-->
logo

081 - At-Takwiyr

التَّكْوِير
At-Takwiyr: 81

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾
1. Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga.


وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ﴿٢﴾
2. Na nyota zitapoanguka na kupuputika na kutawanyika. 


وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ﴿٣﴾
3. Na majabali yatakapoendeshwa.

وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ﴿٤﴾

4. Na ngamia wenye mimba pevu watatelekezwa.


وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ﴿٥﴾
5. Na wanyama mwitu watakapokusanywa.


وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ﴿٦﴾
6. Na bahari zitakapojazwa na kuwashwa moto.

وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ﴿٧﴾
7. Na nafsi zitakapounganishwa na roho kisha kwa aina zake.


وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ﴿٨﴾
8. Na mtoto wa kike aliyezikwa hali akiwa yuhai atakapoulizwa.


بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ﴿٩﴾
9. Kwa dhambi gani aliuliwa?


وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ﴿١٠﴾
10. Na sahifa za kurekodi (‘amali) zitakapotandazwa.


وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ﴿١١﴾
11. Na mbingu zitakapobanduliwa.


وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ﴿١٢﴾
12. Na moto uwakao vikali mno utakapowashwa.


وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ﴿١٣﴾
13. Na Jannah itakapoletwa karibu.


عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ﴿١٤﴾
14. Nafsi itajua yale iliyoyahudhurisha.


فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ﴿١٥﴾
15. Basi Naapa kwa sayari zinazotoweka (mchana na zinadhihirika usiku).


الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ﴿١٦﴾
16. Zinazotembea na kujificha.


وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ﴿١٧﴾
17. Na Naapa kwa usiku unapoingia. 


وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ﴿١٨﴾
18. Na Naapa kwa asubuhi inapopambazuka.


إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾
19. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli (ameifikisha) Mjumbe mtukufu (Jibriyl).


ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ﴿٢٠﴾
20. Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allaah) Anayemiliki ‘Arsh.


مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ﴿٢١﴾
21. Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni).


وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ﴿٢٢﴾
22. Na hakuwa swahibu yenu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) majnuni.


وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾
23. Na kwa yakini alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho ulio bayana.


وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ﴿٢٤﴾
24. Naye si mzuiaji wa (kuelezea mambo ya) ghayb.


وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ﴿٢٥﴾
25. Na hii (Qur-aan) si kauli ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.

فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ﴿٢٦﴾
26. Basi mnakwenda wapi?


إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٢٧﴾
27. Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.


لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ﴿٢٨﴾
28. Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika haki)


وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Rabb wa walimwengu.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.