-->
logo

078 - An-Nabaa

  النَّبَاء
An-Nabaa: 78

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ ﴿١﴾
1. Kuhusu nini wanaulizana?


عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ ﴿٢﴾
2. Kuhusu habari adhimu.


الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ﴿٣﴾
3. Ambayo wao wanakhitilafiana kwayo.


كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٤﴾
4. Laa hasha! Hivi karibuni watajua.


ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٥﴾
5. Kisha laa hasha! Hivi karibuni watajua.


أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا ﴿٦﴾
6. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa tandiko?


وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا ﴿٧﴾
7. Na majabali kuwa kama vigingi?


وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا ﴿٨﴾
8. Na Tukakuumbeni kwa jozi; wanaume na wanawake.


وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا ﴿٩﴾
9. Na Tukafanya usingizi wenu mnono, mapumziko kama kufa.


وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ﴿١٠﴾
10. Na Tukafanya usiku kuwa kama libasi la kufunika.


وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ﴿١١﴾
11. Na Tukafanya mchana kuwa ni wa kutafutia maisha.


وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا ﴿١٢﴾
12. Na Tukajenga juu yenu (mbingu) saba imara.


وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ﴿١٣﴾
13. Na Tukafanya siraji yenye mwanga mkali yenye kuwaka kwa nguvu.


وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا ﴿١٤﴾
14. Na Tukateremsha kutoka mawingu yaliyokurubia kunyesha, maji yenye kutiririka kwa kasi kubwa.


لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا ﴿١٥﴾
15. Ili Tutoe kwayo nafaka na mimea. 


وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا ﴿١٦﴾
16. Na mabustani yanayosongomana na kuota teletele.


إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا ﴿١٧﴾
17. Hakika siku ya hukumu na kutenganisha ni wakati maalumu.


يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا ﴿١٨﴾
18. Siku itakayopulizwa katika baragumu, mtakuja makundi makundi.


وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا ﴿١٩﴾
19. Na mbingu zitafunguliwa, zitakuwa milango ya njia.


وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ﴿٢٠﴾
20. Na majabali yataendeshwa na yatakuwa kama sarabi.


إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾
21. Hakika Jahannam utakuwa wenye kuvizia.


لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾
22. Kwa walioruka mipaka wakaasi, mahali pa kurejea.


لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾
23. Watabakia humo dahari nyingi.


لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾
24. Hawatoonja humo cha baridi na wala kinywaji.


إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾
25. Isipokuwa maji yachemkayo na usaha.


جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾
26. Jazaa inayowafikiana kabisa.


إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾
27. Hakika wao walikuwa hawataraji kuhesabiwa.


وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾
28. Na walikadhibisha Aayaat (na ishara, hoja…) Zetu kabisa!


وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾
29. Na kila kitu Tumekitia hesabuni barabara kwa kuandika.


فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴿٣٠﴾
30. Basi onjeni kwani Hatutokuzidishieni isipokuwa adhabu.


إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾
31. Hakika wenye taqwa watapata mafanikio.


حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾
32. Mabustani na mizabibu.


وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾
33. Na wanawake wenye vifua vya kujaa wa hirimu moja.


وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤﴾
34. Na kikombe kilojaa pomo mvinyo.


لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ﴿٣٥﴾
35. Hawatosikia humo upuuzi na wala kukadhibisha.


جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ﴿٣٦﴾
36. Jazaa kutoka kwa Rabb wako, tunukio la kutosheleza.


رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَـٰنِۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ﴿٣٧﴾
37. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake Ar-Rahmaan, hawatoweza kumsemesha.


يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ﴿٣٨﴾
38. Siku atakayosimama Ruwh (Jibriyl) na Malaika safusafu; hawatozungumza isipokuwa yule ambaye Ar-Rahmaan Amempa idhini na atasema yaliyo sahihi.


ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا ﴿٣٩﴾
39. Hiyo ni Siku ya haki; basi atakaye ashike marudio kwa Rabb wake.


إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا ﴿٤٠﴾
40. Hakika Sisi Tumekuonyeni adhabu ya karibu, Siku mtu atakapotazama yale iliyokadimisha mikono yake; na kafiri atasema: “Laiti ningelikuwa mchanga.”

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.