-->
logo

011 - Huwd

 هُود
Huwd: 12

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Kitabu ambacho Aayaat Zake zimetimizwa barabara, kisha zikafasiliwa waziwazi kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.



أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ﴿٢﴾
2.  Kwamba: “Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلمni mwonyaji kwenu na mbashiriaji.”


وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ وَإِن تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ﴿٣﴾
3. Na kwamba: “Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake, Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu uliokadiriwa; na Atampa kila mwenye fadhila, fadhila Zake. Na mkikengeuka, basi hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa.”



إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٤﴾
4. Kwa Allaah ni marejeo yenu. Naye juu ya kila kitu ni Muweza.



أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا مِنْهُ ۚ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٥﴾
5. Tanabahi! Hakika wao wanageuza vifua vyao ili wamfiche (Allaah). Tanabahi! Wanapojigubika nguo zao, Anajua wanayoyafanya siri na wanayoyatangaza. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.



وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦﴾
6. Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah; na (Allaah) Anajua mahali pake pa kustakiri na pa kuhifadhiwa kwake. Yote yamo katika Kitabu kinachobainisha.[1]



وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۗ وَلَئِن قُلْتَ إِنَّكُم مَّبْعُوثُونَ مِن بَعْدِ الْمَوْتِ لَيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧﴾
7. Na Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita; na ikawa ‘Arshi Yake juu ya maji; (kakuumbeni) ili Akujaribuni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. Na kama ukisema: “Nyinyi mtafufuliwa baada ya mauti”; wale waliokufuru bila shaka watasema: “Hakika haya si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.”



وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِلَىٰ أُمَّةٍ مَّعْدُودَةٍ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحْبِسُهُ ۗ أَلَا يَوْمَ يَأْتِيهِمْ لَيْسَ مَصْرُوفًا عَنْهُمْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٨﴾
8. Na kama Tukiwaakhirishia adhabu mpaka muda uliokwishahesabiwa; bila shaka watasema: “Ni nini kinachoizuia? Tanabahi! Siku itakayowafikia haitaondoshwa kwao, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.



وَلَئِنْ أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَاهَا مِنْهُ إِنَّهُ لَيَئُوسٌ كَفُورٌ﴿٩﴾
9. Na Tunapomuonjesha insani rahmah kutoka Kwetu, kisha Tukamuondolea; hakika yeye huwa ni mwenye kukata tamaa sana asiye na shukurani.



وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ نَعْمَاءَ بَعْدَ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ السَّيِّئَاتُ عَنِّي ۚ إِنَّهُ لَفَرِحٌ فَخُورٌ﴿١٠﴾
10. Na Tunapomuonjesha neema baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: “Maovu yemeniondokea.” Hakika yeye ni mwenye kufurahi sana kwa kujigamba na kujifaharisha.


إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ﴿١١﴾
11. Isipokuwa wale waliosubiri na wakatenda mema hao watapata maghfirah na ujira mkubwa.



فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَضَائِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَن يَقُولُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَاءَ مَعَهُ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَا أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴿١٢﴾
12. Basi labda utaacha baadhi ya yale ulofunuliwa Wahy na kifua chako kitaona dhiki kwa hayo kwa sababu wanasema: “Mbona hakuteremshiwa hazina au hakuja pamoja naye Malaika?” Hakika wewe ni mwonyaji tu, na Allaah juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.



أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٣﴾
13. Je, wanasema” “Ameitunga (hii Qur-aan)?” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasina Allaah mkiwa ni wakweli.”



فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا أُنزِلَ بِعِلْمِ اللَّـهِ وَأَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ﴿١٤﴾
14. Wasipokujibuni, basi jueni kwamba hakika (hii Qur-aan) imeteremshwa kwa ujuzi wa Allaah, na kwamba hapana muabudiwa wa haki ila Yeye; basi je, nyinyi hamtokuwa Waislamu?



مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ﴿١٥﴾
15. Anayetaka uhai wa dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu ‘amali zao humo, nao hawatopunjwa humo. 



أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٦﴾
16. Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa moto. Na yataporomoka yale waliyoyafanya humo (duniani), na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.



أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِّنْهُ وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴿١٧﴾
17. Je, basi yule aliyekuwa na hoja bayana kutoka kwa Rabb wake, na anaifuata shahidi (Jibriyl) kutoka Kwake na kabla yake (kilikuwa) Kitabu cha Muwsaa kilichokuwa kiongozi na rahmah. Hao ndio wanaoiamini (Qur-aan). Na atakayeikanusha kati ya makundi, basi moto ndio mahali pa miadi yake. Basi usiwe katika shaka nacho. Hakika hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wako, lakini watu wengi hawaamini.   



وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ۚ أُولَـٰئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ﴿١٨﴾
18. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia uongo Allaah. Hao watahudhurishwa mbele ya Rabbwao, na mashahidi watasema: “Hawa ndio wale waliomzulia uongo Rabb wao!” Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu.


الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿١٩﴾
19. Wale wanaozuia njia ya Allaah na wanaitafutia ionekane kombo na wao ni wenye kuikanusha Aakhirah.



أُولَـٰئِكَ لَمْ يَكُونُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ۘ يُضَاعَفُ لَهُمُ الْعَذَابُ ۚ مَا كَانُوا يَسْتَطِيعُونَ السَّمْعَ وَمَا كَانُوا يُبْصِرُونَ﴿٢٠﴾
20. Hao hawawezi kushinda kukwepa (adhabu ya Allaah) katika ardhi na hawana walinzi badala ya Allaah. Watazidishiwa adhabu. Hawakuwa wakiweza kusikia na hawakuwa wakiona (haki).



أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٢١﴾
21. Hao ndio wale waliokhasirika nafsi zao, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.



لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ﴿٢٢﴾
22. Hapana shaka kwamba wao huko Aakhira ni wenye kukhasirika zaidi. 



إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَخْبَتُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٣﴾
23. Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakanyenyekea kwa Rabb wao, hao ndio watu wa Jannah, wao humo ni wenye kudumu.



مَثَلُ الْفَرِيقَيْنِ كَالْأَعْمَىٰ وَالْأَصَمِّ وَالْبَصِيرِ وَالسَّمِيعِ ۚ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٢٤﴾
24. Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu na kiziwi na mwenye kuona na kusikia. Je, wanalingana sawa kwa kufananishwa? Basi je, hamkumbuki?



وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢٥﴾
25. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh kwa kaumu yake (akawaambia): “Hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana.”



أَن لَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۖ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ أَلِيمٍ﴿٢٦﴾
26. “Ya kwamba msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku inayoumiza.”



فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا نَرَاكَ إِلَّا بَشَرًا مِّثْلَنَا وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَاذِبِينَ﴿٢٧﴾
27. Wakasema wakuu wa wale waliokufuru katika kaumu yake: “Hatukuoni isipokuwa ni mtu kama sisi, na hatukuoni wanaokufuata isipokuwa wale ambao ni duni wetu, wasiopevuka kifikra; na hatukuoneni kuwa mna fadhila yoyote juu yetu, bali tunakudhanieni ni waongo.”



قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي رَحْمَةً مِّنْ عِندِهِ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمْ لَهَا كَارِهُونَ﴿٢٨﴾
28. (Nuwh) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabbwangu, na Amenipa rahmah (ya Unabiy na risala) kutoka Kwake kisha ikakufichikieni, je, tukulazimisheni kuikubali (Tawhiyd ya Allaah) na hali nyinyi mnaichukia?”



وَيَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۚ وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ إِنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَلَـٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ﴿٢٩﴾
29. “Na enyi kaumu yangu! Sikuombeni mali juu ya (risala) hii. Sina ujira isipokuwa kwa Allaah. Nami sitowafukuza wale walioamini. Hakika wao ni wenye kukutana na Rabb wao, lakini nakuoneni ni watu majahili.”



وَيَا قَوْمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِن طَرَدتُّهُمْ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣٠﴾
30. “Na enyi kaumu yangu! Nani atakayeninusuru kutokana na Allaah nikiwafukuza? Je, hamkumbuki?”



وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ إِنِّي مَلَكٌ وَلَا أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِي أَعْيُنُكُمْ لَن يُؤْتِيَهُمُ اللَّـهُ خَيْرًا ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا فِي أَنفُسِهِمْ ۖ إِنِّي إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ﴿٣١﴾
31. “Na wala sikuambieni kwamba mimi nina hazina za Allaah, na wala sijui ya ghayb; na wala sikuambieni kwamba mimi ni Malaika, na wala siwaambii wale ambao yamewadharau macho yenu kwamba Allaah hatowapa kheri. Allaah Anajua zaidi yaliyomo katika nafsi zao. Hakika mimi hapo (nikifanya), bila shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu.”



قَالُوا يَا نُوحُ قَدْ جَادَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَالَنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٣٢﴾
32. Wakasema: “Ee Nuwh, kwa yakini umejadiliana nasi na umekithirisha majadiliano nasi, basi tuletee hiyo (adhabu) unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa wakweli.”



قَالَ إِنَّمَا يَأْتِيكُم بِهِ اللَّـهُ إِن شَاءَ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ﴿٣٣﴾
33. (Nuwh) Akasema: “Hakika hayo Atakuleteeni Allaah Akitaka, nanyi si wenye kuweza kukwepa.”



وَلَا يَنفَعُكُمْ نُصْحِي إِنْ أَرَدتُّ أَنْ أَنصَحَ لَكُمْ إِن كَانَ اللَّـهُ يُرِيدُ أَن يُغْوِيَكُمْ ۚ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٣٤﴾
34. “Na wala haitokufaeni nasaha yangu nikitaka kukunasihini ikiwa Allaah Anataka kukuacheni kupotea. Yeye ndio Rabb wenu, na Kwake mtarejeshwa.”



أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَعَلَيَّ إِجْرَامِي وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تُجْرِمُونَ﴿٣٥﴾
35. Je, wanasema ameitunga (Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ikiwa nimeitunga, basi ni juu yangu uhalifu wangu, nami sina jukumu na uhalifu mnaoufanya.”



وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ آمَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ﴿٣٦﴾
36.  Na Nuwh akafunuliwa Wahy kwamba: “Hatoamini katika watu wako isipokuwa wale waliokwishaamini. Basi usisononeke kwa yale wanayoyafanya.”



وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚإِنَّهُم مُّغْرَقُونَ﴿٣٧﴾
37. “Na unda jahazi mbele ya macho Yetu na ufunuzi wa Wahy Wetu, na wala usinisemeze kuhusu wale waliodhulumu; hakika wao ni wenye kuzamishwa.”


وَيَصْنَعُ الْفُلْكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ مَلَأٌ مِّن قَوْمِهِ سَخِرُوا مِنْهُ ۚ قَالَ إِن تَسْخَرُوا مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ﴿٣٨﴾
38. (Nuwh) Akawa anaunda jahazi; basi kila walipompitia wakuu katika kaumu yake walimfanyia dhihaka. Akasema: “Ikiwa mnatufanyia dhihaka, basi nasi tunakufanyieni dhihaka kama mnavyotufanyia dhihaka.”



فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٣٩﴾
39. “Mtakuja kujua nani itakayemfikia adhabu itakayomhizi, na itakayemwangukia adhabu ya kudumu”.



حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ وَمَنْ آمَنَ ۚ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٤٠﴾
40. Mpaka ilipokuja amri Yetu na tanuri likafoka, Tukasema: “Beba humo (jahazini) wawili wawili kutoka kila aina; jike na dume na ahli zako; isipokuwa yule ambaye imemtangulia kauli ya hukmu, na walioamaini. Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache.”



وَقَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللَّـهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا ۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٤١﴾
41. Na (Nuwh) akasema: “Pandeni humo! ‘BismiLLaah’ kwenda kwake na kutia nanga kwake. Hakika Rabb wangu bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.”



وَهِيَ تَجْرِي بِهِمْ فِي مَوْجٍ كَالْجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ابْنَهُ وَكَانَ فِي مَعْزِلٍ يَا بُنَيَّ ارْكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ الْكَافِرِينَ﴿٤٢﴾
42. Basi hilo (jahazi) likawa linakwenda nao katika mawimbi kama majabali. Na Nuwh akamwita mwanawe naye alikuwa kandoni: “Ee mwanangu! Panda pamoja nasi, na wala usiwe pamoja na makafiri.”



قَالَ سَآوِي إِلَىٰ جَبَلٍ يَعْصِمُنِي مِنَ الْمَاءِ ۚ قَالَ لَا عَاصِمَ الْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ إِلَّا مَن رَّحِمَ ۚوَحَالَ بَيْنَهُمَا الْمَوْجُ فَكَانَ مِنَ الْمُغْرَقِينَ﴿٤٣﴾
43. Akasema: “Nitakimbilia jabali litanilinda na maji.” (Nuwh) Akasema: “Hapana wa kulindwa leo na amri ya Allaah isipokuwa Aliyemrehemu.” Tahamaki! Mawimbi yakaingia kati baina yao, akawa miongoni mwa waliogharikishwa.”



وَقِيلَ يَا أَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ وَيَا سَمَاءُ أَقْلِعِي وَغِيضَ الْمَاءُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَاسْتَوَتْ عَلَى الْجُودِيِّ ۖ وَقِيلَ بُعْدًا لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿٤٤﴾
44. Na pakasemwa: “Ee ardhi! Meza maji yako na ee mbingu, zuia (mvua),” na maji yakadidimia; na hukmu ikatimizwa, na (jahazi) likatua juu ya (mlima wa) Al-Juwdiyy.  Na pakasemwa: “Wametokomelea mbali watu madhalimu.”



وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ﴿٤٥﴾
45. Na Nuwh akamwita Rabb wake, akasema: “Rabb wangu! Hakika mwanangu ni katika ahli zangu, na hakika ahadi Yako ni ya kweli, Nawe ni Mwadilifu zaidi wa wanaohukumu kuliko mahakimu wote.”



قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ ۖ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ ۖ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۖ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ﴿٤٦﴾
46. Akasema: “Ee Nuwh! Hakika huyo si miongoni mwa ahli zako. Hakika yeye ni (mwenye) ‘amali zisizokuwa njema. Basi usiniombe yale usiyokuwa na elimu nayo. Hakika Mimi nakuwaidhi usijekuwa miongoni mwa majahili.”



قَالَ رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ ۖ وَإِلَّا تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَالْخَاسِرِينَ﴿٤٧﴾
47. Akasema: “Ee Rabb wangu! Hakika mimi najikinga Kwako kukuomba yale nisiyo na elimu nayo. Na Usiponighufuria na Ukanirehemu, nitakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”



قِيلَ يَا نُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِّنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ أُمَمٍ مِّمَّن مَّعَكَ ۚ وَأُمَمٌ سَنُمَتِّعُهُمْ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤٨﴾
48.  Pakasemwa: “Ee Nuwh!  Teremka (jahazini) kwa salama kutoka Kwetu na baraka nyingi juu yako, na juu za umati zilio pamoja na wewe. Na umati Tutakazozistarehesha, kisha itawagusa kutoka Kwetu adhabu iumizayo.”



تِلْكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهَا إِلَيْكَ ۖ مَا كُنتَ تَعْلَمُهَا أَنتَ وَلَا قَوْمُكَ مِن قَبْلِ هَـٰذَا ۖ فَاصْبِرْ ۖ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٤٩﴾
49. Hizo ni katika habari za ghayb Tunazokufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hukuwa unazijua wewe na wala watu wako kabla ya hii (Qur-aan). Basi subiri, hakika hatima (nzuri) ni kwa wenye taqwa.



وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُفْتَرُونَ﴿٥٠﴾
50. Na kwa kina ‘Aad (Tulimpeleka) ndugu yao Huwd. Akasema: “Ee kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna muabudiwa wa haki ghairi Yake. Nyinyi si chochote isipokuwa watungao uongo.”




يَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى الَّذِي فَطَرَنِي ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿٥١﴾
51. “Enyi kaumu yangu! Sikuombeni ujira juu ya hii (risala). Haukuwa ujira wangu isipokuwa kwa Yule Aliyeniumba. Je, basi hamtii akilini?”



وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا مُجْرِمِينَ﴿٥٢﴾
52. “Na enyi kaumu yangu!  Mwombeni maghfirah Rabb wenu, kisha tubieni Kwake, Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua tele ya kumiminika na Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu, na wala msikengeuke mkawa wahalifu.”




قَالُوا يَا هُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِي آلِهَتِنَا عَن قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ﴿٥٣﴾
53. Wakasema: “Ee Huwd!  Hukutuletea hoja bayana, nasi hatutoacha kamwe waabudiwa wetu kutokana na kauli yako, nasi hatutokuwa wenye kukuamini.”



إِن نَّقُولُ إِلَّا اعْتَرَاكَ بَعْضُ آلِهَتِنَا بِسُوءٍ ۗ قَالَ إِنِّي أُشْهِدُ اللَّـهَ وَاشْهَدُوا أَنِّي بَرِيءٌ مِّمَّاتُشْرِكُونَ﴿٥٤﴾
54. “Hatusemi ila kuwa baadhi ya waabudiwa wetu wamekusibu kwa uovu.” (Huwd) Akasema: “Hakika mimi namshuhudisha Allaah, na shuhudieni kwamba mimi niko mbali na ambavyo mnashirikisha.”



مِن دُونِهِ ۖ فَكِيدُونِي جَمِيعًا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ﴿٥٥﴾
55. “Pamoja Naye (Allaah). Basi nifanyieni njama nyote kisha msinipe muhula.”



إِنِّي تَوَكَّلْتُ عَلَى اللَّـهِ رَبِّي وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَابَّةٍ إِلَّا هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍمُّسْتَقِيمٍ﴿٥٦﴾
56. “Hakika mimi nimetawakali kwa Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakuna kiumbe chochote kitembeacho isipokuwa Yeye (Allaah) Anamkamata kwa kipaji chake. Hakika Rabb wangu Yuko juu ya njia iliyonyooka.”



فَإِن تَوَلَّوْا فَقَدْ أَبْلَغْتُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَيْكُمْ ۚ وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّي قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُ شَيْئًا ۚإِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ﴿٥٧﴾
57. “Mkikengeuka basi nimekwishakubalighishieni (risala) niliyotumwa nayo kwenu. Na Rabb wangu Atarithisha watu wengineo wasiokuwa nyinyi, na wala hamtaweza kumdhuru chochote. Hakika Rabb wangu juu ya kila kitu ni Mwenye kuhifadhi.”



وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا هُودًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَنَجَّيْنَاهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ﴿٥٨﴾
58. Na ilipokuja amri Yetu Tulimuokoa Huwd na wale walioamini pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu, na Tukawaokoa kutokana na adhabu ngumu.



وَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا رُسُلَهُ وَاتَّبَعُوا أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ﴿٥٩﴾
59. Na hao ni kina ‘Aad. Wamezikanusha kwa ushupavu Aayaat (ishara, hoja) za Rabb wao, na wakawaasi Rusuli Wake, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.



وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ عَادًا كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّعَادٍ قَوْمِ هُودٍ﴿٦٠﴾
60. Na wakafuatishwa na laana katika dunia hii, na Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Hakika kina ‘Aad walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina ‘Aad; kaumu ya Huwd.



وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ﴿٦١﴾
61. Na kwa Thamuwd (Tulimpeleka) ndugu yao Swaalih. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna muabudiwa wa haki ghairi Yake. Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni katika ardhi, na Akakufanyieni makazi humo; basi mwombeni maghfirah, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Yuko Karibu kwa ujuzi Wake, Mwenye kuitikia.”



قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ﴿٦٢﴾
62. Wakasema: “Ee Swaalih! Kwa yakini ulikuwa kwetu mwenye kutarajiwa (kheri) kabla ya haya. Je, unatukataza kuabudu wale wanaowaabudu baba zetu; na hakika sisi tumo katika shaka na wasiwasi katika unayotuitia.”



قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ﴿٦٣﴾
63. (Swaalih) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, na Amenipa rahmah (Unabiy na risala) kutoka Kwake basi nani atakayeninusuru nikimuasi? Basi hamnizidishii ila khasara.”



وَيَا قَوْمِ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ﴿٦٤﴾
64. “Enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia jike wa Allaah, ni Aayah (miujiza, ishara) kwenu, basi mwacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu ikakupateni adhabu iliyo karibu.”



فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ﴿٦٥﴾
65. Basi wakamuua; (Swaalih) akasema: “Stareheni majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo.



فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿٦٦﴾
66. Basi ilipokuja amri Yetu, Tulimuokoa Swaalih na wale walioamini pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu, na kutokana na hizaya ya Siku hiyo. Hakika Rabb wako Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.


وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾
67. Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).



كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ﴿٦٨﴾
68. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Rabbwao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd.



وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَاءَ بِعِجْلٍحَنِيذٍ﴿٦٩﴾
69. Na kwa yakini walimjia Ibraahiym Wajumbe Wetu kwa bishara, wakasema: “Salaam!”.   (Naye) Akasema: “Salaam”.  Basi hakubakia ila alikuja na ndama aliyebanikwa.



فَلَمَّا رَأَىٰ أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۚ قَالُوا لَا تَخَفْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمِ لُوطٍ﴿٧٠﴾
70. Alipoona mikono yao haifikii (chakula) aliwashangaa na ikamuingia khofu kutokana nao. Wakasema: “Usiogope! Hakika Sisi Tumetumwa kwa kaumu Luwtw.”



وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ﴿٧١﴾
71. Na mkewe amesimama wima, akacheka; Tukambashiria Is-haaq na baada ya Is-haaq ni Ya’quwb.



قَالَتْ يَا وَيْلَتَىٰ أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَـٰذَا بَعْلِي شَيْخًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ﴿٧٢﴾
72.  Akasema: “Ole wangu! Je, nitazaa na hali mimi ni mkongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu!”



قَالُوا أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ ۖ رَحْمَتُ اللَّـهِ وَبَرَكَاتُهُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ ۚ إِنَّهُ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ﴿٧٣﴾
73. (Malaika) Wakasema: “Je, unastaajabia amri ya Allaah? Rahmah ya Allaah na baraka Zake ziko juu yenu enyi Ahlal-Bayt. Hakika Yeye ni Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote, Mwenye utukufu kamili na enzi.”


فَلَمَّا ذَهَبَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ الرَّوْعُ وَجَاءَتْهُ الْبُشْرَىٰ يُجَادِلُنَا فِي قَوْمِ لُوطٍ﴿٧٤﴾
74. Basi kiwewe cha tisho la moyo kilipomuondoka Ibraahiym, na ikamjia bishara; (akaanza) kujadiliana Nasi kuhusu kaumu Luwtw.



إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّاهٌ مُّنِيبٌ﴿٧٥﴾
75. Hakika Ibraahiym bila shaka ni mvumilivu mwenye kurejea kutubia kila mara.  



يَا إِبْرَاهِيمُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۖ إِنَّهُ قَدْ جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَإِنَّهُمْ آتِيهِمْ عَذَابٌ غَيْرُ مَرْدُودٍ﴿٧٦﴾
76. (Malaika wakamwambia): “Ee Ibraahiym! Achilia mbali haya! Hakika imekwishakuja amri ya Rabb wako na kwamba wao itawafikia adhabu isiyorudishwa.”



وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ﴿٧٧﴾
77. Na Wajumbe Wetu walipomjia Luwtw alisononeka kwa ajili yao na akadhikika na kushindwa (la kufanya); akasema: “Hii ni siku ngumu.”



وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ﴿٧٨﴾
78. Wakamjia kaumu yake wakimkimbilia na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Luwtw) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Hawa ni mabinti zangu, wao wametwaharika kwenu (kuwaoa kihalali) Basi mcheni Allaah, na wala msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Je, hakuna miongoni mwenu mtu muongofu?”



قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ﴿٧٩﴾
79. Wakasema: “Kwa yakini umekwishajua kwamba hatuna haki katika mabinti zako, na kwamba bila shaka wewe unajua tunalolitaka.”



قَالَ لَوْ أَنَّ لِي بِكُمْ قُوَّةً أَوْ آوِي إِلَىٰ رُكْنٍ شَدِيدٍ﴿٨٠﴾
80. (Luwtw) Akasema: “Lau ningelikuwa nina nguvu dhidi yenu, au nikimbilie katika nguzo madhubuti.”



قَالُوا يَا لُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوا إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا امْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُ مُصِيبُهَا مَا أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ الصُّبْحُ ۚ أَلَيْسَ الصُّبْحُ بِقَرِيبٍ﴿٨١﴾
81. (Malaika) Wakasema: “Ee Luwtw! Hakika sisi ni Wajumbe wa Rabb wako; hawatoweza kukufikia. Basi toka usiku na ahli zako katika nyakati ya usiku, na wala asitazame nyuma yeyote miongoni mwenu, isipokuwa mke wako (atabaki nyuma); kwani yeye itamsibu yatakayowasibu wao; hakika miadi yao ni asubuhi. Je, kwani asubuhi haiko karibu?”



فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ﴿٨٢﴾
82. Basi ilipokuja amri Yetu, Tuliupindua (mji wao) juu chini, na Tukaunyeshea mvua ya mawe ya udongo uliookwa yaliyo na tabaka na kuandamana.



مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ ۖ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ﴿٨٣﴾
83. Yametiwa alama kutoka kwa Rabb wako. Na adhabu hiyo haiko mbali na madhalimu.



وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ وَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ﴿٨٤﴾
84. Na kwa Madyan (Tulimpeleka) ndugu yao Shu’ayb. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna muabudiwa wa haki ghairi Yake. Na wala msipunguze kipimo na mizani; hakika mimi nakuoneni mko katika kheri (na neema), na hakika mimi nakukhofieni adhabu siku yenye kuzunguka.”



وَيَا قَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ﴿٨٥﴾
85. “Na Enyi kaumu yangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu, na wala msipunje watu vitu vyao, na wala msifanye uovu katika ardhi mkawa mafisadi.”



بَقِيَّتُ اللَّـهِ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ﴿٨٦﴾
86. “Mabakisho ya Allaah ni bora kwenu, mkiwa ni wenye kuamini. Nami si mwenye kuwahifadhi.”



قَالُوا يَا شُعَيْبُ أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا أَوْ أَن نَّفْعَلَ فِي أَمْوَالِنَا مَا نَشَاءُ ۖ إِنَّكَ لَأَنتَ الْحَلِيمُ الرَّشِيدُ﴿٨٧﴾
87. Wakasema: “Ee Shu’ayb! Je, Swalaah zako zinakuamrisha kuwa sisi tuache wale wanaowaabudu baba zetu, au tuache kufanya tunavyotaka katika mali zetu? Hakika wewe bila shaka ni mvumilivu, uliyeongoka.”  



قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ عَلَيْهِتَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ﴿٨٨﴾
88. (Shu’ayb) Akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu na Ameniruzuku humo riziki nzuri. Nami sitaki kukukhalifuni kufanya ninayokukatazeni. Sitaki lolote ila kutengeneza niwezavyo. Na sipati tawfiyq ila kwa Allaah. Kwake natawakali na Kwake narejea kutubu.”



وَيَا قَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِي أَن يُصِيبَكُم مِّثْلُ مَا أَصَابَ قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَالِحٍ ۚوَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِّنكُم بِبَعِيدٍ﴿٨٩﴾
89. “Enyi kaumu yangu! Kupingana nami kwa uhasama kusikuchocheeni kabisa yakakusibuni yale yaliyowasibu kaumu ya Nuwh au kaumu ya Huwd, au watu ya Swaalih. Na kaumu ya Luwtw hawako mbali nanyi.”



وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ﴿٩٠﴾
90. “Na ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Mwenye kurehemu, Mwenye upendo khalisi.”



قَالُوا يَا شُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَاكَ فِينَا ضَعِيفًا ۖ وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَاكَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْنَا بِعَزِيزٍ﴿٩١﴾
91. Wakasema: “Ee Shu’ayb! Hatufahamu mengi unayoyasema, na hakika sisi tunakuona ni dhaifu kati yetu. Na lau si jamaa zako tungelikupiga mawe. Nawe si azizi kwetu.”



قَالَ يَا قَوْمِ أَرَهْطِي أَعَزُّ عَلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَاتَّخَذْتُمُوهُ وَرَاءَكُمْ ظِهْرِيًّا ۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعْمَلُونَمُحِيطٌ﴿٩٢﴾
92. (Shu’ayb) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Je, jamaa zangu wana utukufu zaidi kwenu kuliko Allaah, na mmemuweka Yeye (Allaah) nyuma ya migongo yenu? Hakika Rabb wangu ni Mwenye kuyazunguka yale myatendayo.”



وَيَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ سَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَاذِبٌ ۖ وَارْتَقِبُوا إِنِّي مَعَكُمْ رَقِيبٌ﴿٩٣﴾
93. “Na enyi kaumu yangu! Tendeni kwa tamkini zenu, hakika mimi mtendaji.  Mtakuja kujua nani itamfika adhabu itakayomhizi, na ni nani aliye muongo. Na ngojeeni mchunge. Hakika mimi niko pamoja nanyi nikingojea na kuchunga.”



وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَأَخَذَتِ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٩٤﴾
94. Na ilipokuja amri Yetu; Tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa rahmah kutoka Kwetu. Na ukawachukuwa wale waliodhulumu ukelele angamizi wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).



كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا بُعْدًا لِّمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ﴿٩٥﴾
95. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi!  Watokomee mbali (watu wa) Madyan kama walivyotokomea Thamuwd.



وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿٩٦﴾
96. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa kwa Aayaat (miujiza, ishara) Zetu na dalili bayana.



إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ﴿٩٧﴾
97. Kwa Fir’awn na wakuu wake, lakini walifuata amri ya Fir’awn. Na amri ya Fira’wn haikuwa yenye uongofu.



يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ﴿٩٨﴾
98. (Fira’wn) Atawatangulia watu wake Siku ya Qiyaamah, na atawafikisha motoni. Na ubaya ulioje mahali pa maingio watakapoingizwa.

  

وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ﴿٩٩﴾
99. Na wamefuatishwa na laana katika (dunia) hii na Siku ya Qiyaamah. Ubaya ulioje wa watakayotunukiwa; laana ya dunia na ya Aakhirah.  




ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْقُرَىٰ نَقُصُّهُ عَلَيْكَ ۖ مِنْهَا قَائِمٌ وَحَصِيدٌ﴿١٠٠﴾
100. Hizo ni baadhi ya habari za miji Tunakusimulia kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); miongoni mwake ingalipo bado, na iliyofekwa.



وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ۖ فَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ لَّمَّا جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ﴿١٠١﴾
101. Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu nafsi zao wenyewe. Basi hawakuwafaa kitu chochote waabudiwa wao waliokuwa wakiwaomba badala ya Allaah ilipokuja amri ya Rabb wako. Na wala hawakuwazidishia isipokuwa mateketezo.



وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ﴿١٠٢﴾
102. Na hivyo ndivyo mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji na huku ikifanya dhulma. Hakika mkamato Wake unaumiza vikali.



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ﴿١٠٣﴾
103. Hakika katika hayo mna Aayah (funzo, zingatio, dalili) kwa anayekhofu adhabu ya Aakhirah. Hiyo ni Siku ya kujumuishwa watu, na hiyo ni Siku ya kushuhudiwa.



وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ﴿١٠٤﴾
104. Na hatuiakhirishi isipokuwa kwa muda maalumu unaohesabiwa.  



يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ﴿١٠٥﴾
105. Siku itakapofika; haitosema nafsi yeyote isipokuwa kwa idhini Yake (Allaah). Basi miongoni mwao ni wenye mashaka wanaostahiki adhabu, na wenye furaha na neema.



فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴿١٠٦﴾
106. Basi ama wale walio mashakani, basi watakuwa motoni, lao humo ni upumuaji pumzi kwa mngurumo na uvutaji pumzi kwa mkoromo.



خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ﴿١٠٧﴾
107. Ni wenye kudumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Hakika Rabb wako Anafanya Atakavyo.


وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖعَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ﴿١٠٨﴾
108. Na ama wale walio furahani, basi watakuwa katika Jannah, ni wenye kudumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Ni hiba isiyokatizwa.



فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَـٰؤُلَاءِ ۚ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ آبَاؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَ مَنقُوصٍ﴿١٠٩﴾
109. Basi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) usiwe katika shaka kutokana na wanayoyaabudu hao (washirikina). Hawaabudu ila kama walivyoabudu baba zao kabla. Na hakika Tutawalipa kikamilifu fungu lao bila ya kupunguzwa.



وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ﴿١١٠﴾
110. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu, zikatiwa ikhtilaafu ndani yake. Na kama si neno lilotangulia kutoka kwa Rabb wako, bila shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wako katika shaka juu yake (hii Qur-aan) inayowatia wasiwasi.



وَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ ۚ إِنَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿١١١﴾
111. Na hakika wote Rabb wako Atawalipa kikamilifu ‘amali zao. Hakika Yeye kwa yale wayatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.




فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿١١٢﴾
112. Basi thibitika imara kama ulivyoamrishwa na aliyetubia pamoja nawe, na wala msiruke mipaka. Hakika Yeye kwa myatendayo ni Mwenye kuona.



وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَاتُنصَرُونَ﴿١١٣﴾
113. Na wala msielemee kwa wale waliodhulumu utakuguseni moto, na hamtokuwa na walinzi badala ya Allaah, kisha hamtonusuriwa.



وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾
114. Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. 



وَاصْبِرْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴿١١٥﴾
115. Na vuta subira kwani hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.



فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ﴿١١٦﴾
116. Basi kwanini hawakuweko katika karne za kabla yenu, walio weledi na wasaa wanakataza ufisadi katika ardhi isipokuwa wachache kati ya Tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu wakafuata anasa walizostareheshwa nazo na wakawa wahalifu.


وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ﴿١١٧﴾
117. Na Rabb wako hakuwa Mwenye kuangamiza miji kwa dhulma na hali watu wake ni wenye kutengenea.



وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ﴿١١٨﴾
118. Na kama Angetaka Rabb wako, basi Angejaalia watu wote kuwa ni ummah mmoja. Na hawatoacha kukhitilafiana.



إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ﴿١١٩﴾
119. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Rabb wako. Na kwa hivyo ndivyo Amewaumba. Na limetimia neno la Rabb wako (kwamba): “Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu wote pamoja.”



وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ ۚ وَجَاءَكَ فِي هَـٰذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿١٢٠﴾
120.  Na yote Tunayokusimulia katika habari muhimuu za Rusuli, Tunathibitisha kwazo moyo wako. Na imekujia katika hii haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.


وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنَّا عَامِلُونَ﴿١٢١﴾
121. Na waambie wale wasioamini: “Tendeni kwa tamkini zenu, nasi pia tunatenda.”


وَانتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ﴿١٢٢﴾
122. Na ngojeeni, nasi tunangojea.”


وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ﴿١٢٣﴾
123. Na ni ya Allaah (Pekee) ghayb ya mbingu na ardhi, na Kwake hurudishwa mambo yote; basi mwabudu Yeye na tawakali Kwake. Na Rabb wako si Mwenye kughafilika na yale myatendayo.




 
[1] Faida: Mahali pa kustakiri ni tumboni mwa mama au duniani. Mahali pa kuhifadhiwa ni ima migongoni mwa baba au kaburini.

Tags

advertisement centil

This blog is created for your interest and in our interest as well as a website and social media sharing info Interest and Other Entertainment.