-->
logo

Asbaabun-Nuzuwul (Sababu Ya Kuteremshwa) Surat Al-Ikhlaasw


 
Sababu Ya Kuteremka Surah hii ni kwamba Washirikina wa Makkah walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu ukoo wa Allaah,

عن أبي بن كعب أن المشركين قالوا لرسول الله صلى الله عليه وسلم: انسب لنا ربك فأنزل الله تعالى (قُل هُوَ اللهُ أَحَدٌ اللهُ الصَمَدُ) قال: فالصمد الذي لم يلد ولم يولد لأنه ليس شيء يولد إلا سيموت وليس شيء يموت إلا سيورث وإن الله تعالى لا يموت ولا يورث (وَلَم يَكُن لَّهُ كُفُواً أَحَد) قال: لم يكن له شبيه ولا عدل وليس كمثله شي


Kutoka kwa Ubay bin Ka'ab kwamba Washirikina (makafiri) walimwambia  Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tuhusishe (tujulishe nani aliyehusiana Naye) Mola wako. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akateremsha

(( قُل هُوَ اللهُ أَحَدٌ اللهُ الصَمَدُ))  
((Sema, Yeye Allaah ni wa pekee)) [Al-Ikhlaasw: 112].


Akasema 'Aswamad' (Mkusudiwa) ambaye Hakuzaa wala hakuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kinachozaliwa isipokuwa kitakufa na hakuna kitu kitakachokufa isipokuwa kitarithiwa, na Allaah Hafi wala Harithiwi ((Wa Lam yaku-Llahu kufuwan Ahad)) ((Wala hana anayefanana Naye hata mmoja)) Akasema: Hakuna anayefanana Naye wala aliye sawa na hapana kitu kama mfano Wake

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.