-->
logo

019 - Maryam

مَرْيَم
Maryam: 19

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



كهيعص ﴿١﴾
1. Kaaf Haa Yaa ‘Ayyn Swaad



ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا ﴿٢﴾
2. (Huu ni) Ukumbusho wa rahmah ya Rabb wako kwa mja Wake Zakariyyaa.



إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا ﴿٣﴾
3. Alipomwita Rabb wake mwito wa siri.



قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُن بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا ﴿٤﴾
4. Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi mifupa imeninyong’onyea na kichwa kimeng’aa mvi, na wala sikuwa mwenye kunyimwa katika kukuomba du’aa, ee Rabb wangu.



وَإِنِّي خِفْتُ الْمَوَالِيَ مِن وَرَائِي وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا فَهَبْ لِي مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا ﴿٥﴾
5. “Nami nakhofia jamaa zangu nyuma yangu, na mke wangu ni tasa. Basi Nitunukie kutoka kwako mrithi.”



يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ ۖ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا ﴿٦﴾
6. Anirithi na arithi kizazi cha Ya’quwb, na Mjaalie Rabb wangu awe mwenye kuridhisha”.



يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾
7. (Akaambiwa): “Ee Zakariyyaa! Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.”



قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا وَقَدْ بَلَغْتُ مِنَ الْكِبَرِ عِتِيًّا ﴿٨﴾
8. (Zakariyyah) Akasema: “Ee Rabb wangu! Vipi nitapata ghulamu na hali mke wangu ni tasa, na nimeshafikia uzee wa kupindukia mipaka?”



قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِن قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْئًا ﴿٩﴾
9. Akasema: “Ni hivyo hivyo (lakini) Rabb wako Amesema: Haya ni sahali Kwangu; na kwani Nilikwishakukuumba kabla na wala hukuwa chochote.”


قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۚ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَ لَيَالٍ سَوِيًّا ﴿١٠﴾
10. (Zakariyyah) Akasema: “Rabb wangu! Nijaaliye Aayah (ishara).” Akasema: “Aayah yako ni kwamba hutoweza kuwasemesha watu nyusiku tatu ilhali huna kasoro.”


فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ مِنَ الْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَن سَبِّحُوا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ﴿١١﴾
11. Basi akawatokea watu wake kutoka mihrabuni, akawaashiria kwamba “Msabbihini (Allaah) asubuhi na jioni.”


يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا ﴿١٢﴾
12. “Ee Yahyaa!  Chukua Kitabu kwa nguvu.” Na Tukampa hikma angali mtoto.



وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَاةً ۖ وَكَانَ تَقِيًّا ﴿١٣﴾
13. Na mwenye upole na huruma kutoka Kwetu, na mwenye utakaso, na akawa mwenye taqwa. 


وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا ﴿١٤﴾
14. Na mtiifu mno kwa wazazi wake wawili, na wala hakuwa jabari wala asi.



وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا ﴿١٥﴾
15. Na amani iwe juu yake siku aliyozaliwa, na siku atakayokufa na siku atakayofufuliwa kuwa hai.



وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا ﴿١٦﴾
16. Na mtaje katika Kitabu Maryam alipojiondosha kutoka kwa ahali zake, mahali pa Mashariki.



فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا ﴿١٧﴾
17. Akafanya pazia kujitenga nao, Tukampelekea Ruwh Wetu (Jibriyl عليه السلام) akajimithilisha kwake kama binaadamu timamu.


قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَـٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا ﴿١٨﴾
18. (Maryam) Akasema: “Najikinga kwa Ar-Rahmaan dhidi yako ukiwa ni mwenye taqwa.”




قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا ﴿١٩﴾
19. (Jibriyl عليه السلامAkasema: “Hakika mimi ni Mjumbe wa Rabb wako ili nikubashirie tunu ya ghulamu aliyetakasika.”



قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا ﴿٢٠﴾
20. (Maryam) Akasema: “Itakuwaje niwe na ghulamu na hali hakunigusa mtu yeyote, na wala mimi si kahaba?”



قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا ﴿٢١﴾
21. (Jibriyl) Akasema: “Ni hivyo hivyo (lakini) Rabb wako Amesema. Haya ni sahali Kwangu! Na ili Tumfanye awe Aayah (muujiza, ishara) kwa watu na rahmah kutoka Kwetu, na likawa jambo lilokwisha hukumiwa.”


فَحَمَلَتْهُ فَانتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا ﴿٢٢﴾
22. Basi akaibeba mimba, na akaondoka nayo mahali pa mbali.



فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَـٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا ﴿٢٣﴾
23. Uchungu ukampeleka mpaka katika shina la mtende akasema: “Laiti ningelikufa kabla ya haya na nikawa niliyesahaulika kabisa!”



فَنَادَاهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا ﴿٢٤﴾
24. Akanadiwa kutoka chini yake kwamba: “Usihuzunike! Rabb wako Amekwishakufanyia kijito cha maji.”



وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا ﴿٢٥﴾
25. “Na tingisha kwako shina na mtende, litakuangushia tende ziloiva na  zilizotayari kuchumwa.”



فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنسِيًّا ﴿٢٦﴾
26. “Basi kula na kunywa na litue jicho lako. Na utakapokutana na mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri ya swawm kwa Ar-Rahmaan hivyo leo sitomsemesha mtu yeyote.”



فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا ﴿٢٧﴾
27. Akawafikia watu wake akiwa amembeba (mtoto); wakasema: “Ee Maryam! Kwa yakini umeleta jambo la ajabu, kuu na ovu mno. 



يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا ﴿٢٨﴾
28. “Ee dada wa Haaruwn! Hakuwa baba yako mtu muovu, na wala hakuwa mama yako kahaba.”



فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ ۖ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا ﴿٢٩﴾
29. Akamuashiria. Wakasema: “Vipi tuseme na aliye kwenye mlazi akiwa bado ni mtoto mchanga?”



قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا ﴿٣٠﴾
30. (Mtoto) Akasema: “Hakika mimi ni mja wa Allaah; Amenipa Kitabu (Injiyl) na Amenijaalia kuwa Nabiy.”



وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا ﴿٣١﴾
31. “Na Amenijaalia kuwa mwenye kubarikiwa popote nitakapokuweko, na Ameniusia Swalaah na Zakaah madamu niko katika uhai.”


وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا ﴿٣٢﴾
32. “Na niwe mtiifu kwa mama yangu na wala Hakunijaalia kuwa jeuri, muovu.”



وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا ﴿٣٣﴾
33. “Na amani iwe juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa kuwa hai.”



ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ ﴿٣٤﴾
34. Huyo ndiye ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kauli ya haki ambayo wanaitilia shaka.



مَا كَانَ لِلَّـهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٍ ۖ سُبْحَانَهُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٣٥﴾
35. Haiwi kwa Allaah kamwe Ajichukulie mwana yeyote. Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) Anapokidhia jambo basi huliambia: “Kun!” nalo linakuwa!



وَإِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٣٦﴾

36. (Nabiy ‘Iysaa akasema): “Na kwamba hakika Allaah ni Rabb wangu, na Rabb wenu, basi mwabuduni Yeye (Pekee). Hii ndio njia iliyonyooka.”



فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٣٧﴾
37. Lakini makundi yakakhitilafiana baina yao (kuhusu Nabiy ‘Iysaa).  Basi ole wao wale waliokufuru kwa kuhudhuria  Siku adhimu.



أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا ۖ لَـٰكِنِ الظَّالِمُونَ الْيَوْمَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾
38. Watasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayotujia. Lakini madhalimu siku hiyo watakuwa katika upotofu ulio bayana.



وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na waonye Siku ya majuto itakapohukumiwa amri, na hali wao wamo katika mghafala, wala hawaamini.



إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ الْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ ﴿٤٠﴾
40. Hakika Sisi Tutairithi ardhi na waliokuwemo humo, na Kwetu waterejeshwa.



وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِبْرَاهِيمَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٤١﴾
41. Na mtaje katika Kitabu Ibraahiym. Hakika yeye alikuwa mkweli wa dhati, Nabiy.



إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا ﴿٤٢﴾
42. Pindi alipomwambia baba yake: “Ee baba yangu! Kwa nini unaabudu vile visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa kitu chochote?”



يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا ﴿٤٣﴾
43. “Ee baba yangu! Hakika mimi imekwishanijia elimu isiyokufikia wewe; basi nifuate nikuongoze njia iliyonyooka.”



يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا ﴿٤٤﴾
44. “Ee baba yangu! Usimwabudu shaytwaan. Hakika shaytwaan daima ni mwenye kumuasi Ar-Rahmaan.”



يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا ﴿٤٥﴾
45. “Ee baba yangu! Hakika mimi nakhofu isikushike adhabu kutoka kwa Ar-Rahmaan, ukaja kuwa rafiki kwa shaytwaan.”



قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ ۖ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا ﴿٤٦﴾
46. (Baba yake) Akasema: “Unachukia waabudiwa wangu ee Ibraahiym? Usipokoma, bila shaka nitakupiga mawe; na niondokelee mbali kwa muda mrefu!”



قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ ۖ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي ۖ إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا ﴿٤٧﴾
47. (Ibraahiym) Akasema: “Salaamun ‘alayka.” (Amani iwe juu yako). Nitakuombea maghfirah kwa Rabb wangu. Hakika Yeye daima ni  Mwenye kunihurumia sana.”




وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا ﴿٤٨﴾
48. “Na natengana nanyi na mnavyoviomba badala ya Allaah; na namuomba Rabb wangu asaa nisijekuwa mwenye kunyimwa du’aa yangu kwa kumwomba Rabb wangu.”



فَلَمَّا اعْتَزَلَهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا ﴿٤٩﴾
49. Basi alipotengana nao na wanayoyaabudu badala ya Allaah; Tulimtunukia Is-haaq, na (mjukuu) Ya’quwb; na kila mmoja wao Tulimjaalia kuwa Nabiy.




وَوَهَبْنَا لَهُم مِّن رَّحْمَتِنَا وَجَعَلْنَا لَهُمْ لِسَانَ صِدْقٍ عَلِيًّا ﴿٥٠﴾
50. Na Tukawatunukia katika rahmah Zetu, na Tukawajaalia wenye haiba nzuri za kutukuka.




وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مُوسَىٰ ۚ إِنَّهُ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ﴿٥١﴾
51. Na mtaje katika Kitabu Muwsaa. Hakika yeye alikuwa amekhitariwa kwa ikhlasi yake na alikuwa Rasuli na Nabiy.



وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا ﴿٥٢﴾
52. Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.



وَوَهَبْنَا لَهُ مِن رَّحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيًّا ﴿٥٣﴾
53. Na Tukamtunukia katika rahmah Zetu, kaka yake Haaruwn awe Nabiy.



وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ﴿٥٤﴾
54. Na mtaje katika Kitabu Ismaa’iyl. Hakika yeye alikuwa mkweli wa ahadi na alikuwa Rasuli na Nabiy.



وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا ﴿٥٥﴾
55. Na alikuwa akiwaamrisha ahli zake Swalaah na Zakaah, na alikuwa mridhiwa mbele ya Rabb wake.



وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٥٦﴾
56. Na mtaje katika Kitabu Idriys. Hakika yeye alikuwa mkweli wa dhati na Nabiy.




وَرَفَعْنَاهُ مَكَانًا عَلِيًّا﴿٥٧﴾
57. Na Tukamuinua daraja ya juu.




أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَـٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا۩﴿٥٨﴾
58. Hao ndio ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii katika kizazi cha Aadam, na miongoni mwa Tuliowabeba pamoja na Nuwh (katika jahazi), na katika kizazi cha Ibraahiym na Israaiyl na miongoni mwa Tuliowaongoa na Tukawateua. Wanaposomewa Aayaat za Ar-Rahmaan huporomoka kifudifudi wakisujudu na kulia.



فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا ﴿٥٩﴾
59. Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu motoni.



إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا ﴿٦٠﴾
60. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema; basi hao wataingia Jannah na wala hawatadhulumiwa chochote.



جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدَ الرَّحْمَـٰنُ عِبَادَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّهُ كَانَ وَعْدُهُ مَأْتِيًّا ﴿٦١﴾
61. Jannaat za kudumu milele ambazo Ar-Rahmaan Amewaahidi waja Wake kwa ghayb. Hakika ahadi Yake daima bila shaka itafika.



لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا إِلَّا سَلَامًا ۖ وَلَهُمْ رِزْقُهُمْ فِيهَا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ﴿٦٢﴾
62. Hawatosikia humo upuuzi wowote ule isipokuwa salama tu. Na watapata riziki zao humo asubuhi na jioni.



تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيًّا ﴿٦٣﴾
63. Hiyo ni Jannah ambayo Tutawarithisha miongoni mwa waja Wetu waliokuwa na taqwa.



وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا ﴿٦٤﴾
64. Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyoko baina ya hayo. Na Rabb wako si Mwenye kusahau kamwe.



رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾
65. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua yeyote mwenye Jina kama Lake (Allaah)?



وَيَقُولُ الْإِنسَانُ أَإِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا ﴿٦٦﴾
66. Na insani husema: “Je, nitakapokufa hivi nitatolewa kuwa hai?”




أَوَلَا يَذْكُرُ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْئًا ﴿٦٧﴾
67. Je, hakumbuki insani kwamba Tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?



فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا ﴿٦٨﴾
68. Basi Naapa kwa Rabb wako. Bila shaka Tutawakusanya wao na mashaytwaan, kisha Tutawahudhurisha pembezoni mwa Jahannam wapige magoti.




ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَـٰنِ عِتِيًّا ﴿٦٩﴾
69. Kisha bila shaka Tutawachomoa katika kila kundi wale ambao waliomuasi zaidi Ar-Rahmaan.



ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا ﴿٧٠﴾
70. Kisha bila shaka Sisi Tunawajua zaidi wale wanaostahiki zaidi kuunguzwa humo.



وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا ﴿٧١﴾
71. Na hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ni mwenye kuufikia (moto). Hiyo ni hukumu ya Rabb wako; lazima itimizwe.




ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا ﴿٧٢﴾
72. Kisha Tutawaokoa wale waliokuwa na taqwa, na Tutawaacha madhalimu humo wamepiga magoti.



وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَيُّ الْفَرِيقَيْنِ خَيْرٌ مَّقَامًا وَأَحْسَنُ نَدِيًّا﴿٧٣﴾
73. Na wanaposomewa Aayaat Zetu zilizo wazi; wale waliokufuru huwaambia walioamini: “Kundi lipi kati ya mawili haya lenye cheo bora zaidi na majilisi mazuri zaidi?”



وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَحْسَنُ أَثَاثًا وَرِئْيًا ﴿٧٤﴾
74. Na karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao; wao walikuwa na mapambo mazuri zaidi kwa mandhari? 




قُلْ مَن كَانَ فِي الضَّلَالَةِ فَلْيَمْدُدْ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ مَدًّا ۚ حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ إِمَّا الْعَذَابَ وَإِمَّا السَّاعَةَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضْعَفُ جُندًا ﴿٧٥﴾
75. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Aliyekuwa katika upotofu, basi Ar-Rahmaan Atawapanulia muda. Hata watakapoona waliyotishiwa ima adhabu au ima Saa; basi watakuja kujua ni nani aliye mahali paovu zaidi na mwenye askari dhaifu.”



وَيَزِيدُ اللَّـهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى ۗ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَّرَدًّا ﴿٧٦﴾
76. Na Allaah Atawazidishia hidaaya wale wenye kushika uongofu. Na mema yanayobakia ni bora zaidi mbele ya Rabb wako kwa thawabu na matokeo bora zaidi ya mwisho.



أَفَرَأَيْتَ الَّذِي كَفَرَ بِآيَاتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالًا وَوَلَدًا ﴿٧٧﴾
77. Je, umemuona yule aliyezikufuru Aayaat Zetu na akasema: “Bila shaka nitapewa (Aakhirah) mali na watoto?”



أَطَّلَعَ الْغَيْبَ أَمِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَـٰنِ عَهْدًا ﴿٧٨﴾
78. Je, kwani ameyajua ya ghayb, au amechukua ahadi kwa Ar-Rahmaan?



كَلَّا ۚ سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُ مِنَ الْعَذَابِ مَدًّا ﴿٧٩﴾
79. Laa, hashaTutayaandika yale anayoyasema, na Tutampanulia muda wa adhabu ya kurefuka.



وَنَرِثُهُ مَا يَقُولُ وَيَأْتِينَا فَرْدًا ﴿٨٠﴾
80. Na Tutamrithi yale anayoyasema, na atatujia peke yake!



وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لِّيَكُونُوا لَهُمْ عِزًّا ﴿٨١﴾
81. Na wakachukua badala ya Allaah waabudiwa ili eti iwape taadhima na nguvu.




كَلَّا ۚ سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا ﴿٨٢﴾
82. Laa, hashaWatakanusha ‘ibaadah zao, na watakuwa wapinzani wao.



أَلَمْ تَرَ أَنَّا أَرْسَلْنَا الشَّيَاطِينَ عَلَى الْكَافِرِينَ تَؤُزُّهُمْ أَزًّا ﴿٨٣﴾
83. Je, huoni kwamba Sisi Tunapeleka mashaytwaan kwa makafiri ili wawachochee (uovu) kwa uchochezi?



فَلَا تَعْجَلْ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمْ عَدًّا ﴿٨٤﴾
84. Basi usiwafanyie haraka. Hakika Sisi Tunawahesabia idadi za (siku) zao.



يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَـٰنِ وَفْدًا ﴿٨٥﴾
85. Siku Tutakayowakusanya wenye taqwa kwa Ar-Rahmaan kuwa wakiwa kama ni wakilishi wa heshima.



وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا ﴿٨٦﴾
86. Na Tutawaendesha wahalifu kuelekea Jahannam wakiwa na kiu.




لَّا يَمْلِكُونَ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَـٰنِ عَهْدًا ﴿٨٧﴾
87. Hawatakuwa na mamlaka ya shufaa isipokuwa yule aliyechukua ahadi kwa Ar-Rahmaan.



وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ﴿٨٨﴾
88. Na wamesema: “Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana.”




لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا ﴿٨٩﴾
89. Kwa yakini mmeleta jambo kuu ovu na la kuchukiza mno!



تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾
90. Zinakaribia mbingu zipasuke kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka.



أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا ﴿٩١﴾
91. Kwa kule kudai kuwa Ar-Rahmaan Ana mwana.



وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَـٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا ﴿٩٢﴾
92. Na wala haipasi kwa Ar-Rahmaan kujifanyia mwana.



إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا ﴿٩٣﴾
93. Hakuna yeyote yule aliyeko katika mbingu na ardhi isipokuwa atamfikia Ar-Rahmaan kuwa ni mja.



لَّقَدْ أَحْصَاهُمْ وَعَدَّهُمْ عَدًّا ﴿٩٤﴾
94. Kwa hakika Amewakadiria hesabuni barabara Akawahesabu hesabu ya sawasawa.




وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْدًا ﴿٩٥﴾
95. Na kila mmoja wao atamfikia (Allaah) Siku ya Qiyaamah akiwa peke yake.



إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَـٰنُ وُدًّا ﴿٩٦﴾
96. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Ar-Rahmaan Atawajaalia kwao mapenzi.




فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ الْمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ بِهِ قَوْمًا لُّدًّا ﴿٩٧﴾
97. Basi hakika Tumeiwepesisha (Qur-aan) kwa lisani yako ili uwabashirie kwayo wenye taqwa, na uwaonye kwayo watu makhasimu.




وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هَلْ تُحِسُّ مِنْهُم مِّنْ أَحَدٍ أَوْ تَسْمَعُ لَهُمْ رِكْزًا ﴿٩٨﴾
98. Na karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao; je, unamhisi hata mmoja katika wao, au unasikia mchakato wowote wao?


Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.