zingatio, funzo, ishara n.k) zilizowazi kwa watu wanaotia akilini.


وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَارْجُوا الْيَوْمَ الْآخِرَ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٣٦﴾
36. Na kwa Madyan Tulimtuma ndugu yao Shu’ayb, akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, na tarajieni Siku ya Mwisho na wala msifanye uovu katika ardhi mkifisidi.”


فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٣٧﴾
37. Wakamkadhibisha, basi likawachukuwa tetemeko kali la ardhi wakapambaukiwa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi.


وَعَادًا وَثَمُودَ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَاكِنِهِمْ ۖ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَكَانُوا مُسْتَبْصِرِينَ ﴿٣٨﴾
38. Na kina ‘Aad na Thamuwd; na bila shaka (maangamizi yao) yamekwishakubainikieni katika masikani zao; na shaytwaan aliwapambia ‘amali zao akawazuia na njia japokuwa walikuwa ni wenye kumaizi na kutambua vizuri.


وَقَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانُوا سَابِقِينَ ﴿٣٩﴾
39. Na kina Qaaruwn, na Fir’awn, na Haamaan; na kwa yakini aliwajia Muwsaa kwa hoja bayana wakatakabari katika ardhi, lakini hawakuwa wenye kushinda.


فَكُلًّا أَخَذْنَا بِذَنبِهِ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِ حَاصِبًا وَمِنْهُم مَّنْ أَخَذَتْهُ الصَّيْحَةُ وَمِنْهُم مَّنْ خَسَفْنَا بِهِ الْأَرْضَ وَمِنْهُم مَّنْ أَغْرَقْنَا ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٠﴾
40. Basi kila mmoja Tulimchukuwa kumwadhibu kwa mujibu wa dhambi yake; miongoni mwao wale Tuliowapelekea tufani; na miongoni mwao wale waliochukuliwa na ukelele angamizi; na miongoni mwao wale Tuliowadidimiza ardhini; na miongoni mwao Tuliowagharikisha. Na Allaah Hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.


مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا ۖ وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ ۖ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٤١﴾
41. Mfano wa wale waliochukuwa badala ya Allaah walinzi ni kama mfano wa buibui alivyojitandia nyumba na bila shaka nyumba iliyo dhaifu kuliko zote ni nyumba ya buibui, lau wangelikuwa wanajua!


إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٤٢﴾
42. Hakika Allaah Anavijua vyote vile wanavyoviomba badala Yake, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ ۖ وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu. Lakini hawaifahamu isipokuwa wenye elimu.


خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٤﴾
44. Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Hakika katika hayo mna Aayah (ishara, zingatio) kwa Waumini.


اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ ﴿٤٥﴾
45. Soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyoletewa Wahy katika Kitabu na simamisha Swalaah, hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. Na bila shaka kumdhukuru Allaah ni kubwa zaidi. Na Allaah Anajua yale mnayoyatenda.



وَلَا تُجَادِلُوا أَهْلَ الْكِتَابِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ ۖ وَقُولُوا آمَنَّا بِالَّذِي أُنزِلَ إِلَيْنَا وَأُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَإِلَـٰهُنَا وَإِلَـٰهُكُمْ وَاحِدٌ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na wala msibishane na Ahlal-Kitaabi isipokuwa kwa yale ambayo ni mazuri zaidi; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: “Tumeyaamini ambayo yameteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu, na Ilaah wetu na Ilaaha wenu ni (Allaah) Mmoja Pekee; nasi Kwake tunajisalimisha”


وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ ۚ فَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَمِنْ هَـٰؤُلَاءِ مَن يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا الْكَافِرُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na hivyo ndivyo Tulivyokuteremshia Kitabu (Qur-aan). Basi wale Tuliowapa Maandiko (Tawraat na Injiyl) wanakiamini. Na miongoni mwa hawa (Maquraysh wa Makkah) wako ambao wanakiamini; na hawakanushi Aayaat Zetu isipokuwa makafiri.


وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلَا تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ ۖ إِذًا لَّارْتَابَ الْمُبْطِلُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na wala hukuwa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukisoma kabla yake kitabu chochote, na wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, kwani basi hapo wangetilia shaka wabatilifu.


بَلْ هُوَ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ فِي صُدُورِ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا الظَّالِمُونَ ﴿٤٩﴾
49. Bali hizo ni Aayaat bayana (zimehifadhika) katika vifua vya wale waliopewa elimu. Na hawazikanushi Aayaat Zetu isipokuwa madhalimu.


وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَاتٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥٠﴾
50. Na wakasema: “Kwanini hakuteremshiwa Aayaat (ishara, dalili) kutoka kwa Rabb wake?”  Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika Aayaat ziko kwa Allaah; na hakika mimi ni mwonyaji bayana.


أَوَلَمْ يَكْفِهِمْ أَنَّا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَىٰ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٥١﴾
51. Je, haikuwatosheleza kwamba hakika Sisi Tumekuteremshia Kitabu (Qur-aan) wanachosomewa? Hakika katika hayo bila shaka ni rahmah na ukumbusho (na mawaidha) kwa watu wanaoamini.


قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ شَهِيدًا ۖ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَالَّذِينَ آمَنُوا بِالْبَاطِلِ وَكَفَرُوا بِاللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٥٢﴾
52. Sema: “Anatosheleza Allaah kuwa ni Shahidi baina yangu na baina yenu. Anayajua yale yaliyomo katika mbingu na ardhi. Na wale walioamini ubatilifu na wakamkufuru Allaah, hao ndio waliokhasirika.”


وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ ۚ وَلَوْلَا أَجَلٌ مُّسَمًّى لَّجَاءَهُمُ الْعَذَابُ وَلَيَأْتِيَنَّهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿٥٣﴾
53. Na wanakuharakiza adhabu. Na lau kama si muda maalumu uliokadiriwa, bila shaka ingeliwajia adhabu, na bila shaka itawajia ghafla na hali wao hawahisi.


يَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿٥٤﴾
54. Wanakuharakiza adhabu na hakika Jahannam bila shaka itawazunguka makafiri.


يَوْمَ يَغْشَاهُمُ الْعَذَابُ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِمْ وَيَقُولُ ذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٥٥﴾
55. Siku itakayowafunika adhabu kutoka juu yao na kutoka chini ya miguu yao, na Atasema: “Onjeni yale mliyokuwa mkitenda.”


يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
56. “Enyi waja Wangu walioamini! Hakika ardhi Yangu ni pana, basi Mimi Pekee Niabuduni.”


كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٥٧﴾
57. Kila nafsi itaonja mauti, kisha Kwetu mtarejeshwa.


وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ الْجَنَّةِ غُرَفًا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ نِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na wale walioamini na wakatenda mema, bila shaka Tutawawekea makazi ya ghorofa katika Jannah, yapitayo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Uzuri ulioje ujira wa watendao.



الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٥٩﴾
59. Ambao walisubiri na kwa Rabb wao wanatawakali.


وَكَأَيِّن مِّن دَابَّةٍ لَّا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّـهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Na viumbe wangapi hawabebi riziki zao; Allaah Huwaruzuku wao na nyinyi. Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.


وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٦١﴾
61. Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Basi vipi wanavyoghilibiwa?


اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٦٢﴾
62. Allaah Humkunjulia na Humdhikishia riziki Amtakaye katika waja Wake. Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.


وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ مَوْتِهَا لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٣﴾
63. Na ukiwauliza: “Ni nani Ateremshaye maji kutoka mbinguni, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake?” Bila shaka watasema: “Allaah”.  Sema: “AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah.” Bali wengi wao hawatii akilini.


وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo; na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka hiyo ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua!


فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ ﴿٦٥﴾
65. Wanapopanda merikebu humwomba Allaah wakiwa wenye kumtakasia Yeye Dini, lakini Anapowaokoa katika nchi kavu, tahamaki hao wanamshirikisha.


لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ وَلِيَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Ili wayakanushe yale Tuliyowapa, na ili wastarehe; basi karibuni watakuja kujua.



أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا حَرَمًا آمِنًا وَيُتَخَطَّفُ النَّاسُ مِنْ حَوْلِهِمْ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَةِ اللَّـهِ يَكْفُرُونَ ﴿٦٧﴾
67. Je, hawaoni kwamba hakika Sisi Tumeijaalia (Makkah) kuwa ni mtukufu na amani; na huku wananyakuliwa watu pembezoni mwao? Je, basi wanaamini batili na neema za Allaah wanazikufuru?” 


وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُ ۚ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾
68. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia Allaah uongo, au aliyekadhibisha haki ilipomjia? Je, si katika Jahannam ndio yatakuwa makazi ya makafiri?



وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٦٩﴾
69. Na wale waliofanya juhudi kwa ajili Yetu, bila shaka Tutawaongoza njia Zetu. Na hakika Allaah Yu Pamoja na watendao ihsaan.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.