-->
logo

065 - Atw-Twalaaq

 الطَّلاق
Atw-Twalaaq: 65


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّـهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا﴿١﴾
1. “Ee Nabiy!  Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahaarah) zao, na hesabuni barabara eda; na mcheni Rabb wenu. Msiwatowe katika nyumba zao, na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu ulio bayana. Na hiyo ndio mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayevuka mipaka ya Allaah basi kwa yakini amedhulumu nafsi yake. Hujui; huenda Allaah Atatokezesha jambo jingine baada ya haya. 


فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا﴿٢﴾
2. Na watakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allaah.  Hivyo ndivyo anavyowaidhiwa anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na yeyote anayemcha Allaah; Atamjaalia njia ya kutoka (shidani).


وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّـهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا﴿٣﴾
3. Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii. Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. Hakika Allaah Anatimiza kusudio Lake. Allaah Amejaalia kwa kila kitu makadirio.


وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ ۚوَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا﴿٤﴾
4. Na wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi. Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao. Na yeyote anayemcha Allaah Atamjaalia wepesi katika jambo lake.


ذَٰلِكَ أَمْرُ اللَّـهِ أَنزَلَهُ إِلَيْكُمْ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُعْظِمْ لَهُ أَجْرًا﴿٥﴾
5. Hiyo ni amri ya Allaah Amekuteremshieni; na yeyote anayemcha Allaah, Atamfutia maovu yake na Atamuadhimishia ujira.


أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۖ وَأْتَمِرُوا بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ ۖوَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُ أُخْرَىٰ﴿٦﴾
6. Wawekeni wanawake (mliowataliki) kwenye majumbani mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu, na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wapeni matumizi mpaka wazae mimba zao. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao. Na shaurianeni baina yenu kwa wema. Na mkifanyiana uzito, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.


لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَاآتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا﴿٧﴾
7. Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah. Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa. Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi.


وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِ فَحَاسَبْنَاهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَاهَا عَذَابًا نُّكْرًا﴿٨﴾
8. Na miji mingapi imeasi amri ya Rabb wake na Rusuli Wake, basi Tuliihisabia hisabu shadidi, na Tukaiadhibu adhabu kali kabisa isiyovumilika.


فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَاقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا﴿٩﴾
9. Ikaonja maovu ya mambo yake, na ikawa hatima ya mambo yake kuwa ni khasara.


أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ قَدْ أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا﴿١٠﴾
10. Allaah Amewaandalia adhabu shadidi, basi mcheni Allaah enyi wenye akili mlioamini! Allaah Amekwishakuteremshieni Ukumbusho.


رَّسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّـهِ مُبَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖقَدْ أَحْسَنَ اللَّـهُ لَهُ رِزْقًا﴿١١﴾
11. Ni Rasuli anakusomeeni Aayaat za Allaah zinazobainisha; ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka kwenye viza kuingia katika Nuru. Na yeyote anayemwamini Allaah na akatenda mema, Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo abadi. Allaah Amekwishamfanyia rizki nzuri kabisa.


اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا﴿١٢﴾
12. Allaah ni Yule Aliyeumba mbingu saba na katika ardhi mfano wa hizo,  inateremka amri baina yao ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Muweza, na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu kwa ujuzi (Wake).

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.