-->
logo

086 - Atw-Twaariq

الطَّارِق
At-Twaariq: 86


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mbingu na kinachokuja usiku.


وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ ﴿٢﴾
2. Na nini kitakachokujulisha kinachokuja usiku?


النَّجْمُ الثَّاقِبُ ﴿٣﴾
3.  Ni nyota yenye mwanga mno inayopenya kwa nguvu. 


إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ ﴿٤﴾
4. Hakuna nafsi yeyote isipokuwa inayo mhifadhi juu yake. 


فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ ﴿٥﴾
5. Basi na atazame mwana Aadam ameumbwa kutoka na kitu gani?


خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ ﴿٦﴾
6. Ameumbwa kutokana na maji yatokayo kwa mchupo.


يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ ﴿٧﴾
7. Yanatoka baina ya uti wa mgongo na mbavu.


إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ ﴿٨﴾
8. Hakika Yeye (Allaah) juu ya kumrudisha kwake (uhai) bila shaka ni Muweza.


يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ ﴿٩﴾
9. Siku siri zitakapopekuliwa.


فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ ﴿١٠﴾
10. Basi hatakuwa na nguvu yoyote na wala mwenye kunusuru yeyote.


وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ ﴿١١﴾
11. Naapa kwa mbingu yenye marejeo (ya kuleta mvua).


وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ ﴿١٢﴾
12. Na Naapa kwa ardhi inayopasuka (kutoa mimea).


إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ ﴿١٣﴾
13. Hakika hii (Qur-aan) ni kauli ya kuhukumu (na kupambanua).


وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ ﴿١٤﴾
14. Na wala hiyo si mzaha.


إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا ﴿١٥﴾
15. Hakika wao wanapanga hila.



وَأَكِيدُ كَيْدًا ﴿١٦﴾
16. Nami Natibua hila (zao).


فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا ﴿١٧﴾
17. Basi wape makafiri muhula, wape muhula taratibu.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.