-->
logo

061 - Asw-Swaff

الصَّف
Asw-Swaff: 61


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١﴾
1. Vimemsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Naye ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾
2. Enyi walioamini!  Kwanini mnasema yale msiyoyafanya?


كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾
3. Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.


إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ﴿٤﴾
4. Hakika Allaah Anapenda wale wanaopigana katika njia Yake safusafu kama kwamba wao ni jengo lililoshikamana barabara.


وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِي وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ ۖ فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٥﴾
5. Na pale Muwsaa alipoambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Kwanini mnaniudhi na hali mmekwishajua kwamba hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu?” Basi walipopotoka, Allaah Akapotosha nyoyo zao; na Allaah Haongoi watu mafasiki.


وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٦﴾
6. Na pale ‘Iysaa mwana wa Maryam aliposema: “Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Rasuli baada yangu jina lake: Ahmad.” Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: “Hii ni sihiri bayana.”


وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰ إِلَى الْإِسْلَامِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٧﴾
7. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo na hali yeye analinganiwa katika Uislamu? Na Allaah Haongoi watu madhalimu.


يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿٨﴾
8. Wanataka kuizima nuru ya Allaah kwa midomo yao, lakini Allaah ni Mwenye kuitimiza nuru Yake japo makafiri watachukia.


هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٩﴾
9. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿١٠﴾
10. Enyi walioamini! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?


تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿١١﴾
11. Mumuamini Allaah na Rasuli Wake, na mfanye jihaad katika njia ya Allaah kwa mali zenu, na nafsi zenu. Hivyo ndiyo bora kwenu mkiwa mnajua.


يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٢﴾
12. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito na masikani mazuri katika Jannaat za ‘Adnin milele. Huko ndiko kufuzu adhimu.


وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٣﴾
13. Na jengine mlipendalo; nusura kutoka kwa Allaah na ushindi wa karibu. Na wabashirie Waumini.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنصَارَ اللَّـهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ ۖ فَآمَنَت طَّائِفَةٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَت طَّائِفَةٌ ۖ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ﴿١٤﴾
14. Enyi walioamini! Kuweni wenye kunusuru (Dini ya) Allaah kama alivyosema ‘Iysa mwana wa Maryam kwa wafuasi wake watiifu: “Nani wanusuruji wangu kwa ajili ya Allaah?” Wafuasi watiifu wakasema: “Sisi ni wanusuruji wa Allaah” Basi likaamini kundi miongoni mwa wana wa Israaiyl na likakufuru kundi. Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.