-->
logo

101 - Al-Qaari-'ah

الْقَارِعَة
Al-Qaari’ah: 101


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


الْقَارِعَةُ ﴿١﴾
1. Al-Qaari’ah, janga kuu linalogonga gonga.


مَا الْقَارِعَةُ ﴿٢﴾
2. Ni nini hiyo Al-Qaari’ah?


وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha nini hiyo Al-Qaari’ah?


يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ ﴿٤﴾
4. Siku watakapokuwa watu kama vipepeo waliotawanyika.


وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنفُوشِ ﴿٥﴾
5. Na majabali yatakuwa kama sufi iliyochambuliwa.


فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾
6. Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito.


فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾
7.  Huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha.


وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾
8. Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu. 


فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾
9. Basi makazi yake ni Haawiyah.


وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ ﴿١٠﴾
10. Na nini kitakachokujulisha ni nini hiyo Haawiyah?


نَارٌ حَامِيَةٌ ﴿١١﴾
11. Ni moto mkali mno wa mwako!

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.