-->
logo

021 - Al-Anbiyaa

 الأنْبِيآء
Al-Anbiyaa: 21


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


اقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ ﴿١﴾
1. Imewakaribia watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala wanakengeuka (na wanapuuza).


مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ إِلَّا اسْتَمَعُوهُ وَهُمْ يَلْعَبُونَ ﴿٢﴾
2. Hauwafikii Ukumbusho wowote ule mpya kutoka kwa Rabb wao isipokuwa huusikiliza kwa makini na huku wao wanacheza.


لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ ۗ وَأَسَرُّوا النَّجْوَى الَّذِينَ ظَلَمُوا هَلْ هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ ۖ أَفَتَأْتُونَ السِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ ﴿٣﴾
3. Nyoyo zao zimeshughulika, na wale waliodhulumu hunong’onezana kwa siri:  “Je, ni nani huyu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni binaadamu kama nyinyi? Je, mnaiendea sihiri hii na hali nyinyi mnaona?”

قَالَ رَبِّي يَعْلَمُ الْقَوْلَ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٤﴾
4. (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Akasema: “Rabb wangu Anajua yasemwayo katika mbingu na ardhi; Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.


بَلْ قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ بَلِ افْتَرَاهُ بَلْ هُوَ شَاعِرٌ فَلْيَأْتِنَا بِآيَةٍ كَمَا أُرْسِلَ الْأَوَّلُونَ ﴿٥﴾
5.   Lakini wakasema: (Qur-aan) “Ni ndoto za mkorogano! Bali ameitunga! Bali yeye ni mshairi! Basi atuletee Aayah (muujiza) kama walivyotumwa wa awali.”


مَا آمَنَتْ قَبْلَهُم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا ۖ أَفَهُمْ يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾
6. Hawakuamini kabla yao (umati wa) mji wowote Tuliouangamiza. Je, basi wao wataamini?


وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۖ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٧﴾
7. Na Hatukutuma kabla yako isipokuwa wanaume Tunawafunulia Wahy; basi ulizeni watu wa ukumbusho mkiwa hamjui.


وَمَا جَعَلْنَاهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَمَا كَانُوا خَالِدِينَ ﴿٨﴾
8. Na Hatukuwafanya (hao Rasuli) kuwa na miili isiyokula chakula, na hawakuwa wenye kudumu.


ثُمَّ صَدَقْنَاهُمُ الْوَعْدَ فَأَنجَيْنَاهُمْ وَمَن نَّشَاءُ وَأَهْلَكْنَا الْمُسْرِفِينَ ﴿٩﴾
9. Kisha Tukawasadikishia ahadi Tukawaokoa wao na wale Tuliowataka; na Tukaangamiza wapindukiaji mipaka.


لَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَابًا فِيهِ ذِكْرُكُمْ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٠﴾
10. Kwa yakini Tumekuteremshieni Kitabu (Qur-aan) ndani yake mna makumbusho yenu, je, basi hamtii akilini?


وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا آخَرِينَ ﴿١١﴾
11. Na miji mingapi Tumeiteketeza iliyokuwa ikidhulumu, na Tukaanzisha baada yake kaumu nyengizo.


فَلَمَّا أَحَسُّوا بَأْسَنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَرْكُضُونَ ﴿١٢﴾
12. Basi walipohisi adhabu Yetu; mara wao (walijaribu) kuikimbia.


لَا تَرْكُضُوا وَارْجِعُوا إِلَىٰ مَا أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَاكِنِكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْأَلُونَ ﴿١٣﴾
13. (Waliambiwa) “Msikimbie, na rejeeni kwenye yale mliyojistarehesha nayo, na maskani zenu ili mpate kuulizwa.”

قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿١٤﴾
14. Wakasema: “Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu.”


فَمَا زَالَت تِّلْكَ دَعْوَاهُمْ حَتَّىٰ جَعَلْنَاهُمْ حَصِيدًا خَامِدِينَ ﴿١٥﴾
15. Basi ukaendelea huo kuwa ni wito wao mpaka Tukawafanya waliofekwa wenye kuzimia.


وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ ﴿١٦﴾
16. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na yaliyo baina yake kama wenye kufanya mchezo.


لَوْ أَرَدْنَا أَن نَّتَّخِذَ لَهْوًا لَّاتَّخَذْنَاهُ مِن لَّدُنَّا إِن كُنَّا فَاعِلِينَ ﴿١٧﴾
17. Lau Tungelitaka kufanya burudani bila shaka Tungejifanyia Sisi wenyewe lau kama Tungelikuwa wafanyao (burudani). 


بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ ﴿١٨﴾
18. Bali Tunavurumisha haki dhidi ya batili kisha inaitengua; tahamaki ni yenye kutoweka. Na ole wenu kutokana na ambayo mnayovumisha.


وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ ﴿١٩﴾
19. Na ni milki Yake waliomo katika mbingu na ardhi, na (Malaika) ambao wako Kwake hawatakabari kumwabudu Kwake na wala hawachoki.


يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ ﴿٢٠﴾
20. Wanasabbih usiku na mchana wala hawazembei.


أَمِ اتَّخَذُوا آلِهَةً مِّنَ الْأَرْضِ هُمْ يُنشِرُونَ ﴿٢١﴾
21. Je, wamechukua miungu katika ardhi inayofufua?


لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّـهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَانَ اللَّـهِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿٢٢﴾
22.  Lau wangelikuweko humo (mbinguni na ardhini) waabudiwa badala ya Allaah, bila shaka zingelifisidika. Basi Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah Rabb wa ‘Arsh kutokana na ambayo wanavumisha.

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ ﴿٢٣﴾
23. Haulizwi (Allaah) kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.



أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ ۖ هَـٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِيَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِي ۗ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ الْحَقَّ ۖ فَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٤﴾
24. Je, wamejichukulia badala Yake waabudiwa? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآلهوسلم): “Leteni burhani yenu. Hii (Quraan) ni ukumbusho wa walio pamoja nami, na ni ukumbusho wa walio kabla yangu; bali wengi wao hawajui haki; kisha wao ni wenye kukengeuka.”


وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾
25. Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi Niabuduni.”


وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Na wakasema: “Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana! Subhaanah! Utakasifu ni Wake! Bali (hao) ni waja waliokirimiwa.


لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾
27. Hawamtangulii (Allaah) kwa kauli, nao kwa amri Yake wanatenda.



يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ ﴿٢٨﴾
28. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawataomba shafaa’ah (yeyote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia, nao kutokana na kumkhofu, ni wenye khofu na kutahadhari.


وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: “Mimi ni mwabudiwa badala Yake,” basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu.



أَوَلَمْ يَرَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٠﴾
30. Je, hawakuona wale waliokufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikamana Tukazibabandua na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai. Je, basi hawaamini?


وَجَعَلْنَا فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ ﴿٣١﴾
31. Na Tukajaalia katika ardhi milima thabiti isiwayumbiye yumbiye, na Tukajaalia humo njia pana baina yake kama barabara ili wapate kuongozwa.


وَجَعَلْنَا السَّمَاءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ ﴿٣٢﴾
32. Na Tukajaalia mbingu kuwa ni sakafu ilohifadhiwa. Lakini wao wanazipuuzilia mbali Aayaat (ishara) zake.


وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ ﴿٣٣﴾
33. Naye Ndiye Ambaye Ameumba usiku na mchana, na jua na mwezi; vyote vinaelea angani.


وَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ الْخُلْدَ ۖ أَفَإِن مِّتَّ فَهُمُ الْخَالِدُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na Hatukujaalia kwa mtu yeyote kabla yako kuwa ni mwenye kudumu; Je, kwani ukifa basi wao watadumu?


كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٣٥﴾
35. Kila nafsi itaonja mauti! Na Tutakujaribuni kwa mitihani ya shari na kheri. Na Kwetu mtarejeshwa.


وَإِذَا رَآكَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا الَّذِي يَذْكُرُ آلِهَتَكُمْ وَهُم بِذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ هُمْ كَافِرُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na wanapokuona wale waliokufuru hawakuchukulii isipokuwa mzaha. (Wakisema): “Je, huyu ndiye anayewataja (vibaya) waabudiwa wenu?” Na wao ni wenye kukufuru kwa kutajwa Ar-Rahmaan.


خُلِقَ الْإِنسَانُ مِنْ عَجَلٍ ۚ سَأُرِيكُمْ آيَاتِي فَلَا تَسْتَعْجِلُونِ ﴿٣٧﴾
37. Insani ameumbwa kuwa na pupa. Nitakuonyesheni Aayaat (hukmu, adhabu) Zangu; basi msiharakize.


وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣٨﴾
38. Na wanasema: “Lini itakuwa hiyo ahadi (ya kuadhibiwa) mkiwa ni wakweli?” 


لَوْ يَعْلَمُ الَّذِينَ كَفَرُوا حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ النَّارَ وَلَا عَن ظُهُورِهِمْ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴿٣٩﴾
39. Lau wangelijua wale waliokufuru wakati pale hawatoweza kukinga nyuso zao na moto, na wala migongo yao, na wala wao hawatonusuriwa. 


بَلْ تَأْتِيهِم بَغْتَةً فَتَبْهَتُهُمْ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٤٠﴾
40. Bali utawafikia ghafla; hivyo uwashtue na wapigwe na butwaa, kisha hawatoweza kuurudisha, na wala wao hawatopewa muhula.


وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٤١﴾
41. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Rusuli kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); basi ikawazunguka wale waliofanya dhihaka miongoni mwao yale waliyokuwa wakayifanyia istihzai.


قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مِنَ الرَّحْمَـٰنِ ۗ بَلْ هُمْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ ﴿٤٢﴾
42. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nani awezaye kukulindeni na kukuhifadhini usiku na mchana kutokana na (adhabu ya) Ar-Rahmaan?” Bali wao ni wenye kupuuzilia mbali ukumbusho wa Rabb wao.


أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ ﴿٤٣﴾
43. Je, kwani wana waabudiwa wanaoweza kuwakinga Nasi?  Hawawezi kujinusuru nafsi zao na wala hawatolindwa Nasi.



بَلْ مَتَّعْنَا هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۗ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ أَفَهُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٤٤﴾
44. Bali Tuliwastarehesha hawa (makafiri), na baba zao mpaka ukatawilika umri kwao. Je, hawaoni kwamba Tunaifikia ardhi hii, Tunaipunguza ncha zake? Je, basi wao watashinda?


قُلْ إِنَّمَا أُنذِرُكُم بِالْوَحْيِ ۚ وَلَا يَسْمَعُ الصُّمُّ الدُّعَاءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ ﴿٤٥﴾
45. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi nakuonyeni kwa Wahy. Lakini viziwi hawasikii wito wanapotahadharishwa.”


وَلَئِن مَّسَّتْهُمْ نَفْحَةٌ مِّنْ عَذَابِ رَبِّكَ لَيَقُولُنَّ يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na inapowagusa mpulizo mmoja tu wa adhabu ya Rabb wako kwa hakika husema: “Ole wetu!  Hakika sisi tulikuwa madhalimu.”


وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na Tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Qiyaamah; basi nafsi haitodhulumiwa kitu chochote. Na japo ikiwa uzito wa mbegu ya hardali, Tutaileta. Na inatosheleza Kwetu kuwa Wenye kuhesabu.


وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ وَهَارُونَ الْفُرْقَانَ وَضِيَاءً وَذِكْرًا لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٨﴾
48. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa na Haaruwn pambanuo la haki na batili na mwanga na ukumbusho kwa wenye taqwa.

الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ وَهُم مِّنَ السَّاعَةِ مُشْفِقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Wale wanaomkhofu Rabb wao kwa ghayb nao wanaikhofu Saa.


وَهَـٰذَا ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَاهُ ۚ أَفَأَنتُمْ لَهُ مُنكِرُونَ ﴿٥٠﴾
50. Na hii (Qur-aan) ni ukumbusho wenye baraka Tumeiteremsha. Je, basi nyinyi mtaikanusha?

وَلَقَدْ آتَيْنَا إِبْرَاهِيمَ رُشْدَهُ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِ عَالِمِينَ ﴿٥١﴾
51. Na kwa yakini Tulimpa Ibraahiym uongofu wake kabla, na Tulikuwa Wenye kumjua vizuri.

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا هَـٰذِهِ التَّمَاثِيلُ الَّتِي أَنتُمْ لَهَا عَاكِفُونَ ﴿٥٢﴾
52. Alipomwambia baba yake na watu wake: “Nini haya masanamu ambayo nyinyi mnayakalia kuyaabudu.”

قَالُوا وَجَدْنَا آبَاءَنَا لَهَا عَابِدِينَ ﴿٥٣﴾
53. Wakasema: “Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.”

قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٥٤﴾
54. Akasema: “Kwa yakini mlikuwa nyinyi na baba zenu katika upotofu bayana.”


قَالُوا أَجِئْتَنَا بِالْحَقِّ أَمْ أَنتَ مِنَ اللَّاعِبِينَ ﴿٥٥﴾
55. Wakasema: “Je, umetujia kwa haki, au wewe ni miongoni mwa wafanyao mchezo?”


قَالَ بَل رَّبُّكُمْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الَّذِي فَطَرَهُنَّ وَأَنَا عَلَىٰ ذَٰلِكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٦﴾
56. Akasema: “Bali Rabb wenu ni Rabb wa mbingu na ardhi, Ambaye Amezianzisha; nami ni katika wenye kushuhudia hayo. 

وَتَاللَّـهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَامَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا مُدْبِرِينَ ﴿٥٧﴾
57. “Na naapa kwa Allaah, bila shaka nitafanyia hila masanamu yenu baada ya mkishageuka kwenda zenu.” 

فَجَعَلَهُمْ جُذَاذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ ﴿٥٨﴾
58. Basi akayavunja vipande vipande isipokuwa kubwa lao ili wapate kulirejea.


قَالُوا مَن فَعَلَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا إِنَّهُ لَمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٩﴾
59. Wakasema: “Nani amefanya hivi kwa waabudiwa wetu? Hakika yeye ni miongoni mwa madhalimu.”

قَالُوا سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُ إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Wakasema: “Tulimsikia kijana akiwataja anaitwa Ibraahiym.”


قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ ﴿٦١﴾
61. Wakasema: “Mleteni mbele ya macho ya watu ili wapate kushuhudia.”


قَالُوا أَأَنتَ فَعَلْتَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٢﴾
62. Wakasema: “Je, ni wewe uliyefanya hivi kwa waabudiwa wetu, ee Ibraahiym?”


قَالَ بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَـٰذَا فَاسْأَلُوهُمْ إِن كَانُوا يَنطِقُونَ ﴿٦٣﴾
63. Akasema: “Hapana, bali amefanya hayo hili kubwa lao. Hivyo waulizeni wakiwa wanaweza kunena!”


فَرَجَعُوا إِلَىٰ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوا إِنَّكُمْ أَنتُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Basi wakajirudia nafsi zao, wakasema: “Hakika nyinyi ndio madhalimu.”


ثُمَّ نُكِسُوا عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَـٰؤُلَاءِ يَنطِقُونَ ﴿٦٥﴾
65. Kisha wakarudia hali yao ya mwanzo ya upotofu: (Wakasema): “Umekwishajua kwamba hawa hawasemi.”


قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا يَضُرُّكُمْ ﴿٦٦﴾
66. (Ibraahiym) Akasema: “Je, basi mnaabudu badala ya Allaah isiyokunufaisheni  kitu chochote na wala kukudhuruni?”


أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٧﴾
67. “Aibu yenu nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Allaah. Je, hamtii akilini?”


قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ ﴿٦٨﴾
68. Wakasema: “Muunguzeni na mnusuru waabudiwa wenu, mkiwa ni wafanyao (kunusuru).”


قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾
69. Tukasema: “Ee moto! Kuwa baridi, na salama juu ya Ibraahiym.”


وَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَخْسَرِينَ ﴿٧٠﴾
70. Na wakamkusudia njama; lakini Tukawajaalia wao ndio wenye kukhasirika.


وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾
71. Na Tukamuokoa na Luwtw kuelekea ardhi ambayo Tumeibariki humo kwa walimwengu.


وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا صَالِحِينَ ﴿٧٢﴾
72. Na Tukamtunukia Is-haaq na (mjukuu) Ya’quwb kuwa ni ziada. Na wote Tumewajaalia kuwa Swalihina.


وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ ۖ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾
73. Na Tukawajaalia Maimaam wanaongoza kwa amri Yetu, na Tukawatia ilhamu kufanya kheri, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah. Na wakawa wenye kutuabudu.


وَلُوطًا آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَت تَّعْمَلُ الْخَبَائِثَ ۗ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَاسِقِينَ ﴿٧٤﴾
74. Na Luwtw Tulimpa hikma na elimu; na Tukamuokoa kutoka mji ambao ulikuwa unatenda uhabithi. Hakika wao walikuwa watu waovu, mafasiki.


وَأَدْخَلْنَاهُ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٧٥﴾
75. Na Tukamuingiza katika rahmah Yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa Swalihina.


وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾
76. Na Nuwh alipoita hapo zamani; Tukamuitikia na Tukamuokoa na ahli zake kutokana na janga kuu.


وَنَصَرْنَاهُ مِنَ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na Tukamnusuru kutokana na watu ambao walikadhibisha Aayaat (ishara) Zetu. Hakika wao walikuwa watu waovu, basi Tuliwagharikisha wote.


وَدَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ إِذْ يَحْكُمَانِ فِي الْحَرْثِ إِذْ نَفَشَتْ فِيهِ غَنَمُ الْقَوْمِ وَكُنَّا لِحُكْمِهِمْ شَاهِدِينَ ﴿٧٨﴾
78. Na Daawuwd na Sulaymaan walipotoa hukmu juu ya konde, walipotangatanga malishoni usiku kondoo wa watu, Nasi Tukawa katika hukmu yao hiyo Wenye kushuhudia.


فَفَهَّمْنَاهَا سُلَيْمَانَ ۚ وَكُلًّا آتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَسَخَّرْنَا مَعَ دَاوُودَ الْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَالطَّيْرَ ۚ وَكُنَّا فَاعِلِينَ ﴿٧٩﴾
79. Tukamfahamisha Sulaymaan. Na kila mmoja Tulimpa hikma na elimu. Na Tukatiisha majabali yawe pamoja na Daawuwd yakisabbih na ndege. Na Tukawa wenye kufanya (haya).


وَعَلَّمْنَاهُ صَنْعَةَ لَبُوسٍ لَّكُمْ لِتُحْصِنَكُم مِّن بَأْسِكُمْ ۖ فَهَلْ أَنتُمْ شَاكِرُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na Tukamfunza (Daawuwd) uundaji wa mavazi ya kivita ya chuma kwa ajili yenu ili yakuhifadhini kutokana kupigana vita kwenu. Je, basi mtakuwa wenye kushukuru?


وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِي بِأَمْرِهِ إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَيْءٍ عَالِمِينَ﴿٨١﴾
81. Na kwa Sulaymaan, (Tulimtiishia) upepo wa dhoruba unaokwenda kwa amri yake katika ardhi ambayo Tumeibariki humo. Nasi Tulikuwa kwa kila kitu Wenye kukijua.

وَمِنَ الشَّيَاطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَكُنَّا لَهُمْ حَافِظِينَ ﴿٨٢﴾
82. Na (Tukamtiishia) miongoni mwa mashaytwaan wakimpigia mbizi na wakimfanyia kazi nyinginezo zisizokuwa hizo. Nasi Tulikuwa kwao ni Wenye kuwahifadhi. 


وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٨٣﴾
83. Na Ayyuwb alipomwita Rabb wake: “Hakika mimi imenigusa dhara, Nawe Ndiye Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu”.


فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَكَشَفْنَا مَا بِهِ مِن ضُرٍّ ۖ وَآتَيْنَاهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَابِدِينَ ﴿٨٤﴾
84. Tukamuitikia basi Tukamuondoshea dhara aliyokuwa nayo, na Tukampa ahli zake na mfano wao pamoja nao; ni rahmah kutoka Kwetu na ni ukumbusho kwa wanaoabudu (Allaah).


وَإِسْمَاعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا الْكِفْلِ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّابِرِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na Ismaa’iyl na Idriys na Dhal-Kifli, wote ni miongoni mwa wenye kusubiri.


وَأَدْخَلْنَاهُمْ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُم مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٦﴾
86. Na Tukawaingiza katika rahmah Yetu. Hakika wao ni miongoni mwa Swalihina.


وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na Dhan-Nuwn (Yuwnus) alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha; akaita katika kiza kwamba: “Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Subhaanak! Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”


فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾
88. Basi Tukamuitikia na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokowavyo Waumini.

وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ ﴿٨٩﴾
89. Na Zakariyyaa alipomwita Rabb wake: “Rabb wangu! Usiniache pekee; Nawe Ndiye Mbora wa wenye kurithi.”


فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾
90. Basi Tukamuitikia na Tukamtunukia Yahyaa, na Tukamtengenezea mke wake. Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na wakituomba kwa raghba na khofu, na walikuwa wenye kutunyenyekea.


وَالَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلْنَاهَا وَابْنَهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩١﴾
91. Na (Maryam) ambaye aliyelinda sitara yake, Tukampulizia (nguoni mwake) katika Ruwh Yetu na Tukamjaaliya na mwanawe kuwa ni Aayah (ishara, muujiza) kwa walimwengu.


إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ ﴿٩٢﴾
92. Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja; Nami ni Rabb wenu, basi niabuduni.


وَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ ۖ كُلٌّ إِلَيْنَا رَاجِعُونَ ﴿٩٣﴾
93. Wakakatakata na kufarikiana kuhusu Dini yao. Wote Kwetu ni wenye kurejea.


فَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِ وَإِنَّا لَهُ كَاتِبُونَ ﴿٩٤﴾
94. Basi atakayetenda mema naye ni Muumini, haitakanushwa juhudi yake; na hakika Sisi Tunamuandikia.


وَحَرَامٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿٩٥﴾
95. Na haramisho kwa mji Tuliouangamiza ya kwamba wao hawatorejea (duniani).


حَتَّىٰ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ ﴿٩٦﴾
96. Mpaka watakapofunguliwa Yaajuwj na Maajuwj, nao kutoka kila mwinuko watateremka.



وَاقْتَرَبَ الْوَعْدُ الْحَقُّ فَإِذَا هِيَ شَاخِصَةٌ أَبْصَارُ الَّذِينَ كَفَرُوا يَا وَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا بَلْ كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٩٧﴾
97. Na itakaribia ahadi ya haki (ya Qiyaamah). Tahamaki macho ya wale waliokufuru yanakodoka (watasema): “Ole wetu!  Kwa yakini tulikuwa katika mghafala na haya. Bali tulikuwa madhalimu.”


إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ ﴿٩٨﴾
98. Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni vichochezi vya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia.


لَوْ كَانَ هَـٰؤُلَاءِ آلِهَةً مَّا وَرَدُوهَا ۖ وَكُلٌّ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٩٩﴾
99. Lau wangelikuwa hawa ni waabudiwa wanaostahiki kuabudiwa basi wasingeliuingia; lakini wote humo ni wenye kudumu.

لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَهُمْ فِيهَا لَا يَسْمَعُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Kwao humo, ni kupumua kwa mngurumo nao humo hawatosikia lolote.


إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَـٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ ﴿١٠١﴾
101. Hakika wale ambao umewatangulia wema Wetu, hao watabaidishwa nao (moto).


لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِي مَا اشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَالِدُونَ ﴿١٠٢﴾
102. Hawatosikia mvumo wake. Nao watadumu katika ambayo zimetamani  nafsi zao.


لَا يَحْزُنُهُمُ الْفَزَعُ الْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ هَـٰذَا يَوْمُكُمُ الَّذِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Haitowahuzunisha mfazaiko mkubwa kabisa; na Malaika watawapokea (wakiwaambia): “Hii ni ile Siku yenu mliyokuwa mkiahidiwa.”


يَوْمَ نَطْوِي السَّمَاءَ كَطَيِّ السِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَا ۚ إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ﴿١٠٤﴾
104. Siku Tutakapozikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi zilizoandikwa. Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu Yetu. Hakika Sisi ni Wenye kufanya.


وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Na kwa yakini Tuliandika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu ya kwamba: ardhi watairithi waja Wangu wema.

إِنَّ فِي هَـٰذَا لَبَلَاغًا لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ ﴿١٠٦﴾
106. Hakika katika hii (Qur-aan) bila shaka kuna ubalighisho kwa watu wenye kuabudu.


وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾
107. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni rahmah kwa walimwengu.


قُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٨﴾
108. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika nimefunuliwa Wahy kwamba: Muabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja basi je, nyinyi mumesilimu?”


فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ آذَنتُكُمْ عَلَىٰ سَوَاءٍ ۖ وَإِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ ﴿١٠٩﴾
109. Na kama wakikengeuka, basi sema: “Nimekutangazieni sawasawa, na wala sijui ni yako karibu au baidi yale mliyoahidiwa.”


إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ مِنَ الْقَوْلِ وَيَعْلَمُ مَا تَكْتُمُونَ ﴿١١٠﴾
110. “Hakika Yeye Anajua kauli za kutamkwa jahara, na Anajua mnayoyaficha.”


وَإِنْ أَدْرِي لَعَلَّهُ فِتْنَةٌ لَّكُمْ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١١١﴾
111. “Na wala sijui kama hii huenda ikawa ni mtihani kwenu na starehe mpaka muda fulani.”


قَالَ رَبِّ احْكُم بِالْحَقِّ ۗ وَرَبُّنَا الرَّحْمَـٰنُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ ﴿١١٢﴾
112. Sema: “Rabb wangu! Hukumu kwa haki. Na Rabb wetu ni Ar-Rahmaan Aombwaye msaada juu ya yale mnayovumisha.



Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.