-->
logo

076 - Al-Insaan

  الإِنْسَان
Al-Insaan: 76

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا﴿١﴾
1. Je haikumfikia insani kipindi fulani katika dahari, hakuwa kitu kinachotajwa?


إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا﴿٢﴾
2. Hakika Sisi Tumemuumba insani kutokana na tone la manii iliyochanganyika ili Tumjaribu; Tukamjaalia mwenye kusikia na kuona.


إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumemuongoza njia; ima (awe) ni mwenye kushukuru au mwenye kukufuru.


إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا﴿٤﴾
4. Hakika Sisi Tumewaandalia makafiri minyororo, na pingu na moto uliowashwa vikali mno.


إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا﴿٥﴾
5. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi watakunywa katika vikombe vya mvinyo mchanganyiko wake ni (kutoka chemchemu iitawayo) kaafuwraa.


عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا﴿٦﴾
6. Chemchemu watakayokunywa humo waja wa Allaah, wataibubujua kwa wingi.


يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾
7. Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana.


وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا﴿٨﴾
8. Na wanalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini na mayatima na mateka.


إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا﴿٩﴾
9. “Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya Wajihi wa Allaah, hatukusudii kwenu jazaa na wala shukurani.


إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا﴿١٠﴾
10. “Hakika sisi tunakhofu kutoka kwa Rabb wetu siku ya masononeko, ngumu na ndefu mno.


فَوَقَاهُمُ اللَّـهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا﴿١١﴾
11.  Basi Allaah Atawakinga na shari ya siku hiyo, na Atawapa nuru ya ujamali na furaha.


وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا﴿١٢﴾
12. Na Atawalipa kwa sababu ya kusubiri kwao, Jannah na nguo za hariri.


مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا﴿١٣﴾
13. Wataegemea humo juu ya makochi ya fakhari, hawatoona humo joto la jua wala baridi kali.


وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا﴿١٤﴾
14. Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao na yameinamishwa matunda yake ya kuchumwa, yawakurubie.


وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا﴿١٥﴾
15. Na watazungushiwa vyombo vya fedha, na bilauri zilokuwa za vigae.


قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا﴿١٦﴾
16. Vigae safi kutokana na fedha wamezipima kwa kipimo.


وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا﴿١٧﴾
17. Na watanyweshwa humo kikombe cha mvinyo mchanganyiko wake wa tangawizi.


عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا﴿١٨﴾
18. Chemchemu humo inayoitwa Salsabiylaa.


وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا﴿١٩﴾
19. Na watawazungukia wavulana wa kudumishwa, utakapowaona, utawadhania ni lulu zilizotawanywa.


وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا﴿٢٠﴾
20. Na utakapoona huko,  utaona neema na milki adhimu.


عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا﴿٢١﴾
21. Juu yao wana nguo za hariri nyororo za kijani na za hariri nyororo za makhmel na watapambwa vikuku vya fedha; na Rabb wao Atawanywesha kinywaji cha kitwaharifu.


إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا﴿٢٢﴾
22. (Waatambiwa): “Hakika haya ni jazaa yenu, kwani juhudi zenu zimethaminiwa.”


إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنزِيلًا﴿٢٣﴾
23. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Qur-aan uteremsho wa hatua kwa hatua.


فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا﴿٢٤﴾
24. Basi subiri hukumu ya Rabb wako, na wala usimtii miongoni mwao atendaye dhambi au mwenye kukufuru.


وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٢٥﴾
25. Na lidhukuru Jina la Rabb wako asubuhi na jioni.


وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا﴿٢٦﴾
26. Na katika usiku msujudie na uswali kwa ajili Yake usiku mrefu.


إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا﴿٢٧﴾
27. Hakika hawa wanapenda uhai wa dunia na wanaacha nyuma yao siku nzito (ya Qiyamaah).


نَّحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا﴿٢٨﴾
28. Sisi Tumewaumba, na Tumetia nguvu viungo vyao; na kama Tukitaka, Tutawabadilisha mfano wao badala yao.


إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا﴿٢٩﴾
29. Hakika haya ni mawaidha, basi anayetaka achukue njia ya Rabb wake.



وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٣٠﴾
30. Na hamtoweza kutaka isipokuwa Atake Allaah; hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikimah wa yote.


يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٣١﴾
31. Anamuingiza Amtakaye katika rahmah Yake, na madhalimu Amewaandalia adhabu iumizayo.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.