-->
logo

053 - An-Najm

النَّجْم
An-Najm: 53

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ ﴿١﴾
1. Naapa kwa nyota zinapotua.


مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ ﴿٢﴾
2. Hakupotoka sahibu wenu na wala hakukosea.


وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾
3. Na wala hatamki kwa hawaa.


إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾
4. Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa.


عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ﴿٥﴾
5. Amemfunza (Jibriyl) mwenye nguvu shadidi.


ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ ﴿٦﴾
6. Mwenye muonekano jamili, muruwa na nguvu na kisha akalingamana sawasawa.


وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ ﴿٧﴾
7. Naye yuko juu kabisa katika upeo wa macho.


ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ ﴿٨﴾
8. Kisha akakurubia na akashuka.


فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ ﴿٩﴾
9. Kisha akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.


فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ ﴿١٠﴾
10. (Allaah) Akamfunulia Wahy mja Wake yale Aliyomfunulia Wahy.


مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ ﴿١١﴾
11. Moyo haukukadhibisha yale aliyoyaona.


أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ ﴿١٢﴾
12. Je, mnambishia kuhusu yale aliyoyaona?


وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ﴿١٣﴾
13. Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine.


عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ﴿١٤﴾
14. Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa.  


عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ ﴿١٥﴾
15. Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa.


إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾
16. Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika


مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ ﴿١٧﴾
17. Jicho lake halikukengeuka wala halikupinduka mipaka.


لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ ﴿١٨﴾
18. Kwa yakini aliona miongoni mwa Aayaat (ishara, dalili) za Rabb wake kubwa kabisa.



أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ ﴿١٩﴾
19. Je, mmeona Laata na ‘Uzzaa?


وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَىٰ ﴿٢٠﴾
20. Na Manaata mwengine wa tatu?


أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الْأُنثَىٰ ﴿٢١﴾
21. Je, nyinyi mna wana wa kiume Naye Ana wana wa kike?


تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ ﴿٢٢﴾
22. Hiyo basi hapo ni mgawanyo wa dhulma kubwa!



إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ الْهُدَىٰ ﴿٢٣﴾
23. Hayo si chochote isipokuwa ni majina mmeyaita nyinyi na baba zenu, wala Allaah Hakuyateremshia dalili yoyote. Hawafuati isipokuwa dhana na yale yanayotamani nafsi (zao), na hali imekwishawajia kutoka kwa Rabb wao mwongozo.


أَمْ لِلْإِنسَانِ مَا تَمَنَّىٰ ﴿٢٤﴾
24. Kwani insani anapata kila  anayoyatamani?


فَلِلَّـهِ الْآخِرَةُ وَالْأُولَىٰ ﴿٢٥﴾
25. Basi ni ya Allaah Pekee ya Aakhirah na ya mwanzo (ya dunia).


وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ ﴿٢٦﴾
26. Na Malaika wangapi mbinguni haitowafaa kitu chochote uombezi wao isipokuwa baada ya kuwa Allaah Ametolea idhini kwa Amtakaye na Akaridhia.


إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلَائِكَةَ تَسْمِيَةَ الْأُنثَىٰ ﴿٢٧﴾
27. Hakika wale wasioamini Aakhirah bila shaka wanawaita Malaika kwa majina ya kike.


وَمَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ ۖ وَإِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا ﴿٢٨﴾
28. Na wala hawana ujuzi wowote ule wa hayo; hawafuati isipokuwa dhana, na hakika dhana haifai kitu chochote mbele ya haki.


فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٢٩﴾
29. Basi achana mbali na ambaye ameupa mgongo ukumbusho Wetu na wala hataki isipokuwa uhai wa dunia.


ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ الْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اهْتَدَىٰ ﴿٣٠﴾
30. Huo ndio upeo wao wa elimu. Hakika Rabb wako ni Mjuzi zaidi wa ambaye amepotoka njia Yake, Naye Mjuzi zaidi wa ambaye ameongoka.


وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى ﴿٣١﴾
31. Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini ili Awalipe wale waliofanya uovu kwa yale waliyoyatenda, na Awalipe wale waliofanya mema kwa mema zaidi.


الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ﴿٣٢﴾
32. Wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa makosa madogo-madogo. Hakika Rabb wako ni Mkunjufu wa kughufuria. Yeye Anakujueni vyema, tangu Alipokuanzisheni kutoka katika ardhi, na pale mlipokuwa mimba changa matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa.


أَفَرَأَيْتَ الَّذِي تَوَلَّىٰ ﴿٣٣﴾
33. Je, (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) umemuona yule aliyegeukia mbali?


وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰ ﴿٣٤﴾
34. Na Akatoa kidogo, kisha akazuia.


أَعِندَهُ عِلْمُ الْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰ ﴿٣٥﴾
35. Je, anayo ilimu ya ghayb hivyo basi anaona?


أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ ﴿٣٦﴾
36. Au hakujulishwa kwa yale yaliyomo katika Swuhuf ya Muwsaa?


وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّىٰ ﴿٣٧﴾
37. Na Ibraahiym aliyetimiza (ahadi).


أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ﴿٣٨﴾
38. Na kwamba mbebaji dhambi hatobeba mzigo wa mwenginewe.


وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ﴿٣٩﴾
39. Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.


وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ ﴿٤٠﴾
40. Na kwamba juhudi yake itakuja kuonekana


ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ ﴿٤١﴾
41. Kisha atalipwa jazaa kamilifu.


وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الْمُنتَهَىٰ ﴿٤٢﴾
42. Na kwamba kwa Rabb wako ndio kikomo.


وَأَنَّهُ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ ﴿٤٣﴾
43. Na kwamba Yeye Ndiye Anayesababisha kicheko na kilio.


وَأَنَّهُ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا ﴿٤٤﴾
44. Na kwamba Yeye Ndiye Anayefisha na Anayehuisha.


وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٤٥﴾
45. Na kwamba Yeye Ameumba jozi mbili; dume na jike.


مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ ﴿٤٦﴾
46. Kutokana na tone la manii linapomiminwa


وَأَنَّ عَلَيْهِ النَّشْأَةَ الْأُخْرَىٰ ﴿٤٧﴾
47. Na kwamba ni juu Yake uanzishaji mwengineo (kufufua).


وَأَنَّهُ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ ﴿٤٨﴾
48. Na kwamba Yeye Ndiye Atoshelezaye na Akinaishaye.


وَأَنَّهُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَىٰ ﴿٤٩﴾
49. Na kwamba Yeye ndiye Rabb wa nyota ya Ash-Shi’-raa (inayoabudiwa).


وَأَنَّهُ أَهْلَكَ عَادًا الْأُولَىٰ ﴿٥٠﴾
50. Na kwamba Yeye Ndiye Aliyeangamiza kina ‘Aad wa awali.


وَثَمُودَ فَمَا أَبْقَىٰ ﴿٥١﴾
51. Na kina Thamuwd kisha Hakubakisha.


وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ ﴿٥٢﴾
52. Na kaumu ya Nuwh hapo kabla, hakika wao walikuwa madhalimu zaidi na wapindukaji mipaka zaidi wa kuasi.


وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ ﴿٥٣﴾
53. Na miji iliyopinduliwa Ameiporomosha mbali mbali.


فَغَشَّاهَا مَا غَشَّىٰ ﴿٥٤﴾
54. Vikafunika vilivyofunika.


فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ ﴿٥٥﴾
55. Basi neema gani za Rabb wako unazitilia shaka?


هَـٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ النُّذُرِ الْأُولَىٰ ﴿٥٦﴾
56. Huyu (Rasuli  صلى الله عليه وآله وسلم) ni mwonyaji miongoni mwa waonyaji wa awali.


أَزِفَتِ الْآزِفَةُ ﴿٥٧﴾
57. Kimekaribia kinachokaribia.


لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ كَاشِفَةٌ ﴿٥٨﴾
58. Hakuna asiyekuwa Allaah mwenye uwezo wa kukitenga.


أَفَمِنْ هَـٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ ﴿٥٩﴾
59. Je, mnastaajabu kwa Al-Hadiyth hii (ya Qur-aan)?


وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ ﴿٦٠﴾
60. Na mnacheka na wala hamlii?


وَأَنتُمْ سَامِدُونَ ﴿٦١﴾
61. Na hali nyinyi mnaghafilika, mnadharau na kushughulika na anasa?  


فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا ۩﴿٦٢﴾
62. Basi msujudieni Allaah na mwabuduni Yeye.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.