-->
logo

059 - Al-Hashr

 الْحَشْر
Al-Hashr: 59


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١﴾
1. Vimemsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Naye ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ ۚ مَا ظَنَنتُمْ أَن يَخْرُجُوا ۖوَظَنُّوا أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ اللَّـهِ فَأَتَاهُمُ اللَّـهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا ۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ ۚ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Aliyewatoa wale waliokufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaabi kutoka majumbani mwao katika mkusanyiko wa kwanza. Hamkudhania kwamba watatoka, nao wakadhani kwamba husuni zao zitawakinga dhidi ya Allaah. Lakini hukmu ya Allaah ikawafikia kutoka ambako wasipotazamia, na Akavurumisha kiwewe katika nyoyo zao. Wanaziharibu nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini, basi pateni funzo enyi wenye uoni wa kutia akilini.


وَلَوْلَا أَن كَتَبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمُ الْجَلَاءَ لَعَذَّبَهُمْ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابُ النَّارِ﴿٣﴾
3. Na lau kama Allaah Asingeliwaandikia kufukuzwa nchi, bila shaka Angeliwaadhibu duniani, na Aakhirah watapata adhabu ya moto.


ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۖ وَمَن يُشَاقِّ اللَّـهَ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٤﴾
4. Hivyo kwa kuwa wao wamempinga Allaah na Rasuli Wake. Na yeyote anayempinga Allaah, basi hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.


مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَائِمَةً عَلَىٰ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيُخْزِيَ الْفَاسِقِينَ﴿٥﴾
5. Hamkukata aina yoyote ya mtende au mliouacha umesimama juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Allaah na ili Awahizi mafasiki.


وَمَا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٦﴾
6. Na ngawira yeyote ile Aliyoifanya Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwao; basi hamkuyaendea mbio kwa farasi na wala vipando vya ngamia lakini Allaah Huwapa mamlaka na nguvu Rusuli Wake dhidi ya Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.


مَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ فَلِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ ۚ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚوَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٧﴾
7. Ngawira yoyote ile Aliyoifanya Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwa watu wa vijiji, basi ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli na kwa ajili ya  jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili yasiwe mzunguko wa zamu baina ya matajiri miongoni mwenu. Na lolote analokupeni Rasuli (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.


لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴿٨﴾
8. Wapatiwe (pia) mafuqara Muhaajiriyn ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na mali zao wanatafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah na wananusuru (Dini ya) Allaah na Rasuli Wake hao ndio wakweli.


وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُالْمُفْلِحُونَ﴿٩﴾
9. Na wale waliokuwa na masikani (Madiynah) na wakawa na iymaan kabla yao, wanawapenda wale waliohajiri kwao, na wala hawahisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa (Muhaajiriyn), na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.


وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٠﴾
10. Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini; Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.


أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نَافَقُوا يَقُولُونَ لِإِخْوَانِهِمُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَئِنْ أُخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ مَعَكُمْ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمْ أَحَدًا أَبَدًا وَإِن قُوتِلْتُمْ لَنَنصُرَنَّكُمْ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿١١﴾
11. Je, huoni wale walionafiki wanawaambia ndugu zao waliokufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaabi: “Mkitolewa bila shaka nasi tutatoka pamoja nanyi na wala hatutomtii yeyote abadani dhidi yenu. Na mkipigwa vita, bila shaka tutakunusuruni.” Na Allaah Anashuhudia kwamba wao bila shaka ni waongo.


لَئِنْ أُخْرِجُوا لَا يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِن قُوتِلُوا لَا يَنصُرُونَهُمْ وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ﴿١٢﴾
12. Wakitolewa, hawatotoka pamoja nao, na wakipigwa vita, hawatowasaidia, na hata wakiwasaidia, bila shaka watageukia mbali migongo (wakimbie), kisha hawatonusuriwa.


لَأَنتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِي صُدُورِهِم مِّنَ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿١٣﴾
13. Bila shaka nyinyi (Waumini) ni tisho zaidi katika vifua vyao kuliko Allaah. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiofahamu.


لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ﴿١٤﴾
14. Hawatopigana nanyi wote pamoja isipokuwa katika miji iliyozatitiwa kwa husuni au kutoka nyuma ya kuta. Uadui wao baina yao ni mkali. Utawadhania wameungana pamoja, kumbe nyoyo zao zimetengana. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotia akilini.


كَمَثَلِ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ۖ ذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٥﴾
15. Ni kama mfano wa wale walio kabla yao hivi karibuni tu walionja matokeo ya uovu wa mambo yao, na watapata adhabu iumizayo.


كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ﴿١٦﴾
16. (Wanafiki ni) Kama mfano wa shaytwaan anapomwambia insani: “Kufuru!” Alipokufuru; (shaytwaan) husema: “Hakika mimi sihusiki nawe! Mimi namkhofu Allaah Rabb wa walimwengu.”


فَكَانَ عَاقِبَتَهُمَا أَنَّهُمَا فِي النَّارِ خَالِدَيْنِ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ﴿١٧﴾
17. Basi hatima yao wote wawili kwamba wao wawili watakuwa motoni ni wenye kudumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya madhalimu.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٨﴾
18. Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho, na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo.


وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿١٩﴾
19. Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah, Naye (Allaah) Akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio mafasiki.


لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۚ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾
20. Hawalingani sawa watu wa motoni na watu wa Jannah, watu wa Jannah ndio wenye kufuzu.


لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۚ وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢١﴾
21. Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya jabali, ungeliliona linanyenyekea likipasukapasuka kutokana na khofu ya Allaah. Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu ili wapate kutafakari.


هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾
22. Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.


هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚسُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾
23. Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye ukubwa na uadhama, Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha.


هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾
24. Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.