-->
logo

050 - Qaaf

 ق
Qaaf: 50

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


ق ۚ وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ﴿١﴾
1. Qaaf. Naapa kwa Qur-aan Al-Majiyd: Adhimu, karimu, yenye kheri, baraka na ilmu tele. 


بَلْ عَجِبُوا أَن جَاءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ فَقَالَ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا شَيْءٌ عَجِيبٌ﴿٢﴾
2. Bali wamestaajabu kwamba amewajia mwonyaji miongoni mwao, wakasema makafiri: “Hili ni jambo la ajabu.


أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ۖ ذَٰلِكَ رَجْعٌ بَعِيدٌ﴿٣﴾
3. Je, hivi tukifa na tukawa udongo (tutafufuliwa)? Ni marejeo ya mbali hayo!”


قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ الْأَرْضُ مِنْهُمْ ۖ وَعِندَنَا كِتَابٌ حَفِيظٌ﴿٤﴾
4. Hakika Sisi Tunajua kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao na Tunacho Kitabu kinachohifadhi barabara.


بَلْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ فَهُمْ فِي أَمْرٍ مَّرِيجٍ﴿٥﴾
5. Bali wamekadhibisha haki ilipowajia, basi wao wamo katika jambo la mkorogeko.



أَفَلَمْ يَنظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ﴿٦﴾
6. Je, hawatazami mbingu juu yao, vipi Tumezijenga na Tumezipamba, na wala hazina mipasuko yoyote.


وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ﴿٧﴾
7. Na ardhi Tumeikunjua na Tukaitupia humo milima thabiti, na Tukaotesha humo kila aina ya mimea ya kupendeza.


تَبْصِرَةً وَذِكْرَىٰ لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ﴿٨﴾
8. Ni ufumbuzi macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kurudia rudia kutubu.



وَنَزَّلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً مُّبَارَكًا فَأَنبَتْنَا بِهِ جَنَّاتٍ وَحَبَّ الْحَصِيدِ﴿٩﴾
9. Na Tukateremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa, kisha Tukaotesha kwayo mabustani na nafaka za kuvunwa.


وَالنَّخْلَ بَاسِقَاتٍ لَّهَا طَلْعٌ نَّضِيدٌ﴿١٠﴾
10. Na mitende mirefu yenye mashada ya matunda yenye kupangika tabaka tabaka.



رِّزْقًا لِّلْعِبَادِ ۖ وَأَحْيَيْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ الْخُرُوجُ﴿١١﴾
11. Ni riziki kwa waja; na Tukahuisha kwayo nchi iliyokufa, hivyo ndivyo kufufuliwa.



كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَأَصْحَابُ الرَّسِّ وَثَمُودُ﴿١٢﴾
12. Wamekadhibisha kabla yao (Maquraysh) kaumu ya Nuwh na wakaazi wa  Ar-Rass na kina Thamuwd.


وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَانُ لُوطٍ﴿١٣﴾
13. Na kina ‘Aad na Fir’awn na ndugu wa Luwtw.


وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّعٍ ۚ كُلٌّ كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ﴿١٤﴾
14. Na wakaazi wa Al-Aykah (kichakani) na kaumu ya Tubba’, wote walikadhibisha Rusuli. Basi ikahakiki onyo Langu.


أَفَعَيِينَا بِالْخَلْقِ الْأَوَّلِ ۚ بَلْ هُمْ فِي لَبْسٍ مِّنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ﴿١٥﴾
15. Je, kwani Tulichoka kwa uumbaji wa kwanza? Bali wao wamo katika kuchanganyikiwa akili na uumbaji upya (kufufuliwa).


وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ﴿١٦﴾
16. Na kwa yakini Tumemuumba insani na Tunajua yale yanayowaza nafsi yake, na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa koo.


إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ﴿١٧﴾
17. Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni. 


مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾
18. Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi).



وَجَاءَتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنْهُ تَحِيدُ﴿١٩﴾
19. Na sakarati ya mauti itakapomjia kwa haki. (Itasemwa): “Hayo ndiyo yale uliyokuwa ukiyakimbilia mbali.”


وَنُفِخَ فِي الصُّورِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْوَعِيدِ﴿٢٠﴾
20. Na itapulizwa katika baragumu.  “Hiyo ndio Siku ya makamio.”


وَجَاءَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّعَهَا سَائِقٌ وَشَهِيدٌ﴿٢١﴾
21. Na kila nafsi itakuja pamoja nayo mwendeshaji na shahidi.



لَّقَدْ كُنتَ فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ﴿٢٢﴾
22. (Aambiwe): “Kwa yakini ulikuwa katika mghafala na haya! Basi Tumekuondoshea kifuniko chako, basi kuona kwako leo ni kukali.”


وَقَالَ قَرِينُهُ هَـٰذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ﴿٢٣﴾
23. Na Malaika wake aliyepewa jukumu atasema: “Hii (rekodi) iliyoko kwangu imeshatayarishwa.”



أَلْقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ﴿٢٤﴾
24. (Allaah Atasema): “Mtupeni katika Jahannam kila kafiri mno, mkaidi!


مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُّرِيبٍ﴿٢٥﴾
25. “Mzuiaji wa kheri, mwenye kutaadi, mtiaji shaka.


الَّذِي جَعَلَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِي الْعَذَابِ الشَّدِيدِ﴿٢٦﴾
26. “Ambaye amefanya mwabudiwa mwengine pamoja na Allaah, basi mtupeni katika adhabu shadidi.”


قَالَ قَرِينُهُ رَبَّنَا مَا أَطْغَيْتُهُ وَلَـٰكِن كَانَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ﴿٢٧﴾
27. Shaytwaan mwenzake atasema: “Rabb wetu! Sikumvukisha mipaka kuasi lakini alikuwa (mwenyewe) katika upotofu wa mbali”.


قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا لَدَيَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِالْوَعِيدِ﴿٢٨﴾
28. (Allaah) Atasema: “Msikhasimiane Kwangu, na hali Nilishakukadimishieni onyo Langu!


مَا يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَيَّ وَمَا أَنَا بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ﴿٢٩﴾
29. “Haibadilishwi kauli Kwangu, Nami si mwenye kudhulumu waja.”


يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ﴿٣٠﴾
30. “Siku Tutakapoiambia Jahannam: “Je, umeshajaa?” Nayo itasema: “Je, kuna ziada yoyote?”



وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيدٍ﴿٣١﴾
31. Na italetwa karibu Jannah kwa wenye taqwa isiwe mbali.


هَـٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٍ﴿٣٢﴾
32. (Itasemwa): “Haya ndiyo yale mliyoahidiwa kwa kila mwenye kurudia rudia kutubia mwenye kuhifadhi vyema (amri za Allaah سبحانه وتعالى).


مَّنْ خَشِيَ الرَّحْمَـٰنَ بِالْغَيْبِ وَجَاءَ بِقَلْبٍ مُّنِيبٍ﴿٣٣﴾
33. “Anayemuogopa Ar-Rahmaan kwa ghayb na akaja na moyo wa kurudia kutubia.”



ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُلُودِ﴿٣٤﴾
34. “Iingieni (Jannah) kwa salama.” Hiyo ndio siku yenye kudumu.


لَهُم مَّا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ﴿٣٥﴾
35. Watapata humo wayatakayo, na Kwetu kuna ziada (kumuona Allaah عز وجل).



وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُم بَطْشًا فَنَقَّبُوا فِي الْبِلَادِ هَلْ مِن مَّحِيصٍ﴿٣٦﴾
36. Na karne ngapi Tumeangamiza kabla yao ambao walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao. Basi walitangatanga sana katika nchi. Je, kuna mahali popote pa kukimbilia?


إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ﴿٣٧﴾
37. Hakika katika hayo, bila shaka ni ukumbusho kwa aliyekuwa na moyo au akatega sikio naye mwenyewe awe hadhiri kwa moyo wake.


وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ﴿٣٨﴾
38. Na kwa yakini Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, na wala Haukutugusa uchovu wowote.


فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ﴿٣٩﴾
39. Subiri juu ya yale wanayoyasema, na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.


وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ﴿٤٠﴾
40.  Na katika usiku Msabbih na baada ya kusujudu.


وَاسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ﴿٤١﴾
41. Na sikiliza kwa makini Siku atakayonadi mwenye kunadi kutoka mahali pa karibu.


يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ﴿٤٢﴾
42. Siku watakayosikia ukelele kwa haki. Hiyo ndio Siku ya kutoka (makaburini).


إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا الْمَصِيرُ﴿٤٣﴾
43. Hakika Sisi Tunahuisha na Tunafisha, na Kwetu ni mahali pa kuishia.


يَوْمَ تَشَقَّقُ الْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ۚ ذَٰلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ﴿٤٤﴾
44. Siku itakayowararukia ardhi (watoke) haraka haraka. Huo ndio mkusanyo, Kwetu ni mepesi.


نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ ۖ فَذَكِّرْ بِالْقُرْآنِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ﴿٤٥﴾
45. Sisi Tunajua zaidi kwa yale wanayoyasema; na wala wewe si mwenye kuwalazimisha kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur-aan anayekhofu onyo Langu.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.