-->
logo

027 - An-Naml

 النَّمْل
An-Naml: 27


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


طس ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْقُرْآنِ وَكِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿١﴾
1.      Twaa Siyn.  Hizo ni Aayaat za Qur –aan na Kitabu kilicho bayana.


هُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾
2.  Mwongozo na bishara kwa Waumini. 


الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٣﴾
3. Ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah, nao kuhusu Aakhirah ni wenye yakini nayo.


إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ زَيَّنَّا لَهُمْ أَعْمَالَهُمْ فَهُمْ يَعْمَهُونَ ﴿٤﴾
4. Hakika wale wasioiamini Aakhirah Tumewapambia ‘amali zao, basi wao wanatangatanga kwa upofu.


أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَهُمْ سُوءُ الْعَذَابِ وَهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ ﴿٥﴾
5. Hao ni wale ambao watapata adhabu mbaya kabisa, nao katika Aakhirah ndio wenye kukhasirika zaidi.


وَإِنَّكَ لَتُلَقَّى الْقُرْآنَ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ عَلِيمٍ ﴿٦﴾
6. Na hakika wewe unapokea Qur-aan kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.



إِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِأَهْلِهِ إِنِّي آنَسْتُ نَارًا سَآتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ آتِيكُم بِشِهَابٍ قَبَسٍ لَّعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ﴿٧﴾
7. (Kumbuka) pale Muwsaa alipoiambia ahli yake: “Hakika mimi nimehisi moto, nitakuleteeni kutoka humo habari, au nitakuleteeni kijinga kinachowaka ili mpate kuota moto.


فَلَمَّا جَاءَهَا نُودِيَ أَن بُورِكَ مَن فِي النَّارِ وَمَنْ حَوْلَهَا وَسُبْحَانَ اللَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨﴾
8. Basi alipoujia, ilinadiwa kwamba: “Amebarikiwa alioko kwenye moto, na aliye pembezoni mwake; na Subhaana-Allaah! Utakasifu ni wa Allaah Rabb wa walimwengu.


يَا مُوسَىٰ إِنَّهُ أَنَا اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٩﴾
9. “Ee Muwsaa! Hakika ni Mimi Allaah Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.


وَأَلْقِ عَصَاكَ ۚ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ لَا تَخَفْ إِنِّي لَا يَخَافُ لَدَيَّ الْمُرْسَلُونَ ﴿١٠﴾
10. Na Tupa fimbo yako.” Basi alipoiona inataharuki kama kwamba ni nyoka; akageuka nyuma kukimbia na wala hakurudi. “Ee Muwsaa! Usikhofu; hakika Mimi hawakhofu Mbele Yangu Rusuli.


إِلَّا مَن ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسْنًا بَعْدَ سُوءٍ فَإِنِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١١﴾
11. “Isipokuwa yule aliyedhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya uovu; basi hakika Mimi ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.


وَأَدْخِلْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ ۖ فِي تِسْعِ آيَاتٍ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَقَوْمِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿١٢﴾
12. “Na ingiza mkono wako katika uwazi wa nguo yako kifuani, utatoka kuwa mweupe bila ya dhara yoyote. Ni miongoni mwa Aayaat (ishara, dalili, miujiza) tisa kwa Fira’wn na watu wake. Hakika wao wamekuwa ni watu mafasiki.”


فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ آيَاتُنَا مُبْصِرَةً قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١٣﴾
13. Basi ilipowajia Aayaat (ishara, dalili) Zetu zenye kuonekana wazi, wakasema: “Hii ni sihiri bayana.”


وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا ۚ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤﴾
14. Wakazikanusha kwa dhulma na majivuno na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha.  Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya mafisadi.



وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ عِلْمًا ۖ وَقَالَا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي فَضَّلَنَا عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّنْ عِبَادِهِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٥﴾
15. Na kwa yakini Tulimpa Daawuwd na Sulaymaan ‘ilmu. Wakasema: “AlhamduliLLaahi, Himidi Anastahiki Allaah Ambaye Ametufadhilisha kuliko wengi katika waja Wake Waumini.”



وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ ۖ وَقَالَ يَا أَيُّهَا النَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ الطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَيْءٍ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَضْلُ الْمُبِينُ ﴿١٦﴾
16. Na Sulaymaan alimrithi Daawuwd; akasema: “Enyi watu! Tumefunzwa lugha ya ndege, na Tumepewa kila kitu. Hakika hii bila shaka ndio fadhila bayana.”


وَحُشِرَ لِسُلَيْمَانَ جُنُودُهُ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ وَالطَّيْرِ فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿١٧﴾
17. Na alikusanyiwa Sulaymaan majeshi yake miongoni mwa majini na wanadamu na ndege, nao wamekusanywa na kupangwa safusafu.


حَتَّىٰ إِذَا أَتَوْا عَلَىٰ وَادِ النَّمْلِ قَالَتْ نَمْلَةٌ يَا أَيُّهَا النَّمْلُ ادْخُلُوا مَسَاكِنَكُمْ لَا يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَانُ وَجُنُودُهُ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١٨﴾
18. Mpaka walipofika kwenye bonde la sisimizi, akasema sisimizi mmoja: “Enyi sisimizi! Ingieni masikanini mwenu, asikupondeni Sulaymaan na majeshi yake, na hali wao hawahisi.”



فَتَبَسَّمَ ضَاحِكًا مِّن قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ ﴿١٩﴾
19. (Sulaymaan) Akatabasamu kuchekea kauli yake, akasema: “Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Niingize kwa rahmah Yako katika waja Wako Swalihina.”


وَتَفَقَّدَ الطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِيَ لَا أَرَى الْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ الْغَائِبِينَ ﴿٢٠﴾
20. Akakagua ndege, akasema: “Imekuwaje, mbona simuoni Al-Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walioghibu? [1]


لَأُعَذِّبَنَّهُ عَذَابًا شَدِيدًا أَوْ لَأَذْبَحَنَّهُ أَوْ لَيَأْتِيَنِّي بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٢١﴾
21. Bila shaka nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja bayana.”


فَمَكَثَ غَيْرَ بَعِيدٍ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمْ تُحِطْ بِهِ وَجِئْتُكَ مِن سَبَإٍ بِنَبَإٍ يَقِينٍ ﴿٢٢﴾
22. Basi (Hud-hud) hakukaa mbali akasema: “Nimegundua ambayo wewe hukuyagundua na nimekujia kutoka Sabaa na habari za yakini.


إِنِّي وَجَدتُّ امْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِن كُلِّ شَيْءٍ وَلَهَا عَرْشٌ عَظِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawamiliki, na amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa mno.


وَجَدتُّهَا وَقَوْمَهَا يَسْجُدُونَ لِلشَّمْسِ مِن دُونِ اللَّـهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لَا يَهْتَدُونَ ﴿٢٤﴾
24. Nimemkuta na watu wake wanalisujudia jua badala ya Allaah, na shaytwaan amewapambia ‘amali zao basi akawazuia na njia, kwa hiyo hawakuongoka.


أَلَّا يَسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي يُخْرِجُ الْخَبْءَ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ﴿٢٥﴾
25. Kwamba hawamsujudii Allaah Ambaye Anatoa yenye kufichika katika mbingu na ardhi na Anayajua yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha.


اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ۩﴿٢٦﴾
26. Allaah hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Rabb wa Al-‘Arsh adhimu”.


قَالَ سَنَنظُرُ أَصَدَقْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٢٧﴾
27. (Sulaymaan) Akasema “Tutaona, kama umesema kweli, au ulikuwa miongoni mwa waongo?


اذْهَب بِّكِتَابِي هَـٰذَا فَأَلْقِهْ إِلَيْهِمْ ثُمَّ تَوَلَّ عَنْهُمْ فَانظُرْ مَاذَا يَرْجِعُونَ ﴿٢٨﴾
28. “Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha ujitenge nao utazame watarudisha nini”


قَالَتْ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ إِنِّي أُلْقِيَ إِلَيَّ كِتَابٌ كَرِيمٌ ﴿٢٩﴾
29. (Malkia) Akasema: “Enyi wakuu! Hakika nimeletewa barua tukufu.


إِنَّهُ مِن سُلَيْمَانَ وَإِنَّهُ بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣٠﴾
30. “Hakika hiyo ni kutoka kwa Sulaymaan, na hakika hiyo (imeanza) Kwa Jina la Allaah, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

أَلَّا تَعْلُوا عَلَيَّ وَأْتُونِي مُسْلِمِينَ ﴿٣١﴾
31. “Msinifanyie ujeuri; na nijieni mkiwa mmesilimu.”


قَالَتْ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي أَمْرِي مَا كُنتُ قَاطِعَةً أَمْرًا حَتَّىٰ تَشْهَدُونِ ﴿٣٢﴾
32. (Malkia) Akasema: “Enyi wakuu! Nipeni shauri katika jambo langu maana sikuwa mwenye kuamua jambo mpaka mhudhurie nami”.


قَالُوا نَحْنُ أُولُو قُوَّةٍ وَأُولُو بَأْسٍ شَدِيدٍ وَالْأَمْرُ إِلَيْكِ فَانظُرِي مَاذَا تَأْمُرِينَ ﴿٣٣﴾
33. Wakasema: “Sisi ni wenye nguvu, na wenye uwezo mkali wa vita; na amri iko kwako, basi tazama unaamrisha nini?”


قَالَتْ إِنَّ الْمُلُوكَ إِذَا دَخَلُوا قَرْيَةً أَفْسَدُوهَا وَجَعَلُوا أَعِزَّةَ أَهْلِهَا أَذِلَّةً ۖ وَكَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ ﴿٣٤﴾
34. Akasema: “Hakika wafalme wanapoingia mji huufisidi, na huwafanya watukufu wake kuwa dhalili; na hivyo ndivyo wafanyavyo.


وَإِنِّي مُرْسِلَةٌ إِلَيْهِم بِهَدِيَّةٍ فَنَاظِرَةٌ بِمَ يَرْجِعُ الْمُرْسَلُونَ ﴿٣٥﴾
35. “Nami nitawapelekea hadia, kisha nitangojea kutazama watakayorudi nayo Rusuli.”



فَلَمَّا جَاءَ سُلَيْمَانَ قَالَ أَتُمِدُّونَنِ بِمَالٍ فَمَا آتَانِيَ اللَّـهُ خَيْرٌ مِّمَّا آتَاكُم بَلْ أَنتُم بِهَدِيَّتِكُمْ تَفْرَحُونَ﴿٣٦﴾
36. Basi walipomjia Sulaymaan, alisema: “Je, mnanisaidia kwa mali? Basi Aliyonipa Allaah ni bora kuliko Aliyokupeni nyinyi, bali nyinyi mnafurahia hadia yenu.”


ارْجِعْ إِلَيْهِمْ فَلَنَأْتِيَنَّهُم بِجُنُودٍ لَّا قِبَلَ لَهُم بِهَا وَلَنُخْرِجَنَّهُم مِّنْهَا أَذِلَّةً وَهُمْ صَاغِرُونَ ﴿٣٧﴾
37. “Rudi kwao; bila shaka tutawaendea kwa jeshi wasiloweza kukabiliana nalo, na bila shaka tutawatoa humo hali ya kuwa wamedhalilika na walio duni.”


قَالَ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَيُّكُمْ يَأْتِينِي بِعَرْشِهَا قَبْلَ أَن يَأْتُونِي مُسْلِمِينَ ﴿٣٨﴾
38. Akasema: “Enyi wakuu! Nani kati yenu ataniletea kiti chake cha enzi kabla hawakunijia wakiwa wamesilimu?


قَالَ عِفْرِيتٌ مِّنَ الْجِنِّ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّي عَلَيْهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٌ ﴿٣٩﴾
39. Akasema ‘Ifriti miongoni mwa majini: “Mimi nitakuletea kabla hujasimama kutoka mahali pako na hakika mimi kwa hilo, bila shaka ni mwenye nguvu mwaminifu.”



قَالَ الَّذِي عِندَهُ عِلْمٌ مِّنَ الْكِتَابِ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن يَرْتَدَّ إِلَيْكَ طَرْفُكَ ۚ فَلَمَّا رَآهُ مُسْتَقِرًّا عِندَهُ قَالَ هَـٰذَا مِن فَضْلِ رَبِّي لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ ۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيٌّ كَرِيمٌ ﴿٤٠﴾
40. Akasema yule ambaye ana elimu kutoka katika Kitabu: “Mimi nitakuletea kabla halijapepesa jicho lako.” Basi alipokiona kimewekwa mbele yake; (Sulaymaan) alisema: “Hii ni katika fadhila za Rabb wangu, Anijaribu; je, nitashukuru, au nitakufuru. Na yeyote yule anayeshukuru, basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na yeyote yule asiyekuwa na shukurani, basi hakika Rabb wangu ni Mkwasi, Mkarimu.


قَالَ نَكِّرُوا لَهَا عَرْشَهَا نَنظُرْ أَتَهْتَدِي أَمْ تَكُونُ مِنَ الَّذِينَ لَا يَهْتَدُونَ ﴿٤١﴾
41. (Sulaymaan) Akasema: “Mgeuzieni kiti chake cha enzi tutazame; ataongoka au atakuwa miongoni mwa ambao wasioongoka.


فَلَمَّا جَاءَتْ قِيلَ أَهَـٰكَذَا عَرْشُكِ ۖ قَالَتْ كَأَنَّهُ هُوَ ۚ وَأُوتِينَا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ ﴿٤٢﴾
42. Basi (Malkia) alipokuja, ikasemwa: “Je, ni kama hiki kiti chako cha enzi?” Akasema: “Kama ndicho hicho.” (Sulyamaan akasema): “Na tumepewa elimu kabla yake na tukawa Waislamu.”


وَصَدَّهَا مَا كَانَت تَّعْبُدُ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ إِنَّهَا كَانَتْ مِن قَوْمٍ كَافِرِينَ ﴿٤٣﴾
43. Na yale aliyokuwa akiyaabudu badala ya Allaah yalimzuia (Uislamu). Hakika alikuwa miongoni mwa watu makafiri.


قِيلَ لَهَا ادْخُلِي الصَّرْحَ ۖ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ ۗ قَالَتْ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَانَ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٤﴾
44. Akaambiwa: “Ingia katika kasri fakhari. Alipoliona alilidhania ni bwawa refu la maji, akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaymaan) Akasema: “Hakika hilo kasri la fakhari lilosakafiwa kwa vigae.” (Malkia) Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na nimesilimu pamoja na Sulaymaan kwa Allaah Rabb wa walimwengu.”


وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٥﴾
45. Na kwa yakini Tuliwapelekea kina Thamuwd ndugu yao Swaalih kwamba: “Mwabuduni Allaah.” Tahamaki wakawa makundi mawili yanayokhasimiana.


قَالَ يَا قَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ ۖ لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٦﴾
46. (Swaalih) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnahimiza uovu kabla ya mema; kwa nini msimwombe Allaah maghfirah ili huenda mkarehemewa?”


قَالُوا اطَّيَّرْنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَ ۚ قَالَ طَائِرُكُمْ عِندَ اللَّـهِ ۖ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تُفْتَنُونَ ﴿٤٧﴾
47. Wakasema: “Tumepata nuksi kwa sababu yako na kwa wale walio pamoja nawe.” (Swaalih) Akasema: “Nuksi yenu iko kwa Allaah. Bali nyinyi ni watu mliojaribiwa.”


وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na kulikuweko katika mji ule watu tisa wakifanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenei.



قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّـهِ لَنُبَيِّتَنَّهُ وَأَهْلَهُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Wakasema: “Apishaneni kwa Jina la Allaah kwamba tutamhujumu (Swaalih) kwa siri usiku na ahli yake, kisha tutasema kwa jamaa yake wa karibu: “Hatukushuhudia maangamilizi ya ahli yake; nasi hakika ni wa kweli.”


وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٠﴾
50. Wakapanga njama Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha njama nao huku hawatambui. 



فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥١﴾
51. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya njama zao, kwamba Tuliwadamirisha na watu wao wote.



فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥٢﴾
52. Basi hizo ni nyumba ni magofu kwa sababu ya yale waliyodhulumu. Hakika katika hayo kuna Aayah (ishara, zingatio, funzo n.k) kwa watu wanaojua.


وَأَنجَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na Tukawaokoa wale walioamini, na waliokuwa na taqwa.


وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ ﴿٥٤﴾
54. Na (kumbuka) Luwtw alipowaambia watu wake: “Je, mnafanya machafu na hali nyinyi mnaona?



أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ ﴿٥٥﴾
55. “Je, nyinyi mnawaendea wanaume kwa matamanio badala ya wanawake?!” Bali nyinyi ni watu majahili.”



فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوا آلَ لُوطٍ مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ ﴿٥٦﴾
56. Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: “Watoeni watu wa Luwtw kutoka mji wenu, hakika wao ni watu wanaojiweka katika utakaso.


فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَاهَا مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٥٧﴾
57. Basi Tulimuokoa na ahli yake isipokuwa mke wake Tumekadiria miongoni mwa watakaobakia nyuma.”


وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَاءَ مَطَرُ الْمُنذَرِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na Tukawanyeshea mvua. Basi uovu ulioje mvua ya walioonywa.


قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ وَسَلَامٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَىٰ ۗ آللَّـهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٥٩﴾
59. Sema: AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah na amani iwe juu ya waja Wake Aliowakhitari. Je, Allaah ni bora au wale wanaowashirikisha (Naye)?



أَمَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا بِهِ حَدَائِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنبِتُوا شَجَرَهَا ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Au nani Aliyeumba mbingu na ardhi na Akakuteremshieni kutoka mbinguni maji, kisha Tukaotesha kwayo mabustani anisi za kupendeza kabisa, nyinyi hamna uwezo wa kuotesha miti yake. Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Bali wao ni watu wanaovumisha kusawazisha (na Allaah).



أَمَّن جَعَلَ الْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَالَهَا أَنْهَارًا وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزًاۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦١﴾
61. Au nani Aliyeijaalia ardhi kuwa mahali pa matulio na Akajaalia baina yake mito, na Akaiwekea milima mirefu thabiti na Akajaalia baina ya bahari mbili (ya chumvi na tamu) kizuizi. Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Bali wengi wao hawajui.



أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾
62. Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka.


أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِۚتَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٣﴾
63. Au nani Anayekuongozeni katika viza vya nchi kavu na bahari; na nani anayetuma pepo za bishara kabla ya rahmah Yake. Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ametukuka Allaah kutokana na yale wanayomshirikisha.


أَمَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦٤﴾
64. Au nani Anayeanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha; na nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Sema: “Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli.”


قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾
65. Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa.”


بَلِ ادَّارَكَ عِلْمُهُمْ فِي الْآخِرَةِ ۚ بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّنْهَا ۖ بَلْ هُم مِّنْهَا عَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Bali umefikia kikomo ujuzi wao kuhusu Aakhirah. Bali wao wamo katika shaka nayo. Bali wao ni vipofu nayo.


وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا وَآبَاؤُنَا أَئِنَّا لَمُخْرَجُونَ ﴿٦٧﴾
67. Na wale waliokufuru wakasema: “Je, tukiwa mchanga na baba zetu; hivi sisi kweli tutakuja kutolewa?”


لَقَدْ وُعِدْنَا هَـٰذَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٦٨﴾
68. “Tumekwishaahidiwa haya sisi na baba zetu hapo kabla. Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale.


قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٦٩﴾
69. Sema: “Tembeeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wahalifu.”


وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُن فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ ﴿٧٠﴾
70. Na wala usihuzunike juu yao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na wala usiwe katika dhiki kutokana na wanayofanya njama.


وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٧١﴾
71. Na wanasema: “Ni lini hiyo ahadi mkiwa ni wakweli?


قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ رَدِفَ لَكُم بَعْضُ الَّذِي تَسْتَعْجِلُونَ ﴿٧٢﴾
72. Sema: “Asaa yawe yamekurubia nyuma yenu baadhi ya mnayoyahimiza.”



وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na hakika Rabb wako ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na hakika Rabb wako bila shaka Anajua yale yanayoficha vifua vyao na yale wanayoyatangaza



وَمَا مِنْ غَائِبَةٍ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٧٥﴾
75.  Na hakuna chochote cha ghayb katika mbingu na ardhi isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha.


إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٧٦﴾
76. Hakika hii Qur-aan inasimulia wana wa Israaiyl mengi zaidi ambayo wao wanakhitilafiana nayo.


وَإِنَّهُ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na hakika hii ni Mwongozo na rahmah kwa Waumini.


إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُم بِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ ﴿٧٨﴾
78. Hakika Rabb wako Atahukumu baina yao kwa Hukumu Yake. Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.


فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۖ إِنَّكَ عَلَى الْحَقِّ الْمُبِينِ ﴿٧٩﴾
79. Basi tawakali kwa Allaah. Hakika wewe uko kwenye haki bayana.


إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٨٠﴾
80. Hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu, na wala huwezi kusikilizisha viziwi wito wanapokengeuka wakigeuza migongo yao. 



وَمَا أَنتَ بِهَادِي الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨١﴾
81. Na wala wewe huwezi kuwaongoa vipofu kutoka upotofu wao; huwasikilizishi isipokuwa wale wanaoamini Aayaat Zetu nao ndio wanaojisalimisha (kuwa Waislamu).


وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ﴿٨٢﴾
82. Na itakapotimizwa kauli dhidi yao, Tutawatolea mnyama atembeaye katika ardhi atakayewasemezesha kwa sababu watu walikuwa hawana yakini na Aayaat (na ishara) Zetu.


وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿٨٣﴾
83. Na Siku Tutakayokusanya katika kila Ummah makundi miongoni mwa wale wanaokadhibisha Aayaat (na ishara) Zetu nao watakusanywa waburuzwe.


حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوا قَالَ أَكَذَّبْتُم بِآيَاتِي وَلَمْ تُحِيطُوا بِهَا عِلْمًا أَمَّاذَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾
84. Mpaka watakapokuja (Allaah) Atasema: “Je, si mlikadhibisha Aayaat (na ishara) Zangu bila ya kujizua vyema? Au mlikuwa mnafanya nini?”


وَوَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِم بِمَا ظَلَمُوا فَهُمْ لَا يَنطِقُونَ ﴿٨٥﴾
85. Na itatimizwa kauli dhidi yao kwa yale waliyodhulumu, nao hawatoweza kutamka lolote.


أَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا اللَّيْلَ لِيَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٨٦﴾
86. Je, hawaoni kwamba Tumejaalia usiku ili wapate utulivu humo, na mchana wenye kuangaza? Hakika katika hayo bila shaka mna Aayaat (ishara, zingatio) kwa watu wanaoamini.


وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na Siku itakayopulizwa baragumu, atafazaika kila alioko mbinguni na aliyoko ardhini isipokuwa Amtakaye Allaah. Na wote watamfikia wakiwa duni wamedhalilika.


وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ ۚ صُنْعَ اللَّـهِ الَّذِي أَتْقَنَ كُلَّ شَيْءٍ ۚ إِنَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَفْعَلُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na utaona majabali ukiyadhania yametulia thabiti nayo yanapita mpito wa mawingu. Utengenezaji wa Allaah Ambaye Ametengeneza kwa umahiri kila kitu. Hakika Yeye ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myafanyayo.


مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَهُم مِّن فَزَعٍ يَوْمَئِذٍ آمِنُونَ ﴿٨٩﴾ ﴾
89. Atakayekuja na jema, basi atapata bora zaidi kuliko hilo; nao watakuwa katika amani na mafazaiko ya Siku hiyo.


وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَكُبَّتْ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٩٠﴾
90. Na atakayekuja na ovu, basi zitatupwa gubigubi nyuso zao katika moto; (wataambiwa): “Je, kwani mnalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda?”


إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَـٰذِهِ الْبَلْدَةِ الَّذِي حَرَّمَهَا وَلَهُ كُلُّ شَيْءٍ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩١﴾
91. “Hakika nimeamrishwa nimwabudu Rabb wa mji huu Ambaye Ameufanya mtukufu, na ni Vyake Pekee vitu vyote. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu.


وَأَنْ أَتْلُوَ الْقُرْآنَ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَقُلْ إِنَّمَا أَنَا مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿٩٢﴾
92. “Na kwamba nisome Qur-aan.” Hivyo anayeongoka, basi hakika anaongoka kwa ajili ya manufaa ya nafsi yake. Na anayepotoka, basi sema: “Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.”


وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ سَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَتَعْرِفُونَهَا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٣﴾
93. Na sema: “AlhamduliLLaahi, Himidi Anastahiki Allaah, Atakuonyesheni Aayaat (ishara, dalili) Zake na mtazitambua.” Na Rabb wako si Mwenye kughafilika kuhusu yale wanayoyatenda.”





[1] Faida: Hud-hud ni ndege wenye vishungi wanaotoa ukulele, wenye manyoa ya rangi ya samaki wa samoni.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.